Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali
Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango namna zoezi zima la uhakiki wa
wastaafu kanda ya kaskazini linavyokwenda kabla ya uzinduzi wa zoezi
hilo. Zoezi hili ni kwa mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga.
Zoezi la kuhakiki wastaafu
likiendelea katika Ofisi za Makao Makuu, Halmashauri ya jiji la Arusha,
Pichani ni baadhi ya wastaafu wakifanyiwa uhakiki.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya
Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika akifurahia jambo na baadhi ya
wastaafu wanaolipwa pensheni zao na Hazina, waliojitokeza kuhakikiwa
wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo katika Ofisi za halmashauri ya Jiji la
Arusha, zoezi litakalo dumu kwa siku tano hadi Ijumaa wiki hii katika
mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya
Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika akiongea na baadhi ya wastaafu
waliofika katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa ajili ya
uhakiki ambapo wastaafu hao wameiomba serikali iwaongezee kiwango cha
pensheni wanacholipwa ili waweze kukabiliana na hali ngumu ya maisha.
Baadhi ya Wastaafu wanaolipwa
Pensheni yao na Hazina, waliofika katika Ofisi za Makao Makuu,
Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa ajili ya kuhakikiwa.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya
Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika akihojiwa na baadhi ya waandishi
wa habari wa vyombo mbalimbali mara baada ya kuongea na wastaafu
waliofika kwa ajili ya uhakiki, ambopo wastaafu wengi wameridhishwa na
zoezi hili la wanashukuru zoezi hili linaenda kwa haraka kwani wengi wao
wana nyaraka zote muhimu zinazohitajika.
Wawezeshaji wa zoezi la uhakiki
wakibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango
Bi. Doroth Mwanyika. Kushoto kwake ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali
Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe na Mkaguzi wa Ndani Mkuu Bw. Paison
Mwamnyasi.
Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa
Serikali, Bw. Mohamed Mtonga, akitoa ufafanunuzi kwa wanahabari wa mkoa
wa Arusha kuhusu masuala mbalimbali ya uhakiki wa wastaafu wanaolipwa na
Hazina, unaoendelea katika kanda ya Kaskazini, mikoa ya Arusha,
Manyara, Tanga na Kilimanjaro.
Mstaafu, Mwanakombo Yusuph, mkazi
wa eneo la Kaloleni, Jijini Arusha, akihojiwa na Wanahabari mara baada
ya kuhakikiwa katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ambapo
ameipongeza Serikali kwa kuendesha uhakiki huo utakaosaidia kuhuisha
daftari la wastaafu na kwa uamuzi wake wa kuwalipa wastaafu kila mwezi
badala ya miezi mitatu mitatu.
Bi. Amina Msigiti (kulia) ambaye
ni mstaafu anayelipwa na Wizara ya Fedha na Mipango, akijiandaa kutia
saini fomu yake ya uhakiki mbele ya Afisa wa Hazina, Winfrida Moshi,
kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Baadhi ya Wastaafu wanaolipwa
Pensheni yao na Hazina, Livingstone Kisanga (kulia) na Allen Kijazi,
wakazi wa Arusha, wakisubiri kuhakikiwa katika Ofisi za Halmashauri ya
Jiji la Arusha, wakati wa zoezi la uhakiki wa wastaafu hao linalofanyika
katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na
Manyara).
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango)
No comments:
Post a Comment