Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu ya
ongezeko la bei ya umeme, Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Umeme, Godfrey
Chibulunje katikati Meneja Mawasialiano wa mamlaka hiyo Titus Kaguo.
…………
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za
Nishati na Maji (EWURA) imeidhinisha asilimia 8.5 ya ongezeko la bei ya
huduma za umeme ili kukidhi gharama za uzalishaji wa umeme.
Ongezeko hilo limetangazwa leo
jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Felix
Ngamlagosi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maombi ya
kurekebisha bei za umeme ambapo marekebisho hayo yanatarajiwa kuanza
kutekelezwa kuanzia Januari Mosi mwaka 2017.
Ngamlagosi amesema kuwa TANESCO
iliomba kuidhinishiwa ongezeko la bei ya huduma hizo ili kuliwezesha
shirika hilo kupata fedha za kulipia gharama za uendeshaji, kupata fedha
za uwekezaji katika miundombinu pamoja na kuhakikisha huduma ya umeme
inawafikia asilimia 75 ya wananchi wote ifikapo mwaka 2025.
”Baada ya TANESCO kuwasilisha
taarifa zinazohitajika kwa ajili ya kukamilisha maombi yao, EWURA
ilifanya mikutano ya taftishi, matangazo kwa umma pamoja na kushirikisha
wadau mbalimbali kutoa maoni juu ya ongezeko hilo ambapo baada ya
uchambuzi wa maoni hayo tulilidhia kuongeza asilimia 8.5 tu ya ongezeko
la bei hizo ,” alisema Ngamlagosi.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa
Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) ambalo linanunua umeme wa jumla
kupeleka Zanzibar limeongezewa asilimia 5.7 ya bei ya umeme badala ya
asilimia 19.1 iliyoombwa na TANESCO.
Amefafanua kuwa kulingana na
marekebisho yaliyofanyika, jumla ya mapato yanayohitajika kwa mwaka 2017
ni shilingi bilioni 1,608.47 ambayo ndiyo iliyopelekea ongezeko la bei
la wastani wa asilimia 8.5 hivyo gharama za umeme zimeongezeka kutoka
shilingi 242.34 kwa uniti moja hadi shilingi 263.02 kwa uniti moja.
Aidha, Mkurugenzi huyo ametoa
maagizo kwa TANESCO yakiwemo ya kuanzisha tozo ya mwezi ya shilingi
5,520 kwa wateja wa kundi linalohusisha viwanda vidogo, mabango na
minara ya mawasiliano, kuboresha huduma kwa wateja pamoja na kuacha
kuwaunganisha wateja wadogo kwenye kundi la wateja wakubwa na badala
yake kuwaonganishe moja kwa moja katika kundi la wateja wadogo.
Amewataka wananchi kuelewa kuwa
kundi linalojumuisha wateja wa majumbani ambao matumizi yao ya umeme
hayazidi uniti 75 kwa mwezi hawataathirika na ongezeko hilo la bei
No comments:
Post a Comment