Pages

Wednesday, August 3, 2016

Waziri Wa Afya aitaka MOI kuhudumia wagonjwa kwa haraka zaidi. moi

moi1 
Waziri wa  Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa pili kushoto akitoa maagizokwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Dkt. Samuel Swai  wa kwanza kulia wakati alipotembelea  wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.
moi2 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Dkt. Samuel Swai  wa kwanza kulia akifafanua jambo kwa Waziri wa  Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati alipotembelea  wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam
moi3 
Waziri wa  Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwajulia hali baadhi ya wagonjwa waliopo katika taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI)alipotembelea  wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.
moi4
Waziri wa  Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akimfariji mtoto Rahel Razaro wa kwanza kushoto aliyelazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI) alipotembelea  wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam na wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Taasisi hiyo Dkt. Samuel Swai.
……………………………………………………………………………………………………………..
Na Ally Daud-Maelezo
Serikali chini ya Wizara ya Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto imeitaka Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI) kuhudumia wagonjwa haraka iwezekanavyo ili kuondoa msongamano wa wagonjwa hospitalini hapo na kuwaruhusu wakaendelee na shughuli za kujenga taifa.
Akizungumza hayo alipotembelea wagonjwa  MOI Waziri wa  Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliwataka watumishi wa taasisi hiyo kuwahudumia wagonjwa haraka iwezekanavyo ili kuwapa fursa ya kwenda kufanya shughuli za kimaendeleo kwa ajili ya taifa.
“Mnatakiwa kuhudumia wagonjwa kwa haraka na ufanisi mkubwa ili kuwasaidia watanzania kutotumia muda mwingi wakiwa hospitalina na badala yake wapone waende wakaendelee na shughuli zao za kujenga taifa kwa maendeleo ya Nchi yetu”alisema Mhe. Ummy
Aidha Mhe. Ummy ameongeza kuwa licha ya kuwa na changamoto zinazojitokeza hospitalini hapo Wizara ipo bega kwa began a Taasisi hiyo  kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa wananchi chini ya kitengo hiko ili kufikia malengo ya milenia.
“Nafahamu kama kuna changamoto zinazoikabili taasisi hii kama mlivyonieleza lakini tupo pamoja katika kuziondoa na nyinyi hakikisheni mnafanya kazi kwa bidii ili kuondoa  malalamiko ya wananchi na kuleta huduma bora na kwa wakati” alisisitiza Mhe. Ummy.
Mbali na hayo Mhe. Ummy ameitaka taasisi hiyo kurudisha huduma ya kufanya upasuaji kwa wagonjwa siku za jumamosi bila ya kukosa tena kwa haraka ili kupunguza mlundikano wa wagonjwa kwenye taasisi hiyo.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji MOI Dkt. Samuel Swai amesema kuwa wamepokea agizo hilo na wapo tayari kufanya kazi kwa bidii ili kuokoa maisha ya watanzania kwa haraka na ubora zaidi.
“Tupo tayari kutekeleza agizo la Mheshimiwa Waziri la kufanya kazi kwa bidii ili kuokoa maisha ya watanzania kwa haraka na ataona matokeo mazuri kuanzia leo hii” alisisitiza Dkt. Swai.

DC WA ILALA MH SOPHIA MJEMA AKABIDHIWA MSAADA WA MADAWATI KWA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO WENYE ASILI YA CHINA JIJINI DAR LEO

Muwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania,Gou Haodong akimkabidhi moja ya dawati kati ya 100 yaliyotolewa na Wafanyabiashara wa Karikoo wenye asili ya China ,kwa Mkuu wa Wa Wilaya ya Ilala,Mh Sophia Mjema mapema leo jijini Dar.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mh Sophia Mjema akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa madawati 200 kutoka kwa Wafanyabiashara wa Kariakoo wenye asili ya China leo jijini Dar,kwa ajili ya shule ya msingi Maghorofani iliyopo Gongolamboto,jijini Dar Es Salaam.Wafanyabiashara hao waliahidi kumkabidhi Mh.DC Mjema Madawati 200 lakini leo wamekabidhi nusu ya madawati hayo (100),huku mengine yakiendelea kutengenezwa.Shule hiyo ya Maghorofani ilikuwa na uhitaji wa madawati 525,yakapatikana madawati 250 na kupungukiwa madawati 275.
Muwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania,Gou Haodong akizungumza kwa ufupi mbele ya Waalimu,wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani),kabla ya kukabidhi madawati 100 yaliyotolewa na Wafanyabiashara wa Kariako wenye asili ya China jijini Dar,pichani kulia ni Mkuu wa Wa Wilaya ya Ilala,Mh Sophia Mjema. 
Baadhi ya Wanafunzi wa shule hiyo ya Maghorofani wakiwa wamekalia baadhi ya madawati yaliyotolewa na Wafanyabiashara wa Kariakoo wenye asili ya China jijini Dar. 
Wakiwa katika picha ya pamoja .PICHA NA MICHUZI JR.

MKUU WA MKOA WA SINGIDA AFUNGUA MAONYESHO YA NANE NANE KANDA YA KATI DODOMA

tat1 
Mkuu wa Mkoa wa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe (Kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Nane Nane katika uwanja wa maonyesho ya kilimo Nzuguni Mkoani Dod
tat2 
Viongozi wa Mkoa wa Dodoma na Singida wakitembelea baadhi ya vibanda vya maonyesho wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Nane Nane
tat4 
Mgeni rasmi alipotembelea banda la dawa za kilimo, uvuvi na ufugaji Farmer Centre and Farm base
tat5 
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya za Dodoma na Singida wakiongozwa na Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida Mathew Mtigumwe wakikagua eneo la maonyesho ya kilimo cha zao la zabibu
tat6 
Mgeni rasmi akisikiliza kwa kina maelezo juu ya matumizi ya matrekta kwa ajili ya kilimo
tat8 
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya za Dodoma na Singida wakiongozwa na Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida Mathew Mtigumwe wakikagua eneo la maonyesho ya mboga mboga
tat9 
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya za Dodoma na Singida wakiongozwa na Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida Mathew Mtigumwe wakikagua eneo la maonyesho ya bwawa la samaki lenye samaki aina ya perege, kambare na kamongo liloandaliwa na Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba
tat11 
Zoezi la kutembelea mabanda ya maonyesho likiwa linaendelea
………………………………………………………………………………………………………
Na Mathias Canal, Dodoma
Ufunguzi wa siku kuu ya wakulima Nane nane Kanda ya kati Dodoma mwaka 2016 umefanyika leo katika Uwanja wa Maonyesho ya kilimo Nzuguni Mkoani Dodoma huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni “Kilimo, Ufugaji na Uvuvi ni nguzo ya maendeleo, Kijana shiriki kikamilifu (Hapa Kazi Tu).
Maonyesho haya yanahusisha shughuli za wakulima, wafugaji wa mifugo, wafugaji wa nyuki, wavuvi, wanamazingira, wasindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na mifugo, wizara taasisi/makampuni ya umma, makampuni binafsi, mabenki, taasisi za umma na za binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Akizungumza katika ufunguzi huo Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe amesema kuwa sekta ya kilimo bado ni mhimili wa uchumi wa Tanzania kwa sababu inaajiri zaidi ya asilimia takribani 80 ya watanzania na kwa kuzingatia malengo ya maendeleo ya Taifa ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati unaotegemea viwanda hivyo kilimo kikiboreshwa viwanda vitapata malighafi ya uhakika na kuimarisha masoko kwa wakulima hivyo kuwepo na ajira ya kuaminika kwa vijana na watanzania kwa ujumla.
Rc Mtigumwe amesema kuwa wastani wa ukuaji wa sekta ya kilimo unabadilika mwaka hadi mwaka kutokana na kilimo kwa kiwango kikubwa kutegemea mvua ambazo zimekuwa zikinyesha kwa viwango na mtawanyiko unaotofautiana kila mwaka ambapo kwa mwaka 2010 sekta ya kilimo ilikuwa kwa asilimia 4 ikilinganishwa na asilimia 6.5 ya mwaka 2015.
“Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa kanda ya kati ina rasilimali ya maji yakutosha ya chini ya ardhi hivyo kuendelea kuitamka kama kanda kame hakuna usahihi wa jambo hilo ipo haja ya kuona kuwa rasilimali hiyo inapatikana kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji hivyo kupunguza kilimo cha kutegemea mvua” Alisema Mtigumwe
Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida kabla ya kuwahutubia wananchi waliojitokeza katika ufunguzi huo alitembelea baadhi ya mabanda ya maonesho na kuona shughuli mbalimbali za uzalishaji wa mazao, ufugaji, uvuvi, usindikaji na wauzaji wa zana na pembejeo za kilimo ambapo amejionea matokeo ya juhudi mbalimbali zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kuinua ukuaji wa sekta ya kilimo ambapo juhudi hizo zinajumuisha uzalishaji wa mbegu mbalimbali zinazostahimili hali ya hewa ya maeneo ya kanda ya kati.
“Natoa wito maalumu kwa wakulima, wafugaji, wavuvi, wajasiriamali na wadau wa sekta zingine kuhakikisha kuwa bidhaa zenu zinafikia ubora wa hali ya juu kuanzia shambani zinakozalishwa, zinakosindikwa na kuhifadhiwa na hadi kumfikia mlaji, ikumbukwe kwamba kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu kutawezesha bidhaa zetu kuhimili ushindani wa hapa nchini na nje ya nchi na kuuzwa kwa bei nzuri” Alisema Mtigumwe
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya waandaaji wa maonyesho ya Kilimo, Mifugo na sherehe za nane nane, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa hotuba ya Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Singida itakuwa ya mazingatio ili kurahisisha na kuendeleza kasi ya serikali ya awamu ya Tano kwa vitendo hususani katika kuakisi na kuwasaidia wananchi ambao ni wakulima na wafugaji kupata mbinu bora za kufuga na kulima kisasa ili kupata mazao kwa wingi.
Hata hivyo Dc Mtaturu amesema kuwa ana imani thabiti kuwa baada ya kumalizika kwa maonyesho hayo wakulima, wafugaji na wananchi washiriki watakuwa wamejifunza vyema mbinu bora za kukabiliana na changamoto za kilimo na ufugaji hivyo kujikita zaidi katika mbinu bora na za kisasa za kilimo na ufugaji pia.
Dc Mtaturu amesema kuwa shughuli kuu ya wakazi wa kanda ya kati inayoundwa na mikoa miwili ya Singida na Dodoma yenye jumla ya Wilaya kumi na mbili na Halmashauri 15 shughuli zao kuu ni kilimo na ufugaji.

WAZIRI MKUU ATOA SIKU MOJA KWA MANISPAA YA MOROGORO KUTANGAZA MAENEO KWA AJILI YA WAFANYABIASHARA WADOGO

war8 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku moja kwa uongozi wa Manispaa ya Morogoro kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo na kuyatangaza kesho.
“Mbali na kutenga maeneo pia nawaagiza muwasaidie wafanyabiashara hawa kuunda vikundi kulingana na aina ya biashara wanazozifanya ili kuwawezesha kupata mikopo kwa urahisi kutoka katika taasisi za fedha” alisema.
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo leo (Jumatano, Agosti 03, 2016) wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi Msamvu unaojengwa kwa ubia kati ya Manispaa ya Morogoro na Mfuko wa Pensheni wa LAPF.
Awamu ya kwanza ya mradi huo inatarajiwa kufunguliwa Agosti 12 mwaka huu utakuwa ni kituo cha mabasi cha kwanza cha kisasa Tanzania ambapo Waziri Mkuu amezitaka halmashauri zote zilizoko makao makuu ya mikoa nchini kuiga mfano huo.
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kulipongeza Baraza la Madiwani la Manispaa ya Morogoro na LAPF kwa kubuni mradi huo wa kisasa utawezesha abiria kupata taarifa ya basi lilipo na muda litakapowasili kituoni hapo hivyo kupunguza udanganyifu kutoka kwa mawakala wasiokuwa waaminifu.
Kwa upande wake Meneja wa mradi huo Stanley Mhapa alisema mradi huo umegharimu sh. bilioni 40 ambapo Manispaa inamiliki asilimia 40 ya hisa na mfuko wa LAPF unamiliki asilimia 60.
“Mafanikio ya mradi huu ni pamoja na kuiwezesha Manispaa kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka sh 350,000 kwa siku hadi kufikia sh. milioni 1.7 kwa siku,” alisema.
Mhapa alisema mradi huo utakapokamilika utatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na huduma za kibenki, vibanda vya biashara, sehemu za chakula, ofisi na sehemu ya mapumziko ya abiria na vibanda vya kukatia tiketi.

WAZIRI MKUU AWATAKA WAFUGAJI WAKUBWA KUJIANDAA KUFUGA KISASA

war1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe  Mary wakiteremka kuelekea eneo la kuchinjia ng’ombe katika kiwanda cha nyama Ngulu Hills Ranch kilichopo Morogoro wakati walipokitembelea kiwanda hicho Agosti 3, 2016. (Picha na  Ofisi ya Waziri Mkuu)
war2 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakikagua eneo la kuchinjia ng’ombe katika kiwanda cha nyama cha Nguru Hills Ranch cha Morogoro  Agosti 3, 2016.  Kushoto ni Mkurugenzi na Mshauri wa Kiwanda hicho, Danstan Mrutu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
war3 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakizingumza na Mkurugenzi na mshauri wa kiwanda cha nyama cha Ngulu Hills Ranch cha Morogoro , Dunstan Mrutu (kulia kwa Waziri mkuu) )  wakati walipokitembelea kiwanda hicho Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
war4 
Watoto na wananchi wa kijiji cha Majichumvi  wilayani Mvomero wakionyesha mabango wakati WaziriMkuu,Kassim Majaliwa aliposimama kijijini kwao kuwasikiliza Agosti 3, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
war5 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary  (kulia) wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pesheni wa LAPF, Eliud Sanga wakati alipokagua ujenzi wa stendi  mpya ya Msamvu Morogoro Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
war6 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua jengo la Stendi mpya ya mabasi la Msamvu mjini Morogoro Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
war7 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Mjini  Morogoro baada ya kukagua ujenzi wa stendi mpya ya Msamvu Agosti 3, 2016. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt.Stephene Kebwe na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF,Eliud Sanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
war8 
Awamu ya kwanza ya jengo la stendi mpya ya mabasi ya Msamvu mjini Morogoro iliyokamilika kwa asilimia 90. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliitembelea stendi hiyo na kuzungumza na wadau Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
war9 
Waziri mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bibi Halima Mwishehe alipouliza swali wakati Waziri Mkuu alipozungumza na Wananchi kwenye stendi mpya ya Msamvu Morogoro baada ya kukagua ujenzi wake Agosti 3, 2016.  Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
war10 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wafugaji wenye mifugo mingi nchini kujiweka tayari kwa ajili ya kuhamia kwenye maeneo yatakayotengwa na Serikali katika ranchi mbalimbali nchini ili waweze kufuga kisasa.
Pia aliwataka wafugaji hao kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu ya maeneo hayo ikiwemo ujenzi wa visima vya maji na majosho ili ufugaji wao uwe na tija.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Agosti 03, 2016) wakati alipotembelea kiwanda cha kusindika nyama cha Nguru Hills Ranch kilichoko wilayani Movomero.
Hata hivyo Waziri Mkuu alisema kitendo cha wafugaji hao kuhamia katika ranchi kitawezesha mifugo yao kuwa na ubora kwa sababu aina ya ufugaji wa sasa ya kutembeza mifugo umbali mrefu inasababisha ufugaji wao kuwa na tija ndogo.
Akizungumzia kuhusu uwepo wa kiwanda cha kuchakata nyama wilayani Mvomero Waziri Mkuu alisema kitamaliza mgogoro wa muda mrefu kati ya wakulima na wafugaji kwa kuwa wafugaji watapata fursa ya kuuza mifugo yao kiwandani hapo.
“Uwepo wa viwanda katika maeneo yetu utatuwezesha kupunguza matatizo tuliyonayo katika maeneo yetu ikiwemo suala la migogoro kati ya wafugaji na wakulima. Viwanda ndiyo vitakavyotuondoa kutoka katika uchumi wa chini hadi wa kati,” alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi na Mshauri wa kiwanda cha Nguru Hills Ranch, Dunstan Mrutu alisema kiwanda hicho chenye uwezo wa kuchinja ng’ombe 300, mbuzi na kondoo 1,500 kwa siku kinatarajiwa kufunguliwa mwezi Desemba mwaka huu.
Mkurugenzi huyo alisema takriban asilimia 80 ya nyama itafungashwa na kuuzwa nje ya nchi  hasa Uarabuni kwa sababu nyama ya mbuzi ya Tanzania imebainika kuwa na mvuto maalum katika nchi hizo.
“Mbali na uwekezaji huu wa kiwanda cha nyama pia tunatazamia kuwekeza katika mnyororo wa thamani kuanzia kusindika ngozi inayotoka kiwandani hadi kuzalisha viatu, mikanda na bidhaa zote za ngozi na kupunguza uagizaji wa bidhaa hizo kutoka nje ya nchi,” alisema.
Mrutu alisema nia yao ni kuitikia wito wa Rais Dk. John Magufuli wa kutaka viwanda vizalishe viatu nchini kuanzia vya majeshi na wananchi wote ambapo wamepanga kuanzia mwakani wataanza kuuza bidhaa hizo.
Aliongeza kuwa uwepo wa kiwanda hicho utatoa fursa kwa wafugaji na wakulima kuuza majani, mifugo na mazao ya chakula kama mtama, mahindi, ambapo tayari wameanza kuhamasisha jamii za wafugaji na wakulima wa Mvomero, Ngerengere na sehemu zinazozunguka eneo la kiwanda kuchangamkia fursa hiyo.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa wilaya ya Mvomero kufanya mapitio ya mashamba ili kujua wamiliki wake na kama hawajayaendeleza wachukue uamuzi wa haraka wa kuyatwaa na kuyarudisha mikononi mwa Serikali.
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo wakati akijibu ujumbe uliokuwa katika mabango yaliyobebwa na wananchi wa kijiji cha Maji ya Chumvi wilayani Mvomero waliosimamisha msafara wakati ukitokea kwenye kiwanda cha nyama.

Mama Kanumba azindua “Kanumba Star Search”

index 
Mshiriki Mkuu wa Shindano la Kanumba Star Search, Florence Mutegoa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya AM Arts Promotion pamoja na Mdhamini wa Shindano la “Kanumba Star Search” kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo tarehe 03.08.2016 Jijini Dar es Salaam,
………………………………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Mshiriki Mkuu wa Shindano la Kanumba Star Search, Florence Mutegoa (Mama Kanumba) amezindua shindano la kusaka vipaji vya waigizaji watakaoigiza filamu itakayoenzi maisha ya Marehemu Steven Kanumba.
Uzinduzi huo umefanywa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) ambapo Mshiriki Mkuu wa Shindano hilo ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kudhamini shindano hilo litakaloibua vipaji vipya vya uigizaji.
“Tunatambua thamani ya maigizo ndio sababu tumeamua kuanzisha shindano hili ili kuibua vipaji vilivyojificha, hivyo tunawakaribisha wananchi wote wenye uwezo wa kuigiza waje washiriki kwenye mashindano yetu pia tunaomba wadhamini kujitokeza zaidi ili watusaidie kufanikisha shindano hili”, alisema Mutegoa.
Mutegoa amefafanua kuwa shindano hilo limeandaliwa kwa ushirikiano wa Kampuni ya Kanumba the Great Film na Kampuni ya AM Arts Promotion ambapo hadi sasa shindano hilo lina mdhamini mmoja kutoka Kampuni ya simu za mkononi za KZG – Tanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya AM Arts Promotion, James Mwombeki amesema kuwa marehemu Kanumba alikuwa na mchango mkubwa katika kuitangaza nchi kimataifa pamoja na kuibua vipaji vya wasanii wa maigizo hivyo hatuna budi kumuenzi kwa kuiendeleza Sanaa ya uigizaji.
“Sisi kama AM Arts Promotion tumeamua kushirikiana kwa pamoja na Mama Kanumba kufanya shindano hili kwa nia ya kuendeleza tasnia ya filamu nchini kama vile marehemu Kanumba alivyokua akijitahidi kuwapa fursa ya uigizaji watu wa kila rika”, alisema Mwombeki.
Naye, Msanii wa filamu, Mayasa Mrisho amewasisitiza wananchi kushiriki kwa wingi kwenye mashindano hayo kwani Sanaa ya uigizaji ni njia mojawapo ya kujipatia kipato na kuinua maisha ya mtu binafsi na Taifa kwa ujumla.
Aidha, Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu za Mkononi za KZG – Tanzania, Raymond Kalikawe amesema kuwa wamekubali kuwa wadhamini wa shindano hilo kwa kuwa ukuzaji wa vipaji vya wasanii wa maigizo ni jambo muhimu pia amewaomba wadhamini wengine kujitokeza zaidi kusaidia shindano hilo.
Shindano hilo linatarajiwa kuanza mwezi Septemba mwaka huu, litaanzia Mikoa ya Kanda ya ziwa na baadae kuendelea katika Mikoa mingine.Washindi wataigiza filamu ya kumuenzi marehemu Kanumba itakayojulikana kama “Maisha ya Kanumba.

KITUO CHA TELEVISHENI CHA TV 1 KURUSHA MATANGAZO YA LIGI KUU SOKA YA UINGEREZA EPL

 Mkuu wa TV 1, Joseph Sayi (katikati),akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ,Kituo cha  Televisheni cha TV1 Tanzania kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti  13 mwaka huu. Kulia ni Meneja Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu na Meneja Masoko Startimes, kushoto ni Felix Awino 
 Meneja Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ,Kituo cha  Televisheni cha TV1 Tanzania kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti  13 mwaka huu. Kushoto ni Mkuu wa TV 1, Joseph Sayi na kulia ni Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey Abdallah.  
 Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey Abdallah (katikati), akizungumzia masuala ya mpira katika mkutano huo.
 Production Meneja wa TV 1, Mukhsin Khalfan Mambo akizungumza katika mkutano huo.
 Mkutano ukiendelea.
 Wanahabari wakiwa kazini.
 Taswira ya meza kuu katika mkutano huo.
 Mchambuzi wa michezo, Ally Kashushu (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
 Mmiliki wa Blog ya Kajuna Son, Cathibert Kajuna (kulia), akiuliza swali katika mkutano huo.
 Wapiga picha za habari wakiwa kazini.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TV 1 wakiwa wakifuatilia matukio mbalimbali ya mkutano.
Mkutano ukiendelea.
………………………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
 
KITUO cha  Televisheni cha TV1 Tanzania kinatarajia kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti  13 mwaka huu.
 
Ligi kuu soka nchini Uingereza ndio ligi maarufu zaidi duniani na hii ni kutokana na kushirikisha timu kongwe zenye ubora na mashabiki dunia nzima ikiundwa na timu maarufu duniani kama vile Manchester United,Liverpool, Arsenal pamoja na Chelsea.
 
TV1 Tanzania ndio kitakuwa kituo pekee cha runinga hapa nchini kupewa haki za kurusha matangazo haya yatakayokujia moja kwa moja yaani Live yakihusisha pia uchambuzi wa ligi hiyo ambapo kutakuwa na vipindi vya kabla ya mechi na baada ya mechi husika.
 
Kwa upande Mkuu wa Kituo cha TV 1 Tanzania  Joseph Sayi alisema  hii ni fursa kubwa kwa wadau wa soka hapa nchini kuishuhudia ligi hiyo moja kwa moja, Mkuu wa kitengo cha masoko wa TV1 Gillian Rugumamu alisema lengo ni kuwapelekea watazamaji wao wa Tanzania ligi kuu England ambayo ni ligi inayopendwa na kufuatiliwa na Watanzania.
 
Baadhi ya watangazaji na wachambuzi watakaokuwa wakishiriki katika urushaji wa matangazo  hayo na uchambuzi ni Ally Kashushu na Dkt. Leakey Abdallah ambaye ni mchambuzi mwenye uzoefu wa miaka 20 kwenye tasnia ya michezo husasani uchambuzi.
 
Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey alisema watanzania wategemee uhondo wa ligi hiyo kutokana na uwepo wa wachezaji nyota na makocha mahiri kama Antonio Conte,Arsene Wenger,Jurgen Klopp na makocha hasimu Jose Mourinho wa Manchester United na Pep Guardiola wa Manchester City.
 
 
Tv1 Tanzania ni kituo cha runinga kilianza mwaka 2013 ambapo  kilianza kurusha matangazo yake rasmi  Januari 2014 ambapo kimekuwa kikiandaa na kurushwa vipindi vyenye ubora wa hali ya juu ambapo TV 1 inapatikana kupitia ving’amuzi vya Startimes namba 103,Azam 119 na Ting 36.
 

Filamu mpya ya “The Foundation” by J.Plus

indexWatakushangaa sana pale utakapo zungumzia Tasnia ya filamu za Action Tanzania bila kumtaja Mwasisi wa Filamu hizo Jimmy Mponda  maarufu kama J.Plus ambaye ndiye mmiliki wa ‘Mzimuni Theatre Arts’ aliyewahi kushikiria ubora wake miaka 5 kwa filamu yake ya “Misukosuko” yaani 2005-2010.
Kwa madai yake J.Plus, amesema kuwa baada ya kufanya vizuri kwa muda mrefu miaka kadhaa iliyopita, kisha kukaa kimya ili kuwaachia nafasi wasanii wengine waweze kuonesha uwezo wao katika Tasnia hio, kwa sasa amedai ni wakati wake tena.
Kwa maana hiyo J.Plus ameamua kurejea tena ulingoni ili kuitetea tasnia hiyo coz ameona kama ina legea legea na huenda  ikapoteza ubora kwa mashabiki wa Filamu za Action Tanzania.
Baada ya siku chache, J.Plus anategemea kuachia Filamu yake mpya inayoitwa “The Foundation” ambayo ndani yake amecheza pia Inspector Seba. Akipiga stori na mwandishi wetu J.Plus alimaliza kwa kusema,
“Kwanza Nashukuru Mungu kwa uzima, ukimya wangu haukuwa wa nia mbaya bali ni katika harakati za kuboresha kazi zangu, na kuangalia nini niwaletee mashabiki wangu ili walizike. Ujio huu utakuwa katika kasi kubwa maana lengo ni kutoa kitu juu ya kitu, Nitaanza na Filamu ya “The Foundation” ambayo nimecheza na Inspector Seba ‘I hope’ itarudisha heshima ya Action Movies Tanzania. Ombi langu kwa watanzania ni mapokezi mema kutoka kwao ushauri na maoni pia ni muhimu kwenye ufanisi wa kazi zetu asante”

HALMASHAURI YA MJI WA KIBAHA YADHAMIRIA KUOKOA MIL.516.792

index 
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
HALMASHAURI ya Mji wa Kibaha ,itaokoa sh.mil.516.792 katika mwaka wa fedha 2016/2017,zilizokuwa zikipotea katika makusanyo ya ushuru wa mchanga,machinjio na stend kutokana na udanganyifu uliokuwa ukifanywa na baadhi ya mawakala.
Awali halmashauri hiyo ilikuwa ikitumia mawakala kukusanya ushuru wa vyanzo hivyo vya mapato na kusababisha upotevu huo wa fedha .
Akitoa ufafanuzi juu ya suala hilo,mjini Kibaha,mwenyekiti wa halmashauri ya Mji huo ,Leonard Mloe ,alisema aligundua kuwepo kwa udanganyifu huo hivyo kuamua kuagiza makundi ya madiwani kwenda kufuatilia.
“Baada ya kuwaagiza madiwani hao kufanya uchunguzi ndipo kulipobainika kweli kulikuwa na upotevu mkubwa wa fedha ambazo zilikuwa zikifaidisha mawakala kuliko halmashauri”alisema Mloe.
Mloe alielezea kuwa kati ya fedha hizo zitakazookolewa ni pamoja na mil.335.392 zilizokuwa zikipotea kwa mwaka kwenye ushuru wa mchanga.
Alisema katika ushuru wa mchanga walikuwa wakipokea mil.264.608 kwa mwaka ambapo baada ya kutuma madiwani waligundua watakuwa wakipata mil.600 kwa mwaka.
“Katika ushuru wa stend ,halmashauri ilikuwa ikipokea makusanyo ya sh.mil.320 kwa mwaka baada ya uchunguzi tumebaini tunapata mil.458 kwa kipindi hicho na kuokoa mil 138 zilizokuwa zikipotea”alisema Mloe.
Mloe alisema upande wa machinjio walipata mil.25 kwenye tathmini imebainika fedha halisi zinazopatikana ni mil.68.400 hivyo wameokoa mil 43.400.
Aidha mwenyekiti huyo,alieleza vyanzo vyote,vya halmashauri hiyo, vibadilike hesabu zake kuanzia sasa kwani wanahitaji mapato yanayoendana na chanzo cha mapato.
Mloe alisema kuanzia sasa halmashauri hiyo imeanza kutumia vibarua watakaokuwa wanakusanya ushuru wa vyanzo hivyo kwa usimamizi wa watendaji wa halmashauri badala ya mawakala ambao wamebainika sio waaminifu.
“Vibarua hawa watatumiwa ndani ya miezi mitatu na baada ya hapo watakuwa wakibadilishwa ili kuondokana na tatizo la kupotea kwa fedha”alisisitiza Mloe.
Akingumzia kuhusiana na makusanyo ya mwaka 2015/2016 ,makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Robert Machumbe,alisema halmashauri ilikisia kukusanya zaidi ya bil.31.836.942 kutokana na vyanzo vyake vya mapato mbalimbali.
Alielezea kuwa halmashauri kwa robo ya nne inayoishia mwezi juni 2016 imekusanya bil.7.370.215.637 na kufanya jumla ya mapato yaliyokwisha kukusanywa kwa kipindi cha robo zote nne kuanzia Julai-Juni 2016 kuwa zaidi ya bil.25.938 sawa na asilimia 81 ya makisio ya kipindi hicho.
Machumbe alisema halmashauri ya Mji huo imekisia kutumia zaidi ya bil.31.836  kwa lengo la kutoa huduma kwa wananchi wa mji huo
Alieleza katika utekelezaji wa shughuli zake kwa robo ya nne iliyoishia juni 2016 imetumia bil.5.950.420 na kufanya jumla ya matumizi kwa julai/juni  mwaka huu kufikia bil.21.614.164 sawa na asilimia 67 ya makisio.

POLISI KUBORESHA VITUO VYAKE VYA AFYA.

po1 
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki akizungumza na Washiriki wa Mkutano wa kutathmini mradi wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaotekelezwa na Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi na tano hapa nchini  kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la JSI-AIDS Free tawi la Tanzania.Mkutano huo wa siku tatu unafanyika mkoani Dodoma.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
po2
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki akizungumza na Washiriki wa Mkutano wa kutathmini mradi wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaotekelezwa na Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi na tano hapa nchini  kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la JSI-AIDS Free tawi la Tanzania.Mkutano huo wa siku tatu unafanyika mkoani Dodoma.Kulia ni Mganga mkuu wa Polisi Dk.Janda Lushina na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Lazaro Mambosasa (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi) po3 
Baadhi ya Maofisa wa Polisi ambao ni Washiriki wa Mkutano wa kutathmini mradi wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu ndani ya Jeshi la Polisi wakifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo mkoani Dodoma.Mradi huo unaotekelezwa na Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi na tano hapa nchini  kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la JSI-AIDS Free tawi la Tanzania. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi ……………………………………………………………………………………………………………….
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Dodoma
Jeshi la Polisi nchini litaendelea kuboresha vituo vyake vya afya ili kuwawezesha Askari kupata huduma zilizo bora jambo ambalo litawawezesha kufanya kazi wakiwa na afya pamoja na morali katika kupambana na uhalifu nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki Mkoani Dodoma wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa  kutathmini mradi wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaotekelezwa na Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi na tano hapa nchini  kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la JSI-AIDS Free tawi la Tanzania.
Kaniki alizitaja juhudi zinazoendelea kuchukuliwa kuwa ni pamoja na kuboresha majengo, kutoa mafunzo kwa watendaji pamoja na kuhakikisha kuwa hospitali za Polisi zinakuwa na vifaa bora kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa na Wizara ya Afya .
Aidha alitoa wito kwa Shirika la JSI-AIDS Free kuongeza wigo wa huduma zake katika vituo vngine ambavyo havijafikiwa na mradi huo hapa nchini ili kuhakikisha kuwa kila mahali palipo na kituo cha Afya cha Polisi kunakuwepo na mradi huo ambao umesaidia sana askari na watumiaji wengine wa huduma hizo.
Kwa upande wake Mwakilishi mkazi wa Shirika hilo kwa upande wa Tanzania Dk.Beati Mboya alisema lengo la mkutano huo ni kufanya tathmini ili kubaini mafanikio na changamoto zinazovikabili vituo vinavyotekeleza mradi huo ilikuzipatia ufumbuzi.
Alisema wanatarajia kufanya tathmini hiyo kila baada ya miezi mitatu ili kuhakikisha hakuna ucheleweshaji katika kutoa huduma baada ya kubaini changamoto na kuzifanyia kazi kwa haraka.
Naye Kamanda wa Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Paul Kasabago alisema kikosi hicho kitaendelea kutoa huduma zilizobora ili kuimarisha afya za Askari na familia zao kote nchini licha ya kukabiliwa na upungufu wa wahudumu wa Afya.
 
 

Kilele Maadhimisho Siku ya vijana Kitaifa kufanyika Mkoani Simiyu.

 mavi1 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Anthony Mavunde akiongea na waandishi wa Habari leo Jijijni Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani inayoadhimishwa Kitaifa tarehe 14/10/2016,Mkoani Simiyu ambapo vijana wametakiwa kutumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa na Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajiara na Wenye Ulemavu.
mavu2 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Anthony Mavunde akisisitiza umuhimu wa wa wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia jitihada za Serikali kuwawezesha Vijana kiuchumi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajiara na Wenye Ulemavu.
mav3 
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Anthony Mavunde na waandishi wa Habari leo Jijijni Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani itakayoadhimishwa Kitaifa tarehe 14/10/2016,Mkoani Simiyu.
(Picha na Frank Mvungi-Maelezo
………………………………………………………………………………………………………………..
Frank Mvungi-Maelezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi siku ya Kilele cha maadhimisho ya siku ya Vijana Kitaifa yatakayofanyika Mkoani Simiyu Oktoba 14 mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Antony Mavunde wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.
Mhe Mavunde amebainisha kuwa Kauli mbiu ya Siku ya Vijana mwaka huu ni “Tokomeza umasikini kwa uzalishaji endelevu na matumizi yenye tija”.
Akifafanua kuhusu kauli mbiu hiyo Mhe. Mavunde amesema lengo la kauli mbiu hii ni kuzihimiza nchi wanachama wa umoja wa mataifa kushirikisha kikamilifu Vijana katika shughuli za uzalishaji na kuhakikisha kuwa panakuwepo na matumizi sahihi ya rasilimali za nchi kama vile ardhi,maji,madini na Nishati ili kufikia shabaha ya kuwa na maendeleo endelevu ifikapo 20130.
Akizungumzia maadhimisho hayo Kitaifa Mhe . Mavunde amesema kuwa vijana watapata fursa ya kushiriki shughuli mbalimbali kama makongamano,matamasha,michezo,maonnyesho ya Kazi za Vijana,Shughuli za kujitolea na maandamano ya amani.
“Tanzania tutasherekea siku ya Vijana Duniani Kitaifa kuanzia tarehe 8/10/2016 na kilele kitakuwa tarehe 14/10/2016 Mkoani Simiyu ambapo Sherehe hii itaenda sambamba na Maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Wiki ya Vijana Kitaifa na kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2016.” Alisisitiza Mhe. Mavunde.
Wazo la kuwa na siku ya Vijana Duniani lilitolewa katika Mkutano wa Vijana wa Kimataifa mwaka 1991 Mjini Vienna Australia kwa madhumuni ya kutafuta njia ya kuchangisha fedha za kusaidia mifuko ya Taifa ya Vijana ambapo mwaka 2000 nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Tanzania zilianza kuadhimisha siku ya Vijana Duniani kulingana na mazingira yake kwa kuzingatia kauli mbiu ambayo huandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Wananchi Zanzibar watakiwa kulipia huduma ya maji

tank 
Na Rahma Khamis Maelezo -Zanzibar
Wananchi wa Zanzibar wametakiwa kulipia huduma ya maji kwa wakati ili kuweza kupata huduma hiyo kwa ufanisi zaidi na kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza.
Wito huo umetolewa na Afisa Uhusiano wa  Mamlaka ya Maji Zanzibar  (ZAWA) Zahour Suleiman  Ofisini kwake  Msikiti Mabuluu Mjini Zanzibar wakati akitoa maelezo kuhusiana na ulipaji wa huduma ya maji.
Amesema maji ni moja ya huduma muhimu katika maisha ya wananchi  hivyo ni muhimu  kuhakikisha yanapatikana muda wote  na suala la  kulipia huduma hiyo ili iwe endelevu  ni jambo la msingi.
Afisa huyo amefahamisha kuwa badhi ya wananchi wamekuwa na  mwamko mdogo katika kulipia huduma ya maji na  kusababisha  Mamlaka kukosa uwezo wa kutoa huduma hiyo kwa ufanisi.
Aidha amesema kuwa kwa sasa huduma hiyo inaelekea kuzidiwa kutokana na kukuwa kwa harakati za kimaendeleo hasa kwa matumizi ya kilimo ambacho kinatumia maji mengi  ukilinganisha na matumizi ya majumbani.
Afisa huyo amefahamisha kuwa wameanzisha  utaratibu  wa kupita katika maeneo kwa lengo la kutoa elimu kuhusiana na  umuhimu wa kulipia maji na  wale watakaoshindwa kuufahamu mpango huo Mamlaka huwapa onyo na baadae kusitishwa kupata huduma.
Sambamba na hayo Zahour amewashauri wanajamii kufuata sheria bila ya kushurutishwa kwa kulipia maji kwa wakati ili kuipa uwezo Mmlaka ya maji kutekeleza wajibu wake wa kuwapatia  wananchi huduma hiyo kama kawaida.

MHE SPIKA NDUGAI ALIPOKUTANA NA MHE MBOWE

mbow1 
Kiongozi wa Kambi rasmi  ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe akisalimiana na Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.Spika wa Bunge amerejea nchini hivi karibuni kutoka nchini India alipokwenda kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.
mbow2 
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe aliyemtembelea Nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.
mbow3 
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsikiliza Kiongozi wa Kambi Rasmi ya upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe aliyemtembelea Nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.
mbow4 
Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe  akiagana  na Spika wa Bunge  Mhe. Job Ndugai alipomtembelea Nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Bunge)

Utumishi yapokea vijana wa kujitolea kutoka Japani

SONY DSC 
Serikali ya Tanzania inadhamini mchango mkubwa unaotolewa na Serikali ya Japani kupitia Shirika  la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA)   ambalo limekuwa likishirikiana na Serikali katika kazi mbalimbali  za maendeleo hapa nchini.
Naibu Katibu Mkuu , Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Bi. Susan Mlawi  alisema hayo mapema leo katika ukumbi wa mikutano wa Utumishi wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha watalaam wa kujitolea kutoka Japani.
“Tangu mwaka 1967 hadi sasa zaidi ya vijana wa Japani 1,500  wameshafika  nchini na kufanya  kazi za kujitolea katika maeneo mbalimbali hata katika mazingira magumu” Bi. Mlawi alisema na kuongeza kuwa  kunufaika huko kwa Tanzania kunatokana na ushirikano baina ya Serikali ya Japani na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano huo  na Japani  ili kuendelea kunufaika  hasa katika suala zima la kujengewa uwezo katika sekta ya elimu na maendeleo ya jamii , sekta ambazo pia  zimepewa kipaumbele  katika Awamu ya Pili ya  Mpango wa Serikali wa  miaka Mitano (5) wa Maendeleo inayoanza mwaka 2016/17 na kumalizika mwaka 2021 /22.
Kwa upande wake,  mwakilishi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo Japani (JICA) nchini  Tanzania  Bw. Toshio Nagase  alisema wataalam hao ambao wako sita (6)  watafanyakazi ya kujitolea katika sekta ya elimu kwa miaka miwili na kwa kipindi hicho wanaamini Watanzania watakuwa wamenufaika na ujuzi toka kwa vijana hao.
Alisema watajitolea kufundisha masomo ya Sayansi, Hisabati, Masuala ya Maendeleo ya Jamii  na Michezo  katika shule za Sekondari , Shule za Msingi  na Ofisi za  Maendeleo ya Jamii katika Mikoa ya Morogoro, Pwani , Mtwara , Dodoma na Dar es salaam.

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UTURUKI, MWAKILISHI UNHCR NCHINI

MGU1 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin Eralp masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MGU2 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kulia) akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Viongozi hao walijadili masuala mbalimbali ya kuwahudumia Wakimbizi nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MGU3 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin Eralp alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MGU4 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (katikati) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (kushoto) kuhusu masuala mbalimbali ya kuwahudumia Wakimbizi nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi wa Wizara hiyo, Harrison Mseke. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MGU5 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kulia) akimkaribisha ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin Eralp kwa ajili ya kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MGU6 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kulia) akimkaribisha ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya.Viongozi hao walijadiliana masuala mbalimbali jinsi ya kuwahudumia Wakimbizi nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

NHIF YASHIRIKI MAONESHO YA 8/8 KITAIFA NGONGO MKOANI LINDI KWA UPIMAJI WA AFYA NA UTOAJI ELIMU KWA UMMA

PAU1
Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya mkoa wa Lindi Fortunata Raymond akiwapa maelezo ya mpango wa KIKOA unaowawezesha wanavikundi,wajasiriamali kupata huduma za matibabu kuchangia mara moja kwa mwaka (Shs 76,800),kwa wananchi waliotembelea katika banda la mfuko lililopo kwenye viwanja vya Ngongo mjini Lind
PAU2 
Timu ya wataalamu wa mfuko wa taifa wa bima ya afya wakiendelea na zoezi la upimaji wa afya kwenye magonjwa yasiyoambukiza kwa wananchi waliofika kwenye banda la mfuko ngongo mjini Lindi.
PAU3 
Ofisa matekelezo wa bima ya afya Salvatory Okum akitoa maelezo ya faida na umuhimu wa uchangiaji wa huduma za matibabu kupitia mfuko wa afya ya jamii (CHF) kwa wananchi waliotembelea banda la mfuko ambapo elimu kwa umma ni moja ya huduma zinazotolewa.

CHUO CHA UONGOZI WA FEDHA ZANZIBAR CHAANZISHA MPANGO WA KUWAPELEKA WANAFUNZI WAKE KUFANYA MAZOEZI YA VITENDO KATIKA TAASISI ZA KIJAMII

UK1 
Baadhi ya wanafunzi  wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar wakifuatilia ufungaji wa mafunzo elekezi  yaliyofanyika katika Chuo chao Chwaka Mkoa Kusini Unguja.
UK2 
Mratibu wa mafunzo elekezi ya wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar Said Mohd Khamis akieleza lengo la Chuo kuanzisha mpango wa wanafunzi kufanya mazoezi ya vitendo katika taasisi za kijamii.
UK3 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mauwa Makame Rajab akifunga mafunzo elekezi ya wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar watakaoshiriki mazoezi ya vitendo katika vikundi vya kijamii (kushoto) Mkurugenzi wa Vyama vya Ushirika Zanzibar Khamis Simba na (kulia) Kaimu Mkuu wa Chuo Dkt. Iddi.
…………………………………………………………………………………….
Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar
CHUO cha Uongozi wa Fedha Zanzibar (ZIFA) kimeanzisha mpango wa kuwapeleka wanafunzi wa Chuo hicho kufanya mazoezi ya vitendo katika vikundi vya Kijamii (SACCOS) kuanzia mwaka huu.
Uamuzi huo unafuatia muongozo uliotolewa na Baraza la Chuo baada ya kubaini kuwa wanafunzi wengi wanapokuwa katika mazoezi ya vitendo katika Mawizara, Maidara na Taasisi za Umma wanakaa maofisini bila ya kufanya kazi yoyote na kutofaidika na mazoezi yao.
Jumla ya wanafunzi 130 wa mwaka wa pili shahada ya kwanza wanaosoma fani ya Uhasibu, Manunuzi na Tehama wataanza mazoezi ya vitendo katika SACCOS za Unguja na Pemba baada ya kupatiwa mafunzo elekezi ya siku tatu yaliyotolewa na Idara ya Vyama vya Ushirika kwa kushirikiana na ZIFA.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo,
Mhadhiri wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Maalim Said Mohd Khamis alisema lengo la mpango huo ni kuwawezesha wanafunzi kutoa elimu kwa jamii baada ya masomo yao.
Amesema vyama vingi vya ushirika vinakabiliwa na matatizo hasa katika masuala ya uhasibu, manunuzi na matumizi ya Tehama hivyo wanafunzi wao watakwenda kusaidia katika kutoa elimu kwa wanachama wa vikundi hivyo.
‘’Wanafunzi wetu watakwenda kufundisha matumizi ya Teknolojia ya kisasa, utaratibu mzuri wa manunuzi na masuala ya uhasibu”, alisisitiza Maalim Said.
Ameongeza kuwa mtazamo wa Chuo ni kutoa huduma na fursa zinazopatikana chuoni hapo kwa jamii ili kuisaidia Serikali katika juhudi zake za kuwapunguzia wananchi hali ngumu ya maisha.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mauwa Makame Rajab amewaeleza wanafunzi hao kuwa baadhi ya SACCOS wanachama wake hawana taaluma kubwa katika masuala ya ushirika hivyo mchango wao utasaidia sana katika kuviimarisha vikundi hivyo.
Amewataka vijana hao kuitumia elimu waliyonayo na fursa waliyopata ya kufanyakazi katika vikundi vya kijamii vijijini kujiajiri kwa kuanzisha SACCOS ama kuongoza ziliopo katika kukabiliana na tatizo kubwa la ajira liliopo.
Amewashauri wanafunzi hao kuwa mabalozi wazuri katika sehemu watakazokwenda kupinga vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia vinavyozidi kuongozeka katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba.
Aidha amevishauri vyuo vyengine viliopo Zanzibar na Tanzania kwa jumla kuiga mfano ulioonyeshwa na ZIFA kuwapeleka wanafunzi wao kufanya mazoezi ya vitendo katika vikundi vya kijamii kusaidia masuala mbali mbali ikiwemo sheria, uongozi demokrasia ndani ya vikundi vyao.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar amesema wameupokea mpango wa Chuo kwenda kusaidia vikundi vya ushirika vijijini kwa moyo safi na ameahidi watatoa mchango mkubwa.
Amesema wanauchukulia mpango huo kama ni majaribio kwao na watajitahidi kuweka mazingira mazuri na kuwa mfano wa kuigwa na wanafunzi wenzao watakaofuata hapo baadae.

MTOTO ATOA MSAADA WA MADAWATI DODOMA

DON1 
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christina Mndeme (kushoto) akimshukuru mtoto Aisha Mshantu kwa Msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5.2 aliyoyatoa katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo Kata ya Mbabala Manispaa ya Dodoma. PICHA KWA HISANI YA OFISI YA MKURUGENZI WA MANISPAA
DON2 
Mtoto Aisha Mshantu (kulia )akimkabidhi madawati 50  yenye thamani ya shilingi milioni 5.2 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christina Mndeme aliyoyatoa katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo Kata ya Mbabala Manispaa ya Dodoma. PICHA KWA HISANI YA OFISI YA MKURUGENZI WA MANISPAA
DON3 
 Mtoto Aisha Mshantu na wazazi wake Mzee Mshantu (wa kwanza kulia) na Bi Rehema (wa pili kulia) wakiwa amekaa katika madawati aliyoyatoa mtoto huyo kama msaada  katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo Kata ya Mbabala Manispaa ya Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christina Mndeme. PICHA KWA HISANI YA OFISI YA MKURUGENZI WA MANISPAA

PPF KATIKA MAONYESHO YA NANENANE LINDI

ZA1 
Afisa   uhusiano mwandamizi  wa  mfuko wa Pensheni  wa PPF  Janet  Ezekiel akitoa  maelezo  kwa  mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi shughuli zinazofanya  na mfuko  ikiwemo faida ya  kujiunga  na   mfuko wa wote Scheme wakati  alipokuwa  anatembelea  banda la  mfuko huyo jana
ZA2 
Mfuko wa  Pensheni  wa PPF umeshiriki   maonesho ya  nane nane  yanayofanyika kitaifa Viwanja vya  Ngongo  Manispaa  ya Lindi   ambayo  yamefunguliwa  na  waziri  wa Nishati na  Madini Sospeter Muhongo  kwa  niaba ya  Makamu  wa rais Samia  Suluhu  yenye   kauli mbinu KILIMO MIFUNGO NA UVUVI  NI NGUZO YA  MAENDELEO  VIJANA SHIRIKI KIKAMILIFU HAPA KAZI TU. Kupitia  fursa hiyo  ya  maonyesho  hayo PPF  inakutana na wadau  mbalimbali  kueleza  huduma zinazotolewa   na shirika hilo  ikiwemo  WOTE SCHEME  mfumo  wa  maalumu  wa  kuchangia unazihusisha  sekta  isiyo  rasmi pamoja  na ule  mfumo  wa ziada  kwa sekta iliyo rasmi

No comments:

Post a Comment