Pages

Sunday, October 30, 2016

PROFESA NDALICHAKO AFUNGA KAMBI YA KUFYATUA MATOFALI KATIKA SHULE YA SEKONDARI NASSIBUGAN

ndal1
Waziri wa elimu, sayansi Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiwa na chepe ya mchanga katika ufyatuaji watofali katika Shule ya Sekondari  ya Wavulana Nassibugani kabla ya kufunga kambi ya ufyatuaji tofali, Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, kulia ni Mbunge wa Mkurang Abdallah Ulega.
ndal2
Waziri wa elimu, sayansi Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiwa ameshika kibao chenye tofali pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo kabla  ya kufunga kambi ya ufyatuaji tofali katika katika shule ya Sekondari Wavulana  Nassibugani.
ndal3
Waziri wa elimu, sayansi Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wazaledo wa vyuo vya ndani na nje ya nchi  pamoja na viongozi mbalimbali baada ya kufunga kambi ya ufyatuaji tofali iliyodumu mwezi mmoja.
……………………………………………………………….
Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii
Waziri wa elimu, sayansi Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema wananchi wa Mkuranga wamejitoa katika kupata Mandeleo.
Profesa Joyce Ndalichako ameyasema hayo wakati wa kufunga kambi ya kufyatua tofali zaidi  ya 45000 kwa ajili ujenzi wa Mabweni Matano na Nyumba tano za walimu katika shule ya sekondari Nassibugani iliyopo kata ya Msonga Wilaya Mkuranga.
Profesa Joyce amesema  kuwa wananchi wamejitoa kuhakikisha watoto wanapata elimu bora inayoendana na mazingira.
Amesema kuwa nia yake nikuona Mkuranga inakuwa na  Mapinduzi ya Elimu.
Amesema vijana 53 wazalendo kutoka vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi wameamua kuunga mkono jitihada  za serikali  katika suala la elimu kupewa kiupaumbele katika kusaidia maendeleo ya Taifa.
Amesema ujenzi wa mabweni hayo itakuwa suluhu kwa wavulana kufanya vizuri kutokana kupunguziwa umbali wa kufika shule.
 Profesa Ndalichako, amesena jitihada zinaendelea kutatua baadhi ya changamoto za elimu kwa kushirikiana na wananchi.
Katika ufungaji wa kambi hiyo Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema nia yake ni kuona maendeleo yanapatikana yenye tija.
Waliohudhuria ufungaji ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, Mkuu wa Wilaya, Filberto Sanga na viongozi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment