Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na
Mwenyekiti wa Kikao cha Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi wa Asasi ya
Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika
(SADC Troika), Balozi Dkt. Aziz Mlima akifungua rasmi Kikao cha Makatibu
Wakuu na Maafisa Waandamizi kutoka Asasi hiyo kilichofanyika katika
Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
kupitia agenda mbalimbali zitakazowasilishwa na kujadiliwa kwenye Kikao
cha Mawaziri kitakachofanyika tarehe 03 Novemba, 2016 katika Ukumbi huo.
Asasi ya SADC inaundwa na nchi tatu ambazo ni Tanzania (Mwenyekiti),
Angola (Makamu Mwenyekiti) na Msumbiji (Mwenyekiti aliyemaliza). Kushoto
ni Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa
Afrika, Mhe. Dkt. Stergomena Tax. |
No comments:
Post a Comment