Pages

Wednesday, September 28, 2016

WAZIRI MKUU MSTAAFU WA ISRAELI SHIMON PERES AFARIKI DUNIA, KUZIKWA IJUMAA SEPTEMBA 30, 2016

NA MASHIRIKA YA HABARIWAZIRI Mkuu wa zamani na Rais mstaafu wa Israeli, Shimon Peres, (pichani), amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 93.
Peres alipatwa na kiharusi Wiki mbili zilizopita na alipata nafuu kabla ya hali yake kubadilika ghafla Jumanne Septemba 27, 2016.
Mwanaye Chemi, alimuelezea baba yake kuwa, Peres ni miongoni mwa waanzilishi wa taifa la Israeli ambaye alifanya kazi bila kuchoka
Peres ambaye alipata kuwa Waziri Mkuu wa Israeli mara mbili, na mara moja kuwa Rais wan chi hiyo, ameelezewa na viongozi wa Dunia kuwa taifa la Israeli litakosa ushauzi wa hekima kutoka kwa kiongozi huyo.
Peres anatarajiwa kuzikwa Ijumaa Septemba 30, 2016 mjini Jerusalem na viongozi maarufu Duniani wanatarajiwa kuhudhuria mazishi yake akiwemo Rais Barack Obama wa Marekani, Prince Charles wa Uingereza na Papa Framcis wa Vatican.
Shimon Peres alikuwa mmoja kati ya viongozi wa mwisho wa kizazi cha wanasiasa wa Israeli waliokuwepo katika taifa hilo lililozaliwa mwaka 1948.
Alishinda tuzoya amani ya Nobeli mnamo mwaka 1994 kutokana na mchango wake katika mkataba wa amani wa Oslo kati ya Israeli na Palestina mwaka mmoja kabla, tuzo ambayo walishirikiana na Waziri Mkuu wa wakati huo, Yitzhak Rabin, ambaye baadaye aliuawa kwa kupigwa risasi na kijana wa Kiyahudi Yigal Amin.
Kuna wakati aliwahi kusema, “Wapelestina ni majirani wa karibu na Israeli na ipo siku watakuwa marafiki wa karibu wa Israeli.”
Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponI AMIN



 Peres (katikati), akiwa na marehemuYassar Arafat, (kushoto), aliyewahi kuwa kiongozi wa Mamlakaya Palestina, Marehemu Yitzhak Rabi, (aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Israeli, kabla ya kuawa, wakionyesha mikataba ya amani baina ya Wapelistina na Waisraeli
 Prese, akiwa na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair
 Peres akiwa na mkewe Sonia wakati wa uhai wao
 Peres akiwa na Waziri Mkuu wa Sasa, Benjamin Bibi Netanyahu
Peres akiwa na Bill C,linto, wakati huo Rais wa Marekani

No comments:

Post a Comment