Baada ya kususua kwa takribani majuma mawili sasa hatimaye
hati ya uhamisho ya kiungo Mrisho Khalfan Ngassa imetua kwenye klabu ya
Mbeya City fc asubuhi ya leo .
Akizungumza na mbeyacityfc.com
muda mfupi uliopita Mwenyekiti wa City, Mussa Mapunda amethibitisha
kutua kwa ITC hiyo kutoka shirikisho la soka la Oman ikiwa ni siku
chache baada ya klabu ya Fanja kumruhusu Mrisho Khalfan Ngassa kujiunga
na kikosi cha City, ambayo pia inajulikana kama timu ya kizazi kipya.
Ni kweli tumeipata, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa shirikisho la soka nchini,TFF, cham cha mpira cha Oman, hakika wamefanya kazi kubwa kufanikisha kupatikana kwa ITC hii na pia naishukuru Fanja Fc na watendaji wote kwenye timu yetu, tumekuwa na mawasiliano mazuri muda wote mpaka tumefanikiwa alisema.
Akiendelea zaidi, Mapunda
alisema kuchelewa kufika kwa ITC hii hakukuwa na msuguano wowote baina
ya vilabu hivi viwili kilichokuwa kinatokea ni tofauti ya wakati na
siku za ufanyaji kazi kwenye ofisi kulingana na taratibu za nchi hizi
mbili.
Hakukuwa na msuguano wowote uliosababisha kuchelewa kwa ITC hii, kilichokuwepo ni utofauti wa taratibu za kiofisi mara nyingi Oman siku za Ijumaa na jumamosi inakuwa ni mapumiko na huku kwetu Jumapili inakuwa mapumziko, hapo ndipo palikuwa panatuletea mpishano, jambo jema ni kuwa tayari tumeipata na tunaweza kumtumia mchezaji kwenye michezo yote ya ligi na ingine ambayo inaihusu klabu yetu alisema.
Katika hatua nyingine Mapunda
amesema kuwa maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania
bara dhidi ya Mbao fc uliopangwa kuchezwa jumamosi kwenye uwanja wa
Sokoine jijini hapa yanaenda vizuri huku imani kubwa kwa uongozi wa
City ikiwa ni kushinda mchezo huo hasa baada ya suluhu katika michezo
miwili iliyopita.
No comments:
Post a Comment