Pages

Thursday, August 4, 2016

MUSEVENI KUTAWALA UGANDA "MILELE" VIONGIOZI WA NRM WILAYA YA KYANKWANZI WATAKA KATIBA IBADILISHWE KUONDOA UKOMO WA UMRI KUWANIA URAIS




NA K-VIS MEDIA/MASHIRIKA YA HABARI
RAIS wa Uganda Yoweri Museveni, (71), huenda akawa rais wa “maisha” wa nchi hiyo, endapo kipengele cha katiba ya nchi hiyo kinachoweka ukomo wa umri wa mika 75 kutoruhusiwa kuwania Urais, utaondolewa na bunge.
Tayari pilikapilika za kuondoa zuiohilo zimeanza ambapo kwa mujibu wa taarifa za vyombovya habari zinasema, Maafisa wa chama tawalanchini humo wamepitisha azimio la kuondoa ukomo wa umri kuwania Urais na hivyo Raios Museveni huenda akaweza kuwania tena kiti hicho mwaka 2021 ambapo atatimiza miaka 75 ambayo inachupia matakwa ya sasa ya Katibaya Uganda yanayozuia mtu mwenye umri huo kuwania Urais.
Museveni ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka1986, ni kiongozi mwenye umri mkubwa zaidi kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwa sasa. Rais Museveni anajivunia kuifanya Ugandakuwa na amani tangu aingie madarakani tofauti na watangulizi wake ambapo marais wan chi hiyo walipinduliwa mara kwa mara.
Museveni pia aliingiamadarakani kwa kuipindua serikali.
Mkutano wa Chama tawala cha NRM wilayani Kyankwanzi umepitisha azimio hiloa mbapo Mwenyekiti wake Bi. Anne Maria Nankabirwa amesema, viongozi wa NRM huko Kyankwanzi wanataka ukomo wa umri uondolewe ili kuruhusu viongozi wenye uwezo kama Museveni kuendelea na uongozi.
Ofiri ya Rais Museveni imethibitisha maamuzi hayo Jumanne Agosti 2, 2016 katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Wakati wa mkutano huo uliofanyika Ikulu ndogoya Kyankwanzi, viongozi hao wa NRM wa wilaya hiyo wamemwambia Rais Museveni kuwa wanataka ukomo wa umri kuwania urais uondolewe kwenye katiba ya nchi hiyo.
Hata hivyo Museveni aliwaambia viongozi hao kuwa atajadiliana na KamatiKuu ya chama cha NRM na uongozi wa NRM juu ya swala hilo.
Wachambuzi wa mambo wanasema, kama mabadiliko ya katiba yakifanyika na kupitishwa, na Rais Museveni kuwania tenaurais wan chi hiyo na kushinda mwaka 2021, atakuwa ametawala Uganda kwa kipindi cha miaka 40

MCHUNGAJI DKT.DANIEL KULOLA WA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA MWANZA KUITETEMESHA INJILI KWA MARA NYINGINE NCHINI MAREKANI

Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya la Jijini Mwanza, akihubiri katika moja ya mikutano yake iliyofanyika mkoani Morogoro.

No comments:

Post a Comment