Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana akisalimiana
na Marehemu Profesa Idrissa Ali Mtulia, Mbunge mstaafu wa Jimbo la
Rufiji wakati alipofanya ziara katika mkoa wa pwani miaka miwili
iliyopia.
…………………………………………………………………..
Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi
rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ndg. Mwishehe Shaban Mlao kufuatia
kifo cha Profesa Idrissa Ali Mtulia, Mbunge mstaafu wa Jimbo la Rufiji
kilichotokea jana tarehe 05 Desemba, 2016 jijini Dar es salaam.
Prof Mtulia ameshika nyadhifa
mbalimbali za uongozi na utumishi katika Chama na Serikali. Alikuwa
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mbunge wa Jimbo la Rufiji,
Katibu Mkuu wizara mbalimbali, Daktari wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Awamu ya Pili na Mwenyekiti wa Bodi ya Madawa (MSD)
Prof Mtulia, atakumbukwa na
wanachama wa CCM na Wananchi wa Mkoa wa Pwani kwa jitihada zake za
ujenzi na uimarishaji wa Chama na mchango wake mkubwa katika maendeleo
ya Wananchi wa Rufiji.
Hakika sisi ni wa MwenyeziMungu na kwake yeye ndio marejeo yetu.
Imetolewa na:-
Christopher Ole Sendeka (MNEC)
MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
06.12.2016
No comments:
Post a Comment