Pages

Sunday, October 2, 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA KIOTUO CHA KUFUA UMEME MZAKWE MKOANI DODOMA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa TANESCO wa mkoa wa Dodoma, Mhandisi Zakayo Temu  (katikati) wakati alipotembelea  Kituo cha Umeme cha TANESCO  cha Dodoma Oktoba 2, 2016. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipokea taarifa kutoka kwa Meneja wa TANESCO wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Zakayo  Temu  (kushoto) kuhusu hali ya upatikanaji wa umeme kwenye makao makuu ya nchi Dodoma wakati alipotembelea  Kituo cha Umeme cha TANESCO cha Dodoma Oktoba 2, 2016.  Wengine Pichani kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, Mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma , Christina Mndeme.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanayakazi na viongozi wa kiwanda cha Gypsum cha Premalt cha Dodoma wakati alipokitembelea mjini Dodoma Oktoba 2, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikagua  uzalishaji katika kiwanda  cha Gypsum cha Premalt cha mjini Dodoma wakati alipokitembelea Oktoba 2, 2016
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa mkurugenzi wa kiwanda cha Magodoro Dodma, Haidary Gulamali, magodoro 200 yenye thamani ya shilingi milioni 10 ukiwa ni  msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.  Makabidhiano hayo yalifanyika baada ya Waziri Mkuu kutembelea kiwanda hicho Oktoba 2, 2016. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akitazama Spring zinazotumika kutengeneza magoro  wakati aliopotembelea kiwanda cha Magodoro Dodoma Oktoba 2, 2016. Kushoto ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Haidary Gulamali.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kiwanda cha Magodoro Dodoma baada ya kutembelea kiwanda hicho Oktoba 2, 2016. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho,  Haidary Gulamali na kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana na wapili kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama

Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akitazama moja ya kiti kilichong’olewa jana katika mechi ya Simba na Yanga na Serikali kufikia  uamuzi wa kuzuia timu hizo kutumia Uwanja wa Taifa kutoka na uharibifu wa miundombinu uliotokea katika mechi yao iliyofanyika Oktoba Mosi 2016. (PICHA NA PICHA NA RAYMOND MUSHUMBUSI)


Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akitazama moja ya kiti kilichong’olewa jana katika mechi ya Simba na Yanga na Serikali kufikia  uamuzi wa kuzuia timu hizo kutumia Uwanja wa Taifa kutoka na uharibifu wa miundombinu uliotokea katika mechi yao iliyofanyika Oktoba Mosi 2016.



 NA K-VIS BLOG

SERIKALI imetangaza kuzifungia timu za soka za Yanga na Simba kuutumia uwanja huo, wakati zinapokutana kwenye michezo ya soka.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametangaza leoOktoba 2, 2016 alipofika kwenye uwanja huo kujionea uharibifu uliofanywa na mashabiki wa Simba, kwenye pambano la ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara lililopigwa jana Oktoba 1, 2016, ambapo baadhi ya mashabiki wa Simba wenye hasira, waling’oa viti kufuatia bao la Amisi Tambwe, lililolalamikiwa kuwa lilifungwa baada ya mchezaji huyo kuutuliza mpira wa Kross kwa mkono.
“Nimetembelea uwanja wa Taifa na kukagua uharibifu uliofanywa na mashabiki wa Simba katika mechi dhidi ya Yanga hapo jana. Yafuatayo ni maamuzi yaliyochukuliwa na Serikali,” Ameandika Waziri Nape kwenye ukurasa Wizara ya Habari ulio kwenye Facebook.
Kwa mujibu wa Waziri Nape, maamuzi hayo ni pamoja na:-
1)Simba na Yanga hazitoruhusiwa kutumia uwanja wa taifa hadi hapo itakapo amualiwa vinginevyo.
2)Simba itatakiwa kulipia hasara iliyotokana na uharibifu huu.
3)Simba haitopata mgao wake wa mechi ya jana.
4)Kamera za CCTV zitafungwa uwanja mzima kufuatilia mienendo ya mashabiki wanapokuwa uwanjani ili kuweza kuwatambua watu wote watakao jihusisha na vitendo vya fujo.
Tayari uongozi wa Simba umetoa tamkola kuomba radhi kutokana na hatua ya washabiki wake, lakini ikatupia lawama maamuzi mabovu ya waamuzi wa pambano hilo ikiwa ni pamoja na kuruhusu bao "haramu' alilofunga Amisi Tambwe, kwa vile alipokea pasi kwa mkono kabla ya kufunga, Hali kadhalika taarifa hiyo ya Simba, imesema, mwamuzi huyo pia alikataa bao la mshambuliaji wake Ajib, kwa maelezo kuwa mfungaji alikuwa ameotea kitu ambacho washabiki wengiwa Simba wanadai haikuwa sahihi. Katika pambano hilo la ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba licha ya kucheza wakia pungufu kwa muda mrefu, walifanikiwa kusawazisha bao hilo kwenye dakika za mwisho mwisho na hivyo pambano hilo kuwa sare ya bao 1-1.

 Nape akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea uwanja huo leo Oktoba 2, 2016
Waziri Nape akikagua viti vilivyoharibiwa
S




NA ARON MSIGWA - NEC.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itaendelea kutoa elimu ya Mpiga Kura kote nchini ili kuwajengea wananchi uelewa sahihi juu  majukumu ya Tume na  chaguzi zinazofanyika nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Jaji Lubuva amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakishindwa kutimiza Haki yao ya Kikatiba ya kupiga Kura kuwachagua viongozi wananowapenda kwa sababu ya kukosa uelewa juu ya Sheria, Kanuni na taratibu zinazosimamia Uchaguzi .
Amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 inaipa NEC jukumu la kusimamia na kuendesha Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa upande wa Tanzania Bara  na kubainisha kuwa ili jukumu hilo lifanywe kwa ufanisi wananchi waliotimiza vigezo vya kupiga kura na wale wanaotarajia kupiga kura  miaka  ijayo lazima wapatiwe  elimu sahihi ya Mpiga Kura.
Amefafanua kuwa baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015, NEC ilianza kutekeleza programu mbalimbali ikiwemo kutoa elimu ya Mpiga Kura kuwafikia wananchi moja kwa moja kupitia mikutano mikubwa inayohusisha viongozi mbalimbali,   maonesho ya Sabasaba na  Nane Nane , kutoa elimu ya Mpiga kura kwenye vyombo mbalimbali vya habari pamoja na kuzitembelea baadhi ya shule za Sekondari za mkoa wa Singida na Mara.
" Moja ya shughuli za Tume ni kuendesha na kusimamia uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani nchi nzima kwa upande wa Tanzania Bara, ili shughuli hii tuifanye vizuri ni muhimu sana tuwapatie wananchi elimu sahihi juu ya upigaji wa kura, tutafanya jambo hili tukishirikiana na wadau na Asasi nyingine ambazo tutazipa  kibali cha kutoa elimu hii" Amesisitiza Jaji Lubuva.
Jaji Lubuva amebainisha kwamba utoaji wa elimu hiyo utaongeza idadi ya wapiga kura kwenye chaguzi zijazo akitoa mfano wa idadi pungufu ya wapiga waliojitokeza kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na ule uliofanyika Oktoba 25 , 2015 ambapo baadhi ya wananchi walioandikishwa kwenye daftari la kudumu la Wapiga Kura na kupewa vitambulisho hawakujitokeza kupiga kura.
" Tunalenga kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi pia umuhimu wa wananchi kushiriki Kupiga Kura, baadhi ya wananchi wamekuwa wakijitokeza ili wapate vitambulisho jambo ambalo sio sahihi,  mfano mwaka 2010 wananchi milioni 15 walijiandikisha kupiga kura lakini waliojitokeza kupiga kura ni milioni 8.626 hii ni idadi ya chini, pia  mwaka 2015 wananchi waliojiandikisha walikuwa milioni 23,161,440 lakini waliojitokeza Kupiga Kura ni watu milioni 15,589,639 hapa kuna ongezeko,  tunaamini tukiwapatia elimu wengi zaidi watajitokeza kuwachagua viongozi wanaowapenda " Amesitiza Jaji Lubuva.
Amesema katika kuendelea kupanua wigo wa utoaji wa elimu ya Mpiga Kura kwa wananchi wengi zaidi NEC itashiriki Kongamano na maonesho ya Wiki ya Vijana yatakayoambatana na Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2016 Oktoba 7 hadi 14, 2016 mkoani Simiyu ambapo pamoja na Mambo mengine watendaji na Maafisa wa Tume watatoa elimu ya Mpiga Kura kwa wananchi na kutembelea shule za Sekondari za mkoa huo.
Aidha, ili kuboresha chaguzi zijazo ametoa wito kwa wananchi waendelee  kushirikiana na Tume kwa kujitokeza kwa wingi kuuliza maswali na kupata ufafanuzi wa hoja mbalimbali katika maeneo ambayo watendaji wa NEC watafika kutoa elimu ya Mpiga Kura

Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa,
wakati  wa kufunga Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani Septemba 30, 2016.(PICHA NA IKULU)

Amiri  Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli na meza kuu wakipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa wakati wa kufunga Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016


Amiri  Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli na meza kuu wakipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa wakati wa kufunga Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016


Meli za kivita, Vifaru vikiwa katika zoezi la Amphibious Landing katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016



Ndege vita katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kufunga maadhimisho hayo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu mara baada ya kuwasili katika Kijiji cha Baatini ili kushuhudia zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' na kufunga maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi kabla ya kwenda kushuhudia zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' na kufunga maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kabla ya kuelekea kwenda kushuhudia zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' katika kijiji cha Baatini Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akipita mbele ya Askari mbalimbali wa JWTZ walioshiriki katika zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' katika kijiji cha Baatini Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wakati akielekea kwenye  bendi ya Jeshi ya Mwenge iliyokuwa ikitumbuiza viwanjani hapo.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akipita mbele ya Askari mbalimbali wa JWTZ walioshiriki katika zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' katika kijiji cha Baatini Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wakati akielekea kwenye  bendi ya Jeshi ya Mwenge iliyokuwa ikitumbuiza viwanjani hapo.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma wakati bendi ya Jeshi ya Mwenge Jazz ilipokuwa ikitumbuiza kabla ya kufunga rasmi maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani jana. Pembeni yake ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akimpigia makofi.



 Askari mbalimbali wa JWTZ walioshiriki katika zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' wakipiga makofi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya Askari Mgambo walioshiriki katika zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' katika kijiji cha Baatini Wilayani Bagamoyo mara baada ya kufunga maadhimisho ya miaka 52 ya JWT
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Haji Omar Kheir akilakiwa na makamanda. Nyuma yake ni Katibu Mkuu Kiongozi wa SMZ  Dkt. Abulhamid Yahya Mzee
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akiongea na Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Robert Mboma
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Davies Mwamunyange  alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi  alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu  wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Kipilimba alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu   alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Afande  John Casmir Minja alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna  Valentino Mlowola alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na  Kaimu Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mama  Victoria Lembeli alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea saluti toka kwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Venance Mabeyo alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Venance Mabeyo  alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Robert Mboma alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Mama Suzana Mlawi
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Majenerali wa JWTZ 
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa zoezi hizo Meja Jenerali James Mwakibolwa
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akijiandaa kuweka saini katika kitabu cha wageni akishuhudiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini katika kitabu cha wageni
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine akisikiliza muhtasari wa zoezi hilo
Wanadhimu wa zoezi
Sehemu ya wasimamizi wa zoezi hilo
Mkurugenzi Mkuu wa zoezi hizo Meja Jenerali James Mwakibolwa akisoma taarifa 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine akisikiliza muhtasari wa zoezi hili
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine akisikiliza muhtasari wa zoezi hili
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Robert Mboma
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange kabla ya kuelekea kwenye uwanja wa zoezi la Medani

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongozana  na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange kuelekea kwenye uwanja wa zoezi la Medani
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongozana  na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi kuelekea kwenye uwanja wa zoezi la Medani
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongozana  na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi na  kuelekea kwenye uwanja wa zoezi la Medani
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa akiwa  na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa akiwa  na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa zoezi hilo Meja Jenerali James Mwakibolwa (kushoto)
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kulia) na mmoja wa washereheshaji Meja BMP Mlunga wakipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa
Brass band ya JWTZ ikiwa tayari tayari
Mcheza ngoma hodari wa kikundi cha sanaa cha JWTZ  Private Juma Abdulrahman Juma akikaribishwa jukwaa kuu kupewa zawadi kwa burudani nzuri iliyooneshwa na kikundi chake
Mcheza ngoma hodari wa kikundi cha sanaa cha JWTZ  Private Juma Abdulrahman Juma akiendelea kutoa burdani baada ya kukaribishwa jukwaa kuu kupewa zawadi kwa kazi  nzuri iliyooneshwa na kikundi chake
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimtuza  Private Juma Abdulrahman Juma kwa niaba ya wenzie kwa burudani nzuri.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpongexza kwa burudani nzuri  Private Juma Abdulrahman Juma kwa niaba ya wenzie
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akimtuza  Private Juma Abdulrahman Juma kwa niaba ya wenzie
Makamanda wakipiga bastola za miali kuashiria kuanza kwa zoezi hilo la medani
Kazi imeanza....
Ndege vita zikiwa katika fomesheni 
Ndege vita angani
Sehemu ya ndege vita
Mpiga picha mwandamizi wa magazeti ya Daily News na Habari Leo Mroki Mroki akiwa kazini kurekodi zoezi hilo


NA K-VIS BLOG
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,  ambaye amekuwa kiongozi wa kwanza wa ngazi za juu wa Serikali kuhamia Dodoma tangu nchi hii ipate Uhuru zaidi ya miaka 50 iliyopita, jana Oktoba1, 2016 alifanya ziara  kwenye maeneo mbalimbali ya Manispaa hiyo, ziara ambayo wachambuzi wa mambo wameelezea  ni kujifunza jinsi wakazi wenzake wanavyopambana kuendesha maisha  ili hatimaye aweze kwenda nao sambamba. Maeneo aliyozuru Waziri Mkuu ni pamoja na sehemu za huduma za jamii kama soko kuu la Majengo, Hospitali ya Rudaa ya Mkoa, miradi inayotekelezwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA).  Awali kabla ya kufanya ziara hiyo, Waziri Mkuu alifanya mkutano na viongozi wote wa Manispaa hivyo na kuwaeleza mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujiandaa kupokea watu zaidi watakaohitaji kuja kuwekeza kwenye Manispaa hiyo. Mapema mwaka huu, Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Dakta John Pombe Magufuli, akitoa shukrani kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, aliahidi serikali yake nzima kuhamia Dodoma katika kipindi cha uongozi wake wa miaka mitano ili kuupa hadhi mkoahuo wa kuwa Makao Makuu ya nchi. Kufuatia ahadi hiyo, Waziri Mkuu alianza kwa vitendo kutekeleza ahadi ya Rais, na kusema yeye atakuwa kiongozi wa kwanza kuhamia Dodoma. Pichani, Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa   akitembelea moja ya mabucha ya nyama alipozuru soko kuu la Majengo la Manispaa ya Dodoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu akitembeela soko laMajengo
Kama kawaida ya watanzania wengi siku hizi suala la matumizi ya mbango kama njia ya kuwasilisha ujumbe wao kwa viongozi  wafanyabiashara  hawakuzubaa  wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea soko kuu la manispaa ya Dodoma la majengo Oktoba 1, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa maelekezo ya kuboresha usafi wa mazingira ya hospitali ya Mkoa wa Dodoma wakati alipoitembelea  hospitali hiyo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimjulia hali Bi. Fatuma Yassin wa Swaswa Dodoma wakati alipotebelea hospitali ya mkoa wa Dodoma Oktoba 1, 2016.  Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama.
Baadhi ya watumishi wa hospitali ya mkoa wa Dodoma wakishangilia wakati Waziri Mkuu akitoa hotuba
Baadhi ya watumishi wa hospitali ya mkoa wa Dodoma wakishangilia wakati Waziri Mkuu akitoa hotuba
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa hospitali ya mkoa wa Dodoma baada ya kutembelea hospitali hiyo Oktoba 1, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana
 Waziri Mkuu, akitembelea Hospitaliya Rufaa ya Manispaa ya Dodoma
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wafanyabiashara wa soko Kuu la manispaa ya Dodoma la Majengo
 Waziri Mkuu akitembelea soko kuu la Majengo
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Jordan Rugimbana akimkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuzungumza na wafanyabiashara wa soko kuu la Manispaa ya Dodoma la Majengo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyabiashara wa Soko kuu la Dodoma la Majengo 
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa skisalimiana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) Paskas  Mulagili baada ya kuwasili kwenye nyumba za CDA za Kikuyu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana  na watumishi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Mkuu (CDA) wakati alipokagua ukarabati wa nyumba za CDA za Kikuyu

Nyumba za Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA)  za Kikuyu zinazokarabatiwa  ili zitumiwe na maofisa wa serikali  watakaohamia Dodoma


Nyumba za Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA)  za Kikuyu zinazokarabatiwa  ili zitumiwe na maofisa wa serikali  watakaohamia Dodoma


Nyumba za Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA)  za Kikuyu zinazokarabatiwa  ili zitumiwe na maofisa wa serikali  watakaohamia Dodoma


JOZI LOUNGE YADHAMINI MISS TANZANIA 2016

Club maarufu kwa jina la Jozi Lounge iliopo msasani jijini Dar Es Salaam, imejitokeza hivi karibuni kujiunga na moja katika kampuni na taasisi zilizokwisha kujitokeza kudhamini zoezi zima la kutafuta mrembo wa tanzania atakayepeperusha na kuitangaza Tanzania katika anga za kimataifa katika Nyanja mbalimbali yakiwemo utalii na huduma ya jamii yenye mahitaji maalum.


Akizungumza na warembo kutoka mikoa yote Tanzania ambao wanatarajia kuchuana vikali mwishoni mwa mwezi wa kumi huko jijini Mwanza na hatimaye kumpata mshindi wa Miss Tanzania 2016, Mkurugenzi wa Jozi Lounge Bw.Dismas Massawe amesema Jozi Lounge itawadhamini warembo hao kwa kuwapatia malazi, chakula na mahitaji mengine muhimu kwa kipindi cha siku tatu ambapo jana ilikuwa uzinduzi na leo ni siku ya semina mbalimbali na siku ya jumapili itakuwa siku ya kusherehekea ushindi wa mikoa tayari kuelekea katika mapambano ya ngazi ya Taifa.

Washiriki wa shindano la Miss Tanzania 2016 wakiwa katika moja ya pozi jana mara baada ya kuwasili Jozi Lounge, ambapo watakuwa hapo kwa siku tatu mfululizo. Jozi lounge ni mojawapo wa wadhamini wa mashindano ya miss tanzania mwaka huu 2016
 Wakipata vinywaji kwa pamoja huku wakifurahia utulivu mwanana ndani ya Jozi Club
Baadhi ya Washiriki wa shindano la Miss Tanzania 2016,ambapo jana wameingia kambini pia walipata muda wa kuserebuka ndani ya Club maarufu kwa jina la Jozi Lounge iliopo msasani jiji Dar EsSalaam.
 Washiriki wa Miss Tanzania 2016 wakiserubuka ndani ya Jozi Club kwa raha zao
 Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akizungumza na watumishi wa serikali na Taasisi zake mjini Dodoma Oktoba 1, 2016. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Baadhi ya watumishi wa serikali na Taasisi zake wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao mjini Dodoma Oktoba 1, 2016. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi(kulia), akimkabidhi moja ya meza Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu.(Mwenye suti nyeusi), kwa ajili ya shule ya sekondari Ikoma iliyoko wilayani huko. TPB imetoa madawati 50, ikiwa ni pamoja na viti na meza kama msaada wa benki kusaidia sekta ya elimu nchini. Msaada huo una thamani ya shilingi milioni 4.
Mkuu wa wilaya. Nurdin Babu, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi madawati.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, akikaribushwa na Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu kwenye shule ya sekondari Ikoma, wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati.
                                                                            TPB yachangia madawati Serengeti
Benki ya Posta Tanzania (TPB) imetoa mchango wa madawati na viti 50 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni Nane kwa Shule ya Sekondari ya Ikoma, iliyopo Wilayani Serengeti Mkoani Mara. Mchango huo wa madawati ulikabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Nurdin Babu na Afisa Mtendaji Mkuu wa (TPB) Sabasaba Moshingi, kwenye hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Sabasaba Moshingi alisema kuwa benki yake imeamua kutoa viti pamoja na madawati hayo ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wote watakaoanza kutumia shule hiyo hapo mwakani watakaa kwenye mazingira mazuri yanayofaa. Pia alitoa pongezi nyingi kwa uongozi wa Kijiji hicho cha Ikoma kwa bidii zao zilizohakikisha kuwa wanakamilisha ujenzi wa madarasa pamoja na maabara, tayari kwa kupokea wanafunzi mwaka ujao. Aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa uongozi huo ili kuweza kukabiliana na changamoto nyingine kama vile uhaba wa nyumba za waalimu na mabweni zinazoendelea kuikabili shule hiyo.
Naye mgeni rasmi kwenye shughuli hiyo Mhe. Nurdin Babu aliishukuru Benki ya Posta kwa msaada huo uliofika wakati muafaka, ambapo shule hiyo inajiandaa kupokea wanafunzi wapya. Alisema kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania mwenye mapenzi mema kuhakikisha kuwa anatoa kipaumbele kwa sekta ya elimu ili kuwawezesha watoto wetu kupata elimu kwenye mazingira mazuri. Alitoa wito kwa taasisi nyingine kuendelea 
kuchangia sekta ya elimu hususan shule hiyo, ili waweze kutatua changamoto nyingi zinazoikabili shule hiyo.
    


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika eneo la JKT Mgulani ambapo shughuli za uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika jiji la Dar es Salaam zilifanyika.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe. January Makamba akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti iliyofanyika JKT Mgulani, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti jijini Dar es salaam inayokwenda kwa jina la MTI WANGU iliyozinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka udongo katika mti alioupanda eneo la JKT Mgulani Barabara ya kilwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika jiji la Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijiunga na mtandao kwenye eneo la Gymkhana ambalo huduma ya WI-FI inapatikanika bure kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
....................................................................................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo tarehe 1 Oktoba 2016 ameongoza mamia ya wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam katika uzinduzi rasmi wa kampeni ya upandaji miti inayojulikana kama Mti wangu Jijini Dar es Salaam.

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo katika eneo la barabara ya Kilwa – Kurasini katika wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais ameviagiza vyombo vya dola mkoani Dar es Salaam ambavyo vimepewa jukumu la kutunza miti hiyo iliyopandwa ili isiharibiwe vihakikishe vinatekeleze jukumu ili kikamilifu ili kuhakikisha miti hiyo iliyopandwa inakuwa vizuri ili kulifanya jiji la Dar es Salaam kuwa miongoni mwa Majiji bora katika utunzaji wa Manzingira.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa kampeni hiyo ambayo ameizindua Jijini Dar es Salaam inatakiwa ifanyike nchini kote kama hatua ya kurejesha uoto wa asili na utunzaji wa vyanzo vya maji kote nchini.

Amesema kuwa jitihada za kupanda miti nchini zinatakiwa kuimarishwa maradufu kwani zitasaidia katika uhifadhi wa mazingira hususani katika suala zima la kupambana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.

Makamu wa Rais katika hotuba yake ameeleza kuwa tafiti mbalimbali zinaonyesha kuongezeka hewa ya ukaa katika jiji la Dar es Salaam kutokana na ongezeko la viwanda na idadi kuwa ya watu hivyo jitihada za pamoja kati ya serikali,taasisi binafsi,asasi za kiraia na wananchi zinahitajika katika kutunza mazingira na kupanda miti.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pia amepongeza jitihada za uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam katika uboreshaji na uimarishaji wa mifumo ya maji katika barabara itakayosaidia kurahisisha umwagiliaji wa miti iliyopandwa.


Amesema anafaraja na matumaini makubwa kuwa kampeni aliyoizindua ya upandaji miti itakuwa endelevu na miaka michache ijayo italifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa kivutio na mfano wa kuigwa na mikoa mingine kwa kuwa na mwonekano mpya na wa kuvutia.
Baada ya kuzindua kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais ambaye aliambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu Rais Mazingira na Muungano January Makamba na Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe alifanya ziara fupi ya kutembelea na kukagua mifumo wa maji katika barabara ya Nyerere na Ally Hassan Mwinyi itakayotumika kumwagilia miti iliyopandwa pamoja na kuongeza na wananchi walioshiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la Gymkana.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella, akizungumza kwenye Ufunguzi wa Mkutano wa Robo Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu JMAT, tawi la Mwanza na Geita, unaofanyika leo kwenye ukumbi wa jengo la NSSF Jijini Mwanza.

Mongella amewataka wajumbe wa mkutano huo kujadili kwa uwazi masuala ya maadili kwa watumishi wa umma na kwamba yawe ajenda ya kudumu katika ngazi mbalimbali za utendaji serikalini hususani katika ngazi ya mahakama.

Amesisitiza mkutano huo kutoka na maadhimio yanayohimiza mahakama kutenda haki na kuleta manufaa kwa wananchi na kuondokana na malalamiko kwamba mahakama hazitendi haki katika maamuzi yake.

Mwenyekiti wa JMAT tawi la Mwanza, Francis Kishenyi, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, chama hicho kinahakikisha watumishi wa mahakama wakiwemo Majaji na Mahakimu wanafanya kazi kwa kutenda haki na kuwafanya wananchi kutambua umuhimu wa chombo hicho katika utoaji wa haki.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ikiwemo maadili ya viongozi wa Umma. 
Na BMG
Jaji Mfawidhi Kanda ya Ziwa, Mhe.Robert Makaramba, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa JMAT tawi la Mwanza, Francis Kishenyi, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, akizungumza na wanahabari nje ya mkutano huo.
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi mkoani Mwanza, Mhe.Wilbert Martin Chuma, akizungumza kwenye mkutano wa robo Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu mikoa ya Mwanza na Geita, unaofanyika leo Jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu kwenye mkutano huo
Viongozi mbalimbali wa vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani Mwanza, wakiwa kwenye mkutano huo.
Viongozi mbalimbali kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii NSSF mkoani Mwanza, wakiwa kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa mkuatno huo
Katibu wa JMAT ambaye pia ni Hakimu Mkazi mkoani Mwanza, Bittony Mwakisu (kulia) akiwa pamoja na Domician Mlashani, Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo wilayani Sengerema na mjumbe wa Kamati tendaji JMAT (kushoto).
Picha ya pamoja
Viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Pamoja na mambo mengine, mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ikiwemo maadili ya viongozi wa Umma.

Baadhi ya warembo wakiwasili kwenye Duka na Mgahawa wa Kampuni ya Tomoni Farm, la 'The Farm Fresh Market', maeneo ya Victoria jijini Dar es Salaam kujionea shughuli mbalimbali zifanywazo na kampuni hiyo, pia kujipatia chakula cha mchana.
Mkurugenzi wa Lino Agency, waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundega akizungumza na waandishi wa habari hotelini hapo mara baada ya idadi kubwa ya warembo hao kuwasili tayari kuanza kambi rasmi. Kushoto ni Mkuu wa Itifaki Albert Makoye na kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Miss Tanzania, Deo Captain.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tomoni, wauzaji wa mbogamboga za majani, nyama, vyakula na juisi za matunda halisi, Franklin Bagalla, akiwapatia maelezo warembo hao walipotembelea duka la kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam. 
Warembo watakaoshiriki shindano la Miss Tanzania, 2016, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Tomoni, wauzaji wa mbogamboga za majani, nyama, vyakula na juisi za matunda halisi, Franklin Bagalla (katikati), nje ya duka la The Farm Fresh Market, Victoria jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tomoni, wauzaji wa mbogamboga za majani, nyama, vyakula na juisi za matunda halisi, Franklin Bagalla (katikati), akiwapatia maelezo warembo hao, wakati akiwambeza kwenye sehemu mbalimbali za kampuni hiyo, leo jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya warembo wa Miss Tanzania wakiangalia Menu walipofika Mgahawa wa Kampuni ya Tomoni Farms, Victoria jijini Dar es Salaam.
Washiriki hao ambao ni washindi kutoka Kanda 9 na mikoa mbalimbali Tanzania watapokelewa katika Hotel ya Regency Park iliyopo Mikocheni D’salaam, na baadae watapiga kambi ya siku 4 katika Hotel ya Jozi Lounge iliyopo Msasani jijini D’salaam.

Mara baada ya kuingia kambini washiriki hao 30 pamoja na Wasimamizi wao watakuwa na Semina ya pamoja ambapo watafundishwa masuala mbalimbali yahusuyo mashindano pamoja na kambi kwa ujumla. 

Wakiwa kambini washiriki hao watafanya ziara katika mikoa ya Dodoma, Singida, Arusha, Geita na Mwanza kwa shughuli mbalimbali za kijamii.

Kauli mbiu ya mashindano ya Miss Tanzania 2016 ni Urembo na Mazingira Safi, hivyo washiriki wote watafanya kazi mbalimbali kijamii ikiwa ni pamoja na  usafi wa mazingira, kutunza mazingira na pia kushiriki katika kampeni ya kupanda miti itakayofanyika tarehe 1 Oktoba 2016 nchini pote.

Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016 yamekuwa na changamoto kubwa ya kupata wadhamini wachache waliojitokeza kudhamini mashindano haya katika mikoa na sehemu mbalimbali.

Tunachukua fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru Wadhamini wote waliojitokeza na kuchangia kwa njia mbalimbali katika kufanikisha mashindano ya mwaka huu.

Tunawashukuru pia washiriki wote katika ngazi zote waliojitokeza kushiriki na pia shukrani kwa wazazi na walezi walioruhusu watoto wao kushiriki mashindano ya urembo ya miss Tanzania 2016.

Ni matarajio yetu kwamba wadau wote wa tasnia hii ya urembo nchini mtajitokeza kwa wingi katika Fainali za Shindano la Miss Tanzania 2016 linalo tarajia kufanyika mwishoni  mwa mwezi Oktoba 2016.

 ORODHA YA WAREMBO WA MISS TANZANIA 2016 

JINA 
MKOA/ KITUO 
KANDA
  1. JULITHA KABETHE
  2. NURU KONDO
  3. GRACE MALIKITA
  4. SPORA LUHENDE
DAR CITY CENTRE
UKONGA
TABATA
DAR CITY CENTRE
         
KANDA YA ILALA
  1. DIANA EDWARD
  2. REGINA NDIMBO
  3. NDEONANSIA PIUS
  4. HAFSA ABDUL
UBUNGO
DAR INDIAN OCEAN
SINZA
SINZA
KANDA YA KINONDONI
  1. UPENDO DICKSON
  2. ABELLA JOHN
  3. ELINEEMA CHAGULA
  4. IRENE NDIBALEMA
LINDI
MOROGORO
MOROGORO
MTWARA
KANDA YA MASHARIKI
  1. ANNA NITWA
  2. LISA MDOLO
  3. IRENE MASSAWE
DODOMA
SINGIDA
SINGIDA
KANDA YA KATI
  1. LAURA KWAY
IRINGA UNIVERSITY
KANDA YA ELIMU YA JUU
  1. ILUMINATHA DOMINIC
  2. MARIA PETER
  3. LUCY MICHAEL
GEITA
MWANZA
GEITA
KANDA YA ZIWA
  1. MOURINE  AYOUB
  2. GLORY STEPHANO
  3. ELGIVER MWASHA
  4. BAHATI MFINANGA
ARUSHA
KILIMANJARO
TANGA
MANYARA
KANDA YA KASKAZINI
  1. MOURINE KOMANYA
  2. ANITHA MLAY
  3. IRENE MSABAHA
  4. EUNICE ROBERT
IRINGA
IRINGA
RUVUMA
MBEYA
KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI 
  1. MWANTUMU ALLY
  2. ESTHER MNAHI
  3. ANITHA KISIMA
.
MBAGALA
KIGAMBONI
MBAGALA
KANDA YA TEMEKE

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waumini wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya katika Mkutano wa 47 wa jumuiya hiyo nchini unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, anayefuata ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry. Masauni katika hotuba yake aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. (PICHA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI).

Rais Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi akizungumza wakati katika Mkutano wa 47 wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry. Masauni ambaye aliiwakilisha Serikali katika Mkutano huo, katika hotuba yake aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho

Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry akitoa hotuba yake katika Mkutano huo wa 47 wa Jumuiya hiyo

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Rais Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi wakiwapungia waumini wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya (hawapo pichani) wakati walipokuwa wanawasili katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Masaunia ambaye alikuwa mgeni maalum katika mkutano huo wa 47 wa jumuiya hiyo nchini, aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Kulia ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akipokea zawadi ya vitabu vya dini kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry

Sehemu ya Waumini wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya nchini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
Nimeamua kukuonjesha kidogo...Naomba utumie dakika zako mbili tu kutazama "Filamu ya Nyama ya Ulimi"

Bongo Movie Shinyanga inakuletea filamu ya kusisimua,kutisha,kuhuzunisha,kufurahisha,kuonya na kuelimisha inaitwa “Nyama ya Ulimi”.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu ziara ya Makamu wa Rais wa Cuba Nchini, Mhe.Salvador Antonio Valdes Mesa anayetarajiwa kuwasili nchini kwa ziara ya siku tatu kuanzia tarehe 2 hadi 4 Septemba 2016.
Mhe. Waziri Mahiga akiendelea kuzungumza na Waandishi wa Habari kama wanavyoonekana pichani. =============================================

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ziara ya Makamu wa Rais wa Cuba nchini Tanzania
Makamu wa Rais wa Baraza la Taifa la Jamhuri ya Cuba, Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 02 Oktoba, 2016 kwa ziara rasmi ya siku tatu. Lengo la ziara hiyo ni kukuza na kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo baina ya Tanzania na Cuba pamoja na kuangalia maeneo mapya ya ushirikiano. Nchi nyingine anazotarajiwa kuzitembelea ni pamoja na Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Botswana na Zimbabwe.
Shughuli mbalimbali zitakazofanyika wakati wa ziara
Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Valdes Mesa atapokelewa na mwenyeji wake Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tarehe 03 Oktoba, 2016 Mhe. Mesa atakutana kwa mazungumzo ya faragha na Mhe. Samia Suluhu Ikulu yakifuatiwa na mazungumzo rasmi kati yao na wajumbe waliofuatana nao.
Aidha, Mhe. Mesa atakutana kwa mazungumzo mafupi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli.
Baada ya mazungumzo hayo, Mhe. Mesa na Mhe. Suluhu watakuwa na mkutano wa pamoja na Waandishi wa Habari kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba.
Katika hatua nyingine, Mhe. Mesa atakutana kwa mazungumzo mafupi na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Y. Ndugai katika Hoteli ya Hyatt Regency. Baadaye siku hiyo hiyo, atakutana na Ujumbe wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Hotelini hapo kabla ya kushiriki Chakula rasmi cha Mchana, Ikulu kilichoandaliwa kwa heshima yake na Mwenyeji wake Mhe. Suluhu.
Mhe. Mesa ataondoka Dar es Salaam tarehe 03 Oktoba, 2016 alasiri kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kuendelea na ziara yake Visiwani humo. Akiwa Zanzibar, Mhe. Mesa ambaye atapokelewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi atakutana kwa mazungumzo rasmi na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt.  Ali Mohamed Shein, Ikulu ya Zanzibar.
Tarehe 04 Oktoba, 2016 Mhe. Mesa akiwa ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba atarejea Dar es Salaam akitokea Zanzibar kwa ajili ya kuendelea na ziara yake ambapo atatembelea Makumbusho ya Taifa.
Uhusiano wa Tanzania na Cuba
Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Cuba ulianzishwa zaidi ya  miaka 50 iliyopita  na Viongozi Waasisi wa mataifa haya mawili, Rais Mstaafu wa Cuba, Mheshimiwa Fidel Castro na Baba wa Taifa, Hayati Julius K. Nyerere. Tangu Tanzania ipate uhuru Cuba imekuwa ikitusaidia katika maeneo mbalimbali ikiwemo afya, utamaduni, elimu, michezo, utalii, nishati, teknolojia na kilimo.
Ushirikiano katika Sekta ya Afya
Tanzania na Cuba zimekuwa zikishirikiana kwenye sekta ya afya ambapo hadi sasa kuna jumla ya Madaktari 30 kutoka Cuba wanaofanya kazi kwenye Hospitali mbalimbali Tanzania Bara na Zanzibar. Kati ya Madaktari hao 10 wapo Bara na 20 wapo Zanzibar wakiwemo wanaofundisha katika Kitivo cha Tiba, Chuo Kikuu cha Zanzibar na kutibu katika Hospitali mbalimbali Zanzibar.
Aidha, katika jitihada za Serikali za kupambana na malaria Serikali ya Cuba na Tanzania zilikubaliana kujenga Kiwanda cha Viuatilifu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu ambacho kimejengwa kwenye eneo la Viwanda Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani na kuzinduliwa mwezi Julai, 2015.
Kiwanda hicho ambacho kilijengwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Kampuni ya LABIOFAM ya Cuba kimekamilika na kwa sasa kinazalisha dawa za majaribio. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 6 za viuatilifu kwa mwaka ambazo zinatosheleza kwa matumizi ya Tanzania na hata kuuzwa nchi nyingine za Afrika.
Sekta ya Elimu
Katika Sekta ya Elimu Tanzania na Cuba zimekuwa zikishirikiana kwenye programu mbalimbali ikiwemo nafasi za ufadhili wa masomo nchini Cuba kwa wanafunzi kutoka Tanzania. Kuanzia mwaka 2008 hadi 2014 jumla ya Watanzania 64 walipata ufadhili wa mafunzo nchini Cuba katika fani mbalimbali ikiwemo udaktari, uchumi, TEHAMA na Michezo.
Pia Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Cuba ilianzisha Programu ya Elimu kwa Vijana na Watu Wazima ambayo hutolewa kwa kutumia vifaa vya kufundishia vinavyomwezesha mwanafunzi kusikia na kuona (audiovisual). Inatarajiwa kwamba zaidi ya vijana na watu wazima milioni 3 watakuwa wameshiriki programu hii ifikapo mwaka 2017. Mradi wa majaribio ya program hii ulizinduliwa mwaka 2014 katika Manispaa za Ilala, Temeke, Kinondoni, Ilemela, Mwanga, Bagamoyo, Mkuranga na Songea.
Sekta ya Michezo
Katika Sekta ya michezo Serikali ya Cuba wametupatia Wakufunzi wa Ngumi, Judo na Riadha. Hivi sasa wanatoa nafasi za mafunzo nne kila mwaka kwenye mafunzo ya michezo na utaalamu wa mazoezi ya viungo.
Hivyo, pamoja na kutumia fursa ya ziara hiyo kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili Tanzania itatumia nafasi hiyo kujikita katika kuanzisha ushirikiano kwenye maeneo mapya hususan biashara na uwekezaji.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 30 Septemba 2016.

Taasisi ya Demokrasia na Utawala bora nchini ADLG, imebainisha kwamba kukosekana kwa uwajibikaji miongoni mwa baadhi ya viongozi, kunasababisha maendeleo duni kwenye baadhi ya maeneo/vijiji yenye wawekezaji ikiwemo migodi.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jimmy Luhende, ameyasema hayo leo kwenye mdahalo wa kila mwezi unaoendeshwa na taasisi hiyo kujadili masuala mbalimbali yanayohusu rasilimali asilia ikiwemo madini, gesi na mafuta.

Amesema katika tafiti zilizofanywa na taasisi hiyo katika vijiji mbalimbali vinavyozungukwa na migodi katika mikoa ya kanda ya ziwa, wamebaini kukosekana kwa huduma muhimu za kijamii ikiwemo zahanati, shule, miundombinu bora ya barabara pamoja na maji safi na salama.
Amesema taasisi hiyo imeanzisha midahalo mbalimbali inayowahusisha wananchi pamoja na viongozi katika vijiji 147 vya mikoa minne ya kanda ya ziwa yenye uwekezaji wa madini ili kuwajengea uwezo wananchi kutumia uwekezaji ulio kwenye maeneo yao kurahishisha maendeleo.
Afisa Miradi (Sheria na Mikataba) kutoka taasisi ya ADLG, Carolina Tizeba, amesema katika tafiti zilizofanywa na taasisi hiyo kwenye Vijiji vinne vya Nyenze, Ikonongo, Songwa na Maganzo katika Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, umebaini kuwepo kwa ushiriki mdogo wa wananchi pamoja na uwajibikaji wa viongozi wao katika masuala ya uwekezaji wa madini jambo ambalo linasababisha kushindwa kufuatilia manufaa ya uwekezaji katika vijiji vyao na hivyo kuchangia kuwepo kwa huduma duni za kijamii katika vijiji hivyo ambavyo kuna wawekezaji wa madini.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jimmy Luhende, akizungumza jambo kwenye mdahalo huo uliofanyika Isamilo Jijini Mwanza.
Nicholaus Ngelea ambaye ni Afisa Miradi ADLD, akiwasilisha mada kwenye mdahalo huo uliofanyika Isamilo Jijini Mwanza.
Carolina Tizeba ambaye ni Afisa Miradi (Sheria na Mikataba) ADLG, akiwasilisha taarifa ya utafiti uliofanywa na taasisi hiyo kwenye vijiji vinavyozungukwa na migodi mkoani Shinyanga.
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Mshiriki akichangia mada
Mshiriki akichangia mada
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Washiriki wa mdahalo huo
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Bonyeza HAPA Kwa Mdahalo uliopita. Imeandaliwa na BMG.



Meya wa Manispaa ya Dodoma, Jafar Mwanyemba, (kushoto), akimkabidhi mfano wa funguo, Waziri Mkuu KassimMajaliwa, ikiwa niishara ya kumkaribisha Dodoma kama mkazi wa Manispaa hiyo, alipowasili kwenye makazi yake mjini humo Septemba 30, 2016.Waziri Mkuu ametimiza ahadi yake ya kuhamia Dodoma aliyoitoa bungeni ifikapo mwishoni mwa mwezihuu. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

 Waziri Mkuu akionyesha funguo hiyo yamfano baada ya kukabidhiwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa Dodoma  baada ya kukaribishwa kimira na wazee hao Septemba 30, 2016

Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akizawadiwa kimira  na wanawake wa Dodoma ikiwa ni ishara ya kumkaribisha karika Manispaa hiyo, Septemba 30, 2016
Viongozi wa Manispaa na wananchi wakishangilia ujio wa Waziri Mkuu
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokewa na Meya wa Manispaa ya Dodoma Jafar Mwanyemba na viongozi wengine wa mkoa huo 
Waziri Mkuu, Kasim Majliwa akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye makazi yake mjini Dodoma Septemba 30, 2016.
 Waziri Mkuu akiwapungia viongozi na wananchi wa mkoa wa Dodoma alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma leo Septemba 30, 3016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisalimiana na Madiwani wa Manispaa ya Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa na mkewe Mary wakiagana na watuimishi wa Makazi ya Waziri Mkuu ya Dar es salaam kabla ya kuondoka kuelekea Dodoma Septemba 30, 2016.

Baadhi ya Washiriki watakaowania Taji la Miss Tanzania 2016 wakiwa katika picha pamoja muda mfupi baada ya kuwasili kambini. Jumla ya Washiriki 30 kutoka kanda mbalimbali nchini wameingia Kambini leo Septemba 30, 2016 tayari kwa maandalizi ya Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi ujao.
Mrembo anaeshikilia Taji la Miss Tanzania kwa sasa, Lilian Kamazima akizungumza na Warembo alipokutana nao leo Septemba 30, 2016 kwenye Hoteli ya Regency, Jijini Dar es salaam. ambapo jumla ya Washiriki 30 wameingia kambini leo tayari kwa maandalizi ya Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi ujao.

Baadhi ya Washiriki wa Miss Tanzania 2016 wakimsikiliza kwa makini Mrembo anaeshikilia Taji la Miss Tanzania kwa sasa, Lilian Kamazim.
 Warembo wakifanyiwa Usaili na viongozi wa Miss Tanzania.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni tano kutoka kwa Mbunge wa Afrika ya Mashariki ShyroseBhanj ukiwa ni mchango wa waathiri wa tetemeko, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016.Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji , CharlesMwijage.(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)


 Waziri Mkuu akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Hajjat Amina Masenza kwa mchango wa wana Iringa
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi 18,681,000/= kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa, Hajjat Amina Masenza ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya sh. 415,800,000/= kutoka  Chama cha  Waagizaji wakubwa  wa mafuta nchini  (TAUMA ) ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni 50 kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Tasisi ya Aga khan nchini, Amin Kurji (kulia) ukiwa ni mchango kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 30, 2016. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Augustine Mahiga na wapili kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 80 kutoka kwa Balozi wa Pakistan nchini, Amir Khan  (wapili kushoto ukiwa ni mchango  kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani  Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye hoteli ya Kyatt Regency jijini Dar es salaam Septemba 30, 2016. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Augustine Mahiga na  kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.

Baadhi ya watu walioshiki katika tukio la kukabidhi  jumla ya shilingi 190  ukiwa ni mchngo wa   waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera kutoka kwa balozi wa Pakistan nchini Mhe. Amir Khan, Kaimu Balozi wa China Mhe. Gou Haodong na Taasisi ya Aga Khan wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza baada ya kupokea mchngo huo kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam Septemba 30, 2016

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya upatikanaji  wa tiketi za kieletroniki  kuelekea mechi ya Ligi kuu Tanzania Bara ya watani wa jadi  Yanga na Simba itakayochezwa kesho Oktoba Mosi leo ,2016 kushoto ni Meneja Mradi kutoka kampuni ya Selcom Tanzania Bw. Gallius Runyeta.



NA RAYMOND MUSHUMBUSI WHUS
Mashabiki wa soka nchini wameondolewa wasiwasi kuhusu upatikanaji wa tiketi kuelekea mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara kati ya watani wa Jadi Yanga na Simba na kuhakikishiwa kuwa mfumo wa upatikanaji tiketi uko vizuri na mpaka sasa tiketi zinaendelea kuuzwa katika maeneo mbalimbali.
Wasiwasi huo umetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu matumizi ya tiketi za kieletroniki kuelekea mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Yanga na Simba.
Waziri Nape amesema kuwa kuna kuna taarifa kutoka mitaani kuwa kuna uwezekano wa mfumo huu kutofanya kazi  katika mechi hii na malalamiko ya watu wengi  kulalamika kukosa tiketi za mchezo wa kesho.
“kwa kila anayetaka kwenda uwanjani kesho kadi zinapatikana nimewaagiza Selcom wahakikishe wanazungusha  magari  yao mtaani  kuangalia  mahali penye upungufu na  yawe na watu wenye kadi hizo aidha,  watu waongezwe kwenye vituo ambayo vina idadi kubwa ya wateja wanaohitaji kadi” Alisema Mhe Nnauye.
Aidha Waziri Nape Nnauye amewahakikishia watanzania kuwa atausimamia mfumo huu kikamilifu na kwa gharama yoyote na  atahakikisha  hautakuwa  na mapungufu na endapo  yatajotokeza yatashughulikiwa na wataalamu ili kuufanya mfumo huu kufanya kazi ipasavyo kama ulivyokusudiwa.
Kwa upande wake Meneja Mradi kutoka Selcom Tanzania Galius Runyeta  amefafanua kuwa mfumo huu uko wazi kabisa kwa wadau wote wanaohusika na mapato ya uwanjani na utakuwa  njia mbadala ya kudhibiti mapato yatokanayo na mechi.
“ Kwa mfumo huu hakuna njia ya mkato kila kitu kiko wazi na kwa kila dakika utaona mabadiliko ya idadi ya tiketi zinazonunuliwa na mpaka sasa zaidi ya tiketi 10,000 zimenunuliwa na zinazidi kununuliwa” Alisema Runyeta.
Kwa miaka mingi kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wadau wa soka nchini kuwepo kwa upotevu wa mapato katika mechi za ligi na kimataifa katika viwanja vya soka nchini kwa kuliona hilo Serikali iliamua kuanzisha mfumo utakaomaliza tatizo hilo na kukomesha mianya yote ya ulaji iliyokuwepo katika mfumo uliopita.

Meneja Mradi kutoka kampuni ya Selcom Tanzania Bw. Gallius Runyeta akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari
 Waandishi wa habari wakiendelea na kazi
Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini

TANESCO YAFANYA KIKAO CHA UJIRANI MWEMA NA VIONGOZI WA JAMII INAYOZUNGUKA VITUO VYA KUFUA UMEME WA GESI VYA KINYEREZI JIJINI DAR ES SALAAM


 Meneja wa Kituo cha kufua umeme kinyerezi I, Mhandisi Lucas Busunge, akifungua kikao cha ujirani mwema kati ya TANESCO, TPDC na viongozi wa jamii inayozunguka Vituo vya kufua umeme wa Gesi vya Kineterezi jijini Dar es Salaam Septemba 30, 2016.
 Mkuu wa Kitengo cha Usalama, TANESCO Makao makuu, Misana Gamba

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme nchini TANESCO na viongozi wa dini, vyombo vya dola na viongozi wa Serikali za Mitaa sita inayozungu vituo vya kufua umeme wa Gesi asili vya Kinyerezi jijini Dar es Salaam, wamekubaliana kuweka mikakati ya pamoja kuhakikisha jamii inashiriki katika ulinzi wa miundombinu ya umeme.
Makubaliano hayo yamefikiwa leo Septemba 30, 2016, kwenye kikao cha ujirani mwema kati ya TANESCO, TPDC, viongozi wa dini, viongozi wa serikali za mitaa na vyombo vya dola ili kujadili namna bora ya kulinda miundombinu ya umeme kwenye vituo hivyo.
“Umeme wa Gesi ni umeme salama kabisa, hata hivyo ni wajibu wetu kushirikiana pamoja kuhakikisha miundombinu ya umeme huu wa Gesi inatunzwa na kulindwa,”, Meneja wa Kituo cha Umeme Kinyerezi I, Mhandisi Lucas Busunge alianza kwa kusema wakati akiwakaribisha wajumbe kwenye kikao hicho.
Tumeona tuitane hapa leo ili tujadiliane pamoja namna bora ya kuhakikisha umeme huu utokanao na Gesi ambao Serikali imeiingia gharama kubwa, miundombinu yake inalindwa na nyinyi viongozi mnao wajibu mkubwa wa kuwafikishia ujumbe wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka mitambo hii. Alisema Mhandisi Busunge.
Akitoa mada juu ya Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa miundombinu ya umeme wa Gesi na hasara inayoweza kulikumba taifa na jamii kwa ujumla, Mkuu wa Usalama wa TANESCO makao makuu, Misana Gamba alisema, “Lazima tutambue kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa vituo hivi na fedha hizi ni za walipa kodi wa Tanzania, kwa hivyo ni wajibu wetu sote na sio TANESCO pekee kuhakikisha tunalinda miundombinu hii kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo,” alisema Gamba
Akifafanua zaidi, Mkuu huyo wa usalama alibainisha mambo ambayo jamii inapaswa kuelewa kuwa ni hatari dhidi ya miundombinu ya umeme ambayo ni pamoja na kuwasha moto, kulima au kuchimba mchanga, mmomonyoko wa udongo, wezi wa vyuma, uvuvi haramu, kujenga, kufanya biashara au kuendesha magari makubwa sehemu ambayo miundombinu hiyo ya umeme wa Gesi inapita.
Mkuu huyo wa usalama wa TANESCO alisema, hatari inayoweza kutokea endapo mambo hayo yatafanywa ni pamoja na kurudisha nyuma jiyihada za Serikali katika kuwaletea umeme wananchi, lakini pia hatari ya kulipuka kwa mitambo hiyo ambapo madhama makubwa yanaweza kuwakumba wananchi.
Akichangia kwenye mazungumzo hayo, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, ambaye ndiye alikuwa muendesha kikao, alisema, Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO, imekuwa ikitoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kutunza miundombinu ya umeme kwa faida ya Watanzania wote, na hatua ya kikao hicho ni mwendelezo wa utoaji elimu na kuwataka viongozi hao kuwa mabalozi katika maeneo yao, kwenye nyumba za ibada, ili kusudi wananchi wengi waelewe umuhimu wa kuunza miundombinu ya umeme ambayo kimsingi ni mali ya Watanzania wote.
Naye afisa mwandamizi wa usalama Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini, (TPDC), Elias Muganda, alitahadharisha juu ya shughuli za kiuchumi kwenye eneo linakopita bomba la Gesi na ksuema hiyo ni hatari. “Kwa sasa kuna mabomba mawili yenye Gesi tayari, ambayo yako umbali wa mita 2 kwenda chini, yakipata mgandamizo unaosababishwa na magari makubwa kupita juu yake inaweza kupelekea leakge na kusababisha Gesi kuvuja na matokeo yake kila mtu anayajua ni moto.” Alifafanua
Akatoalea mfano wa mabomba yaitwayo Carthodic Protection, ambayo huzuia kutu, lakini tayari kuna watu wanang’oa vyuma hivyo na hii inaweza kusababisha kutu na mabomba kutoboka,alitahadharisha, Muganda.
Wakichangia mazungumzo hayo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kanga, Shamte Mlanzi Mkali, alitoa wito kwa viongozi wenzake wa Mitaa, kila wanapokutana kwenye vikao, moja ya ajenda ya kuzungumza ni pamoja na usalama wa mitambo ya Gesi.
Hata hivyo viongozi wengi walionyesha umuhimu wa TANESCO kutoa ajira kwa vijana waishio maeneo ya jirani na mradi ili waweze kuona manufaa ya moja kwa moja ya ujio wa mradi huo.
Mambo yaliyoazimiwa kwenye kikao hicho ni pamoja na ulinzi wa miundombinu ya Gesi iwe ni moja ya ajenda za vikao vya Serikali za Mitaa, na iwe marufuku kwa mtu kupita au kukatiza eneo la Mitambo bila ya kibali maalum, uwepo utaratibu wa kuwaalika viongozi wa TANESCO/TPDC kwenye vikao vya Serikali za Mitaa kama itahitajika.
Maazimio mengine ya kikao hicho kilichomuhusisha pia Mkuu wa upelelezi wa Kituo cha Sitakishari-Ukonga,  SSP, Hassan Okello, ni pamoja na kampuni za ulinzi kwenye eneo la mitambo zijulikane kwa viongozi wa Serikali za mitaa yote inayozunguka eneo la mradi.
Mitaa iliyoshiriki kwenye kikao hicho ni pamona na Mtaa wa Kanga, Kibaga, Kinyerezi, Kichangani, na Kifura.

 Mhandisi Busunge
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji (aliyesimama), akizungumzia umuhimu wa viongozi wa mitaa kushirikiana na TANESCO katika kuelimisha umma, kutunza miundombinu ya umeme
 Afisa Usalama wa TANESCO makao makuu, Fidelis Almasi, akielezea namna viongozi wanavyoweza kushiriki katika kuelimisha wananchi umuhimu wa kutunza miundombinu ya umeme na athari za zitokanazo na uharibifu wa miundombinu hiyo kwa jamii na serikali
 Mkuu wa upelelezi, Kituo cha polisi Sitakishari-Ukonga, MrakibuMsaidizi wa Polisi, (ASP), Hassan Okello, akiwatoa hofu viongzoi hao kuhusu kutunza siri wanapotoa taarifa za wahalifu na uhalifu na kwamba yeye binafsi yuko tayari siku zote kuhakikisha usalama kwenye eneo hilo unazingatiwa
 Afisa Usalama Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini, (TPDC), Eliasi Muganda, amesema, mabomba mawili ya gesi tayari yana gesi na yako umbali wa kina cha mita 2 kutoka uso wa ardji na hivyo hayahitaji mgandamizo kutoka juu kwani ni hatari yanaeza kupata nyufa na kuvujisha Gesi

 Afisa Elimu wa Kata ya Kinyerezi, Mwalimu Mercy Mtei, (kulia), yeye amesema, atawashirikisha walimu na wanafunzi kueneza ujumbe kwenye jamii
 Sheikh Juma Swaleh wa Msikiti wa Othman Bin-Afan wa Kinyerezi
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kichangani, Niyukuli Leonard (kulia)
 Mchungaji Jacob Msami,  akizungumza
 Ustaadhi Ally akizungumza
 Mchungaji Ariel Mungereja wa Kanisa la EAGT, Kinyerezi
 Afisa Usalama wa Kituo cha Kinyerezi I, Furaha Munisi, akifafanua mambo mbalimbali ya kiusalama ambayo viongozi hao wanapaswa kuyachukua na kuwaelimisha wananchi
Picha ya pamoja baada ya kikao


 Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka akionesha tuzo ya kimataifa (UN) ya Maendeleo Endelevu ya Mwana Mfalme Khalifa Bin Salman Al Khalifa aliyotunukiwa hivi karibuni New York Marekani wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo.
 Profesa Anna Tibaijuka akionesha cheti alichokabidhiwa sanjari na tuzo hiyo.
 Profesa Tibaijuka akisisitiza jambo katika mkutano huo na wanahabari. Kulia ni Mratibu wa mkutano huo, Mussa Ally.
 wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale


MBUNGE wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka amekacha kuchukua dola 300,000 alizopewa baada ya kutunukiwa tuzo ya  Maendeleo Endelevu aliyopewa na Umoja wa Mataifa (UN), kutokana na sakata la fedha za Escrow Tegeta.



Tuzo hiyo aliipokea Septemba 23 mwaka huu New York Marekani ambayo mfadhili wa tuzo hiyo ni wa waziri mkuu wa Bahrain mwana mfalume Khalifa bin Al Khalifa.


Akizungumza jana Dar es Salaam Profesa Tibaijuka alisema kwa sasa umoja wa mataifa umeingia katika awamu ya pili ya maendeleo, ambao umekuja kupisha yale malengo 17 ya mileniam ambayo yote yeye alikuwepo, hivyo aliokuwa wanatoa tuzo walinona kwa namna alivyoshiriki kwa kiasi kikubwa.

"Tuzo hizi si za kuomba, ni watu wanakaa na kupendekeza mtu wa kupewa, na hii ni mara ya pili, mara ya kwanza   nilipewa mwaka 2009 nchini Swideni," alisema na kuongeza.

"Tuzo zinatoka kwa niaba ya jamii inayotoka au kuitumikia na kufanya nayo kazi, hivyo wamatambua mchango wangu katika kuwatumikia wananchi wa Muleba," alisema.

Aidha Profesa tibaijuka alitaja sababu zilizpokekea yeye kutochua dola 300,000 za Marekeni za tuzo hiyo.

"Sikuichukua kwa sababu ya yaliyonikuta hapo mapema, kulikuwa na uwezekano wa kuichukua lakini nikasema kwa hali halisi ya nyumbani, hatuna sheria ya kupokea tuzo, michango na zawadi kwa hiyo mimi nikaicha mezani wao wafanye wanayotaka," alisema na kuongeza. 

"Unapoona mtu kama mimi nafanya kazi nakwenda kuchafulia kwenye kitu ambacho siusiki nacho, sasa Unapoipokea hapa utaonekana kama umevunja maadili au umejinufaisha kwa kuwa ndio mambo ya kwetu, hivyo nikawaachia," alisema.

Aliongeza kwa sasa umeshapeleka mswada binafsi bungeni wa kuweka sheria ya michango ili vitu vya hiari kama hivi vinapokuja katika jamii visimamiwe na si kupotoshwa kisiasa.

"Kwa maana jambo hili halina kificho, yaani huwezi kumzungumzia Anna Tibaijuka bila kutaja suala la Escro, hayo hayakwepeki kwa sababu yalitengenezwa yakawa hivyo, mtu asiyehusika anavalishwa joho lisilo muhusu.

"Lakini kwa sababu jamii haina uwezo wa kuchimba chini, unabaki kuwa uongo na kushindwa kujua ukweli umesimama wapi, lakini wao (UN) wanajua hii ni propanda la sivyo nisingesimama hapa na tuzo," alisema.

Aliongeza licha ya yeye kuwa mstaafu wa umoja wa mataifa bado wanamfuatilia katika shughuli za kimaendeleo ambazo anazifanya akiwa ndani na nje ya nchi.

"Kama ukijikwaa, ukianguka na kusimama watu wanaangalia kulikoni, na huu ni utamaduni wao, kwa hiyo pale uongo na fitina havina nafasi," alisema kwa msisitizo wakati akizungumza na wanahabari.
Diwani wa Kata ya Karambi ambaye pia ni Mjumbe wa mkutano Mkuu wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),  Felix Bwahama ambaye aliongozana na  Profesa Tibaijuka alishukuru UN kwa kumtunuku tuzo hiyo ambapo alisema ni fahari kwa wanakagera na taifa kwa ujumla licha ya baadhi ya watu nchini kubeza kazi anazizifanya ambazo zinaonekana kimataifa.

 Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka akionesha tuzo ya kimataifa (UN) ya Maendeleo Endelevu ya Mwana Mfalme Khalifa Bin Salman Al Khalifa aliyotunukiwa hivi karibuni New York Marekani wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo.
 Profesa Anna Tibaijuka akionesha cheti alichokabidhiwa sanjari na tuzo hiyo.
 Profesa Tibaijuka akisisitiza jambo katika mkutano huo na wanahabari. Kulia ni Mratibu wa mkutano huo, Mussa Ally.
 wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale


MBUNGE wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka amekacha kuchukua dola 300,000 alizopewa baada ya kutunukiwa tuzo ya  Maendeleo Endelevu aliyopewa na Umoja wa Mataifa (UN), kutokana na sakata la fedha za Escrow Tegeta.



Tuzo hiyo aliipokea Septemba 23 mwaka huu New York Marekani ambayo mfadhili wa tuzo hiyo ni wa waziri mkuu wa Bahrain mwana mfalume Khalifa bin Al Khalifa.

Akizungumza jana Dar es Salaam Profesa Tibaijuka alisema kwa sasa umoja wa mataifa umeingia katika awamu ya pili ya maendeleo, ambao umekuja kupisha yale malengo 17 ya mileniam ambayo yote yeye alikuwepo, hivyo aliokuwa wanatoa tuzo walinona kwa namna alivyoshiriki kwa kiasi kikubwa.

"Tuzo hizi si za kuomba, ni watu wanakaa na kupendekeza mtu wa kupewa, na hii ni mara ya pili, mara ya kwanza   nilipewa mwaka 2009 nchini Swideni," alisema na kuongeza.

"Tuzo zinatoka kwa niaba ya jamii inayotoka au kuitumikia na kufanya nayo kazi, hivyo wamatambua mchango wangu katika kuwatumikia wananchi wa Muleba," alisema.

Aidha Profesa tibaijuka alitaja sababu zilizpokekea yeye kutochua dola 300,000 za Marekeni za tuzo hiyo.

"Sikuichukua kwa sababu ya yaliyonikuta hapo mapema, kulikuwa na uwezekano wa kuichukua lakini nikasema kwa hali halisi ya nyumbani, hatuna sheria ya kupokea tuzo, michango na zawadi kwa hiyo mimi nikaicha mezani wao wafanye wanayotaka," alisema na kuongeza. 

"Unapoona mtu kama mimi nafanya kazi nakwenda kuchafulia kwenye kitu ambacho siusiki nacho, sasa Unapoipokea hapa utaonekana kama umevunja maadili au umejinufaisha kwa kuwa ndio mambo ya kwetu, hivyo nikawaachia," alisema.

Aliongeza kwa sasa umeshapeleka mswada binafsi bungeni wa kuweka sheria ya michango ili vitu vya hiari kama hivi vinapokuja katika jamii visimamiwe na si kupotoshwa kisiasa.

"Kwa maana jambo hili halina kificho, yaani huwezi kumzungumzia Anna Tibaijuka bila kutaja suala la Escro, hayo hayakwepeki kwa sababu yalitengenezwa yakawa hivyo, mtu asiyehusika anavalishwa joho lisilo muhusu.

"Lakini kwa sababu jamii haina uwezo wa kuchimba chini, unabaki kuwa uongo na kushindwa kujua ukweli umesimama wapi, lakini wao (UN) wanajua hii ni propanda la sivyo nisingesimama hapa na tuzo," alisema.

Aliongeza licha ya yeye kuwa mstaafu wa umoja wa mataifa bado wanamfuatilia katika shughuli za kimaendeleo ambazo anazifanya akiwa ndani na nje ya nchi.

"Kama ukijikwaa, ukianguka na kusimama watu wanaangalia kulikoni, na huu ni utamaduni wao, kwa hiyo pale uongo na fitina havina nafasi," alisema kwa msisitizo wakati akizungumza na wanahabari.
Diwani wa Kata ya Karambi ambaye pia ni Mjumbe wa mkutano Mkuu wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),  Felix Bwahama ambaye aliongozana na  Profesa Tibaijuka alishukuru UN kwa kumtunuku tuzo hiyo ambapo alisema ni fahari kwa wanakagera na taifa kwa ujumla licha ya baadhi ya watu nchini kubeza kazi anazizifanya ambazo zinaonekana kimataifa.


Maafisa watatu wa serikali akiwa Afisa Tawala mkoa wa Kagera, (RAS), Amantius Msole, Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Kelvin Makonda, na meneja wa benki ya CRDB tawi la Bukoba wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mjiniBukoba leo Septemba 29, 2016wakikabiliwa na mashtaka ya kula njama kwa kufungua akaunti ya bandia inayofanana na ile inayotumika kukusanya fedha za waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo Septemba 10, 2016.

 RAS Amantius Msole (katikati), na watuhumiwa wenzake wakisindikizwa na maaskari kanzu kuelekea mahakamani leo
 Watuhumiwa wakiwa kwenyechumba chamahakama wakisubiri shauri lao
RAS Amantius Msole, (wakwanza kushoto), akijadiliana jambo na wakili wake


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, (kulia-katikati) akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2016




Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiongea mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2016. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. (PICHA NA IKULU)

No comments:

Post a Comment