Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akizungumza
katika kikao cha wadau wanaohusika na mgogoro wa pori tengefu la
Loliondo alichokiitisha katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Ngorongoro, katika tarafa ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro
mkoani Arusha jana. Kupitia kikao hicho aliunda kamati maalum ya kutatua
mgogoro wa muda mrefu wa pori tengefu la Loliondo. Kushoto ni Mkuu wa
Wilaya ya Ngorongoro, Mfaume Taka.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya wadau wanaohusika na mgogoro wa pori tengefu la Loliondo wakiwa kwenye mkutano huo.
NA HAMZA TEMBA -WMU
……………………………………………………………..
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani amesema hakuna
mamlaka nyingine ya Serikali chini ya ofisi ya waziri mkuu yenye mamlaka
ya kutoa tamko au ufafanuzi kuhusiana na Faru John kwa sasa kwakua
jambo hilo bado lipo kwenye uchunguzi.
Amesema
hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika tarafa ya
Loliondo, Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha akiwa kwenye ziara yake ya
kikazi ya siku mbili wialayani humo kwa ajili ya kufuatilia changamoto
za uhifadhi pamoja na utekelezaji wa maagizo wa Waziri Mkuu aliyoyatoa
hivi karibuni akiwa ziarani mkoani Arusha.
Amesema
miongoni mwa maagizo aliyoyatoa Waziri Mkuu katika ziara hiyo ni
kuwasilishwa kwa taarifa ya inayoelezea utaratibu uliotumika kumuhamisha
Faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black
Rhino Sanctuary iliyoko kwenye Hifadhi ya Grumeti pamoja na kuwasilishwa
kwa pembe zake ambapo baadae aliunda tume ya kuthibitisha ukweli wa
taarifa hiyo.
.
“Ripoti
hii ya uchunguzi ni mali ya Waziri Mkuu atakayeweza kutoa ripoti hii
nje kwa ajili ya matumizi ya kila mmoja wetu ni Waziri Mkuu, kwa maana
ya mamlaka, kwa hiyo hakuna mamlaka nyingine yeyote ya Serikali chini ya
Waziri Mkuu yenye uhalali wa kutoa tamko au ufafanuzi wa jambo hili,
mpaka pale Waziri Mkuu atakapokamilisha kusoma ripoti kwa kina kwa
kutumia wataalam wake, kufanya vipimo kama ambavyo tunasikia amevipeleka
kwa mkemia mkuu wa Serikali, pamoja na udadavuzi wa ripoti.
“Kwa
kipindi hiki nnapozungumza, zaidi ya kwamba tunasubiri maagizo au
maelekezo au muelekeo sasa juu ya jambo hili kutoka ofisi ya Waziri
Mkuu, hakuna jambo jingine ambalo Wizara inaweza kufanya wala kusema
kuhusiana na suala la Faru John, hatuna mamlaka hiyo”, amesema.
Akizungumzia
tukio la hivi karibuni la baadhi ya watumishi wa wizara kuonekana
kwenye chombo kimoja cha habari wakitoa ufafanuzi juu ya jambo hilo
amesema “Mimi kwa sasa nnachoweza kusema kwa chochote kilichofanyika
kama kuna utaratibu umetumika kuwafanya waweze kwenda mbele ya vyombo
vya habari, kwenda kutoa taarifa hizo, lakini pia tukijua kabisa kwamba
wao sio wasemaji wa wizara na wala kwa level (hatua) ya jambo lenyewe
pale lilipofikia wao hawana mamlaka ya kuweza kutosha kulizungumzia
jambo hilo, sasa kwanini limekua hivo jana ni jambo ambalo tunalifanyia
kazi, bila shaka walipoitwa pengine hawakuambiwa sawasawa wanaenda
kuzungumzia nini”,.
“Kama
wizara tutachukua sasa muda wa kuweza kuzungumza nao tujue nini
kilitokea lakini kimsingi baada ya hiki nnachokisema hapa sasahivi
ieleweke hivo na taifa zima kwa ujumla kuwa hakuna tunachoweza kusema
sasa hakuna tunachoweza kufanya sasa mpaka uchunguzi unaofanyika chini
ya ofisi ya waziri mkuu ukamilike mpaka waziri mkuu asome aridhike na
taarifa yetu na aweze kuina taarifa ile inafaa kwa namna gani na kama
kuna maagizo mengine atayatoa baada ya hatua hiyo.
Wakati
huo huo ametoa wito kwa wananchi kuwa na subira juu ya taarifa sahihi
za faru John “Unaweza kusikiliza habari kutoka vyanzo vingi tu, lakini
ukishapata habari usiifanyie kazi haraka haraka bila ya kujiridhisha juu
ya ubora wa taarifa unayoipata, wawe na subira, wananchi waendelee
kusubiri, si waliapata taarifa ya faru John kupitia kwa Waziri Mkuu?,
busara ya kawaida inasema kwamba wangesubiri kutoka kwa Waziri Mkuu au
mtu atakayekasimiwa madaraka na Waziri Mkuu atasema kitu kingine
kinachofuatia baada ya pale na si vinginevyo”.
Katika
hatua nyingine Naibu Waziri Makani ameunda kamati maalum ya kuushulikia
mgogoro wa muda mrefu katika pori tengefu la Loliondo baina ya
wananchi, wawekezaji na hifadhi hiyo. Hatua hiyo imekuja ikiwa ni
utekelezaji wa maagizo ya waziri mkuu ya kuwakutanisha wadau katika eneo
hilo kumaliza mgogoro huo.
Kamati
hiyo imehusisha taasisi za serikali, asasi za kiraia, viongozi wa dini,
wazee wa kimila (Leigwanan), viongozi wa vijiji, wajumbe wa kamati
teule za vijiji, wawakilishi wa wanawake na vijana. Ameunda pia kamati
ya kuandaa kanuni za kundesha vikao vya kamati hiyo.
“Kuna
watu humu ndani na hata nje ambao hawataki tumalize migogoro Loliondo,
nitoe rai kwao, waache chokochoko. Wananchi muone umuhimu wa jitihada za
Serikali kumaliza changamoto hii na kutuunga mkono”, alisema Makani.
No comments:
Post a Comment