Pages

Monday, November 28, 2016

SERIKALI KUENDELEA KUVIFUTIA USAJILI VYUO AMBAVYO HAVINA SIFA NCHINI



Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila (kushoto), Naibu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Dk. Magreth Shawa na Naibu Ktibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo (kulia), wakiteta jambo kabla ya maandamano ya kuelekea eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya mahafali ya 11 ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam jana.
 
Picha mbalimbali zikichukuliwa.
Maandamano ya wanafunzi kuelekea eneo maalumu la mahafali hayo yakifanyika.
Maandamano yakiendelea.
Wanafunzi wa chuo hicho wakiwafurahia wenzao wakati 
wakipita na maandamo.
Wanafunzi wakichukua picha. huku wengine wakiwapungia mikono wahitimu.

Baadhi ya walimu wa chuo hicho wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mshereheshaji wa mahafali hayo MC Obed Kipelo akiwa kazini.
Taswira meza kuu. Kutoka kulia ni Naibu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Dk. Magreth Shawa, Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, Mkurugenzi wa Elimu ya Ufunzi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Thomas Katebalirwe, Naibu Ktibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo, Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila, Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Dk. Thomas Ndaluka na Katibu Tawala Wilaya ya Kigamboni, Rahel Mhando.
Brass Band ya Jeshi la Polisi ikitoa burudani. 

Naibu Ktibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo (kulia), akitoa cheti kwa mmoja wa wahitimu.
Wazazi, walezi na ndugu jamaa wa wahitimu hao pamoja na wafanyakazi wa chuo hicho wakijumuika kwenye ahafali hayo.
Matukio mbalimbali yakifuatiliwa.
Mkuu wa Idara ya Uchumi wa chuo hicho, DK. Venance Mutayoba akizungumza katika mahafali hayo.
Mkuu wa Idara ya Ualimu Dk. Bertha Losioki akizungumza
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wafanyakazi wa chuo hicho wakishiriki mahafali hayo. Kutoka kulia ni Anuar Uvila, Evelyne Mpasha na Lilian Kapinga Mduma.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mkuu wa Idara ya Jinsia katika chuo hicho, Dk. Patricia Mwesiga akizungumza.
Ms Calista Francis akizungumza.
Mkuu wa Idara ya Taaluma za Jamii, Dk. Rose Mbwete akizungumza.
Kaimu Mkuu wa Kampasi ya Zanzibar, Ernest Haonga akizungumza kwenye mahafali hayo.
Picha ziukichukuliwa.
Hapa ni safari ya kwenda jengo la utawala kupiga picha.
Picha ya pamoja viongozi mbalimbali, mgeni rasmi na wanafunzi waliofanya vizuri.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Mhitimu Neema Peter Mapunda akionesha cheti chake na mwanafunzi bora alichotunukiwa kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wa ngazi mbalimbali katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wakiwa wameinua kofia zao katika mahafali hayo.
Na Dotto Mwaibale
 
SERIKALI imesema itaendelea kuvifutia usajili vyuo vyote vya
taaluma mbalimbali ambavyo havikidhi viwango nchini.
 
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu
Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo wakati akihutubia katika mahafali ya
11 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam jana.
 
“Wizara kupitia Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na Baraza la
Taifa la Mafunzo ya Ufundi (NACTE) inaendelea na mchakato wa tathmini ya vyuo
vyote kuanzia vyuo vikuu hadi vyuo vya ngazi ya kati ili kubaini ubora
wake” alisema Dk. Akwilapo.
 
Alisema Serikali inaangalia ubora wa Wahadhiri na Wakufunzi,
miundombinu ya chuo husika kama inakidhi utoaji wa elimu bora na usimamizi na
utaratibu wa masomo katika vyuo hivyo na kila kitu kilicho katika mahitaji ya
kufanya chuo kitoe elimu bora.
 
Alisema kwa lengo la kusimamia utoaji bora wa elimu serikali
haitasita kukiondolea usajili chuo chochote ambacho kitadhihirika kutokuwa na
sifa za kukifanya kiwe chuo na kuwa mchakato huo utafanyika kwa kufuata
taratibu za kisheria na kwa uwazi.
 
Dk. Akwilapo alisema uamuzi huo wa Wizara utakuwa endelevu
na hautaishia katika Vyuo tu bali utateremka mpaka kufikia katika ngazi ya
shule za msingi lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa katika miaka michache ijayo
tunaondokana na suala la kuwa na taasisi uchwara katika mlolongo mzima wa
utoaji elimu hapa nchini.
 
Alisema katika suala hilo Baraza la Taifa la Mafunzo ya
Ufundi wiki chache zilizopita ilifuta baadhi ya vyuo ambavyo vilikuwa havikidhi
matakwa ya usajili wao.
 
“Napenda kutamka wazi kwamba kama unaona huwezi
kuendesha taasisi inayotoa elimu kwa ubora unaotakiwa basi nenda kawekeze fedha
zako kwenye sekta nyingine sio elimu kwani imetosha sasa. Na huko kwingine uwe
makini vilevile kwa sababu nako huko utatimuliwa pia” alisema Akwilapo.
 
Aliongeza kuwa mchakato huo hautaishia kwa vyuo pekee badi
na kuangalia udahili wa wanafunzi katika vyuo vya ngazi ya kati na vyuo vikuu
na sifa zao na kuwa mchakato huo utafanyika na kwa wakufunzi.
 
Mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila alisema idadi
ya wahitimu imeongezeka kutoka wahitimu 567 mwaka jana hadi kufikia wahitimu
1013 mwaka huu abapo katika kampasi ya Kivukoni idadi ya wanafunzi imeongezeka
sana katika kipindi cha mwaka wa masomo 2016/2017 na kufikia wanafunzi 5,000
ukilinganisha na wanafunzi 1517 katika mwaka 2014/2015.
 
Akizungumzia katika kampasi ya Zanzibar alisema idadi
imeongezeka hadi kufikia wanafunzi 900 ukilinganisha na wanafunzi 22 katika
mwaka wa masomo 2014/2015 na kuwa hali hiyo inaonesha dalili njema kwa chuo
jinsi gani wananchi walivyo na imani na ubora wa mafunzo yanayotolewa na chuo
hicho.
 

No comments:

Post a Comment