CHELSEA YAMREJESHA TENA LIGI KUU YA UINGEREZA BEKI DAVID LUIZ
Chelsea imemrejesha tena katika
dimba la Stamford Bridge, David Luiz, baada ya kukamilisha uhamisho
wa paundi milioni 32.
Beki huyo raia wa Brazil amejiunga
tena na ligi kuu ya Uingereza kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya
kuondoka muda wa miaka miwili, baada ya kuondoka kujiunga na Paris
Saint-Germain ya Ufaransa.
David Luiz akionyesha ishara ya dole gumba kuashiria mambo ni safi
RC ARUSHA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA DINI
Askofu wa Kanisa la Anglikan,Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay (kushoto) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mheshimiwa Mrisho Gambo akiagana na Askofu wa Kanisa la Anglikan Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kulia) baada ya mazungumzo yao.
Nteghenjwa Hosseah – Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo ameendelea na ziara yake ya kujitambulisha kwa viongozi wa dini ukiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana na viongozi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni.
Mh.Gambo amekutana na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini Kati,Mchungaji Solomon Masangwa , Askofu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God(EAGT) mkoa wa Arusha,Leonard Mwizarubi na Askofu Stanley Hotay wa Kanisa la Anglikana , Dayosisi ya Mount Kilimanjaro.
Katika mazungumzo na viongozi hao kwa nyakati tofauti mbali na kujitambulisha aliwahakikisha dhamira ya serikali kulinda na kuheshimu uhuru na haki ya kuabudu ambayo imekuwepo nchini kwa muda mrefu ikiwa ni njia ya kuwa na taifa la watu wenye hofu ya Mungu.
ALICHOKISEMA ALIYEKUWA KATIBU WA CHADEMA MKOANI MWANZA BAADA YA KUTIMKIA CCM.
Nzwalile ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema Taifa, Mjumbe Baraza Kuu Chadema Taifa, Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano Chadema Mkoa wa Mwanza, amefikia uamuzi huo baada ya jana kujivua vyeo hivyo.
Amesema amefikia hatua hiyo kutokana na kwamba Chadema imepoteza mwelekeo kwani kimekuwa kikiibuka na oparesheni za kuichonganisha serikali na wananchi huku pia demokrasia ikikosekana ndani ya chama hicho.
"Kama ni udikiteta basi mimi niseme Chadema ndiko kuna udikiteta kwani zaidi ya mara tatu nimemsikia Lowasa (Edward Lowasa, aliyekuwa mgombea urais 2015) akisema yeye ndiye mgombea urais mwaka 2020, kwa kikao gani". Amesema Nzwalile na kuongeza kwamba yale mambo yote mabaya yaliyokuwa yakifanyika ndani ya CCM yamenyooshwa hivyo hakuna haja ya yeye kuendelea kukaa Chadema.
Amesema atazunguka Wilaya zote ili kuhakikisha anawarejesha wengine ndani ya CCM huku akiwa na jukumu moja la kuubomoa Ukuta unaoelezwa kujengwa na Chadema kwani ni ukuta wa tope hivyo atatumia tu maji kuubomoa.
Nzwalile amekaribishwa ndani ya CCM na Mwenyekiti wa Chama hicho mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo, ambaye pia amewakaribisha makada wengine wa upinzani kuhamia CCM akisema kwamba chama hicho kinaendesha mambo yake kidemokrasia.
No comments:
Post a Comment