Mkurugenzi wa TBL Group,Roberto Jarrin (kushoto) akipata maelezo alipotembelea baa ya Shetemba jijini Mwanza
Mkurugenzi wa TBL Group,Roberto Jarrin na maofisa waandamizi wa kampuni wakiwa katiba baa ya Changamoto
Roberto na maafisa wengine waandamizi wa kampuni wakiangalia bidhaa za kampuni zilizopo kwenye masoko
Mmoja wa maofisa wa kampuni ya TBL akiangalia mpangilio wa bia kwenye jokofu kwenye baa ya Changamoto jijini Mwanza
…………………………………………………………………
Katika
kutekeleza majukumu yake kwa Kasi Mpya,Mkurugenzi Mkuu wa TBL
Group,Roberto Jarrin, ambaye pia ni Rais wa kitengo cha Masoko cha
kampuni mama ya kampuni hiyo ukanda wa Afrika Mashariki,mwishoni mwa
wiki alitembelea masoko ya bidhaa za kampuni katika mikoa ya Mwanza na
Mbeya.
Katika
ziara yake hiyo Roberto alifuatana na maofisa waandamizi wa kampuni ya
TBL Group ambapo waliweza kutembelea mabaa mbalimbali na kukutana na
wamiliki wa mabaa .
Ziara
hiyo iliwawezesha kujua changamoto mbalimbali zilizopo kwenye masoko na
kuwawezesha kuzitafutia suluhisho ikiwemo kubuni mikakati ya
kujiimarisha zaidi kwenye masoko hususani katika kukabiliana na
ushindani mkubwa uliopo katika sekta ya uuzaji vinywaji.
TBL Group kwa muda mrefu imekuwa na mkakati wa kufanya kazi kwa karibu na wauzaji wa mwisho wa bidhaa zake wanaozifikisha kwa wateja.
Moja
ya program ambayo inatekeleza kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano mzuri
na wasambazaji hao na kuwawezesha kuwa na biashara imara na endelevu ni
kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali kupitia mpango unaojulikana kama
Retail Development Programme (RDP) ambao umeonyesha kuwa na mafanikio
makubwa.
No comments:
Post a Comment