Jengo
pacha la mfuko wa pensheni wa PSPF ambalo ni mojawapo ya vitega uchumi ya
hifadhi ya jamii vinavyotokana na michango ya wanachama
Christian Gaya Majira 27 Septemba 2016
Hifadhi ya jamii ni mfumo wa jamii ambao
umekuwapo tangu mwanzo wa mwanadamu. Tangu enzi za kale, jamii zote zimekuwa na
taratibu mbali mbali za kuhakikisha ya kwamba kila mtu anakuwa na uhakika wa
kuishi maisha yake katika mazingira yo yote yanayoweza kumkwaza kuishi kama
majanga, maradhi, ulemavu, umri na kadhalika
Mfumo
wa hifadhi ya jamii ambao ni wa lazima kisheria ambapo wafanyakazi pamoja na
mwajiri wanachangia pamoja na kupeleka michango kwenye chombo cha mfuko wa
pensheni au mfuko wa akiba ya wafanyakazi
Ingawa mpaka sasa idadi kubwa ya nguvukazi ndiyo
inayojitoa kwa kuondoa mafao yao kabla haiyaifa na kwenda kinyume na malengo ya
hifadhi ya jamii ambalo ni kumwezesha mwananchi kuishi maisha yenye staha kwa
kuwawezesha kupata huduma za msingi pale wanapokuwa hawana kipato kutokana na
sababu mbalimbali zinatokana na uzee, kifo,ugonjwa, uzazi n.k.
Kwa mujibu wa shirika la kazi duniani (ILO)
hifadhi ya jamii ni mfumo ambao jamii husika imejiwekea kwa lengo ya kujikinga
dhidi ya matukio yasiyotarajiwa.
Hifadhi ya jamii ni haki ya kila mtu na ndiyo
maana haki hii imeanzishwa katika katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania
ibara ya 11(1) na sera ya taifa ya hifadhi ya jamii ya mwaka 2003.
Haki hii pia imeiainishwa kwenye mkataba wa
kimataifa wa haki za binadamu wa mwaka 1948 pamoja na mikataba ya shirika la
kazi duniani (ILO) ibara ya 102 ya mwaka 1952.
Wazee, watoto, yatima, wajane, na wagonjwa
ambao kutokana na hali zao hawawezi kujikimu ni baadhi ya makundi ambayo
yamekuwa yakipata kinga maalumu tangu enzi hizo hadi sasa, kama sehemu ya mfumo
wa jamii ya mwanadamu duniani kote.
Jamii ilikuwa inahakikisha kuwa vikundi hivyo
vya watu wasiojiweza wanapata hifadhi ya jamii kwa maana ya msaada wa chakula,
malazi na matibabu.
Ili kuweza kutoa hifadhi hiyo jamii
ilijiwekea taratibu na kanuni ambazo ilibidi zifuatwe kabla ya mtu hajapewa
hifadhi kwa nia ya kuhakikisha kuwa ni wale tu wanaohitaji msaada ndiyo
wanaopata.
Na utaratibu mpaka leo unafanyika ndani ya
jamii za Kitanzania na penginepo pale hapa afrika na hata ulaya.
Hifadhi ya jamii ni haki ya msingi ambayo
kila mtu anastahili kupata kutoka katika jamii. Jamii zilijiwekea utaratibu na
sheria ambazo hutumika kuhakikisha jamii inapoondokana na utegemezi.
Sheria ya kwanza kabisa kutungwa na kuandikwa
kuhusu hifadhi ya jamii ilikuwa in ile sheria ya kusaidia maskini huko
uingereza iliyotungwa karne ya 16. Sheria hiyo ilifuatiwa na nyingine
iliyotungwa mwaka 1883 kwa ajili ya matibabu.
Baadaye nchi nyingi hasa za ulaya zilianza
kutunga sheria mbalimbali kwa ajili ya kuanzisha mifumo ya hifadhi ya jamii. Na
hiyo ilitokana na mapinduzi ya viwanda (industrial revolution) yaliyo tokea
ulaya wakati huo, ambapo watu wengi walikimbilia mijini kutoka mashambani kwa
kazi ya kuajiriwa viwandani.
Hivyo misingi ya kusaidiana kifamilia kwa
watu wa mashambani, kifamilia kwa watu wa mashambani ikaanza kupotea. Kwa
sababu nguvu kazi yote iliyokuwa ukitoa huduma katika koo mbalimbali iliishia
kwenda mijini kwenda kufanya kazi.
Lakini ikumbukwe kuwa hifadhi ya jamii
ilitolewa na mpaka sasa bado inatolewa ndani ya jamii mbalimbali za kiafrika.
Na ndiyo maana wazee wengi wana imani hata ya
kuzaa watoto wengi zaidi kama hifadhi yao ya jamii ya sasa na ya baadaye ingawa
lengo kubwa ni kuendeleza ukoo na kufanya kuwa ni wajibu kuwa na watoto.
Watu wanateuliwa kubaki na wazee na wale
wengine wasiojiweza ili kuwapa hifadhi.
Hata wakunga wa jadi tunao mpaka sasa ambao
hutoa huduma kwa akina mama wajawazito na wanapojifungua.
Watoto waliofiwa na wazazi wao wana ukoo
waligawana na kuwapa hifadhi ya jamii mpaka wanapofikia umri wa miaka 18 wa
kujitegemewa na yule anayesoma anapewa hifadhi mpaka anapomaliza elimu ya juu.
Huo ni utaratibu ambao unawekwa na wanajamii
hasa ndani ya koo mbalimbali.
Tumeona mara nyingi karibu mikoa yote hapa
nchini huduma ya kupatiwa msaada wa mazishi unapotolewa ndani ya vikundi
mbalimbali.
Na watu sasa wamegundua kuwa njia nzuri ya
hifadhi ya jamii ni kwa ile isiyokuwa rasmi ambapo kuna vikundi mbalimbali vya
kufa na kuzikana, kuweka na kukopa, ambapo wanachama wake hutokana na mkoa au
wilaya anakotoka.
Na hata viongozi wakuu wa mashirika ya umma,
mashirika yasiyo ya kiserikari, na wa serikali wamekuwa wanachama wachagiaji
wazuri sana kwenye mifuko hii isiyo rasmi.
Na hii imeleta changamoto kubwa kwa hifadhi
za jamii zilizo rasmi kama vile mashirika ya hifadhi ya jamii yaliyopo hapa
nchini na sehemu zingine za kiafrika.
Kwa kawaida anayetakiwa kuwajibika kutoa
hifadhi ya jamii kwa wazee, walemavu, wategemezi, na kwa watu wasio na kazi ni
serikali na jamii ya kitanzania kwa ujumla.
Umaskini zaidi ambao husababishwa na kukosa
chakula, malazi, nguo au fedha kwa ajili ya kununuliwa hayo mahitaji muhimu
huwa yanasababishwa na magojwa na hali ya uzee ukilinganisha na sababu zingine.
Kwa sababu hata mshahara wa mtu wa kila mwezi
hautoshi kwa ajili ya kutimiza mipango ya leo na kwa siku sijazo. Kwa ujumla ni
kwamba haitoshi kwa ajili ya mipango ya leo.
Kwa sababu ya kuwa na upungufu wa fedha hivyo
inakuwa ni vigumu sana kwa mtu hata kuchangia kwa hiari kwenye mashirika ya
hifadhi jamii kwa ajili ya siku za usoni.
Na ndiyo maana imekuwa in kawaida ya kuwa
kila nchi inawajibika kuhakikisha kuwa siyo tu kwa wale ambao wanaokufa kwa
njaa ila pia inawajibika kuhakikisha kuwa maliasili ya nchi inagawanywa sawa
ili kupunguza hali kama hii.
Hifadhi
ya jamii ina maana ni aina ya hatua madhubuti au shughuli zilizobuniwa za
kuhakikisha kuwa wananchi wa jamii hiyo wanapata mahitaji yao ya lazima na ya
msingi na wanapewa kinga ya hifadhi ya
kutokana na majanga ili kuwawezesha kuwa na kiwango cha maisha ya kuishi
kulingana na mila na desturi za jamii
Christian Gaya ni mwanzilishi wa
Kituo cha HakiPensheni Tanzania na mshauri wa masuala ya pensheni. Kwa maelezo
zaidi gayagmc@yahoo.com Au kwa habari
zaidi za kila siku juu ya HakiPensheni unaweza kutembelea tovuti www.hakipensheni.co,tz
au hakipensheni.blogspot.com Simu namba +255 655 13 13 41
No comments:
Post a Comment