Pages

Wednesday, December 28, 2016

MAAMUZI YA RUFAA YA KESI YA LEMA KUJULIKANA JANUARI 4, 2017


url
Na.Vero
Ignatus Arusha.



Mahakama kuu kanda ya Arusha imesikiliza maombi ya rufaa yayaliyowasilishwa na upande wa jamhuri na ule wa mshtakiwa Godbless Lema ambapo pande zote

mbili wamekubaliana kusikilizwa rufaa ya upande wa jamhuri ambapo
upande wa serikali wameiomba mahakama kuwasilisha kwa hati ya
maandishi hapo kesho tarehe 30 disemba 2016

Aidha
rufaa hizo ni pamoja na ile ya upande wa Jamhuri kutoridhika na maauzi
ya Jaji Dkt. Modesta Opiyo la kuwapa siku kumi (10) upande wa
mshtakiwa Lema kufaili notisi ya rufaa ,na upande wa wamshtakiwa ni
ile ya kupinga uamuzi wa mahakama ya chini kushindwa kumpa lema
masharti ya dhamana
Jaji
aliyekuwa anasikiliza kesi ya rufaa hizo Salma Magimbi amesema kuwa
mara baada ya upande wa jamhuri kuleta rufaa kwa njia ya maandishi
upande wa mshtakiwa Lema wataijibu tarehe 30 disemba 2016 ambapo
tarehe 2 januari watakutana pande zote kwaajili ya kufanya majumuisho
na maamuzi ya rufaa hiyo yatatolewa tarehe 4 januari 2017
Hata
hivyo baada ya kusikiliza rufaa hizo mahakama imeibua hoja yenyewe na
kuwapa kazi mawakili wa pande zote mbili kuangalia kuwa notisi
iliyowasilishwa na mahakama ya chini imekidhi matakwa ya
kisheria?
Kwa
upande wa wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala amesema kuwa kwa upande
wao wameiomba mahakama kusubirisha rufaa yao ili wasikilize kwanza
rufaa ya upande wa jamhuri kwani rufaa zote zimegongana na zinaelekea
sehemu moja  
“Unajua
leo rufaa mbili zimegongana ile ya upande wa jamhuri na ile ya kwetu
sisi,hivyo basi sisis tumeiomba mahakama kusitisha rufaa yetui
isikilizwe ile ya serikali kwanza,kwani rufaa zote zinaelekea
upandemmoja ,wandege apande ndege na wa basi apande basi “alisema
Kibatala.
Hata
hivyo mbunge huyo wa Arusha mjini Godbless lema amerudishwa rumande
hadi hapo maamuzi yatakapotolewa na mahakam

No comments:

Post a Comment