Pages

Wednesday, November 30, 2016

MTANZANIA WA KWANZA KUPANDA MLIMA EVAREST KATIKA MWAKA 2012. NA MUAFRIKA WA TATU KUPANDA MLIMA HUO MKUBWA DUNIANI


Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said (Mpaka Basi) akiwa na mgeni wake Ndg Wilfred Moshi wakiwasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar, kutembelea na kujionea shughuli za Mkutano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ndg Wilfred Moshi ni Mtanzania wa Kwanza kupanda Mlima Mkubwa Duniani wa Evarest ukiwa na Mita 8,848, Mtanzania huyo Ndg Wilfred Moshi amepanda mlima huo mwaka 2012. akiwa ni Mwaafrika wa Tatu kupanda mlima huo na mwafrika wa Pili mweusi kupanda mlima huo Duniani kwa ukubwa.
Ndg Wilfred Moshi akiwa Zanzibar kwa matembezi na kuangalia Utalii wa Zanzibar na kupata nafasi kutembelea Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar kwa mualiko wa Mhe Mwakilishi wa Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said.
Ndg Wilfred Moshi akitambulishwa kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akiwa Mgeni wa Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said (Mpaka Basi) akisalimia Wajumbe wa Baraza wakati wa kutambulishwa kwake.
Mtanzania wa Kwanza kupanda Mlima Evarest Ndg Wifred Moshi akiwa katika Ukumbi wa Mkutano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akiwa mgeni wa Mhe Simai Mohammed Said. akiwa katika sehemu ya wageni katika ukumbi huo wa Baraza Chukwani Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said, akimtambulisha Mgeni wake Ndg Wilfred Moshi kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid, alipofika kutembelea na kujionea shughuli za Baraza la Wawakilishi wakati wa Mkutano wake leo asubuhi.  
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mtanzania wa Kwanza na Muafrika wa Tatu Duniani kupanda Mlima wa Evarest Ndg Wilfred Moshi alipofika katika jengo la Baraza la wawakilishi Zanzibar akiwa mgeni wa Mhe Simai Mohammed Said Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akitowa maelezo ya mgeni wake Ndg Wilfred Moshi ambae ni Mtanzania wa Kwanza kupanda Mlima Evarest.
Ndg Wilfred Moshi akitowa historia yake kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika katika majengo ya Baraza la Wawakilishi kwa mualiko wa Mhe. Simai Mohammed Said Mwakilishi wa Tunguu Zanzibar. akitowa historia yake ya kufanikiwa kupanda mlima huo mkubwa duniani na kuelezea tayari ameshapanda Mlima Kilimanjaro zaidi ya mara 100.  
Ndg Wilfred Moshi akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya kumbukumbu yake alipofika kutembelea Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar leo. 29-11-2016 akiwa mgeni wa Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika picha ya pamoja na Mtanzania wa Kwanza kupanda Mlima Mkubwa Duniani wa Evarest Ndg Wilfred Moshi alipofika katika jengo la Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.
Zanzinews.com.
othmanmaulid@gmail.com


Meneja Usalama wa SBL, Sebastian Kalugulu  akimkabidhi  Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu baadhi ya mifuko ya saruji 500 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa wahanga wa janga la tetemeko la ardhi lililotoa mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera mjini Bukoba mapema leo.
Meneja Usalama wa SBL, Sebastian Kalugulu  akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu mara baada ya makabidhiano ya mifuko ya saruji 500 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa wahanga wa janga la tetemeko la ardhi lililotoa mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera mjini Bukoba mapema leo.


Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akifurahi jambo na  Meneja Usalama wa SBL, Sebastian Kalugul    mara baada ya makabidhiano ya mifuko ya saruji 500 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa wahanga wa janga la tetemeko la ardhi lililotoa mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera mjini Bukoba mapema leo.




Waandishi wa habari wakichukua matukio wakati wa makabidhiano ya msaada wa mifuko ya mifuko ya saruji 500 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa wahanga wa janga la tetemeko la ardhi lililotoa mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera mjini Bukoba mapema leo.


Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akiongea na wafanyakazi wa SBL waliowakilisha katika kutoa msaada wa mifuko ya mifuko ya saruji 500 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa wahanga wa janga la tetemeko la ardhi lililotoa mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera mjini Bukoba mapema leo.
Bukoba, Novemba 29, 2016-Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetoa msaada  mifuko ya saruji 500 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa wahanga wa janga la tetemeko la ardhi lililotoa mkoani Kagera. Msaada huo ni kuitikia wito wa serikali  kwa mashirika, watu binafsi  na watu wenye mapenzi mema wa kujitoa kusaidia wahanga wa tukio hilo.
Akizungumza katika tukio la kukabidhi msaada huo katika Ofisi ya Mkuuu wa Mkoa wa Kagera mjini Bukoba, Meneja Usalama wa SBL, Sebastian Kalugulu  aliwapa pole  wahanga wa tetemeko hilo  kwa kuwahakikishia kwamba SBL  kila mara iko tayari kusaidia  pindi inapohitajiwa na jamii.
 “”Tunatoa pole ya dhati na masikitiko yetu kwa wahanga wa  tetemeko la ardhi  na tunawaombea majeruhi wote wapone haraka,” alisema Kalugulu, na kuongeza kwamba SBL  inaungana na watu wengine wenye mapenzi mema kutoa msaada wa kibinadamu kwa ajili ya kuwasaidia  kuhimili kadhia iliyowapata  na kurudi katika shughuli zao kawaida.
Kalugulu alithibitisha tena kwamba kampuni hiyo ya bia  imejikita katika kuunga mkono  serikali  na watu binafsi wenye mapenzi mema, mashirika  na makampuni  katika kuisaidia jamii katika maeneo SBL inapoendesha shughuli zake.
 “Ni matumaini yetu kwamba msaada huu utachangia katika michango  iliyokwishatolewa na wasamaria wengine  na kwamba itawawezesha  wahanga hao kujenga  miundombinu iliyoharibika  na hata kuboresha maisha yao.”
 Akizungumzia mchango uliotolewa na SBL, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu alisema kwamba msaada huo unachangia katika michango  mingine  kutoka kwa watu wenye mapenzi mema kutoka ndani, mikoani  na kimataifa  ambao kmwa ukarimu waliitikia wito wa serikali wa kusaidia.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa atahakikisha kuwa  msaada huo unaenda kwenye lengo lililokusudiwa  na kutoa wito  kwa watu zaidi  kuendelea kuwasaidia wahanga.

Mwisho



Katibu Mtendaji wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Fabian Magoma  (kulia), akizungumza katika Kongamano la 33 la siku tano la Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) linaloendelea Hoteli ya Kebby Mwenge jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni  Mwenyekiti wa TPHA anayemaliza muda wake, Daktari Bingwa  Elihuruma Nangawe.

Dk. Manase Frank akitoa mada kwenye kongamano hilo.

 Profesa Andrew Swai akitoa mada.
 Wadau wa sekta ya afya wakifuatilia kwa karibu mada zilizokuwa zikitolewa katika kongamano hilo.
 Kongamano likiendelea.
 Dk. Andronicus Aloyce Rwelamila kutoka Hospitali ya Tumbi Kibaha (kushoto) na Muuguzi wa Hospitali hiyo, Mary Gowele wakiwa kwenye kongamano hilo.
 Kongamano likiendelea

Usikivu katika kongamano hilo. Kushoto ni Mwenyekiti wa TPHA, Dk. Elihuruma Nangawe

 Profesa Japhet Kileo (kulia), akiuliza maswali kwenye 
kongamano hilo.
 Dk. Mwanahamisi Magwangwara (kushoto), akizungumza wakati akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa wadau wa sekta ya afya katika kongamano la 33 la siku tano la Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) linaloendelea Hoteli ya Kebby Mwenge jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni mtoa mada, Profesa Andrew Swai. 
Dk.Chilolo Edward (katikati), akijibu maswali kuhusu changamoto ya waendesha bodaboda. Kushoto ni Profesa Andrew Swai na Dk. Manase Frank. 
Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Jitihada za Maendeleo (WAJIKI), Janeth Mawinza akielezea changamoto ya matumizi ya pombe katika Manispaa ya Kinondoni.

Na Dotto Mwaibale

MADAKTARI nchini wametakiwa kufanya mikutano ya kijamii au wananchi ili kuwapa fursa ya kujua magonjwa yanayo wakabili.

Hayo yalielezwa na Dk. Manase Frank wakati akitoa mada katika kongamano la 33 la siku tano la Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) linaloendelea Hoteli ya Kebby Mwenge jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

"Changamoto kubwa tuliyonayo ni wananchi wengi kutojua magonjwa yanayowasumbua hivyo ni muhimu kwa madakatari kuitisha mikutano itakayowakutanisha na wananchi ili kuondoa changamoto hiyo" alisema Dk. Frank.

Alisema wagonjwa wengi wamekuwa wakikata tamaa kwa kuchangiwa na kauli za baadhi ya madaktari ambao wanashindwa kujua tatizo la mgonjwa husika hivyo wakati umefika wa madaktari kushirikiana kwa karibu na jamii, viongozi wa dini  ili kuondoa changamoto hiyo.

Akitolea mfano wa kijana mmoja ambaye alifiwa na ndugu zake wote wa karibu kutokana na ugonjwa wa ukimwi na kuishi kwa kunyanyapaliwa lakini baadaye afya yake ilikuja kuimarika kufuatia ushauri uliotolewa na daktari kwa  jamii iliyokuwa ikimzunguka wakati wa ugonjwa wake.

Mtoa mada mwingine Profesa Andrew Swai aliomba serikali wakati wa siku ya Jumamosi na Jumapili kufunga baadhi ya barabara ili zitumike kwa wananchi kufanya mazoezi ya kutembea ili kujenga afya za miili yako na kuepukana na magonjwa kama kisukari.

Akizungumzia changamoto ya matumizi ya bodaboda Dk.Chilolo Edward alisema kwa mwaka jana katika Hospitali za mikoa ya  Morogoro, Tumbi Pwani na Shinyanga kulikuwa na ajali 895 huku majeruhi wakiwa 4813.

Alisema majeruhi waliolazwa katika hospitali hizo walikuwa ni 4525, waliopewa rufaa kwenda hospitali za Bugando na Muhimbili walikuwa 71 na waliolazwa ni 702.

Alisema vifo vilikuwa 81 hivyo vilitokea baada ya kufikishwa Hospitalini ni 70 na vilivyotokea eneo la ajali vilikuwa 11.

Dk.Chilolo alisema ili kupunguza changamoto hiyo inapaswa watoa huduma za afya kutoa elimu kwa waendesha boda boda pale wanapofikishwa mahospitali kuhusu umuhimu wao katika familia na taifa kwa ujumla hivyo kuwa makini wanapoendesha vyombo hivyo vya moto badala ya kuacha kazi hiyo kufanywa na polisi au Sumatra.

No comments:

Post a Comment