Pages

Tuesday, December 6, 2016

MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA BARA KATIKA PICHA

1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe.Jenister Mhagama akiongea na Katibu Mkuu Ofisi hiyo (Sera na Uratibu) Dkt Hamis Mwinyimvua wakati akikagua maandalizi ya maandhimisho ya miaka 55 ya Uhuru Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.Wa mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maadhimisho na Sherehe za kitaifa Ofisi ya Wazir Mkuu Bi.Flora Mazelengwa na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Venanche Salvatory Mabeyo.
2
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera na Uratibu) Dkt Hamis Mwinyimvua akimweleza maendeleo ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe.Jenister Mhagama leo uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.Kulia kwa Waziri ni Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Venanche Salvatory Mabeyo.
3
Mkurugenzi wa Idara ya Maadhimisho na Sherehe za kitaifa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Flora Mazelengwa akizungumza na Katibu Mkuu Ofisi hiyo (Sera na Uratibu) Dkt. Hamis Mwinyimvua baada ya ukaguzi wa maandalizi ya ukaguzi wa maandalizi ya maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
4
Viongozi mbalimbali wa Jeshi na Serikali wakifuatilia maandalizi ya miaka 55 ya Uhuru yatakayofanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 9 Desemba.
5 6
Kikosi cha Komando kikiwa katika mazoezi ya kujiweka sawa na maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru yanayotarajiwa kufanyika tarehe 9 katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
7
Bendi ya Jeshi nayo ikiwa katika mazoezi ya nyimbo mbalimbali zitakazotumika katika kuadhimisha miaka 55 ya Uhuru yanayotarajiwa kufanyika tarehe 9 katika Uwanja wa Uhuru JIjini Dar es Salaam.
8
Upakaji wa rangi ukiendelea katika kuupendezesha uwanja wa Uhuru tayari kwa maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru yanayotarajiwa kufanyika tarehe 9 katika Uwanja wa huo.

No comments:

Post a Comment