Rais Dkt. John
Magufuli akikagua eneo la Gati la Mafuta la Kurasini KOJ, wakati alipofanya
ziara kwenye bandari ya Dar es Salaam, Septemba 26, 2016. (PICHA NA IKULU)
Rais Dkt. John
Magufuli akikagua utendaji kazi na vitendea kazi vya bandari katika eneo la
ofisi ya mtambo wa kuhakiki mizigo katika eneo la Bandari jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John
Magufuli akikagua utendaji kazi na vitendea kazi vya bandari katika eneo la
ofisi ya mtambo wa kuhakiki mizigo katika eneo la Bandari jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John
Magufuli akitoa maelekezo kwa Mhandisi Marry Mhayaya katika eneo la Gati la
Mafuta la Kurasini KOJ.
Rais Dkt. John
Magufuli akisisitiza jambo wakati akielekea eneo la Gati la upakuaji wa mafuta
la kurasini KOJ katika Bandari ya Dar es
Salaam.
Kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo
Kidata akitoa maelezo kuhusu utendaji kazi wa Taasisi yake inavyofanyakazi
Bandarini huku Rais Dkt. Magufuli akimsikiliza.
Rais akiongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Mhandisi Deusdedit
Kakoko
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja Katibu Mkuu wa Sekta ya
Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho wakitaza utendaji kazi wa mashine mbalimbali
katika Bandari ya Dar es Salaam.
Rais Dkt. John
Magufuli akisisitiza jambo mara baada ya kukagua eneo la upakuaji wa mizigo
mbalimbali katika eneo la Bandari jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John
Magufuli akisisitiza jambo mara baada ya kukagua eneo la upakuaji wa mizigo
mbalimbali katika eneo la Bandari jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekeza jambo wakati
akikagua mtambo wa kukagulia mizigo ulioharibika
kwa muda mrefu.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao (kushoto)
akimkambidhi mmojawapo wa washindi wa mashindano ya sauti, Hilda
Malecela mfano wa runinga ya kisasa yenye ukubwa wa inchi 40 kutoka
kampuni hiyo. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia
fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes
yaliyopo jijini Beijing, China.
Mmoja wapo wa washindi wa sindano la vipaji vya sauti, Hilda Malecela
akikumbatiana na majaji baada ya shindano ilo kuisha, akishuhudia tukio
hilo kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao
na kulia ni majaji na washindi wengine. Washindi 10 walipatikana katika
shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za
makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
Spika
wa Bunge Mhe Job Ndugai akiwasili Mjini Zanzibar kwa kutumia Boti
wakati alipofanya ziara ya kutembelea Baraza la Wawakilishi mapema leo
Septemba 2016.
Spika
wa Bunge Mhe Job Ndugai akisalimiana na Spika wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid (katikati) alipowasili
katika Ofisi za Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Kushoto ni Naibu Spika
wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan Juma.
Spika
wa Bunge Mhe Job Ndugai (kulia) akizungumza na Spika wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid (katikati) na Naibu Spika wa
Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan Juma wakati alipowatembelea.
Spika
wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa tatu toka kulia) akifuatilia kikao cha
Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati alipowatembelea. Wapili kulia ni
Spika wa Baraza hilo Mhe Zuberi Ali Maulid na wa kwanza kulia ni Naibu
Spika wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan Juma.
Rais
wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kulia) akipanda ngazi ya moja ya nyumba zinazojengwa na Kampuni ya
Ujenzi ya Azam Group akifuatana na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Bw.Said
Salim Bakhresa wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za
kisasa huko Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi leo
alipofanya ziara maalum kuangalia ujenzi wa nyumba hizo,[Picha
Ikulu.]26/09/2016.
RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM LEO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea
bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 akiwa ameongozana na
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu
Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoka
kuangalia sehemu ya kupakulia mafuta kutoka kwenye meli katika bandari
ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu
Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
ZIARA YA MAJALIWA KIBITI NA KILWA
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiingia kwenye uwanja wa michezo
wa Kibiti wilayani Kilwa ambapo Waziri Mkuu alihutubia mkutano wa
hadhara , Septemba 26, 2016. . Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Pwani
Mhandisi Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea magodoro 10 kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha
Mendeleo ya Wananchi cha Kibiti, Bi. Cecilia Mfuko ukukiwa ni mchango
uliotolewa na Chuo hicho kwa Hospitali ya Kibiti. Makabidhiano hayo
yalifanyika kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye
uwanja wa michezo mjini Kibiti Septemba 26, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akimshukuru Mzee Abadallah Ngwele baada ya
kupokea madawati 10 yaliyotolewa na wazee wa Kibiti katika mkutano wa
hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa michezo wa Kibiti, Septemba 26,
2016. Kushoto ni mkewe Mary na watatu kulia ni Mkuu wa mkoa wa Pwani,
Mhandisi Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MASAUNI AZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI, KITAIFA MJINI GEITA LEO
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akitoa
hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama
Barabarani alioizindua Kitaifa mjini Geita leo. Kauli mbiu ya
Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki Ajali, Tunataka Kuishi”. Katika
hotuba yake, Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS)
kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva
wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za
kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni
(kulia), akimsikiliza Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka
Makao Makuu, Koplo Faustina Ndunguru wakati alipokuwa anatoa maelezo
jinsi magari mbalimbali yanavyovunja sheria za barabarani. Katika hotuba
yake ya ufunguzi wa maonyesho hayo yanayofanyika Kitaifa mjini Geita,
Mhandisi Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS)
kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva
wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za
kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia)
akiyaangalia maandamano ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo
yanafanyika Kitaifa katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita,
yalipokuwa yanaingia katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuadhimisha wiki
hiyo. Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa
matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote
nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za
kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
IRAN YAAHIDI KUENDELEA KUTOA FURSA ZAIDI YA MAFUNZO YA ELIMU YA JUU KWA WANAFUNZI WA ZANZIBAR
Mkurugenzi Mkuu kutoka Idara ya
Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Jamuhuri ya Kiislamu ya
Iran Balozi Hussein Mollale Abdullahi akizungumza na Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Jengo la Baraza la
Wawakilishi lilipo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Picha na –
OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akipokea zawadi kutoka
kwa Mkurugenzi Mkuu kutoka Idara ya Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nchi
za Nje ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Balozi Hussein Mollale mara
baada ya mazungumzo yao. Wa kwanza kutoka Kulia ni Katibu wa kwanza
Msaidizi wa Ubalozi wa Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Mjini Dar es
salaam bwana Mohammad Dehghani.
Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran
imeahidi kuendelea kutoa fursa zaidi ya Mafunzo ya Elimu ya juu kwa
wanafunzi wa Zanzibar katika mpango wake wa kuimarisha uhusiano
uliopo kati yake na Zanzibar uliodumu kwa muda mrefu sasa.
Fursa hizo zitazingatiwa zaidi
katika fani ya Uhandisi kwa vile Visiwa vya Zanzibar tayari viko
katika maandalizi ya utafiti wa mafuta na gesi ikijiandaa kuelekea
katika uimarishaji wa Sekta ya nishati itakayosaidia kubadilisha
uchumi wa Zanzibar katika miaka michache ijayo.
Mkurugenzi Mkuu kutoka Idara ya
Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Jamuhuri ya Kiislamu ya
Iran Balozi Hussein Mollale Abdullahi alieleza hayo wakati
akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi Ofisini kwake Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa
Zanzibar.
Balozi Hussein alisema Iran kwa vile
imebarikiwa kuwa na rasilmali nyingi zilizopelekea kuongoza nafasi ya
Pili katika uzalishaji wa mafuta na Gesi Duniani imejitolea kuunga
mkono Mataifa Rafiki katika azma ya Mataifa hayo kujenga uwezo zaidi
wa kujitegemea.
Akizungumzia miradi ya kujitegemea
Balozi Hussein alisema Taifa lake lilioko Mashariki ya Kati tarayi
limeshatoa msaada mkubwa wa Vifaa na mashine kwa ajili ya chuo cha
Amali kiliopo Mkokotoni ili kuwajengea uwezo vijana wanaopata mafunzo
ya ujasiri amali kwenye chuo hicho.
MAFUNZO KUHUSU MWONGOZO WA USIMAMIZI WA UWEKEZAJI WA MIRADI YA UMMA KANDA YA MOROGORO YAFUMGULIWA RASMI
Mgeni
Rasmi, Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi
Jumla, Tume ya Mipango, akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya
siku tano kuhusu Usimamizi wa Uwekezaji wa Miradi ya Umma Kanda ya
Morogoro kwa Maofisa na Watendaji wa Idara za Sera na Mipango. Waliokaa
ni Bi. Anna Kimwela, Mchumi, Tume ya Mipango na Dr. Jehovaness Aikaeli,
Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam. Washiriki
wa Mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Miradi ya Umma
ambao ni Maofisa na Watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka Kanda
ya Morogoro wakimsikiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa
ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika katika Ukumbi wa Mkutano katika
Chuo Kikuu cha Kilimo Morogroro (SUA).
WAZIRI MKUU AMPA OFISA ELIMU WIKI MOJA KUPELEKA WALIMU RUFIJI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa
wiki moja kwa Afisa Elimu Mkoa wa Pwani, Yussuph Kipengele kupeleka
walimu wa kufundisha masomo ya kidato cha tano na sita katika shule
za sekondari za Mkongo na Utete wilayani Rufiji.
Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu,
Septemba 26, 2016) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Jumba la Maendeleo wilayani
Rufiji.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada
ya Mbunge wa Rufiji, Muhammed Mchengelwa kumwambia kuwa wilaya hiyo
inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu wa kidato cha tano na
sita licha ya kuwa na shule.
"Hatuwezi kuwa na shule ambazo
hazina walimu, nasikia hapa anayefundisha ni Mkuu wa shule na mwalimu
mmoja tu, wakati kule Kibaha kuna walimu walmerundikana ,sasa fanya
realocation tarehe 4,Oktoba uniletee taarifa walimu wamefika
Rufiji.",alisema Waziri Mkuu.
Akizungumzia suala la upungufu wa
watumishi wa umma kwenye sekta mbalimbali, Waziri Mkuu alisema baada
ya kazi ya uhakiki watumishi hewa itakapokamilika, serikali
itaangalia kwenye maeneo yenye upungufu na hivyo kutangaza ajira.
"Hivi sasa serikali
inakamilisha masuala ya uhakiki wa watumishi, tukimakamilisha na
kujua idadi ya watumishi na maeneo yenye upungufu tutaanza tena
kuajiri, tulisitisha kupisha kwanza kazi hii,alisema Waziri Majaliwa.
Kuhusu migogoro ya wakulima na
wafugaji Waziri, Mkuu alisema watendaji wa halmashauri na vijiji
wanapaswa kutenga maeneo ya wafugaji na wakulima na kutaka mifugo
isiongezwe kwenye maeneo ambayo hayajaruhusiwa.
Alisema wenyeviti wa vijiji
wanapaswa kusimamia utekelezaji wake katika mpango wa matumizi bora
ya ardhi na kwamba atakayeruhusu idadi kubwa ya mifugo kuingia
kijijini zaidi ya ile iliyokubalika atawajibishwa ikiwemo kufukuzwa
kazi na hatua nyingine za kisheria.
"Hatuwezi kuendelea kuwa na
watumishi wasio na nidhamu, wale wote watakaoingia mifugo zaidi ya
uwezo wa kijiji wafukuzwe kazi na kuchukuliwa hatua, lakini pia
wafugaji ni marufuko kuingiza mifugo kwenye mazao ya wakulima"alisema
Waziri Mkuu.
WATANZANIA 10 KWENDA KUFANYA KAZI STARTIMES NCHINI CHINA
washindi
10 wa shindano la vipaji vya sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa
kushirikiana na ubalozi wa China Tanzania wakiwa mbele ya jukwaa baada
ya kutangazwa washindi. Washindi hao 10 walipatikana katika shindano
hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao
makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
SPIKA NDUGAI ATEMBELEA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR
RAIS DK.SHEIN ATEMBELEA MRADI UJENZI WA NYUMBA ZA KISASA FUMBA
Rais
wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said
Salim Bakhresa alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko
Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara
maalum kuangalia ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa na Kampuni ya Azam
Group,(kulia ) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu Nd,Ayoub Mohamed
Mahmoud,[Picha na Ikulu.]26/09/2016.
Rais
wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(wa pili kushoto) akifuatana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group
Bw.Said Salim Bakhresa (kushoto) pamoja na Viongozi mbali mbali wa
Serikali wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko
Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara
maalum kuangalia ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa na Kampuni ya Azam
Group,(wa tatu kushoto) Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar
(ZIPA) Salum Nassor Khamis,akifuatiwa na Waziri wa Fedha na Mipango
Dkt.Khalid Salum Mohamed,[Picha Ikulu.]26/09/2016.
TIGO FIESTA YAITIKISA MKOA WA KILIMANJARO
CHINA DONATES US$200, 000 TO EAC FOR INTER-BURUNDI DIALOGUE
Mr.
Gou Haodong, Minister-Counsellor at the Chinese Embassy in Dar es
Salaam, with the Director of Infrastructure at the EAC Secretariat, Mr.
Philip Wambugu. On the left is the Dr. James Njagu, the Chef de Cabinet
to the EAC Secretary General.
Mr.
Gou Haodong, Minister-Counsellor at the Chinese Embassy in Dar es
Salaam, with the Director of Infrastructure at the EAC Secretariat, Mr.
Philip Wambugu, sign an agreement under which China is to give the EAC
$200,000 to support the Burundi peace process. Looking on (standing) is
Mr. Xia Riu Jiu, First Counsellor at the Chinese Embassy, and Dr. James
Njagu, the CdC to the EAC Secretary General (seated left).
The People’s Republic of China has donated US$200,000 to the East African Community Secretariat as part of support to the ongoing Inter-Burundi Dialogue.
Making the announcement at the EAC Headquarters in Arusha, Mr. Gou Haodong, the Minister-Counsellor at the Chinese Embassy in Dar es Salaam, Tanzania General reaffirmed China’s commitment to the success of the Burundi peace process.
Mr. Haodong hailed the EAC for playing a leading role in facilitating the talks, adding that China would continue to support the talks until Burundi realized a genuine and lasting peace.
Mr. Philip Wambugu, the Director of Infrastructure at the Secretariat, who received the donation on behalf of the EAC Secretary General, thanked China for its generous contributions which he said have kept the talks going.
Mr. Wambugu said the Summit had at its 17th Extra-Ordinary Meeting held in State House Dar es Salaam on 8th September, 2016 directed the EAC Secretariat to continue mobilizing resources for the purpose of supporting the peace talks.
Also present at the talks were First Secretary at the Chinese Embassy, Mr. Xia Riu Jiu, and Dr. James Njagu, the Chef de Cabinet to the Secretary General.
The People’s Republic of China has donated US$200,000 to the East African Community Secretariat as part of support to the ongoing Inter-Burundi Dialogue.
Making the announcement at the EAC Headquarters in Arusha, Mr. Gou Haodong, the Minister-Counsellor at the Chinese Embassy in Dar es Salaam, Tanzania General reaffirmed China’s commitment to the success of the Burundi peace process.
Mr. Haodong hailed the EAC for playing a leading role in facilitating the talks, adding that China would continue to support the talks until Burundi realized a genuine and lasting peace.
Mr. Philip Wambugu, the Director of Infrastructure at the Secretariat, who received the donation on behalf of the EAC Secretary General, thanked China for its generous contributions which he said have kept the talks going.
Mr. Wambugu said the Summit had at its 17th Extra-Ordinary Meeting held in State House Dar es Salaam on 8th September, 2016 directed the EAC Secretariat to continue mobilizing resources for the purpose of supporting the peace talks.
Also present at the talks were First Secretary at the Chinese Embassy, Mr. Xia Riu Jiu, and Dr. James Njagu, the Chef de Cabinet to the Secretary General.
PANYA ROAD' WAIBUKA UPYA NA KUTESA WANANCHI MOSHI BAA JIJINI DAR ES SALAAM
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar. Simon Sirro |
Na Dotto Mwaibale
KUNDI la uhalifu la watoto wenye umri
kuanzia miaka 18 hadi 25 maarufu kama panya road linatishia usalama wa
wananchi na mali zao maeneo ya Moshi Baa na vitongoji vingine katika
Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Kufuatia kukithiri kwa vitendo hivyo
katika kipindi kisichopungua wiki mbili tayari watoto watatu walikuwa
wakidaiwa kuhusika na kundi hilo wameuawa na wananchi wenye hasira kali.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi
Dar es Salaa leo hii mkazi wa eneo la Moshi Baa Relini aliyejitambulisha
kwa jina la Mwarami Abubakar alisema hali sio shwari katika eneo
kufuatia matukio ya kila siku ya kuvamiwa wananchi kujeruhiwa na kuporwa
mali zao na kundi hilo.
"Tayari vijana wawili wiki iliyopita
wamechomwa moto na wananchi wenye hasira huku mwingine akipigwa juzi
hadi kutolewa utumbo na kufariki papo hapo" alisema Abubakar.
Mkazi mwingine wa eneo la Kwa Mkolemba
Khamisi Fadhil alisema kundi hilo limekuwa likifanya vitendo hivyo
mchana kweupe na wanatembea kuanzia vijana nane hadi 10 wakiwa na silaha
za jadi kama nondo, visu na mapanga na mtu yeyote wanayekutana naye ni
lazima wampige na kumpora.
"Wenye maduka wanalazimika kufunga
kuanzia saa moja jioni kuhofia kundi hilo ambalo huvunja milango ya
nyumba na kufanya uporaji" alisema Fadhil.
Fadhil alisema maeneo ambayo vijana hao wameshamiri ni Moshi Baa Relini, Kwa Mkolemba, Diwani na Bomba mbili.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa
Ilala, Kamishna Msaidizi (ACP), Salum Hamdan alisema polisi imejipanga
vilivyokukabiliana na vitendo hivyo katika mkoa wake.
"Kwanza napenda kukuambia kwamba hakuna
kundi linalojiita panya road wote tuna wahesabu ni wahalifu kama walivyo
wahalifu wengine na hivi ninavyongea na wewe tupo katika siku ya sita
ya operesheni ya kukakamta watu wanaojihusisha na uhalifu wa ujambazi
wakiwemo wanaouza pombe haramu ya gongo " alisema Kamanda Hamdan.
Aliongeza kuwa katika mkoa wake hivi
karibuni utakuwa shwari baada ya askari wake kusambaratisha watu hao
wanaofanya vitendo hivyo.
Mafundi wa Shirika la Mamlaka ya Reli
Tanzania na Zambia (Tazara), wakikarabati Reli katika makutano ya Reli
na Barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa Dar es Salaam jana.
Wananchi wakivusha relini pikipiki yao.
Pikipiki ikivushwa.
Waendesha bodaboda wakivusha pikipiki
zao kwenye reli baada ya kufungwa kwa muda barabara katika makutano ya
Reli ya Tazara na Barabara ya Mombasa Moshi Baa Dar es Salaam jana
wakati mafundi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara),
wakifanya ukarabati katika eneo hilo.
Mafundi wa Shirika la Mamlaka ya Reli
Tanzania na Zambia (Tazara), wakikarabati Reli katika makutano ya Reli
na Barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa Dar es Salaam.
Na Dotto Mwaibale
MAMLAKA ya Reli Tanzania na Zambia
(Tazara) imelalamikiwa na wananchi kwa kutozingatia muda muafaka wa
kufanyia ukarabati wa reli zake jambo linalowaletea usumbufu.
Malalamiko hayo waliyatoa Dar es Salaam
jana wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusu kadhia
waliopata baada ya kufungwa kwa muda Barabara ya Mombasa kwenda Moshi
Baa kupisha ukarabati eneo la reli inayokutana na barabara hiyo.
"Kazi ya ukarabati wanayoifanya ni nzuri
lakini wangekuwa wakiifanya nyakati za usiku ili kuepusha usumbufu huu
tunao upata wa kuvusha pikipiki zetu relini" alisema Gedion Robert.
Robert alisema katika nchi za wenzetu
kazi za kusafisha miji na ukarabati wa namna hii hufanyika usiku ili
kuondoa adha kwa wananchi wanaotumia barabara kwa ajili ya kwenda kwenye
shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.
Mkazi mwingine kwa Diwani Stellah Urio
alisema amelazimika kulipa sh. 400 kutoka kwa Diwani hadi Relini ambapo
pia alilipa sh. 400 baada ya kubadilisha gari ili kufika Ukonga Mombasa
na kujikuta akitumia sh.800 badala ya 400.
Jitihada za kumpata msemaji wa Tazara ,
Conrad Simuchile, ili kuzungumzia suala hilo zilishindika baada ya
kufika ofisini kwake na kuambiwa mwandishi arudi baadae alikuwa nje ya
ofisi kikazi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes
Tanzania, Lanfang Liao (kushoto) akimkambidhi mmojawapo wa washindi wa
mashindano ya sauti, Hilda Malecela mfano wa runinga ya kisasa yenye
ukubwa wa inchi 40 kutoka kampuni hiyo. Washindi 10 walipatikana katika
shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za
makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
Mmojawapo wa washindi wa sindano la
vipaji vya sauti, Hilda Malecela akikumbatiana na majaji baada ya
shindano ilo kuisha, akishuhudia tukio hilo kushoto ni Afisa Mtendaji
Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao na kulia ni majaji na washindi
wengine. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia
fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes
yaliyopo jijini Beijing, China.
washindi 10 wa shindano la vipaji vya
sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China
Tanzania wakiwa mbele ya jukwaa baada ya kutangazwa washindi. Washindi
hao 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda
kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini
Beijing, China.
Washindi 10 wa shindano la vipaji vya
sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China
Tanzania wakiwa mbele ya jukwaa baada ya kutangazwa washindi. Washindi
hao 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda
kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini
Beijing, China.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes
Tanzania, Lanfang Liao akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara
baada ya kumalizika kwa shindano la vipaji vya sauti lililoandaliwa na
StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China Tanzania. Washindi 10
walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya
kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing,
China.
Mmoja wa washiriki wa shindano la
vipaji vya sauti, Hilda Malecela akionyesha uwezo wake wa kuigiza sauti
mbele ya majaji jukwaani. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo
na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya
StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
Mmoja wa washiriki wa shindano la
vipaji vya sauti, Rukia Hamdani akiwa mbele ya majaji jukwaani baada ya
kuonyesha uwezo wake wa kuigiza. Washindi 10 walipatikana katika
shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za
makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
Mshiriki wa shindano la vipaji vya
sauti, Coletha Raymond akiwa mbele ya majaji jukwaani baada ya kuonyesha
uwezo wake wa kuigiza. Washindi 10 walipatikana katika shindano.
Na Dotto Mwaibale
Hatimaye shindano la kusaka vipaji vya
sauti lililoandaliwa na kampuni ya StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi
wa Chini nchini Tanzania limemalizika mwishoni mwa wiki hii kwa
watanzania 10 kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika makao makuu
yake yaliyopo jijini Beijing.
Akizungumza baada ya shindano hilo Dar
es Salaam juzi , Hilda Malecela kutoka Dar es Salaam ambaye ndiye
aliyeongoza kwa kupata alama nyingi kutoka kwa majaji alisema kuwa
anashukuru sana kupata fursa hiyo ya kuonyesha kila kipaji alichonacho
kwani haikuwa kazi rahisi.
‘’Kwanza kabisa nashukuru kwa ushindi
huu, haikuwa kazi rahisi kwani ushindani ulikuwa ni mkubwa ukizingatia
washiriki walioingia hatua ya fainali wote walikuwa wana uwezo mkubwa
sana. Nawashukuru majaji kwa kunipa moyo tangu awali na hatimaye
kuniamini kwamba nina kitu ambacho ninaweza kukitoa kwa watanzania
kupitia kipaji change cha sauti. Fursa niliyoipata mimi pamoja na
washindi wenzangu tisa ni jambo la kujivunia na kuitumia ipasavyo.’’
alisema . Malecela
‘’Napenda kuwaahidi watanzania kuwa
nitaitumia nafasi hii vema kuhakikisha nafanya kazi nzuri ili wao
waendelea kuburudika na kujifunza zaidi kupitia filamu na tamthiliya.
Nawapongeza pia StarTimes kwa kutambua umuhimu wa Kiswahili na kuja
ubunifu huu ambao haujawahi kutokea nchini. Mara nyingi tumekuwa tukiona
mashindano ya kuimba, kuigiza na kucheza lakini si kwa upande wa sauti.
Wamepiga hatua kubwa sana kwa kweli ambayo inastahili kuigwa na
makampuni mengine.’’ alimalizia mshindi huyo aliyeongoza kwa kuwa na
alama nyingi zaidi kutoka kwa majaji
Naye kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu
wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao amebainisha kuwa amefurahi kuona
shindano la kusaka vipaji vya sauti limepokewa kwa muitikio mkubwa na
watanzania sehemu mbalimbali za nchi.
‘’Hatukutegemea kama watanzania wengi
wangevutiwa na shindano hili lakini imekuwa ni kinyume chake kwani
imedhihirika kuwa wapo wasanii wengi sana wenye vipaji vya sauti. Sanaa
ina uwanja mpana sana ni namna tu msanii mwenyewe anavyoamua anakitumia
vipi kipaji alichonacho. StarTimes tumebaini kutoka kwa wateja wetu kuwa
filamu na tamthiliya zilizotafsiriwa na kuingiziwa sauti kwa lugha ya
Kiswahili zinapendwa sana. Hivyo tukaona ni vema kuviibua vipaji ili
tufanye nao kazi hiyo kwa manufaa ya watanzania.’’ alisema Liao
‘’Tunaamini kupitia shindano hili
tumeweza kutoa ajira kwa watanzania 10 watakaokwenda kujumuika na
wenzetu waliopo makao makuu jijini Beijing, China katika kuzalisha kazi
zilizo bora kabisa. Nawasihi washindi waliopata fursa hii kuitumia vema
kwa kufanya kazi kwa bidii kwani ninaamini wanastahili mpaka kuchaguliwa
na majaji kuwa vinara dhidi ya wenzao 18 waliofikia hatua ya fainali.
StarTimes tunaahidi kuendelea na zoezi hili wakati ujao kwani bado
uhitaji ni mkubwa na sisi siku zote tupo kwa ajili ya kuwapatia kile
wateja wetu wanachokitaka.’’ alihitimisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa
StarTime nchini
Katika fainali hizo washindi wa kwanza,
pili na watatu; Hilda Malecela - kutoka DSM, Safiya Ahmed kutoka
Zanzibar na Sadiq Kututwa - kutoka Zanzibar) walizadiwa runinga za
kisasa zenye ukubwa wa inchi 40, 32 na 24 kila mmoja na StarTimes
kutokana na kuongoza kwa alama nyingi katika fainali hizo huku washindi
saba wakipatiwa simu za mkononi za kisasa kutoka StarTimes.
Kwa ujumla washindi kumi waliopatikana
ni; Hilda Malecela(DSM), Safiya Ahmed(ZNZ), Sadiq Kututwa(ZNZ),
Mathew Philip Mgeni(Arusha), Maisala Abdul(DSM), Rukia Hamdan(ZNZ),
Richard Rusasa(DSM), Happiness Stanslaus - Nyamayao(DSM), Jamila
Hassan(DSM) na Abraham Richard(DSM). Na wote watapata fursa ya kwenda
kufanya kazi katika makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing,
China kwa mkataba wa muda wa mwaka mmoja.
Katika mashindano hayo takribani
washiriki zaidi ya 547 walijitokeza katika usaili uliofanyika katika
mikoa ya Arusha (Agosti 27), Zanzibar (Septemba 3) na Dar es Salaam
(Septemba 10) na hatimaye washiriki 18 tu wakabakia na kutinga hatua ya
fainali.
Washiriki 18 waliotinga hatua ya fainali
ni kama ifuatavyo: kwa mkoa wa Arusha ni Mathew Philip Mgeni, Dorcas
Francis, Halima Hussein, Janeth N Molely na Hilda Kinabo; Zanzibar ni
Safiya Ahmed Said, Sadiq Kututwa Abdalahh, Rukia Hamdan, Imatu Obeid
Fabian na Mohamed Said Mohamed; na Dar es Salaam ni Hilda Malecela,
Abraham Richard, Happiness Stanslaus ‘Nyamayao’, Richard Rusasa, Emanuel
Landey, Coletha Raymond, Jamila Hassan na Maisala Abdul.
No comments:
Post a Comment