DOGO DEMBELE AONYESHA KIWANGO KATIKA TIMU YA SCOTLAND U16
Kinda mwenye kipaji Karamoko
Dembele, 13, ameshuka dimbani kwa mara ya kwanza na timu ya taifa ya
Scotland U16, na kuonyesha uwezo mkubwa wa kusakata soka katika
mchezo dhidi ya Wales.
Kocha wa Scotland, Brian McLaughlin,
amemmwagia sifa Dembele, kwa kuonyesha uwezo wa hali ya juu na
kuongeza nguvu katika kikosi cha Scotland katika mchezo huo ulioishia
kwa sare ya magoli 2-2.
Dogo Karamoko
Dembele akimtoka mchezaji wa Wales
Dogo Karamoko
Dembele akiwafungasha tela wachezaji wa Wales
TIMU YA MANCHESTER CITY YALIPA KISASI KWA BARCELONA
Manchester City imepambana kiume na
kulipa kisasi cha kufungwa na Barcelona katika mchezo wa awali, baada
ya kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 kwenye dimba la Etihad katika
mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika mchezo huo Lionel Messi
alifunga kiufundi goli lake la 90 katika ligi hiyo akimalizia pasi
nzuri ya Neymar, hata hivyo goli hilo lilisawazishwa na Ilkay Gundogan
akiunganisha pande la Raheem Sterling.
Manchester City ambao walikuwa
wakitafuta ushindi wao wa kwanza dhidi ya Barcelona, waliandika goli
la pili kupitia kwa mpira wa adhabu uliopigwa na Kevin de Bruyne na kisha Gundogan kuongeza la
tatu.
Kevin de Bruyne akipiga mpira wa adhabu ulioandika goli la pili
Ilkay Gundogan akifunga goli katika usiku ambao alijikuta akipachika magoli mawili
Lionel Messi akishangilia goli lake akiwa na Luis Suarez na Neymar
No comments:
Post a Comment