KAMPUNI YA TTCL YAZINDUA KITUO KIPYA CHA HUDUMA KWA WATEJA UBUNGO PLAZA, DAR
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba (kushoto) akikata
keki maalum kuashiria uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja Ubungo
jijini Dar es Salaam leo. Kituo hicho kipya pamoja na duka la bidhaa za
kampuni ya TTCL kipo katika Jengo la Ubungo Plaza la jijini Dar es
Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja cha
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Ubungo leo jijini Dar es Salaam. Kituo hicho kipya pamoja na duka la bidhaa za kampuni ya TTCL kipo katika Jengo la Ubungo Plaza la jijini Dar es Salaam.
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Ubungo leo jijini Dar es Salaam. Kituo hicho kipya pamoja na duka la bidhaa za kampuni ya TTCL kipo katika Jengo la Ubungo Plaza la jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja TTCL, Leonard Lubu akizungumza na wanahabari mara baada ya uzinduzi.
MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGUA KONGAMANO LA 30 LA NIMR JIJINI DAR LEO
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan
akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya
Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), lililoanza leo Oktoba 4 na
kilelele chake kukoma Oktoba 6,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Washiriki kutoka sehemu mbalimbali ndani nje ya nchi wakisikiliza
hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia
Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa
ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), lililoanza leo Oktoba 4 na
kilelele chake kukoma Oktoba 6,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
Mkuu,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele
Malecela akizungumza mapema leo,alipokuwa akimkaribisha Makamu wa Rais
Mama Samia Suluhu Hassan,wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30
lililoanza leo Oktoba 4 na kilelele chake kukoma Oktoba 6,2016 katika
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es
Salaam.Katika kongamano hilo kauli mbiu yake ni “Uwekezaji katika tafiti
zenye ubunifu ili kufikia malengo endelevu ya dunia.
Dkt
Mwele alieleza pia Mada zitakazojadiliwa ndani ya kongamano hilo kuwa
zitajikita zaid kwenye maeneo kama vile 1. Mkakati wa kuboresha afya ya
uzazi, ya mama, watoto wachanga na vijana. 2. Magonjwa sugu
yasiyoambukiza na changamoto zake,3. Kuendeleza mafanikio yaliyopatikana
katika mapambano dhidi ya UKIMWI, kifua kikuu na malaria,4. Usalama wa
Maji, Usafi wa mazingira na usafi binafsi,5. Mkakati wa afya moja katika
kudhibiti magonjwa ya milipuko,pamoja na 6. Magonjwa ya kitropiki
yasiyopewa kipaumbele
RAIS DKT MAGUFULI NA RAIS KABILA WA DRC WASHUHUDIA KUSAINIWA KWA MOU YA USHIRIKIANO NA KUONGEA NA WANANCHI KUPITIA VYOMBO VYA HABARI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ujumbe wake wakitoka katika
mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe Joseph
kabila na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016
Mawaziri
wa Nishati wa Tanzania na DRC wakitia saini mkataba wa makubaliano ya
pamoja (MOU) wa utafutaji na uendelezaji wa mafuta katika eneo la
upande wa magharibi mwa afrika Mashariki hususan katika ziwa Tanganyika
Mawaziri
wa Nishati wa Tanzania na DRC wakibadilishana nyaraka baada ya kutia
saini mkataba wa makubaliano ya pamoja (MOU) wa utafutaji na
uendelezaji wa mafuta katika eneo la upande wa magharibi mwa afrika
Mashariki hususan katika ziwa Tanganyika
Rais
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe Joseph kabila akiongea
na wanahabari Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016
BALOZI SEIF AKUTANA NA VIONGOZI WA UMOJA WA VIJANA WA CCM ZANZIBAR
Naibu
Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi {UVCCM } Tanzania
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi wa Umoja wa Vijana
wa CCM Zanzibar uliofika kumkabidhi hati maalum ya heshima kwa
kuuongoza vyema umoja huo.
Wa
kwanza kulia ya Balozi Seif ni Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM
Zanzibar Nd. Abdulgharaf Idriss Juma na kushoto ya Balozi Seif wa
kwanza ni Mkuu wa Utawala wa Umoja huo Nd.Salum Simai Tale.
Kaimu
Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Nd. Abdulgharaf Idriss Juma kushoto
akimkabidhi Naibu Kamanda wa {UVCCM } Tanzania Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi hati maalum ya heshima kwa kuuongoza vyema umoja huo.
Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ.Naibu Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi {UVCCM } Tanzania Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwaasa vijana wa Umoja huo ambao ndio muhimili wa CCM kuhakikisha kwamba Viongozi watakaopatikana kwenye uchaguzi ujao wa Chama hicho wanakuwa na uwezo unaokubalika na wanachama watakaowaongoza.
Alisema Tabia ya kuchagua viongozi kwa kutumia vigezo vya nasaba, urafiki au uwezo wa kifedha huzua balaa na malalamiko ya wanachama ndani ya kipindi kifupi baada ya uchaguzi huo na hatimae kupunguza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Ilani na Sera za Chama hicho.
Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM alitoa nasaha hizo wakati akizungumza na Uongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar ukiongozwa na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Nd. Abdulgharaf Idriss Juma mara baada ya kupokea Hati Maalum ya Heshima kwa kuwa mlezi mwema wa Jumuiya hiyo kikao kilichofanyika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Alisema Chama cha Mapinduzi kimechoshwa na tabia za baadhi ya wanachama wake wanaojenga tamaa ya kujipenyeza ndani ya fursa za Uongozi wanazoomba kwenye nafasi mbali mbali jambo ambalo baadaye huleta usumbufu na maudhi kwa wale waliowachagua ili wawatumikie.
Balozi Seif alitahadharisha kwamba wanachama wa Chama cha Mapinduzi wanapaswa kuwa makini kuwapima wale wote wanaoomba nafasi za Uongozi kwa vigezo vya kuangalia Historia ya kila anayeomba nafasi hizo.
No comments:
Post a Comment