Rais John Magufuli, akiongozana na
Mgeni wake, Rais wa Zambia Edgar Lungu, (kushoto), wakati wakisalimiana
na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Naibu
Spika wa bunge, Dkt.Tulia Ackson, wakati wa dhifa ya kitaifa ambayo Rais
Magufuli alimuandalia Mgeni wake usiku wa kuamkia leo Novemba 29/2016
Ikulu jijini Dar es Salaam.(PICHA NA IKULU).
Mwananchi wa Kerege Bagamoyo, akipatiwa matibabu wakati wa zoezi la kambi ya matibabu bure katika mji huo. Klabu
ya Rotary ya Oyster Bay pamoja na madaktari na wafanyakazi wa kujitolea
wametoa huduma za matibabu kwa wakazi wa Kerege wilayani Bagamoyo.
Kambi hiyo ya matibabu imeeefanyika Jumapili tarehe 27 Novemba katika
shule ya Msingi ya Kerege.
Klabu
ya Rotary ya Oyster Bay pamoja na madaktari na wafanyakazi wa kujitolea
wametoa huduma za matibabu kwa wakazi wa Kerege wilayani Bagamoyo.
Kambi hiyo ya matibabu imeeefanyika Jumapili tarehe 27 Novemba katika
shule ya Msingi ya Kerege.
Vipimo
na matibabu vilitolewa bure kwa magonjwa kama vile malaria, upungufu wa
damu, kisukari na shinikizo la damu, masikio, pua na koo (ENT),
magonjwa ya ngozi, macho pamoja na meno. Huduma nyingine zilizotolewa
zilikuwa pamoja na ugawaji wa miwani zilizotolewa kwa watu waliokutwa na
matatizo ya macho.
Huduma
za ushauri kwa wajawazito na vifaa vya kujifungulia vilitolewa bure kwa
wajawazito; huduma za ushauri nasaha na upimaji wa UKIMWI pia
zilitolewa. Kwa mara ya kwanza, elimu ya usafi na taulo za wanawake
zilitolewa kwa wasichana.
Akizungumza
katika kambi hiyo, Alfred Woiso, Rais wa Klabu ya Rotary ya Oyster Bay
alisema, “Ni furaha yetu kuwa hapa kwa mara nyingine tena na tunafurahi
kuona wakazi wa Kerege wamejitokeza kuja kupata huduma hizi. Tumetoa
huduma kwa watu waliokuwa na matatizo mbalimbali. Tumeona wagonjwa wengi
wenye magonjwa sugu kama kisukari na shinikizo la damu. Inaonekana kuna
haja ya kupanua wigo wa huduma zetu kwa vile kuna mahitaji ya huduma za
matibabu ya magonjwa mengine.”
Kambi
hiyo ya matibabu ilihudhuriwa na wagonjwa wapatao 800 kutoka Kerege na
maeneo ya jirani. Kambi hii inayoandaliwa na Klabu ya Rotary ya Oyster
Bay imefanyika Kerege kwa mara ya sita sasa kwa lengo la kuwasaidia
wakazi wa Kerege kupata huduma za matibabu, wakazi ambao kwa kawaida
hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.
Kambi
hiyo ya matibabu imedhaminiwa na Diamond Trust Bank na kuandaliwa kwa
ushirikiano na Shree Hindu Mandal Hospital, Vital Supplies, Whitedent,
vClick Concepts Inc, MAK Books and Brains, ABACUS Pharmaceuticals, Fazel
Foundation na wanachama wa Klabu ya Rotary na Rotaractor.
Rais John Pombe Magufuli, akizungumza
huku mgeni wake, Rais wa Zambia, Edgar Lungu, akimsikiliza, wakati Rais
alipomkaribisha Ikulu jijini Dar es Salaam, Novemba 28, 2016. (PICHA NA
IKULU)
Rais Lungu akizungumza
Rais Magufuli akizungumza
Rais Magufuli na mgeni wake, Rais
Lungu, wakifurahia jambo, wakati Rais huyo wa Zambia alipowasili Ikulu
jijini Dar es Salaam, Novemba 28, 2016
Rais Magufuli, na mgeni wake Rais Lungu, wakitazama ngoma za asili
Rais Magufuli na mgeni wake, wakipita
katikati ya gwaride la wanajeshi wa JWTZ, wakati wa mapokezi yake Ikulu
jijini Dar es Salaam
Rais Magufuli akimpokea Rais Lungu alipowasili Ikulu
No comments:
Post a Comment