picha
wa kwanza kushoto ni meneja Utalii na masoko wa Tanapa Ibrahimu Musa
katikati ni Mkurugenzi wa Tanapa Allen Kijazi wa kwanza kushoto ni
mkurugenzi wa kampuni ya Zara Zainabu Ansell wakati wa mkutano wao na waandisi wa habari juu ya maandalizi ya miaka 55 ya uhuru ambayo yanatarajiwa kufanyika december 9
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Zara Tours Zainabu Anselm akiongea juu ya kampuni yake
ambapo aliwataka wananchi wajitokeze kwa wingi kutembelea vivutio
vilivyopo ndani ya nchi yetu na sio kuendelea kuviona kwa mbali tu na
kuvisikia
Mkurugenzi wa mamlaka ya hifadhi za taifa (Tanapa) Allen Kijazi akiongea na waandishi wa habari
meneja Utalii na masoko wa Tanapa Ibrahimu Musa katikati ni Mkurugenzi wa Tanapa Allen Kijazi wa kwanza kushoto ni Afisa uhusiano wa Tanapa Paschal Shelutete
Habari Picha na Woinde Shizza,Arusha
Aliyekuwa mkuu wa
majeshi na mwenyekiti wa bodi ya tanapa jenerali msataafu geogre waitara
anatarajiwa kuongoza msafara wa zoezi la kupanda mlima kilimanjaro
desemba 5 hadi kumi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru
wa tanzania,
Aidha katika msafara
huo wa kupanda mlima kilimanjaro watakuwepo pia wanajeshi kutoka jeshi
la wananchi tanzania pamoja na wanahabari ambao watakuwa wanahabarisha
jamii kuhusiana na tukio hilo.
Akizungumza na
vyombo vya habari mkurugenzi mkuu wa tanapa allan kijazi alisema kuwa
mwaka huu tanzania itaadhimisha miaka 55 ya uhuru na hivyo shrikia hilo
imeshirikiana na kampuni ya utalii ya zara pamoja na bodi ya utalii
(ttb) kuandaa zoezi la kupanda mlima kilimnajro ili kuweza kuhamasisha
watanzania kuvifahamu vifutio vya utalii.
Alisema kuwa zoezi
hilo la upandaji mlima litahusissha baadhi ya viongozi mashuhuri wa
jeshi awastaafu akiwemo aliyekuwa mkuu wa majeshi ili kuhamasisha
watanzania waweze kupanda mlima ambapo tukio hilo litajulikana kama
Uhuru Epedition .
Kijazi alifafanua
kuwa pamoja na kuadhimisha uhuru wa nchi ,lakini madhumuni mengine ya
zoezi hilo ni kuhamasisha utalii na kuhimiza uhifadhi wa mazingira kwani
bado watanzania wengi hawana muamko wa kutembelea vufutio vya utalii
hivyo kujikuta asilimia kubwa ya watalii ni kutoka nje ya nchi.
“Katika maadhimisho
haya tuna malengo ya kuhamasisha watanzania ili wajitokoze kupanda mlima
kilimanajaro pamoja na kutembela hifadhi mbali mbaki kwani tunavyo
vivutio 16 ambavyo vipo ndani ya tanzania na vinahitaji watanzania wote
wanufaike navyo sio tu wageni kutoka nje ya nchi bali hata wa hapa wajue
wanazo fursa “aliongeza kijazi.
Kwa upande wake
mkurugenzi wa zara Zainabu Ansell alisema kuwa watanzania wanapaswa
kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la kihistoria kwani wengi wao
wamekuwa na mawazo potofu ya kufikiria wanaopaswa kupanda mlima na
kutembelea hifadhi ni wazungu tu na wageni kutoka nje ya nchi hali
inayowafanya watanzania kupoteza haki yao.
Kauli mbiu ya zoezi la kupanda mlima kilimanjaro mwaka huu ni endelea kuweka mazingira safi na salama ya fahari ya afrika.
No comments:
Post a Comment