Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (Katikati) akiwasili kwenye Kikao na waendesha bodaboda wa Jiji la Arusha.
Baadhi ya waendesha boda boda wakifuatilia kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya
Ndg. Polycarp Nkuyumba(aliyesimama) akiwakaribisha viongozi na wadau
kwenye Kikao na waendesha boda boda wa Wilaya ya Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Mashaka Gambo (aliyesimama) akiongea na madereva wa boda boda
kuwaelezea mpango wa Serikali wa kuwapatia Pikipiki 200.
Lucas Malusu ni dereva wa boda
boda Kutoka Kata ya Elerai (aliyesimama katikati) akitoa maoni yake
katika kikao chao na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Serafini Shirima(aliyesimama) ni
dereva wa boda boda kutoka Kata ya Levolosi akichangia uanzishwaji wa
umoja wa wandesha boda boda Wilaya ya Arusha (UBOJA)
Viongozi wa mpito waliochanguliwa
kusimamia taratibu za uanzishjwaji wa Umoja huo pamoja na utoaji wa
Pikipiki wa vijana nane wa Kila Kata.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Gambo (aliyesimama mbele) akihitimisha kikao chake na waendesha
boda boda wa Wilaya ya Arusha.
…………………………………………………….
Nteghenjwa Hosseah
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Mashaka Gambo amekutana na waendesha bodaboda wa Jiji la Arusha
na kuwajulisha kuhusu mpango wa Serikali wa kuwakwamua kiuchumi kwa
kuwawezesha kupata Pikipiki bila Riba wala dhamana.
Rc Gambo amekuja na Mpango huu wa
Kuinua uchumi wa Vijana kwa kuwapatia Pikipiki baada ya kukutana na
kundi hili la waendesha boda boda kwa mara na kusikiliza malalamiko yao
huku miongoni mwa kero yao kubwa ni kutozwa fedha nyingi na wamiliki wa
boda boda hizo.
Akiongea na waendesha boda boda
Rc Gambo alisema ninaona jinsi mnavyojituma katika kujitafutia riziki
lakini hamthaminiki na kazi hii imekua ikidharaulika, sasa muda umefika
kwa kazi hii kuwa ya heshima mbele ya Jamii, kila kijana aliyepo
katika biashara hii ataweza kumiliki Pikipiki yake na sio kuendesha
Pikipiki za watu ambao wamekuwa wakiwanyonya kila siku kwa kuwatoza
Fedha nyingi na wao kuzidi kuneemeka wakati ninyi mnazidi kuwa masikini.
“Kundi hili limekuwa likitumiwa
kwa maslahi ya watu wachache kwa kuwa wamekuwa wakipewa Pikipiki hizo
kwa faidi kubwa na mmiliki anapokea Fedha zaidi yya mara mbili ya bei ya
kununulia Pikipiki hiyo ndipo aamue kummilikisha kijana pikipiki hiyo
au aamue kuendelea kupokea Fedha kwa kipindi chote wakati ninyi mnapata
tabu barabarani huko na mnaambulia Fedha kidogo kiasi ambacho hamuwezi
fikia hatua ya kumiliki Pikipiki zenu” Alisema Gambo.
Aliongeza kuwa Serikali ya Mkoa
wa Arusha imeona ni vyema ikawajengea uwezo vijana waliopo katika kazi
hii kwa kuwapa mafunzo na kuwapatia Pikipiki ambazo mtatakiwa kurejesha
kiasi cha Fedha halali iliyonunuliwa Pikipiki hiyo kisha kumilikishwa
chombo bila ya riba yeyote wala dhamana.
Aliendelea kusema utoaji wa
Pikipiki hizi utazingatia Kata zote zilizopo katika Jiji la Arusha ili
Pikipiki ziweze kuwafikia walengwa na zoezi hili litaendelea kwa vijana
wengine kadiri ya mahitaji; Tutaongeza usimamizi kwa wote watakaopata
Pikipiki hizi ili waweze kurejesha Fedha kama inavyotakiwa na tuweze
kuwanunulia vijana wengine hatimaye tuwafikie vijana wote wenye uhitaji
wa kumiliki na kufanya biashara ya bodaboda.
Serafini Shirima ni dereva wa
boda boda Kata ya Levolosi akizungumza katika Kikao hicho alisema kwa
mara ya kwanza Katika Mkoa huu wamepata mlezi anayetambua na kuthamini
kazi ya boda boda na aliyethubutu kuwatafutia Pikipiki za bei nafuu ili
kuongeza kipato cha vijana wa Arusha.
Shirima alishauri kuundwa kwa
kamati ya mpito itakayosimamia na kuratibu mchakato mzima wa vijana
watakaoanza kupewa Pikipiki hizo na kukamilisha taratibu zote za
uanzishaji wa umoja wa wandesha Boda boda utakaofahamika kwa jina la
(UBOJA) chini ya Mlezi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Gambo.
RC Gambo alikamilisha Kikao hicho
kwa kusimamia uchaguzi wa viongozi wa mpito kutoka katika Kila Kata na
hatimaye kupatikana viongozi watano watakaoratibu mpango wa awali wa
utoaji wa Pikipiki kwa vijana.
Pikipiki zitakazotolewa katika
awamu ya kwanza ni 200 zikiwa na thamani ya Tsh Mil 400 na zitatolewa
sanjari na Bima kubwa(Comprehensive Insurance) kwa vijana 200 ambapo
kila Kata itatakiwa kutoa vijana 8.
Vijana wa Arusha watakabidhiwa
Pikipiki hizi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Kassimu Majaliwa tarehe 03/12/2016 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
No comments:
Post a Comment