Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (kushoto) wakipata maelezo kutoka
kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama kuhusu ujenzi wa makazi mapya ya
Waziri Mkuu, kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia kwake ) wakikagua ujenzi wa
makazi mapya ya Waziri Mkuu kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma
Septemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU AKIWA BUNGENI MJINI DODOMA LEO
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Iringa Mjini,
Mchungaji Peter Msigwa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 7,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless
Lema kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 7, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Isimani na Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kwenye viwanja vya
Bunge mjini Dodoma Septemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa
Anna Tibaijuka kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Septemba 7,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumsalimia aliposimama
Nangurukuru, wilaya ya Kilwa mkoani Lindi wakati akiwa njiani kuelekea
mkoa wa Mtwara ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku nne.
Sehemu ya Wakazi wa Nangurukuru mkoani Lindi wakishangilia ujio wa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumsalimia alipowasili
kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambapo atakuwa na ziara ya kikazi
ya siku nne.
..........................................................
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali
itatuma kikosi maalum cha kukabiliana na uvuvi haramu unaoendelea katika bahari
ili kudhibiti na tatizo hilo ambalo limeathiri sana mazalia ya samaki na
kuchangia kupungua kwa samaki baharini.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 7-Sept-2016
wakati akisalimiana na wananchi wa Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi ambao
walijitokeza kumsalimia wakati akielekea mkoani Mtwara katika ziara yake ya
kikazi ya siku NNE mkoani huo.
Makamu wa
Rais amesema katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika vizuri serikali pia
itatuma wataalamu wa mazingira ambao watafanya tathmini ya uharibifu wa
mazingira katika bahari ili kujua uharibifu uliofanyika na kuchukua hatua ya
kukabiliana na hali hiyo.
Ameeleza
kuwa serikali itachukua hatua hizo ili kuinusuru bahari kwa sababu imekuwa ni
chanzo kizuri ya mapato kwa wananchi kutokana na shughuli za uvuvi na shughuli
nyingine zikiwemo za utalii.
“Bahari yetu ndio
mapato yetu, bahari yetu ndio maisha yetu
tumeitumia vibaya mapato yamepungua na maisha hayawi mazuri hivyo ni
muhimu tuitunze ili iendelee kutulea kwa manufaa mazuri.”
Kuhusu
uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Kilwa, Makamu wa Rais Samia Suluhu
Hassan amesema serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti zinazolenga
kuhakikisha wananchi wote nchini wanapata huduma bora za afya katika ngazi
zote.
Amesema
mpango huo wa uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi nchini utaenda pamoja
na utoaji wa elimu bora wa wanafunzi kote nchini chini ya mkakati wa serikali
wa kutoa elimu bure kuanzia wanafunzi darasa
la kwanza hadi kidato cha nne.
Katika ziara
yake mkoani Mtwara, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suluhu Hassan kesho 8-Sep-16 atazindua
jengo la ofisi za Tume ya Maadili ya
Uongozi wa Umma Kanda ya Kusini na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo
mkoani humo.
Makamu wa
Rais tayari amewasili mkoani Mtwara na kupokelewa na Viongozi mbalimbali wa
mkoa huo wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego pamoja na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angela
Kairuki.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akizungumza na Balozi mpya wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Bibi,Monica Patricio mara alipofika Ikulu Mjini
Zanzibar kujitambulisha leo Septemba 7, 2016. (PICHA NA IKULU YA ZANZIBAR)
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)
akizungumza na Balozi mpya wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Bibi,Monica Patricio (wa pili kulia) akiwa na ujumbe aliofuatana
nao mara walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)
akisalimiana na Bibi,Monica Patricio Balozi mpya wa Msumbiji katika Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha kwa Rais
leo,(katikati) Balozi Mdogo wa Msumbiji anyefanyia kazi zake Zanzibae Bw. Jorge
Augusto Menezes
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiweka jiwe la msingi la funguzi wa hotel ya Ramada Encore
yenye hadhi ya nyota 5 jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli hiyo Bw. Abdul Ismail.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akihutubia wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa hoteli ya Ramada Encore iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan (kulia)akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli Ramada
Encore Bw. Abdul Ismail wakati wa halfa fupi wa uzinduzi wa Hotel ya
Ramada Encore jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua hoteli
ya nyota 5 ya Ramada Encore katikati ya jiji la Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment