Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri
Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa
kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo
Septemba 29, 2016
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, (kulia-katikati) akiongoza kikao cha Baraza
la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2016
Waziri
Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiongea mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Baraza
la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2016. Kushoto ni Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. (PICHA NA IKULU)
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO)
linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kusini kuwa kutakuwa na katizo
la umeme kama ifuatavyo:-
TAREHE:
Jumamosi 01 Oktoba, 2016
MUDA:
02:00 Asubuhi hadi 11:00 jioni
SABABU:
Kujenga laini mpya ya Mburahati na ukarabati wa laini za Tandale Textile
ili
kuboresha hali ya umeme.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Maeneo yote ya Tandale, Manzese, Sinza Uwanja
wa TP, Sinza Vatican, Namnani Hotel, Iteba, Sinza Kijiweni, Sinza Kumekucha, Sinza Mwika, TTCL Manzese ,
Urafiki Quarters, Urafiki Textile,TSP Ltd Millenium business, Sinza Lion Hotel,
Rombo Sunflower, Strabag compound, Engen petrol station, Masamaki Plastic Bags
Ltd pamoja na maeneo ya jirani.
TAREHE:
Jumapili 2 Octoba, 2016
MUDA:
02:00 Asubuhi hadi 11:00 jioni
SABABU:
Matengenezo kwenye Kituo cha Kupozea Umeme Ubungo 33kv ili kuboresha
hali
ya umeme.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Parts of Mandela road, I ndustrial area near
Mandela road, Ubungo NBC, Tbs Ubungo,
Ubungo Bus Terminal, Parts of Sinza,
Part of Kimara, Baruti,Kimara Kimara Korogwe,Kimara Mwisho, Kimara Matangini,
Kimara Mavurunza, Ubungo Maziwa, TTCL Ubungo Kisiwani, Mabibo,TGNP Mabibo, Mabibo Hostel, Mabibo
Jeshini, Mabibo, Makabe, Mpigi Magohe, Goba,Kimara King’ong’o, Tegeta
A,Mavurunza, Suka, Stopover, Changanyikeni, Makongo Mwisho pamoja na maeneo ya
jirani.
Tafadhali usishike waya uliokatika, toa
taarifa kupitia simu zifuatazo Magomeni 0222171759/66, 0784/0715271461, Kimara
Ofisi ya Wilaya 0717/0788379696, Au Kituo cha miito ya simu 2194400 Au 0768
985100.
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote
utakaojitokeza.
Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano, TANESCO Makao Makuu
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina
Chuwa akitoa taarifa ya Pato la Taifa Robo ya Pili (Aprili – Juni) ya Mwaka
2016 kwa waandishi wa habari leoSeptemba 29, 2016, jijini Dar es Salaam.
Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa ofisi hiyo Bi. Joy
Sawe. Taarifa hiyo imeonyesha kuwa Pato la Taifa limekua kwa kasi ya asilimia
7.9 katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni 2016 ikilinganishwa na kasi ya
asilimia 5.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2015.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina
Chuwa akitoa taarifa ya Pato la Taifa Robo ya Pili (Aprili – Juni) ya Mwaka
2016 kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja wa
Takwimu za Pato la Taifa wa Ofisi hiyo Daniel Masolwa. Taarifa hiyo imeonyesha
kuwa Pato la Taifa limekua kwa kasi ya asilimia 7.9 katika kipindi cha mwezi
Aprili hadi Juni 2016 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 5.8 katika kipindi
kama hicho mwaka 2015.
(PICHA
NA EMMANUEL GHULA)
NA VERONICA KAZIMOTO
PATO
la Taifa limekua kwa jumla ya thamani ya Shilingi trilioni 11.7 katika kipindi
cha robo ya pili ya mwaka 2016 ikilinganishwa na Shilingi trilioni 10.9 katika
kipindi kama hicho cha mwaka 2015.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa amesema ukuaji wa pato la Taifa
umetokana na shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo, mifugo, misitu na uvuvi
ambapo shughuli hizo zimekuwa kwa asilimia 3.2 ikilinganishwa
na ukuaji wa asilimia 1.9 katika kipindi kama hicho mwaka 2015.
Kwa
upande wa shughuli za uchumi za viwanda na ujenzi, Dkt. Chuwa alisema kumekua na
ongezeko la asilimia 20.5 katika kipindi hicho ukilinganisha na ukuaji wa
asilimia 11.2 mwaka 2015 katika shughuli za uchimbaji madini, mawe na kokoto.
Aidha
shughuli za uzalishaji bidhaa na viwanda zimeongeza kwa asilimia 9.1 katika
kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2016 ukilinganisha na kasi ya asilimia 5.2 ya
mwaka 2015.
Shughuli
za uchukuzi na uhifadhi, Dkt. Chuwa amesema kuwa shughuli hizo zimekua kwa
kiwango cha asilimia 30.6 zikisababishwa na usafirishaji wa abiria
kwa njia ya reli na barabara ikiwa ni pamoja na usafiri wa UDART.
Vilevile,
shughuli za fedha na bima zimeongezeka kwa kasi ya asilimia 12.5 ikilinganishwa
na asilimia 10.0 iliyopatikana katika kipindi kama hicho mwaka 2015.
Dkt.
Chuwa amefafanua kuwa huduma za elimu zimekua kwa kasi ya asilimia
8.0 katika robo hiyo ya mwaka ikilinganishwa na aslimia 7.4 ya kipindi kama
hicho kwa mwaka 2015 ambapo ukuaji wa shughuli hii imetokana na ongezeko la
wanafunzi waliodahiliwa mwaka 2016.
Kwa upande wa Nchi za Afrika Mashariki ambazo zimeshachambua na
kutoa Pato la Taifa katika kipindi kinachoishia Juni 2016 ni Rwanda ambapo Pato
halisi la Nchi ya Rwanda katika kipindi cha Aprili – Juni 2016 limeendelea
kukua kwa asilimia 5.4 ikilinganisha na asilimia 7.2 ya miezi kama hiyo mwaka
2015.
Takwimu za Pato la Taifa kwa robo mwaka hupimwa kwa kutumia thamani
ya bidhaa na huduma zilizozalishwa nchini katika vipindi vya miezi mitatu
mitatu ambavyo ni Januari – Machi, Aprili – Juni, Julai – Septemba na Oktoba –
Desemba ambapo hujumuisha shughuli zote za kiuchumi, na hutumika katika
kutathmini, kupanga mipango na kutayarisha sera za kiuchumi.
TAREHE YA MWISHO YA UFUNGAJI WA MASHINE ZA KIELEKTRONIKI (EFPP) KWENYE VITUO VYA KUUZA MAFUTA NCHINI
Kufuatia
changamoto zilizojitokeza katika zoezi la ufungaji wa mashine za
kielektroniki zinazojulikana kama Electronic Fuel Pump Printer (EFPP)
kwenye Vituo vya kuuza mafuta ya Petroli, Dizeli na mafuta ya taa na
kufuatia agizo la Serikali kuwa wamiliki wa vituo vyote wawe wamefunga
mashine hizo ifikapo tarehe 30 Septemba 2016, Wizara ya Fedha na
Mipango, Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na
Chama cha Wamiliki na
Waendeshaji
wa Vituo vya Kuuza Mafuta Nchini (TAPSOA) umekutana na kujadiliana
changamoto zilizopo katika zoezi la ufungaji wa mashine za EFPP na
kukubaliana yafuatayo;-
a)Serikali
imesogeza mbele tarehe ya mwisho ya kufunga mashine za EFPP, ili kutoa
nafasi kwa TRA ikishirikiana na TAPSOA kutatua changamoto zilizopo kwa
sasa.
b)Wamiliki
wa vituo vya kuuza mafuta ambao hawajakamilisha ufungaji wa mashine za
EFPP waendelee kutumia mashine za mkono (ETR) mpaka hapo
watakapotaarifiwa vinginevyo.
c)TRA
inawakumbusha wamiliki wote wa vituo vya kuuza mafuta kuhakikisha kuwa
wanatoa stakabadhi za kielektroniki kwa kila mauzo wanayofanya ili
kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza ikiwemo adhabu kwa kukaidi agizo
hili la kisheria.
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu
Kanisa
la EAGT Posta “B” Mabatini Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Lameck
Nkumba, linawakaribisha watu wote kwenye mkutano mkubwa wa injili
utakaofanyika katika viwanja vya kanisa hilo vinavyotizamana na geti la
polisi Mabatini nyuma ya iliyokuwa Orange Tree Hotel.
Mhubiri
wa kitaifa na kimataifa ambaye amehubiri mataifa mbalimbali duniani
ikiwemo Marekani, Canada, Uingereza, Ireland, Wales , Scotland,
Ujerumani, Dernmark, Swirtzland, Afrika Kusini, DRC Congo na mengine
mengi, Dkt.Daniel Moses Kulola (pichani), atahudumu kwenye mkutano huo
akishirikiana na wahubiri wengine.
Ni
wiki moja yenye miujiza na uponyaji wa nguvu ya Mungu, kuanzia jumapili
tarehe 9.10.2016 hadi jumapili tarehe 16.10. 2016 muda ni kuanzia saa
9.00 mchana hadi saa 12 jioni, kila siku.
Waimbaji
mbalimbali akiwemo Mwanyamaki kutoka Morogoro, Emannuel Mgogo kutoka
Dar es salaam pamoja na kwaya zinatotamba Jijii Mwanza kama vile
Havillah Gospel Singers kutoka EAGT Lumala Mpya, na kwaya ya EAGT Posta
“B” zitahudumu kwenye mkutano huo.
Ewe
baba, mama, kaka, dada, ndugu, jamaa na marafiki, fika kwenye mkutano
huo ili ukutane na nguvu ya Mungu ambapo wagonjwa mbalimbali, wenye
mapepo, mikosi na waliofungwa na vifungo vya ibirisi watafunguliwa kwa
jina la Yesu, bila malipo.
Kwa msaada wa Kiroho, piga simu nambari 0784 43 77 82
Bonyeza HAPA Kusikiliza, Au Bonyeza Play hapo chini .
Katika
kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi yenye maendeleo na iliyo na watu
ambao wamefanikiwa kimaisha, vijana nchini wametakiwa kufanya kazi kwa
bidii ili kujikomboa na janga la umaskini lakini pia kulisaidia taifa
kupata maendeleo.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International,
Paul Mashauri wakati akizungumza na vijana ambao wanajifunza
ujasiriamali na kuwambia ni vyema wakaongeza bidii katika ndoto
wanazotamani kuzifikia ambazo pia zitawasaidia kuondokana na umaskini
ambao umekithiri nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri akizungumza na vijana kuhusu ujasiriamali. |
Alisema
ili mtu kufanikiwa kimaisha haitaji zaidi elimu ya darasani bali ni
muhusika mwenyewe kujiongeza kwa kufanya kazi kwa bidii katika jambo
ambalo anatamani kulifikia na akiwatolea mfano yeye mwenyewe kuwa tangu
amalize masomo yake katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hajawahi kurudi
chuoni kuchukua cheti chake lakini amefanikiwa kimaisha.
"Mimi
simchukii mtu ila nauchukia umaskini alionao, ukiwa na juhudi katika
biashara na kujituma hata Rais Magufuli hatakufikia mshahara watu
wanaweza kusema unafanya biashara ya kawaida lakini inakulipa sana, ni
wewe tu na juhudi zako unazofanya ili ufanikiwe,
"Maisha
hayana formula kuwa kufanikiwa ni lazima uwe na masters ndiyo upate
mafanikio, masters ya maisha ni kuwa mtaani maisha yakupige alafu uinuke
upambane na uyashinde hapo ndiyo umeyashinda maisha, ukitaka kufanikiwa
lazima ufanye kazi kwa bidii hata mimi natumia muda wangu mwingi
kujifunza ili nizidi kufanikiwa," alisema Mashauri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri akiwaonyesha moja ya mashine ambazo Kampuni ya HiTech International inaziuza. |
Nae
mwendesha mafunzo kwa vijana hao kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO),
Benny Mwambela alisema mafunzo hayo yameanzishwa Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ili kuwasaidia vijana kupata
mbinu za jinsi gani wanaweza kufanikiwa kibiashara na baada ya mafunzo
hayo, wahitimu watakwenda kutoa elimu kwa vijana wengine.
"Tunafundisha
walimu ambao watakwenda kufundisha watu wengine kuhusu ujasiriamali,
kuna watu wasiopungua 10,000 wamejiandikisha kujifunza ujasiriamali
kwahiyo tunawafundisha watu hawa ili wakawafunze na wengine ili na wao
wajue jinsi gani wanaweza kufanya biashara,
"Wanafundishwa
jinsi ya kubuni wazo la biashara, kuna wengine wana mawazo ya biashara
watafundishwa jinsi ya kuanzisha biashara, na kuna wengine wanafanya
biashara wanafundishwa jinsi ya kutanua biashara na watafundishwa kuhusu
kuanzisha vikundi na jinsi gani ya kutumia fedha," alisema Mwambela.
Na Rabi Hume, MO BLOG
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri akiwaeleza vijana jinsi wanavyoweza kuepuka umaskini kwa kufanya kazi kwa bidii. |
Baadhi ya vijana walioshiriki semina hiyo. |
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi mteule
wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke mara baada ya kupokea hati zake
za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.Bi
Theresa May
Ametoa kiasi cha
Paundiza Uingereza Milioni 2.3, sawa na Shilingi za Kitanzania, Bilioni 6 kwa
ajili ya kusaidia waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho
kutoka kwa Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akipokea
Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini
Sarah Catherine Cooke Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi mteule
wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke mara baada ya kupokea hati zake
za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akimshukuru Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah
Catherine Cooke kufatia mchango wa Waziri Mkuu wa Uingereza alioutoa kwa Serikali
ya Tanzania kwa ajili ya kusaidia waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera
kiasi cha Paundi za Uingereza Milioni 2.3 sawa na Takribani Shilingi Bilioni
sita za Kitanzania
No comments:
Post a Comment