Pages

Tuesday, August 30, 2016

WAZIRI MKUU APOKEA MILIONI 50 ZA UKARABATI NA UJENZI WA SEKONFARI YA LINDI

Waandishi wa habari waliohudhuria katika tukio la NSSF kumkabidhi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa hundi ya sh. milioni 50 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Lindi iliyoungua . Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jjini Dar es salaam Agosti 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni 50 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Shule ya Sokondari ya Lindi iliyoungua moto. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Kwaziri Mkuu jijini Dar es salaam Agosti 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wazri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza badaa ya kupokea hundi ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Lindi ambayo iliungua moto. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kanyarara, Wapili kulia ni Mkurugenzi wa manispaa ya Lindi, Jomaary Satura na wapili kushoto ni Meya wa Manispaa ya Lindi, Mohamed Lihumbo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Meya wa manispaa ya Lindi, Mohamed Lihumbo akizungumza baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kukabidhiwa hundi ya Shilingi milioni 50 kwa ajili ukarabati na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Lindi iliyoungua Moto . Makabidhiano ya hundi hiyo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Agosti 30, 2016. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kanyarara na wapili kulia ni Mkurugenzi wa manispaa ya Lindi, Jomaary Satura.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

DKT. SHEIN AFANYA UTEUZI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dkt. Ali Mohamed Shein

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee, ACP Sida Mohammed Himid ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ anayeshughulikia Idara maalum za SMZ.

Ndugu Hassan Khatib Hassan ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto anayeshughulikia masuala ya Wazee, vijana, wanawake na Watoto.

Dkt. Ali Salim Ali ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi mmoja katika Wizara ya Afya.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 30 Agosti, 2016 huku kwa Bw. Mohammed Kheir Mtumwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kuanzia tarehe 28 Agosti, 2016.

No comments:

Post a Comment