Pages

Wednesday, September 28, 2016

RAIS MAGUFULI AZINDUA NDEGE MPYA ZA ATCL ZILIZONUNULIWA NA SERIKALI KUTOKA CANADA ANAYESEMA NDEGE HIZI HAZIKIMBII AJE NIMUNULIE TIKETI AKAE MBELE AONE MAWINGU YANAVYOPIGWA; JPM





Dondoo za hotuba ya Rais John Pombe Magufuli wakati akizindua ndege mpya za ATCL jijini Dar es Salaam leo Septemba 28, 2016


*“Tulipochukua hatua ya kuwashika RAS, DED Kagera leo balozi wa Uingereza ametuchangia Bil 6 kwa ajili ya wananchi Kagera”
*"Tunataka kuanza ujenzi wa treni za umeme Dar, haya si Ulaya tu, hata hapa yatafanyika"- Rais…
* "RAS na DED tuliowafukuza jana, leo wameshafikishwa mahakamani
*"Ujenzi wa daraja la Coco Beach hadi Agha Khan umeanza, Interchange ya Ubungo itaanza karibuni"-
 *“Wengine wameajiriwa na watu fulani kazi yao kutukana kila linalofanywa na Serikali, vihela wanavyopewa kidogo na wanafikiri hatuwajui'-JPM
*“Jana TANESCO wametangaza tenda ya ku-supply nguzo za zege kwa kanda ya mashariki, Kaskazini, Lake Zone na Southern Highlands
*“kama huzitaki ndege hizi bora ukae kimya kiherehere chanini.”
* “Huyo aliyesema ndege hii haikimbii awe mtu wa kwanza mimi nitamlipia nauli halafu akae mbele akaone mawingu yanavyopiga.”
 * "Ndani ya ATCL kuna wake wa Mawaziri, Shirika halizalishi lakini wake wa Mawaziri wameng'ang'ani tu.”
*“ Kwa hiyo kulikuwa na wanafunzi hewa, wafanyakazi hewa na mafuta hewa.”
* "ATCL walikuwa wakinunua mafuta hewa, unaambiwa ndege imeenda Mwanza kumbe iko Dar uwanjani"


RAIS MAGUFULI AZINDUA NDEGE MPYA ZA ATCL ZILIZONUNULIWA NA SERIKALI KUTOKA CANADA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo Septemba 28, 2016, amezindua ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 kwenyeuwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Ndege hizo zilinunuliwa ili zitumiwe na Kampuni ya Ndege ya Tanzania, (ATCL), ambayo inamilikiwa na serikali. Pichani, Rais amkisalimiana na muhudumu wa ndege hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi huo. (PICHAN A IKULU)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe akishuka  kwenye ndege mojawapo baada  kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiingia kwenye ndege mojawapo baada ya kukata  utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na maafisa na viongozi wengine mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli  pamoja na maafisa wengine waandamizi wakiwa kwenye ndege mojawapo baada  kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016




 Rais katika picha ya pamoja na viongozi, wahudumu wa ndege na maafisa waandamizi wa serikali

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe Isaya Mwita(mwenye tai nyekundu) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masanju  wakishuka  kwenye ndege mojawapo baada ya Rais Magufuli  kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles baada ya kukata  utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dk Leornad Akwilapo amewataka vijana kutafuta ajira sehemu mbalimbali kwa kutumia fursa zilizopo badala ya kutegemea fursa za serikali.
Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua warsha iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, iliyolenga kuweka mkakati wa pamoja kati ya wadau wa elimu, serikali katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu lengo la nne.
Alisema kwamba ni imani yake kwamba elimu waliyonayo vijana inawaruhusu kufanya shughuli mbalimbali ambazo si lazima kuajiriwa na serikali.
Alisema hakuna nchi duniani ambayo inaweza kuajiri kila mmoja lakini elimu zinazotolewa pamoja na ya Tanzania zinawaandaa vijana kujiajiri wenyewe.
Akizungumzia warsha hiyo alisema kwamba wadau wanakutana kutengeneza mkakati wa pamoja wa kutoa elimu bora kwa wananchi wa Tanzania na namna ambavyo malengo ya maendeleo endelevu (SDG’s) yanavyoshirikishwa katika utoaji elimu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leornad Akwilapo akifungua warsha ya kutengeneza mkakati mmoja kati ya serikali na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu uliondaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) unaofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa NACTE jijini Dar es Saalam. 

Alisema lengo la nne la Maendeleo endelevu la Umoja wa Mataifa linasisitiza elimu bora isyokuwa ya kibaguzi kwa watu wote na hivyo mkutano wao ni kuangalia namna wanavyoweza kushirikiana kutoa elimu bora inayowezesha watu wake kujiajiri.

Alisema kwamba mtazamo huo ambao tayari Tanzania ilikuwa nao miaka ya mwanzo ya uhuru ambapo kulikuwa na kisoma cha watu wazima kitu ambacho kilillenga kuwafanya watu kuwa na elimu ya kutosha kuhusu mazingira yao na maisha yao. Naye Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania, Zulmira Rodrigues alisema kwamba wameandaa warsha hiyo kwa lengo la kuelezana utoaji bora wa elimu ambao utaendana na matakwa ya sasa ya kumwezesha anayepata elimu hiyo kujiajiri mwenyewe. Aidha amesema lengo la kushirikisha wadau wa elimu ni kuhakikisha kwamba lengo la maendeleo endelevu la nne la Umoja wa Mataifa linashirikishwa katika utoaji elimu kwani lengo hilo ni kuhakikisha elimu kwa wananchi wote bila ubaguzi huku hatua zikichukuliwa katika kuwezesha wanawake kusonga mbele. 

Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akizungumza kuhusu lake lilivyojipanga kushirikiana na Serikali katika nyanja mbalimbali ya ukuzaji wa elimu haapa nchini.
Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Makuru Petro akiwasilisha mada wakati wa kongamano lililoshirikisha Serikali pamoja na wadau mbalimbali kujadili ni kwa jinsi gani wanatengeneza mkakati bora ili kuweza kuisaidia serikali kutoa elimu bora na bila ubaguzi wa aina yoyote.Afisa Elimu Mkuu Hilda K. Mkandawire kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia akiwasilisha mada wakati wa kongamano lililowakutanisha wadau mbalimbali wa elimu.Baadhi ya wadau mbalimbali wa sekta ya elimu wakifuatilia kwa makini mkutano uliokuwa unaendelea.Criana Connal kutoka UNESCO akizungumza jambo wakati wa warsha iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa elimu ili kujadili mpango mkakati utakaosaidia kuinua kiwango cha elimu nchini Tanzania.Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UNWOMEN), Maria Karadenizli (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues wakati wa kongamano lililowakutanisha wadau mbalimbali wa elimu.Mkutano ukiendelea.Baadhi ya makundi ya wadau wa sekta ya elimu wakijadiliana ili kutengeneza mpango mkakati wa pamoja kati ya serikali na wadau mbalimbali wa elimu utakaosaidia serikali kutoa elimu bila ubaguzi wa aina yoyote na kwa makundi yote ili kufanikisha lengo namba nne la Mpango wa maendeleo endelevu (SDG’s) linalohusu elimu bora kwa wote.


R

MAJALIWA AWASILI KIBITI KWA ZIARA YA SIKU MOJA

BALOZI SEIF AIKABIDHI SEKONDARI YA KITOPE MILIONI 13 ILI KUKAMILISHA JENGO LAKE LA MAABARA

Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” Nd. Issa Juma kushoto yake wakikaguwa maendeleo ya ujenzi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Kijiji cha Fujoni.
Haiba ya muonekano wa Jengo la Msikiti wa Ijumaa Fujoni unavyoonekana nje ukiendelea ujenzi wake ambao unatarajiwa kuezeskwa mapema wiki ijayo.

Balozi Seif kati kati akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi Hundi kwa ajili ya kugharamia uendelezaji wa ujenzi wa jengo la Maabara la Skuli ya Sekondari ya Kitope. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Wiaya ya Kaskazini B Nd. Issa Juma na Mkurugenzi wa Idara ya Elimu, Maandalizi na Msingi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bibi Safia Ali Rijali.

Kulia ya Balozi Seif ni Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Kitope Mwalimu Suleiman Juma Makame na Msimamizi wa Ujenzi wa Jengo la Maabara ya Skuli za Fujoni na Kitope Nd. Yasir De Costa.

Msimamizi wa Ujenzi wa Majengo ya Maabara ya Skuli za Fujoni na Kitope Nd. Yasir De Costa wa kwanza kushoto akitoa ufafanuzi wa ujenzi wa majengo ya Maabara ya skuli hizo. Picha na – OMPR – ZNZ.

Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi amewakumbusha Viongozi na washirika wa maendeleo katika Sekta ya Elimu kuzijengea uwezo zaidi wa miundombinu skuli mbali mbali Nchini ili ziwe na uwezo kamili wa kuhimili ushindani wa kitaaluma uliopo katika kiwango cha Kitaifa na Kimataifa.

Alisema wakati wa sasa ni ule wa sayansi uliobadilika kabisa Kiteknolojia tofauti na uliopita kiasi kwamba jamii inapaswa kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira yanayokubalika kivifaa pamoja na walimu waliobobea.

Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitoa kumbusho hilo wakati akikabidhi Hundi ya shilingi Milioni 13,078,000/- kwa ajili ya ukamilishaji wa Jengo la Kisasa la Maabara ya Skuli ya Sekondari ya Kitope iliyomo ndani ya Jimbo la Mahonda.

Katika hafla hiyo fupi ambayo pia alikabidhi hundi ya shilingi Milioni 1.7 kukamilisha gharama za ujenzi wa Maabara ya Skuli ya Sekondari ya Fujoni kwa msimamizi wake Nd. Yasir De Costa Balozi Seif aliahidi kutoa vifaa vyote vya Maabara kwa Skuli ya Sekondari ya Kitope mara baada ya kukamilika kwa ujenzi huo.

WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AHUTUBIA KIBITI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara katika Mji wa Kibiti akiwa katika ziara ya wilaya hiyo Septemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara katika Mji wa Kibiti akiwa katika ziara ya wilaya hiyo Septemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi wa Kibiti wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia Septemba 28, 2016 licha ya mvua kubwa iliyonyesha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi wa Kibiti wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia Septemba 28, 2016 licha ya mvua kubwa iliyonyesha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment