Pages

Monday, August 1, 2016

Nibu Waziri Mh. Anastazia Wambura akagua eneo la ujenzi wa mageti ya kieletroniki katika Uwanja wa Taifa Leo


WU1 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura eneo eneo la ujenzi wa mageti ya kieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Agosti 1, 2016 Jijini Dar es Salaam.
WU2 
Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw.Julius Mgaya (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura na Katibu Mkuu Wizara ya hiyo Prof Elisante Ole Gabriel kuhusu ujenzi wa mageti ya kieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Agosti 1, 2016  Jijini Dar es Salaam.

MAJALIWA AFUNGUA MAONYESHO YA NANENANE MOROROGORO

NAN1 
Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akisikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva wakati alipotembelea Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Monyesho ya Wakulima Nane  mjini Morogoro Agosti 1, 2016,    Kushoto ni mkewe Mary. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAN2 
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na Mkewe Mary (kulia kwake)wakitazama kilimo cha mbogamboga kwa mtindo wa kilimo kichuguu  wakati walipotembelea banda la Chuo Kikuucha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwenye maonyeshoya Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAN3 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama viatu vilivyotengenezwa katika gereza la Karanga  mkoani Kilimanjaro wakati alipotembelea  banda la Magereza katika  maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoroo Agosti 1, 2016, kulia ni  Mratibu wa Magereza wa maonyesho hayo na Mkuu wa Gereza la  Mtego wa Simba, Oman Msekwa. (Picha  na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAN4 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary (Kulia kwake) wakatazama bwawa la samaki  na banda la kufugia  bata  wakati alipotembelea banda la Magereza katika monyesho ya  wakulima Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016. (Picha na Ofisi ya waziri Mkuu)
NAN5 
Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa na Mkewe Mary wakitazama mboga zilizokaushwa na mtambo wa kukaushia mboga hizo  katika  katika maonyesho ya wakulima Nanene nane  mjini Morogoro Agosti 1, 2016. (Picha na Ofisi a waziri Mkuu)
NAN6 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizundua Banda la Maonyesho la wilaya ya  Temeke  kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016. Kushoto ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAN7 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizundua Banda la Maonyesho la wilaya ya  Temeke  kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016. Kulia kwake ni mkewe Mary  na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam , Paul Makonda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
NAN8 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama bidha mbalimbali  zinazotokana na zao la mronge zikiwema, dawa, mafuta na sabuni wakati alipoembelea meza ya Bibi Salome Kaiza   (kulia) kwenye banda la wilaya ya Tameke katika  maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro, Agosti, 1, 2016.  Kulia kwake ni Mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAN9 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama matikiti maji wakati walipotembelea meza ya Bwana Diocresty Theonesy kwenye banda la wilaya ya Temeke katika maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agost 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAN11 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakipokezana  tikiti maji wakiwa kwenye meza ya Bwana  Diocresty Theonesy kwenye banda la Wilaya ya Temeke katika Maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agost 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAN12 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakikagua mtama uliopandwa kwenye eneo la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agost 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

JPM amaliza mgogoro wa makazi Magomeni Kota

index 
Na Jonas Kamaleki, MAELEZO
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemaliza mgogoro wa makazi wa Magomeni Kota uliodumu kwa kipindi kirefu.
Hayo yamesbainishwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi wakati akiongea na Kamati ya Mgogoro wa Makazi ya Magomeni Kota mbele ya waandishi wa habari.
“Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefuta hati na mikataba yote inayohusiana na ardhi ya yaliyokuwa makazi ya Magomeni Kota, Dar es Salaam”,alisema Lukuvi.
Kwa mujibu wa Lukuvi Rais ameondoa umiliki wa eneo hilo toka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kumilikisha Serikali Kuu ambayo ndiyo itakayosimamia ujenzi wa nyumba 644 ambazo zitauzwa kwa bei nafuu kwa waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota.
“Tutajenga nyumba 644 na kuwauzia kwa bei ya jengo na siyo ya ardhi ili kuwapeni unafuu katika kununua,”alisema Lukuvi huku akishangiliwa na baadhi ya wakazi wa Magomeni.
Aidha, Lukuvi amesema kuwa anampongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kumaliza mgogoro huu ambao umedumu kwa muda mrefu na kuongeza kuwa ameagiza  timu ya wataalamu wa Wizara kupima na kuchora michoro kwa ajili ya ujenzi.
Lukuvi amesema katika eneo hilo zitajengwa nyumba za heshima ambazo kila moja itakuwa na vyumba vitatu ili kukidhi mahitaji ya kifamilia kwani watu hawa wamekaa kwa miaka takribani 50 hadi wameshapata wajukuu. Ameongeza kuwa kila mmiliki wa nyumba hiyo atapewa hati yake hata kama nyumba hiyo itakuwa kwenye ghorofa.
Lukuvi amesema kuwa Rais ameagiza maeneo kama ya Magomeni Kota katika mikoa ishirini ya Tanzania Bara nayo yatakuwa katika mfumo huo wa Magomeni. Kwa mujibu wa Lukuvi wazee ambao wanakaa kwenye nyumba kama hizo sehemu nyingine wasiondolewe kwani hao walikuwa watumishi wa umma hivyo Rais amesema wasibughudhiwe.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Mgogoro wa Makazi Magomeni Kota, George Abel ameshukur Mhe Rais Magufuli na Wazir Lukuvi kwa kutatua mgogoro huo ambao anadai umewasumbua sana.
Ameahidi kutoa ushirikiana kwa Serikali pindi suala la ujenzi litakapokuwa linaendelea ili kuhakikishaujenzi unaenda haraka.
Naye Wakili ambaye alikuwa akiendesha kesi hiyo kabla ya Mhe. Rais kuingilia kati, Mhe. Twaha Tasilima ameonyesha kuridhishwa na utendaji wa Rais Magufuli.
“Rais Dkt Magufuli na Mhe. Waziri Lukuvi ni watu wa vitendo na si maneno na kweli wanawajali wanyonge, nawashukuru sana,”alisema Tasilima.
Uamuzi wa kurudisha eneo hilo kwenye Serikali Kuu umetolewa na Rais Magufuli tarehe 10/7/ 2016.

WAZIRI MKUU AITAKA WIZARA KUWEKA MIKAKATI YA KUENDELEZA UVUVI KATIKA KINA KIREFU CHA BAHARI

MAJI1 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuweka mikakati endelevu ya kuwawezesha wananchi kuvua katika maji ya kina kirefu cha bahari kwa kutumia meli kubwa na za kisasa ili Taifa liweze kunufaika na rasilimali hiyo ambayo imekuwa ikichukuliwa na wavuvi wenye vyombo vya kisasa kutoka nje ya nchi.
Aidha, amezitaka halmashauri zote nchini ziweke mikakati na mipango ya kuifanya mito na maziwa mbalimbali nchini kuwa na uvuvi endelevu kwa kufuatilia kwa karibu shughuli za wavuvi na kuwaadhibu wote watakaovua kinyume na sheria.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Agosti 01, 2016) wakati akifungua maadhimisho ya 23 ya sherehe za maonesho ya wakulima Kanda ya Mashariki katika Uwanja wa Mwalimu J.K Nyerere yanayofanyika katika mkoa wa Morogoro ambapo amesema bado nchi haijaweza kutumia rasilimali hiyo kikamilifu.
Amesema halmashauri zinatakiwa zihamasishe vijana kuunda vikundi vya kuanzisha miradi ya kufuga samaki katika maeneo yao na wewezeshwe kupata teknolojia ya ufugaji huo.
Akizungumzia vikundi vya wajasiariamali wanaovua katika maeneo ya bahari na maziwa alishauri waelimishwe kuhusu namna ya kupata mikopo ya kununulia zana bora za kisasa za uvuvi ili shughuli zao ziwe na tija.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema wakulima wanatakiwa  kuzingatia matumizi ya kanuni bora za kilimo ikiwemo matumizi sahihi ya zana za kisasa, pembejeo na viuatilifu vilivyopendekezwa na wataalam ili kufanikisha mapinduzi ya kilimo kuelekea kilimo cha biashara.
Akizungumzia kuhusu suala la usindikaji alisema wakati anatembelea mabanda mbalimbali alipata fursa ya kuona teknolojia zinazoweza kutumiwa na wakulima, wafugaji na wavuvi katika kuongeza uzalishaji bora wenye tija.
Amesema amefurahi kuona wakulima, wafugaji na wafanyabiashara wa mazao, pembejeo na zana za kilimo wana ari kubwa ya kushiriki katika kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo ili kwenda sambamba na kasi ya Serikali ya kuifanya nchi kujitosheleza kwa chakula na kuendeleza uchumi wa viwanda.
“Naamini kuwa pamoja na lengo la kujitosheleza kwa chakula, wakulima, wafugaji na wavuvi wataongeza ari ya uzalishaji kwa kushirikiana na sekta za umma na binafsi katika kuvipatia viwanda vyetu malighafi na kuongeza thamani ya mazao,” alisema.
Kufuatia hatua hiyo Waziri Mkuu aliziagiza halmashauri zote kuhamasisha uanzishaji na uendelezaji wa viwanda vidogo vya kusindika mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kushirikisha taasisi za umma na binafsi, mashirika na vikundi vya ujasiriamali katika maeneo yao.
Akizungumzia namna Serikali ilivyojipanga kutatua changamoto ya migogoro baina ya wafugaji na wakulima Waziri Mkuu alisema wafugaji wenye mifugo mingi watahamishiwa katika vitalu vinavyomilikiwa na ranchi za Taifa na wenye mifugo michache watatengewa maeneo katika vijiji.
Awali Waziri Mkuu alitembelea baadhi ya mabanda na maeneo ya vipando vya mazao mbali mbali yaliyoko katika viwanja hivyo ambapo alisema ameridhishwa na juhudi zilizofanyika katika maandalizi ya maonesho ya mwaka huu ikiwa ni pamoja na uendelezaji wa uwanja huo.
“Napenda kutoa pongezi za dhati kwa kujenga miundombinu na nyumba za kudumu za kufanyia maonesho. Aidha, natoa shukrani za pekee kwa Halmashauri zetu, Mashirika yetu ya Umma na binafsi; na watu binafsi ambao wamejenga na wanaendelea kujenga majengo mazuri na ya kudumu,” alisema.
Pia alizindua jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Temeke na kusema kuwa uboreshaji wa viwanja hivyo unaonesha jinsi wadau wote katika sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi na ushirika wanavyotambua umuhimu wa maonesho hayo kama njia ya kuongeza maarifa na kumuenzi mkulima, mfugaji na mvuvi kwa kutambua mchango wao katika uchumi wa Taifa.
Kauli mbiu ya maonyesho hayo kwa mwaka huu ni kilimo, mifugo na uvuvi ni nguzo ya maendeleo: vijana shiriki kikamilifu   (“HAPA KAZI TU”)         

Mrema akutana na Madereva Bodaboda wa Kinondoni.

MRE1Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (katikati)akisitiza jambo kwa madereva wa pikipiki toka Wilaya ya kinondoni wakati alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwenekiti wa Waendesha Bodaboda na Bajaj wilaya ya Kinondoni Bw. Almano Mdede na kushoto ni Katibu wake Bw. George Mbwale.
MRE2Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema ( Mwenye Kofia Katikati) akisisitiza jambo kwa madereva wa pikipiki toka Wilaya ya kinondoni wakati alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
MRE3 
Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema wakati akizungumza na  madereva wa pikipiki toka Wilaya ya kinondoni wakati alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam
MRE4Mwenyekiti wa Madereva wa pikpiki Wilaya ya Kinondoni Bw. Almano Mdede akifafanua jambo kwa madereva pikipiki wa Wilaya ya Kinondoni wa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (katikati) alipowatembelea madereva hao na kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni Katibu wa Madereva Pikipiki Wilaya hiyo Bw. George Mbwale.
MRE5 
Baadhi ya madereva Pikipiki wa Wilaya ya Kinondoni wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (hayupo pichani) alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.    Picha na Eliphace Marwa.
Picha zote na Eliphace Marwa -Maelezo
……………………………………………………………………………………………………

MRI, CT-Scan Zapiga Mzigo Saa 24 Muhimbili, Wagonjwa 41,101 Wapimwa

MRI1 
Mgonjwa akiwa katika mashine ya MRI LEO katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Pembeni ya mgonjwa ni Mtaalamu wa Mionzi, Medard Mallya akimsaidia mgonjwa kukaa vizuri kwenye mashine hiyo.
MRI2 
Mtaalamu wa Mionzi, Medard Mallya akichukua picha LEO wakati mgonjwa akipimwa mgongo kwenye mashine ya MRI.
MRI3 
Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali Ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Flora Lwakatare akifuatilia mgonjwa anavyochukuliwa vipimo LEO mchana katika hospitali hiyo.
…………………………………………………………………………………………..
Na John Stephen, MNH
 Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inaendelea kutoa huduma bora hasa ya vipimo kwa wagonjwa mbalimbali na kufanikiwa kupima wagonjwa 41,101 katika mwaka 2015/2016 kutoka wagonjwa 32,010 waliopimwa mwaka wa fedha 2014/2015.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Buberwa Aligaesha imeeleza kwamba mashine zinafanya kazi vizuri na kwamba hakuna mashine mbovu hadi kusababisha wagonjwa kukosa huduma za vipimo.
“Hospitali inahakikisha kila mgonjwa anayehitaji vipimo anapata na kwa gharama nafuu. Kama mashine ilisimama kufanya kazi tangu Januari hadu Juni, 2016 ni kwa muda wa kati ya siku moja hadi mbili kupisha matengenezo kinga,” amesema Bwana Aligaesha katika taarifa yake aliyoitoa LEO kwa vyombo vya habari.

RAIS DKT MAGUFULI AHITIMISHA ZIARA YA SIKU NNE MIKOA YA SINGIDA, TABORA NA SHINYANGA

GEI1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wananchi wa Katoro na Buseresere wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
GEI2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Chato na Naibu Waziri wa Nishati na Mdini Mhe. Dkt Medard Kalemani baada ya kuhutubia wananchi wa Katoro na Buseresere wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
GEI3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na madiwani na viongozi wa Katoro na Buseresere baada ya kuhutubia wananchi wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
GEI4 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsabahi mtoto Shabani Kalemani (miezi 8) na mama yake Asha  Simon baada ya kuhutubia wananchi wa Katoro na Buseresere wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
GEI5 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa kwa furaha kijijini Bwanga  wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
GEI6 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia wananchi  kijijini Bwanga  wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016

UGONJWA WA KIPINDUPINDU BADO UPO JIJINI DAR ES SALAAM

KIP 
Hussein Makame-MAELEZO
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa kipindupindu bado upo jijini Dar es Salaam baada ya wagonjwa wapya wanne kugundulika katika Manispaa ya Temeke jijini hapa.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya magonjwa ya milipuko na magonjwa mengine nchini.
Alisema mwenendo wa ugonjwa huo kuanzia Julai 2016 ulikuwa wa kuridhisha kwani wagonjwa walipungua hadi kufikia 173 kwa mwezi bila kifo kutoka wagonjwa 555 walioripotiwa mwezi Juni 2016 na vifo vya watu saba.
“Mkoa wa Morogoro ni mkoa pekee umekuwa ukiripoti wagonjwa wa kipindupindu kwa kipindi kirefu hadi sasa.Vilivile mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa haujaripoti wagonjwa tangu Mei 19, 2016 ila wiki iliyopita siku ya Jumamosi waliripotiwa  wagonjwa wapya wanne katika wilaya ya Temeke” alisema Waziri Ummy.
Alisema katika kipindi cha wiki iliyopita idadi ya wagonjwa wa kipindupindu imeongezeka hadi wagonjwa 41 kutoka wagonjwa 30 wa wiki iliyotangulia ingawa hakuna aliyepoteza maisha.
“Hivyo kuna dalili za kuwepo tena ongezeko la ugonjwa wa kipindupindu jambo ambalo linafanyiwa kazi kwa haraka sana na Wizara yangu” alisema.
Alifafanua kuwa Wizara yake imeelekeza nguvu kubwa kuendelea kuudhibiti ugonjwa huo hapa Dar es Salaam na huko mkoani Morogoro na inafuatilia ugonjwa wa kuharisha katika mikoa mingine ili kubaini kama kuna mgonjwa yeyote wa kipindupindu na kuudhibiti mapema.
Aliongeza kuwa kikosi kazi cha Taifa kinaainisha maeneo makuu ya kuyafanyia kazi mkoani Morogoro ambapo yatajumuisha elimu kwa jamii, uvumbuzi wa namna gani ya kupatikana maji safi na salama na matumizi vya vyoo bora.
Mbali na kueleza mikakati hiyo, Waziri Ummy alisisitiza mikoa na halmashauri zote nchini kuendelea kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu ugonjwa huo ili kuweza kuudhibiti endapo utabainika kuwepo sehemu yoyote nchini.
Alisema timu ya wataalamu kutoka ngazi ya Taifa ilifanya tathmini mnamo Juni, 2016 na kubaini upungufu katika utoaji taarifa katika baadhi ya mikoa na hivyo Wizara yake inashirikiana na TAMISEMI kuhakikisha inafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa.
Ugonjwa wa kipindupindu ulianza nchini tarehe 15 Agost mwaka 2015 na hadi kufikia tarehe 31 Julai, 2016 watu 22,375 wameugua na kati yao wagonjwa 345 walipoteza maisha.

Watu 14 wafariki kwa ugonjwa unaosababishwa na sumukuvu

index 
Hussein Makame-MAELEZO
Watu 14 wamefariki dunia katika wilaya za Chemba mkoani Dodoma na Kiteto mkoani Manyara kutokana na ugonjwa unaojulikana kitaalamu kama ‘Aflatoxicosis’ unaosababishwa na sumu kuvu (Aflatoxins) kwenye nafaka iliyoharibika.
Hayo yamesema na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya magonjwa ya milipuko na magonjwa mengine leo jijini Dar es Salaam.
“Ugonjwa uliosababishwa na sumu kuvu (Aflatoxins) uliripotiwa kwa mara ya kwanza tarehe 13 Juni, 2016 katika wilaya za Chemba mkoani Dodoma na baadaye mkoani Manyara katika wilaya ya Kiteteo” alisema Waziri Ummy na kuongeza kuwa:
“Wagonjwa walikuwa na dalili za kuumwa tumbo, kuharisha, kutapika, tumbo kuvimba na kuwa manjano sehemu mbalimbali za mwili ambayo inaashiria kuathirika kwa ini”
Alisema mbali na vifo hivyo, hadi kufikia Julai 31 mwaka huu wagonjwa 54 waliripotiwa kuugua ugonjwa hu huku wagonjwa wanne wakilazwa kutokana na kuugua.
“Hadi kufikia tarehe 31, Juni 2016 kulikuwa na wagonjwa 54 na watu 14 walipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.Aidha katika wiki iliyopita aliripotiwa mgonjwa mmoja mpya kutoka wilaya ya Kondoa” alisema Waziri Ummy na kufafanua kuwa:
“Jumla ya wagonjwa waliolazwa wodini ni wanne kati yao mmoja yupo Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na watatu wapo katika Hospitali ya Kondoa”
Waziri Ummy alitaja wilaya zilizoripoti wagonjwa hao na idadi ya wagonjwa kuwa ni wilaya ya Chemba wagonjwa 38, Kondoa wagonjwa tisa , Kiteto wagonjwa watatu, Chamwino wagonjwa wawili na Dodoma Manispaa  mgonjwa mmoja.
“Vijiji vilivyoathirika zaidi na ugonjwa huo ni kutoka wilaya ya Chemba ambavyo ni Kinkima, Itolwa, Mwailanje na katika wilaya ya Kondoa ni kijijini cha Ubembeni” alisema Waziri Ummy.
Hivyo, aliitoa hofu familia iliyopoteza watu wanne katika kijiji cha Mwaikuzabe na kusema vifo hivyo havihusiani na uchawi au kuwekewa sumu bali ni chakula cha siku ile kilithibitika kwamba kilikuwa na sumukuvu.
Kufuatia athari hizo Serikali itafanya uchunguzi wa kina katika wilaya kumi  za Chemba, Kondoa, Chamwino na Kiteto na wilaya nyingine za mikoa ya Sindida, Dodoma na Manyara zinazopakana na wilaya hizo.
Alisema uchunguzi huo unalenga kubaini hali ya usalama wa vyakula vinavyotumiwa na jamii ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo na kuwaathiri wananchi wengi zaidi wanaoishi katika wilaya hizo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taifa wa Afya wa Wizara hiyo Dkt. Fausta Mosha alisema wizara imeandaa  vipepereshi vyenye maelekezo yanayotoa elimu juu ya kijikinga kwa kuandaa chakula kuanzia hatua ya uvunaji shambani hadi wakati wa kula.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Otilia Gowelle alisema njia bora ya kupambana na ugonjwa huo ni kuukinga kwa kuhakikisha sumu kuvu haizalishwi kutoka kwenye nafaka.
Akifafanua kuhusu udhibiti, Waziri Ummy alisema wanashirikiana na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kutoa elimu kwa wananchi juu ya njia sahihi ya uhifadhi na uandaaji wa chakula utakaosaidia kupunguza kiasi cha sumukuvu kwa nafaka ambazo hazijaharibika sana.
“Njia hizi ni pamoja na kuhifadhi nafaka zilizokauka vizuri na kuchambua nafaka zilizoharibika (zilizooza, kuvunjika, zilizobadilika rangi), kukoboa mahindi kabla ya kusaga au kuacha kutumia nafaka zitakazoonekana kuharibika rangi” alisema.
Waziri Ummy alisisitiza Serikali kuendelea kuimarisha mikakati ya kitaifa ya kupunguza uchafuzi wa sumukuvu katika vyakula, ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo wa kupima sumukuvu katika damu na choo kidogo miongoni mwa taasisi za ndani ya nchi.
Inaelezwa kuwa ugojwa wa‘Aflatoxicosis’unaosababishwa na sumu kuvu (Aflatoxins) kwenye nafaka uliwahi kutokea nchini Kenya mwaka 2004 na kusababisha vifo vya zaida ya watu 100 huku wengine 200 waliathirika.

Viwanda vya TBL Group vyashinda tuzo ya Kimataifa ya Usalama na Afya

TUO1Wafanyakazi wakiwa wanaburudika wakisheherekea kupata tuzo na NOSA
TUO3Wafanyakazi wakipongezana kutokana na mafanikio ya kampuni ya kushinda tuzo ya NOSA
TUO5 
Wakipata burudani ya muziki kusheherekea mafanikio hayo
………………………………………………………………………………………….
Viwanda cha kutengeneza vinywaji vya TBL Dar es Salaam na TBL Mbeya vimepata tuzo ya utekelezaji kanuni za Usalama na Afya  mahali pa kazi kutoka shirikisho la kimataifa la kusimamia masuala ya usalama mahali pa kazi lenye makao makuu nchini Afrika ya Kusini  lijulikanalo kama National Occupational Safety Association (NOSA).
Tuzo hii ambayo viwanda vya TBL Group vya Mbeya,Mwanza na Dar es Salaam vimeipata mfululizo imekuwa ikitolewa kutokana na kukidhi viwango vya kimataifa vya utekelezaji kanuni za afya,usafi na usalama mahali pa kazi ambapo wataalamu kutoka taasisi ya NOSA wamekuwa wakija nchini kufanya ukaguzi kwenye viwanda vyake na vimekuwa vikipata alama ya  kufanya vizuri kwenye kiwango cha nyota nne na nyota tano.
Akiongea wakati wa hafla ya kusherehekea tuzo  hiyo mwishoni iliyofanyika  katika kiwanda cha Ilala,Meneja wa kiwanda cha TBL cha Dar es Salaam,Calvin Martin alisema kuwa kampuni inajivunia kuendelea kufanya vizuri katika suala la Usalama na Afya mahali pa kazi ambapo mwaka huu imeshinda kwa kiwango cha nyota tano ambacho ni kiwango cha ufanisi cha hali ya juu
“Tunayo sababu ya kusherehekea kupata tuzo hii tena katika kipindi cha mwaka huu kwa kuwa  inadhihirisha kuwa kampuni inajali suala la usalama na afya kwa wafanyakazi na hili ni jambo la msingi kwa kuwa usalama na Afya ukikosekana mazingira yetu ya kufanyia kazi yatakuwa hatarini na  ufanisi hautakuwepo”.Alisema.
Aliwapongeza wafanyakazi wote kwa jinsi wanavyoshiriki kuzingatia kanuni na miongozo inayowekwa na kampuni hali  ambayo inachangia kuleta mafanikio na kuvifanya viwanda vilivyopo chini ya TBL Group kuongoza kufanya vizuri na kuwa mfano wa kuigwa na viwanda vingine  nchini.
Kwa upande wake Meneja wa Usalama na Afya kwa TBL,Renatus Nyanda,amesema kuwa kampuni imeweka mikakati kuhakikisha viwanda vyake vyote vinatekeleza kanuni za Afya na Usalama kwa viwango vya kimataifa na ndio maana inaendelea kupata tuzo hizi za Usalama kuazia zinazotolewa na taasisi za hapa nchini na nje ya nchi “Leo tunaposheherekea kupata tuzo hii wenzetu wa Mbeya nao wanasheherekea na ukaguzi unaendelea katika viwanda vingine”.Alisema
Alitoa wito kwa wafanyakazi wote wa viwanda vya TBL Group kuendelea kutekeleza miongozo mbalimbali ya utendaji wenye kuleta ufanisi ili waendelee kuwa kioo hususani katika suala hili la usalama na Afya kwa kuwa linawagusa moja kwa moja katika maisha yao ya kila siku.

KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI NA BALOZI WA ITALIA WAKIKAGUA RAMANI YA BARABARA

BEN1 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga kushoto  akimuonyesha Balozi wa Italia Bwana Roberto Mengoni baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia.
BEN2 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga  akimuonyesha Balozi wa Italia Bwana Roberto Mengoni( kulia) baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia, kushoto ni Mkurugenzi wa barabara nchini Injinia Ven Ndiyamukama
BEN3 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga  akimuonyesha Balozi wa Italia Bwana Roberto Mengoni( kulia) baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia, kushoto ni Mkurugenzi wa barabara nchini Injinia Ven Ndiyamukama
BEN4 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga  akimuonyesha Balozi wa Italia Bwana Roberto Mengoni( kulia) baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia, kushoto ni Mkurugenzi wa barabara nchini Injinia Ven Ndiyamukama

SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA GGM KUTOA UAMUZI

ggm1 
Afisa Madini wa Geita, Fabian Mshai (aliyesimama) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (katikati), namna ambavyo Ofisi yake ilitekeleza maagizo aliyoyatoa kwao kuhusu malalamiko ya baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) likiwemo suala la mipasuko ya nyumba zao. Wengine pichani ni maafisa kutoka Wizarani.
ggm2 
Baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza na uongozi wa Mkoa wa Geita na wawakilishi wa wananchi kuhusu ripoti ya wataalam wa mipasuko kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) juu ya chanzo cha mipasuko ya baadhi ya nyumba na majengo yaliyo karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).
ggm3 
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani kuhusu uamuzi wa Serikali kufuatia malalamiko mbalimbali yaliyotolewa na baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kuwa shughuli zinazoendeshwa na Mgodi huo zinawaathiri kwa namna mbalimbali.
ggm4 
Mbunge wa Viti Maalum Geita (CHADEMA), Upendo Peneza, akizungumza wakati wa kikao baina ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani na wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani husika kuhusu malalamiko mbalimbali kutoka kwa baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwamba shughuli zinazofanywa na Mgodi huo zinawaathiri kwa namna mbalimbali.
ggm5 
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (katikati) akitoa maagizo mbalimbali kwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kuhusu malalamiko ya baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na Mgodi huo kuwa shughuli zinazofanywa na Mgodi zinawaathiri kwa namna mbalimbali. Waliokaa Kulia ni viongozi kutoka GGM. Kushoto ni baadhi ya wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani na Maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini.
…………………………………………………………………………………………………..
Na Veronica Simba – GEITA
Serikali imetoa siku 30 kwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kuwalipa fidia wananchi wanaoishi ndani ya eneo la leseni ya Mgodi huo au kuwaruhusu rasmi waendelee kuishi humo na kufanya shughuli za kiuchumi.
Sambamba na agizo hilo, pia Serikali imeupa Mgodi huo siku 14 kuziba Tuta lililopasuka ambalo huzuia maji machafu kutoka Mgodini yasiende katika makazi ya wananchi.  
Aidha, kufuatia taarifa iliyowasilishwa na timu ya wataalam wa mitetemo kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), baada ya kukamilisha kazi waliyopewa kutafiti chanzo cha mipasuko ya baadhi ya nyumba za wananchi na majengo mbalimbali yaliyo jirani na Mgodi wa GGM, Serikali imeagiza timu hiyo kufanya tathmini maalum ya idadi ya waathirika.
Iliagizwa kazi hiyo ifanyike kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, Kitengo cha Maafa na Kitengo cha Mazingira pamoja na uongozi kuanzia ngazi za vijiji mpaka madiwani na wabunge husika kwa muda wa siku Saba tu kuanzia tarehe 29 mwezi huu na kuiwasilisha serikalini ili hatua stahiki zichukuliwe.
Maagizo hayo yalitolewa hivi karibuni mjini Geita na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani katika kikao chake kilichomshirikisha Mkuu wa Mkoa wa Geita na wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani.
Dkt Kalemani alisema kuwa maagizo hayo ni kufuatia maelekezo aliyoyatoa mapema mwezi Februari mwaka huu alipotembelea mkoani humo na kusikiliza kero za wananchi wa vitongoji vya Katoma na Nyamalembo. Alisema maagizo hayo yasipotekelezwa ipasavyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa, chini ya sheria ya madini na sheria nyingine za nchi.
Akifafanua zaidi kuhusu masuala hayo yaliyosababisha Serikali kufikia hatua husika, Naibu Waziri alisema kuwa mwezi Februari alipotembelea Geita, wananchi walieleza kero kubwa walizokuwa nazo kuwa ni baadhi ya nyumba zao kupasuka kiasi cha kutoweza kukalika na nyingine kukalika lakini zimeharibika kutokana na ulipuaji wa baruti (blasting) wa Mgodi wa GGM.
Malalamiko mengine yalihusu wananchi ambao wanaendelea kuwa na makazi ndani ya eneo la leseni ya GGM, ambayo ina ukubwa wa kilomita za mraba 196. 7 ambao walikuwa wanadai fidia ili waondoke katika eneo husika au waendelee kubaki na kufanya shughuli zao za maendeleo.
Pia, baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na Mgodi na hasa maeneo ya chini ya Mgodi, walilalamikia maji machafu ambayo yalikuwa yanakingwa na tuta ambalo lilikuwa limebomoka na kuruhusu maji kutiririka kuelekea kwenye makazi yao na hivyo kuwepo uwezekano wa kuathiri afya zao. Walitaka hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia mtiririko huo wa maji.
Alisema kuwa, baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili, kwa suala la mipasuko, aliunda timu ya wataalam wa Serikali kutoka GST na kuiagiza kufanya utafiti wa kisayansi ili kubaini chanzo cha mipasuko husika kwa kushirikiana na wawakilishi wa wananchi wa maeneo hayo.
Timu hiyo ilikamilisha kazi hiyo na kukabidhi taarifa yake kwa Serikali mwezi Julai mwaka huu ambapo ilibainisha vyanzo vikuu viwili vya mipasuko hiyo kuwa ni udhaifu wa majengo yaliyoathirika lakini pia milipuko inayofanywa na GGM hasa ya miaka ya nyuma hususan kuanzia mwaka 2007 hadi 2010 ambayo ilikuwa na kipimo cha juu cha mitetemo kinachofikia 57.
Kuhusu wananchi wanaoishi kwenye eneo la leseni, Dkt Kalemani alisema kuwa alimwagiza Afisa Madini wa Geita kuwaandikia GGM ili wathibitishe kwa maandishi kati ya kuwaondoa wananchi wale kwa kuwafidia kama eneo hilo lilivyo kwenye leseni yao au kuwaruhusu waendelee kuishi na kufanya shughuli za maendeleo, jambo ambalo Mgodi haukutekeleza badala yake walisema wananchi hao ni wavamizi.
Aidha, kuhusu suala la Tuta, Naibu Waziri alieleza kuwa, aliagiza lizibwe mara moja ili kuepusha madhara ambayo yangeweza kujitokeza kama maji yangeendelea kutiririka kuelekea kwenye makazi ya wananchi, ambalo pia halijatekelezwa hadi sasa.
“Ni kutokana na hali hiyo, sasa Serikali tumeona tutoe maagizo ya mwisho ili yatekelezwe na yasipotekelezwa, hatua kali za kisheria zitachukuliwa.”
Naibu Waziri alisema kuwa Serikali haina nia mbaya kwa Mgodi husika isipokuwa ni wajibu wa Serikali kuhakikisha pia sheria zinafuatwa ili pande zote zipate haki stahiki.
“Tunapenda sana wawekezaji muwekeze kwa sababu ndiyo mnatupa ajira, mnalipa mirabaha na kodi lakini lazima tuzingatie sheria.”
Dkt Kalemani alizitaka Mamlaka zinazohusika kusimamia zoezi hilo kikamilifu.

MPANGO WA CHANDARUA KLINIKI WAWAFIKIA MWANZA



Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha, akimkabidhi Chandarua kwa mtoto Mwasiti Abdallah(miezi 9) aliyebebwa na Mama yake Geni Elias,kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupambana na Malaria ujulikanaao kama Chandarua Kliniki,uliofanyika mkoani Mwanza kwa ushirikiano wa serikali na USAID.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha,akimkabidhi chandarua mama mjamzito mkazi wa Mkolani jijini Mwanza Elizabeth Edward, kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupambana na Malaria iitwayo Chandarua Kliniki ulioganyika mkoani Mwanza.mradi huo wa chandarua kliniki unatekelezwa na USAID chini ya mradi wa Vectorworks wakishirikiana na serikali.

Msanii wa muziki wa taarabu Khadija Kopa, akitumbuiza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupambana Malaria ujulikanao kama chandarua kliniki unaotekelezwa na USAID chini ya mradi wa Vectorworks wakishirikiana na serikali, uzinduzi ulifanyika jijini
Mwanza jana

Msanii wa muziki wa taarabu Khadija Kopa, akitumbuiza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupambana Malaria ujulikanao kama chandarua kliniki unaotekelezwa na USAID chini ya mradi wa Vectorworks wakishirikiana na serikali, uzinduzi ulifanyika jijini Mwanza jana.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mo Music, akitumbuiza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupambana na Malaria Chandarua Kliniki unaotekelezwa na USAID chini ya mradi wa Vectorworks wakishirikiana na serikali uliofanyika jijini Mwanza jana.
Mpango wa Chandarua Kliniki wagawa vyandarua mkoani Mwanza.
Malaria yapungua mkoani mwanza
Mpango wa ugawaji wa vyandarua unaojulikana kama CHANDARUA KILINIKI ulioanzishwa na serikali ya Marekani kupitia shirika la USAID umewafikia wananchi wa Mwanza mwishoni mwa wiki ikiwa lengo lake ni kuendeleza dhamira yake yakupambana na malaria nchini hasa kwa Mama wajawazito na watoto.
Akitoa taarifa, wakati wa utambulisho wa mpango na ugawaji vyandarua kupitia kliniki ya wajawazito na watoto,Mratibu wa Malaria mkoa wa Mwanza Dk Saula Baichumila alisema Jumla ya wagonjwa 235 wa Malaria katika Mkoa wa Mwanza wamepoteza maisha kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu ambapo vifo 121 sawa na asilimia 51.5 ni vya watoto chini ya miaka mitano.
“Kutokana na vifo hivyo halmashauri ya Sengerema inaongoza kwa asilimia 27.6, Magu 20.4, Ukerwe 14.5, Nyamagana 11.9, Misungwi 11.1, Kwimba 8.5, Buchosa 3.4 na Ilemela 2.6,” alisema Dk Baichumila
Alisema mkoa umeendelea kupambana na ugonjwa huo kwa kushirikiana wadau mbalimbali ambapo kumekuwa na matokeo mazuri kwa ugonjwa huo kupungua hasa toka waliposhirikiana na USAID kupitia mpango wa CHANDARUA KLININKI mkoani Mwanza hadi sasa jumla ya vyandarua 142,360 tayari vimesambazwa kupitia vituo vya kutolea huduma za afya mkoani hapo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Marry Onesmo, alisema maambukizi ya ugonjwa wa Malaria mkoani hapo yamepungua kutoka asilimia 19.1 ya mwaka 2011/12 hadi kufikia asilimia 15.1 mwaka2015/16.
Alisema lengo la mpango huo ni kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano vinavyosababishwa na malaria.Alisema takwimu za kitaifa za mwaka 2012 zinaonyesha kuwa kila vizazi hai 1000, watoto 54 hupoteza maisha huku malaria ikiongoza kuchangia vifo hivyo, huku kila vizazi hai 100,000 wajawazito 432 hupoteza maisha wakati wa kujifungua.
Mpango wa chandarua kliniki unatekelezwa na USAID chini ya mradi wa Vectorworks ambao ni mradi wa miaka mitano 2014-2019 ukiwa na dhumuni la kuongeza upatikanaji na matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu vya muda mrefu kwa kushirikikiana na serikali ambapo wamejiweke lengo kuwa hadi kufikia mwaka 2016 kitaifa iwe imefikia asilimia 6 na mwaka 2020 iwe asilimia 1 kutoka asilimia 9 ya sasa.

MBUNGE WA KIBAHA VIJIJINI AKABIDHI MADAWATI 537 NA VITABU KWA UONGOZI WA HALMASHAURI

kibah1 
Baadhi ya walimu,madiwani, watendaji wa serikali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa halfa fupi ya ugawaji wa madawati pamoja na vitabu sherehe zilizofanyika kwenye shule ya sekondari Kilinaga langa. kibh2 
Mbunge wa jimbo la Kibaha vijijini Hamoud Juma wa kulia akimkabidhi madawati 537  Mwenyekiti wa halmashauri ya Kibaha vijijini Mansouri Kisebengo katika sherehe ya makabidhiano iliyofanyika katika shule ya sekondari kilanga langa(PICHA ZOTE  NA VICTOR MASANGU)
………………………………………………………………………………………..
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA  
WANAFUNZI wa shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya Kibaha Vijijini  Mkoa wa Pwani waliokuwa wanakabiliwa na chanagamoto ya uhaba wa madawati na viti na kusababisha baadhi yao kuwa tabia ya utoro kwa sasa wameanza kunufaika na agizo la Rais Dr.John Magufuli la kutaka wanafunzi wote nchini kuhakikisha wanasoma wakiwa wamekaa kwenye madawati.
Agizo hilo la Rais limetekelezwa  na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud  Jumaa kupitia kupitia fedha ambazo zimepatikana kutokana na kubana matumizi yasiyo ya lazima katika ofisi yake kwa lengo la kuweza kusaidia katika kuboresha sekta ya elimu.
Akikabidhi jumla ya  madawati 537 Mbunge wa Jimbo hilo kwa uongozi wa halmashauri ya kibaha vijijini katika halfa fupi zilizofanyika katika shule ya sekondari kilangalanga iliyopo Mlandizi, amesema kwamba ametoa  madawati hao pamoja na vitabu kwa lengo la kuweza kupunguza kero  na kuondokana na adha  ambayo walikuwa wanaipata wanafunzi wa jimbo lake katika siku za nyuma.
Kwa upande wake Afisa elimu katika halmashauri ya kibaha vijijini Coskansia Mafuru amebainisha kwamba awali kabla ya agizo la Rais walikuwa wana upungufu wa madawati 1923 kwa shule za msingi, hivyo msaada huo utaweza kumaliza changamoto zilizokuwa zikiwakabili na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.
Alisema kwamba kukamilisha agizo ambalo limetolewa na rais litaweza kuwa ni mkombozi mkubwa sana kwa wanafunzi na wataweza kuongeza kasi ya ufaulu kwani hapo awali walikuwa wanasoma katika mazingira ambayo sio rafiki kwao na wengine kusoma wakiwa wamekaa chini.
“Katika kukamilisha zoezi hili na agizo lililotolewa na Rais kuhakikisha kwamba tunafanya kila jitihada ili kuweza kuhakikisha wote wanasoma wakiwa wamekaa kwenye madawati na sio chini hivyo madawati hayo yametokana na kubana matumizi mbali mbali katika ofisi ya Mbunge hivyo nina imani ni moja ya hatua nzuri katika kuendelea kuboresha sekta ya elimu katika jimbo langu,”alisema Jumaa.
Pia alisema kwamba pamoja na agioz hilo pia ataendelea kujitahidi kushirikiana na wa madiwani wote katika halmashauri ya Kibaha vijiji pamoja na wadau wengine ili kuweza kuendeleza kutoa sapoti katika kununua mahitaji mengine muhimu ikiwemo vitabu ambavyo viyaweza kuwapa fursa wanafunzi kuweza kujisomea.
Naye Mkuu wa shule ya sekondari Kilangalanga Albert Mabiki, pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya Kibaha vijijini Mansouri Kisebengo hapa wanazungumza changamoto zilizokuwa zinawakabili wanafunzi pamoja na kushindwa kufanya vizuri kutokana na kuwepo kwa mlundikano mkubwa wa wanafunzi pamoja na hali ya kuwepo kwa  utoro.
“Ni kweli changamoto ya watoto wetu walikuwa wanasoma katika mazingira ya mlundikano, na wakati mwingine baadhi ya wanafunzi wanakuwa ni watoro hawafiki shuleni nah ii ni kutokana na kutokuwepo kwa madawati na viti vya kutosha lakini kwa hali hii na agizo la Rais wetu hakika kwa sasa hata huu utoro utamalizika katika baadhi ya maeneo.
MADAWATI hayo pamoja na vitabu  ambayo vimetolewa  na ofisi ya Mbunge wa jimbo la Kibaha vijijini vimegharimu  kiasi cha  zaidi ya shilingi  milioni 100 ambapo kata zote 14 ambapo kuna shule za msingi na sekondari zimeweza kupatiwa mgao huo kwa baadhi ya shulezenye mahitaji makubwa  kwa ajili ya kuweza kutekeleza agizo lililotolewa na Rais.

Haki Madini waendesha mdahalo wa maendeleo ya uchumi na uwekezaji kwenye madini Simanjiro.

sim1Mkurugenzi wa Shirika la Haki Madini, Amani Mustafa Mhinda akizungumzia juu ya ugatuzi na ugatuaji wa madaraka kwa wadau wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, katika mdahalo wa siku mbili wa maendeleo ya uchumi na uwekezaji kwenye madini unaofanyika Mirerani na kuandaliwa na shirika hilo.
sim2 
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Albert Msole (katikati), Diwani wa Kata ya Mirerani Yohana Onyango, (kushoto) na Mwenyekiti wa mtaa wa Twiga Anthony Musiba, wakifuatilia mdahalo siku mbili wa wa maendeleo ya uchumi na uwekezaji kwenye madini, juu ya mpango wa uhamasishaji na uwazi katika katika mapato ya madini, gesi asilia na mafuta unaonyika Mji mdogo wa Mirerani na kuandaliwa na shirika la Haki Madini.
sim3 
Wadau wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakifuatilia mdahalo wa siku mbili wa maendeleo ya uchumi na uwekezaji kwenye madini uliondaliwa na shirika la Haki Madini.

Ali Kiba kupamba shamrashamra za tamasha la chaneli ya StarTimes Kiswahili

TIM1Mkurugenzi Msaidizi wa Masoko na Maudhui wa StarTimes Tanzania, Bw. Damien Li (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Kushoto ni msanii Ali Kiba ambaye atakuwepo kutumbuiza na kutoka kulia ni Msanii Madee pamoja na Meneja Mauzo wa Huawei, Bw. Zhang Heng, ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL.
TIM2 
Msanii wa muziki wa bongo flava Ali Kiba (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Wakimsikiliza kwa makini kulia ni Msaidizi wa Masoko na Maudhui wa StarTimes Tanzania, Bw. Damien Li na kushoto ni Meneja wa chaneli ya StarTimes Swahili, Bi. Wang Qian. Huawei ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL.
TIM5 
Msanii wa bongo flava kutoka kundi la TipTop Connenction lenye maskani yake Manzese, Madee akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Huawei ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL.
TIM6 
Msanii wa kizazi kipya Bi. Snura alimaarufu ‘Mama Majanga’ akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Msanii Madee wa kundi la Tip Top Connection.
TIM7 
Msanii wa muziki wa singeli Eskide akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa chaneli ya StarTimes Swahili, Bi. Wang Qian. Huawei ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL.
TIM8 
Meneja wa chaneli ya StarTimes Swahili, Bi. Wang Qian akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Huawei ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL. Kulia ni Msanii Ali Kiba.
TIM11 
Kutoka kulia ni Meneja Mauzo wa Huawei, Bw. Zhang Heng, ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la StarTimes Kiswahili linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL, Msaidizi wa Masoko na Maudhui wa StarTimes Tanzania, Bw. Damien Li, Msanii wa muziki wa bongo flava Ali Kiba na Meneja wa chaneli ya StarTimes Swahili, Bi. Wang Qian wakikata keki kuashiria uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Wasanii wakubwa nchini kulishambulia jukwaa, wakiwemo Ali Kiba, Lady Jaydee, Yamoto Band, Madee, Juma Nature, Snura, Stamina, Eskide (msanii wa muziki wa singeli) na bila ya kusahau wakali wa bongo movie pia watakuwepo.
…………………………………………………………………………………………………..
Wasanii wa muziki wa Bongo Flava Ali Kiba na Lady Jaydee wanatarajiwa kutumbuiza katika tamasha la kusherehekea miaka miwili tangu kuanzishwa kwa chaneli ya StarTimes Kiswahili siku ya Jumamosi ya Agosti 13, 2016 katika viwanja vya Posta, Kijitonyama.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha hilo Mkurugenzi Msaidizi wa Masoko na Maudhui wa StarTimes Tanzania, Bw. Damien Li amesema kuwa tamasha hilo linadhamiria kusherehekea kwa pamoja na wateja wao mafanikio yaliyofikiwa na chaneli ya StarTimes Kiswahili katika kuonyesha vipindi vyenye maudhui ya Kiswahili nchini Tanzania na Kenya.
“Chaneli hii mwaka huu mwezi wa Agosti inatimiza miaka miwili tangu kuanzishwa kwake mnamo Agosti mosi mwaka 2014. Chaneli ya StarTimes Kiswahili inaonekana katika nchi mbili za Tanzania na Kenya na hivyo kutoa wigo mpana kwa wasanii na watayarishaji wa vipindi hapa nchini kupata fursa ya kuonekana maeneo hayo. Vipindi vingi katika chaneli hii huangazia masuala ya filamu, muziki, burudani, vyakula, mitindo ya maisha na mavazi pamoja na tamaduni za watu wa Afrika ya Mashariki hususani kwa nchi hizo mbili ambavyo huwasilishwa kwa lugha ya Kiswahili.” Alisema Bw. Li
“Tamasha hili litahusisha shughuli mbalimbali hususani kuangazia maudhui yanayopatikana kwenye chaneli ya StarTimes Kiswahili lakini pia litapambwa na burudani kadhaa kutoka kwa wasanii watakaoalikwa. Siku hiyo watanzania watawashuhudia wasanii wakubwa wa muziki wa bongo flava jukwaani kama vile Ali Kiba, Lady Jaydee, Juma Nature, Madee, Yamoto Band, Snura na Stamina. Pia kutakuwepo na wasanii mashuhuri kutoka katika tasnia ya bongo movie ambao filamu zao zinaonekana kupitia chaneli hii kama vile Wema Sepetu, JB, Steve Nyerere na Ray Kigosi.” Aliongezea Bw. Li
Chaneli ya StarTimes Kiswahili inapatikana katika visimbuzi vyote viwili vya StarTimes yaani cha antenna kuazia kifurushi cha NYOTA kwa shilingi 6000/- na cha dishi kuanzia kifurushi cha NYOTA PLUS kwa shilingi 8000/- kama malipo ya mwezi. Kampuni hiyo inajivunia kuwa ya kipekee nchini Tanzania kwa kutoa matangazo bora ya dijitali kwa gharama nafuu ambayo kila mtu anaweza kuimudu.
“Ningependa kutoa wito kwa wateja wa StarTimes na watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika tamasha hili litakalofanyika siku ya Jumamosi ya Agosti 13 mwaka huu pale viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Tiketi zitapatikana kwa bei ya kawaida kabisa ya kuanzia shilingi 5000/- na kupatikana katika vituo vitakavyoanza kutangazwa kwa njia mbalimbali. Tamasha hili ni maalumu kwa ajili ya kuwashukuru watanzania kwa kuipokea vizuri chaneli hii na kuifanya kuwa chaguo lao kubwa pindi watazamapo luninga, hivyo naomba wajitokeze kwa wingi.” Alimalizia Bw. Li
Naye kwa upande wake msanii wa bongo flava Ali Kiba akizungumza mbele ya waandishi wa habari amewaahidi makubwa wateja wa StarTimes na watanzania watakaohudhuria siku hiyo kuwa watapata burudani ya aina yake.
“Kwanza kabisa ningependa kutoa pongezi za dhati kwa kampuni ya StarTimes kwa kutambua mchango wa lugha ya Kiswahili na kuikuza miongoni mwa nchi wanazofanya biashara. Hii ni fursa ya kipekee kwa wasanii na watayarishaji wa kitanzania kuweza kupanua wigo wa kazi zao na kuweza kuonekana sehemu zingine. Kusema ukweli hapo awali wakati matangazo ya dijitali yanaingia nchini sikuweza kuiona fursa hii lakini sasa ninaona kazi za wasanii wetu zinaonekana na kutambulika kimataifa.” Alisema Ali Kiba
“Ningependa kutoa wito kwa StarTimes kupanua wigo zaidi wa chaneli hii ifike katika nchi zingine za jirani kama vile Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Kongo hata Afrika ya Kusini kwani kuna watanzania kule na waafrika ambao wanapenda kufahamu lugha ya Kiswahili na tamaduni za waswahili wenyewe. Na mwisho kabisa ningependa kuwaalika watanzania wote siku hiyo waweze kuhudhuria kwa wingi kwani tamasha hili ni lao, nawaomba waje kwa wingi kusherehekea kwa pamoja maudhui mazuri na ya kusisimua yanayopatikana ndani yake.” Alihitimisha Ali Kiba au King Kiba kama anavyojulikana miongoni mwa mashabiki wake

Airtel Money yaingia ubia na NMB bank kuongeza ufanisi kwa wakala wake.

indexMkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colasso akiongea wakati wa kutambulisha kuhusu Money airtel kuingia ushirikiano na NMB banki ili banki ya NMB ihudumie wakala wa Airtel Money
……………………………………………………………………………………………………..
Wakala wa Airtel kupata Airtel Money salio kwenye benki ya NMB popote.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake inayokuwa kwa kasi ya Airtel Money imeingia ubia na Benki ya NMB ili kutoa huduma kwa wakala wake wanaotoa huduma za Airtel Money kujipatia huduma ya salio na pesa taslim katika matawi ya benki hiyo popote nchini.
Akiongelea ubia huo, Mkurugenzi wa Airtel Bw, Sunil Colaso alisema “tunachofanya Airtel na benki ya NMB ni mundelezo wa mikakati tuliyojiwekea ya kuhakikisha tunaleta maendeleo katika huduma za kifedha nchini ili wateja wetu wapate huduma za uhakika na  nafuu. Pia kuwepo kwa sera bora za udhibiti na uwekezaji itachochea wawekezaji kuendelea kuboresha na kuweka miundombinu bora zaidi ya huduma ili kugusa mahitaji ya wateja wengi”
Tunajisikia fahari kuona NMB banki anakuwa nguzo muhimu ya kutoa huduma za Airtel Money kwa kuwafikishia wakala wetu salio kila walipo ili waweze kuhudumia wateja wetu, hii inaonyesha dhairi huduma za kifedha kwa mtandao zinazidi kupanuka kutokana na jitihada na ubunifu wa watoa huduma kwa lengo la  kuwahakikishia wateja usalama na unafuu katika kufanya malipo, Nina uhakika Tanzania itaendelea kukua katika swala la huduma za fedha endapo tu kutakuwa na mahusiano ya wadau kibiashara kama haya ya Airtel Money na Banki ya NMB”
“NMB itahudumia wakala wetu zaidi ya 45,000 ili kuweka na kutoa salio la Airtel Money wakati wowote katika matawi yao 160 nchi nzima, haya ni maendeleo makubwa sana hata kwa biashara yetu”. alieleza Colaso 
NMB na Airtel inaingia Ubia kipindi ambacho Airtel Money pia imezindua kampeni yake kabambe ya Mr Money kwa lengo la kuwafikishia wateja wake taarifa za uhakika na unafuu katika huduma za Airtel Money. Airtel Money imefanikiwa pia kuleta huduma pekee za mikopo isiyokuwa na maharti magumu ya TIMIZA ambapo inawawezesha wateja na mawakala wake zaidi ya milioni 2 kujipatia mikopo kila wakati.

DC MTATURU ATENGA SIKU YA JUMAPILI KUKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo Wilayani humo

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akielekezwa jambo na muwekezaji wa miche ya miti Wikayani humo Mr Choi
Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakikagua ujenzi wa matundu ya choo
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akipokea maelekezo ya namna ya kuitumia miche iliyooteshwa na muwekezaji Mr Choi


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu alipata nafasi ya kukutana na Club inayopambana na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi na UKIMWI kwenye Shule ya Sekondari ya Issuna
…………………………………………………………………………………………………………..
Na Mathias Canal, Singida Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu Leo amekagua miradi ya maendeleo katika kijiji cha Utaho A
ambapo inajengwa shule mpya ili kupunguza adha ya watoto kwenda umbali mrefu na kuvuka barabara ambapo pamoja na kupatiwa mafunzo ya usalama barabarani lakini bado ni Hatari kwao.
Mtaturu amewapongeza wananchi kwa kazi nzuri wakishirikiana na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki kingu na Diwani wa Kata ya Kituntu kusimamia vyema shughuli za maendeleo na hatimaye kufanikiwa kupaua madarasa mawili na ofisi ya walimu.
Sawia na pongezi hizo Mkuu huyo wa Wilaya amewapongeza viongozi wote katika Wilaya hiyo kwa kusimamia ujenzi wa choo cha wanafunzi ambacho kina jumla ya matundu 12.
Dc Mtaturu amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuhakikisha serikali inaunga mkono juhudi za wananchi ili kuwasaidie kujenga nyumba za walimu ili kufikia Januari 2017 shule ianze kupokea wanafunzi wa darasa la kwanza.
Mkuu huyo wa Wilaya pia ametembelea vikundi viwili vilivyopo katika Kijiji cha Makyungu, kikundi cha Muungano ambacho kinatarajia kutotolesha vifaranga baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kuwanunulia mashine(Equbator )kwa thamani ya shilingi 8,700,000/- na kikundi cha pili kinaitwa Wajefia kinachotarajia kutengeneza chakula cha kuku kwa kutumia mashine maalumu waliyoinunua toka Shirika la Viwanda vidogo SIDO cha Mkoani Mbeya.
Sawia na hayo Mtaturu pia amebaini Changamoto waliyonayo ikiwa ni pamoja na elimu ya kuendesha Shuguli zao kibiashara na mtaji ambapo amewapa nafasi ya kupeleka wajumbe watatu kwa kila kikundi kwenye viwanja vyanane nane mjini
Dodoma kwa ajili ya kupata mafunzo na mtaji wa shilingi milioni moja kwa ajilinya kuwasaidia kuanza ununuzi wa vifaa vya kusaga chakula cha kuku na mayai ili waanze uzalishaji wa vifaranga.
Dc Mtaturu pia amemtembelea Mr Choi raia wa Korea aliyeamua kuanzisha kitalu cha miche ya miti na matunda kwa ajili ya utunzaji wa mazingira katika kijiji cha Kimbwi na pia amewekeza katika elimu ambapo anajenga shule ya Awali hadi kidato cha Sita.
Aidha Dc Mtaturu amempongeza muwekezaji huyo na kuwaalika wawekezaji wengine kwa ajili ya kuwekeza wilayani Ikungi katika sekta mbalimbali kwani kuna ardhi ya kutosha ambapo pia amemwagiza Mkurugenzi wa Halmshauri kuwaelekeza watendaji wa Kata kwa ajili ya kuchukua miche ya miti na matunda kwa Mr Choi ambaye ameamua kuungana na serikali katika kampeni ya kutunza mazingira kwa kugawa miche bure.
“Naomba mfahamu kuwa Gharama za mashine ya kusagia chakula cha kuku ni shilingi milioni 9.1 zilizotolewa na Halmashauri na wananchi walichangia kujenga majengo” Alisema Mtaturu
Mtaturu pia amekagua ujenzi wa maabara uliokwama katika Sekondari ya Mkiwa hadi umeanza kubomoka hivyo
amemuagiza Diwani kukaa na Kamati ya maendeleo ya Kata yake kuweka mikakati ya kuwashirikisha wananchi katika Kata wapatao 2009 ili serikali iwaunge mkono kupaua na hatimaye ifikapo Januari mwakani maabara ianze kazi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu anatekeleza kauli ya serikali ya awamu ya tano kwa vitendo
ya Hapa Kazi Tu ambapo ametenga Siku ya Jumapili kuwa Maalumu kwa ajili ya kukagua shughuli za maendeleo.
Katika kutembelea shughuli za maendeleo Wilayani humo pia Mtaturu alipatanafasi ya kukutana na Club inayopambana na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi na UKIMWI kwenye Shule ya Sekondari ya Issuna ambayo kitaaluma matokeo ya kidato cha nne mwaka jana ilishika nafasi ya 10 bora.

MSHAMA: WALIMU WALEVI NA WATORO WASILINDWE/WAFICHULIWE

msha1 
Mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama,akizungumza na walimu wakuu wa shule za Msingi wilayani humo  ambapo alitoa maagizo mbalimbali ikiwemo kuacha kuwalinda walimu wasio na maadili kazini.Mkuu huyo anaendelea na zoezi la  kukutana na makundi mbalimbali. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
msha2 
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
MKUU wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama ,ametoa rai kwa walimu wakuu wa shule za msingi wilayani humo, kuwafichua walimu walevi kazini na watoro pasipo kuwalinda ili kulinda nidhamu kazini.
Amesema wapo baadhi ya walimu wanaoshindwa kufuata maadili yao ya kazi ambapo hakuna hatua zinazochukuliwa.
Aidha Assumpter amewataka walimu hao wakuu kuacha kuwaonea haya walimu hao wanaoshindwa kutimiza wajibu wao wa kazi.
Alitoa rai hiyo ,wakati alipokuwa anazungumza na walimu wakuu wa shule za msingi wilayani hapa ,katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya.
Assumpter aliwaomba wasikubali kukalia tabia hizo ikiwemo kulewa wakati wa kazi kwani kwa walimu wataoshindwa kuwachukulia hatua wanaojihusisha na ulevi,utoro wanaweza kujiweka katika mazingira magumu ya kazi.
Aliwaasa walimu kufanya kazi kwa wito, ari na molari ya kazi ili kuinua kiwango cha taaluma wilayani Kibaha.
“Kufanya vibaya kwa baadhi ya shule ,kunasababishwa na changamoto mbalimbali ikiwemo walimu kujiingiza  na vitendo vya ulevi na utoro,wanakuwa kikwazo katika kuendeleza sekta hii muhimu”
“Walimu wakuu msikubali kuwafumbia macho walimu wa aina hiyo kwani kama mnavyosikia ngazi za juu wanavyowatumbua, huku nako wasipokuwa makini tusiwafumbie macho,” alisema Assumpter.
Nae afisa taaluma halmadhauri ya wilaya hiyo, Damas Kimaro alielezea changamoto ambazo zinasababisha kushuka katika ufaulu kitaifa kutoka nafasi ya 4 mpaka ya 9 imechangiwa na mchakato wa uchaguzi mkuu uliomalizika.
Mwalimu Uhai Legeza ,alimtaka mkuu huyo atembelee katika shule mbalimbali ili aweze kujionea namna walimu hao wanavyofanyakazi katika mazingira magumu .
Alisema kuwa baadhi ya walimu hukaa katika ofisi ambazo hazina thamani bora ikiwemo viti na meza wanazotumia hazilingani na nyingi hazina ubora.
“Mkuu tembelea katika shule zetu uone viti na meza tunazotumia katika kutimiza majukumu yetu ya kazi,” alisema Legeza.
Kufuatia ombi hilo Assumpter aliahidi kutembelea shule hizo kujionea hali hiyo .
Anasema baada ya serikali kumaliza tatizo la madawati sasa itageukia uboreshaji wa miundombinu ya majengo ili kuhakikisha sekta ya elimu inaboreka zaidi.

TANZIA: KAMISHNA MSTAAFU WA MAGEREZA EGNO KAMILIUS KOMBA AFARIKI DUNIA JIJINI DAR

                   Marehemu Kamishna Mstaafu wa Magereza, Egno Kamilius 
…………………………
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini – CGP. John Casmir Minja anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Kamishna Mstaafu wa Sheria na Utawala wa Magereza – CP(Rtd) Egno Kamilius Komba  kilichotokea jana Julai 31, 2016 akiwa nyumbani kwake Mvuti, Chanika Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza anatoa pole kwa Watumishi wote wa Jeshi la Magereza nchini, familia ya Marehemu na wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna tofauti tofauti.
Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na familia ya Marehemu linaendelea kuratibu shughuli za msiba huo na taarifa za mazishi zitatolewa baadaye baada ya taratibu zote kukamilika.
                    Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amina.

PINK RIBBON ITASHIRIKIANA NA SERIKALI KUFANYA UCHUNGUZI NA TIBA YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

pink1 
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi Mtendaji  wa shirika la Pink Red Ribbon toka nchini Marekani Bi.Celina Schocken,shirika hilo limeahidi kushirikiana na Tanzania kwenye masuala mazima ya saratani ya matiti na mlango wa kizazi ili kuwezesha huduma kuwa endelevu,kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNAIDS Dkt.Warren Naamara
pink2 
Waziri Ummy Mwalimu akizungumza kwenye kikao hicho,kushoto ni mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha afya na mtoto-wizara ya afya dkt.Georgina Msemo
pink3 
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Pink Ribon Red Itinerary  Bi. Celina Schocken

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiongea na wanamichezo na wadau wa michezo  katika hafla ya kuwaaga wanamichezo wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil  katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 leo Agosti 1, 2016.
 
Serikali imewashukuru wadau wa michezo nchini kwa kujitokeza na kuwa mstari wa mbele kushiriki na kudhamini michezo mbalimbali nchini.


Shukrani hizo zimetolewa leo na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokuwa akizungumza na  wanamichezo wanaokwenda kushiriki mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 yanayofanyika Jijini Rio dejaneiro nchini Brazil.


Mhe. Anastazia Wambura amesema kuwa wadau wa michezo wamekuwa wakishirikiana na Serikali sio katika suala la michezo pekee hata katika habari na Sanaa na amewapongeza kampuni ya ving’amuzi ya Multichoice Tanzania (DSTV) na Bodi ya Utalii katika azma yao ya kuunga mkono maendeleo ya sera ya michezo nchini.


“Napenda kuwashukuru wadau wetu Dstv na Bodi ya Utalii, nawapongeza kwa kuona fursa hii muhimu na kuitumia kuwatia moyo wawakilishi wa nchi yetu katika michezo ya Olimpiki kwa mwaka 2016 mueendelee kuiunga mkono Serikali katika kutekeleza sera ya maendeleo ya Michezo ili kufikia malengo” alisema Mhe. Anastazia.


Aidha amewataka wawakilishi wa Olimpiki kutumia fursa hii ya wadau wa michezo waliojitokeza kuwaunga mkono ikiwemo Bodi ya Utalii kutangaza utalii wa Tanzania kwa mataifa  mengine watakayo kutana nayo katika mashindano ya Olimpiki nchini Brazil.


Kwa upande wake Mkurungezi Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw.Maharage Chande ameishukuru Serikali kwa kuwapa fursa ya kushirikiana na timu ya Olimpiki kuitangaza michezo na kuitangaza Tanzania kimataifa na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuendeleza michezo nchini.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge akizungumza katika hafla ya kuwaaga wanamichezo wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil  katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 leo Agosti 1, 2016.

Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Maharage Chande  akishukuru Serikali kwa fursa ya kuunga mkono jitihada za kuendeleza michezo wakati wa hafla ya kuwaaga wanamichezo wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil  katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 leo Agosti 1, 2016.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza na wanamichezo na wadau wa michezo  katika hafla ya kuwaaga wanamichezo wanaoenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil  katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 leo Agosti 1, 2016.
SERIKALI YAWASHUKURU WADAU WA MICHEZO KWA KUSHIRIKI KATIKA MAENDELEO YA MICHEZO NCHINI

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiongea na wanamichezo na wadau wa michezo  katika hafla ya kuwaaga wanamichezo wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil  katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 leo Agosti 1, 2016.
Picha/Habari na Raymond Mushumbusi
Serikali imewashukuru wadau wa michezo nchini kwa kujitokeza na kuwa mstari wa mbele kushiriki na kudhamini michezo mbalimbali nchini.

Shukrani hizo zimetolewa leo na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokuwa akizungumza na  wanamichezo wanaokwenda kushiriki mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 yanayofanyika Jijini Rio dejaneiro nchini Brazil.

Mhe. Anastazia Wambura amesema kuwa wadau wa michezo wamekuwa wakishirikiana na Serikali sio katika suala la michezo pekee hata katika habari na Sanaa na amewapongeza kampuni ya ving’amuzi ya Multichoice Tanzania (DSTV) na Bodi ya Utalii katika azma yao ya kuunga mkono maendeleo ya sera ya michezo nchini.

“Napenda kuwashukuru wadau wetu Dstv na Bodi ya Utalii, nawapongeza kwa kuona fursa hii muhimu na kuitumia kuwatia moyo wawakilishi wa nchi yetu katika michezo ya Olimpiki kwa mwaka 2016 mueendelee kuiunga mkono Serikali katika kutekeleza sera ya maendeleo ya Michezo ili kufikia malengo” alisema Mhe. Anastazia.

Aidha amewataka wawakilishi wa Olimpiki kutumia fursa hii ya wadau wa michezo waliojitokeza kuwaunga mkono ikiwemo Bodi ya Utalii kutangaza utalii wa Tanzania kwa mataifa  mengine watakayo kutana nayo katika mashindano ya Olimpiki nchini Brazil.

Kwa upande wake Mkurungezi Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw.Maharage Chande ameishukuru Serikali kwa kuwapa fursa ya kushirikiana na timu ya Olimpiki kuitangaza michezo na kuitangaza Tanzania kimataifa na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuendeleza michezo nchini.

No comments:

Post a Comment