Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa akitoa neno la
ukaribisho kwa washiriki (hawapo pichani) wa Kongamano la
Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016)
lililoanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Rais
wa Jumuiya ya wafanyabiashara wa Madini nchini Afrika Kusini, Sipho
Nkosi akitoa hotuba kwenye Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016
(African Leadership Forum 2016) lililoanza leo jijini Dar Es Salaam
katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Rais
mstaafu wa Afrika Kusini Mh. Thabo Mbeki akichangia mada katika
Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum
2016) lililoanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt
Kilimanjaro.
Kutoka
kushoto ni Rais wa zamani wa Namibia, Mh. Hifikepunye Pohamba, Rais wa
zamani wa Mozambique, Joaquim Chissano, Rais mstaafu, Mh. Benjamin
William Mkapa, Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Mh. Thabo Mbeki pamoja
na Rais wa zamani wa Mozambique, Mh. Armando Guebuza wakiwa meza kuu
katika Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016
(African Leadership Forum 2016) lililoanza leo jijini Dar Es Salaam
katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Mwakilishi wa Vijana kutoka nchini Nigeria akishiriki kwenye Kongamano
la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016)
lililoanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Mfanyabiashara
na mmliki wa makampuni ya Excel Management, Mikono Speakers na Focus
Outdoor Deogratius Kilawe akitoa maoni katika Kongamano la
Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016)
ulioanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Mawaziri
wakuu wastaafu kutoka kushoto ni Mh. Salim Ahmed Salim, Mh. John
Malecela pamoja na Mh. Cleopa Msuya walikuwa miongoni mwa wageni
waalikwa katika Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African
Leadership Forum 2016) ulioanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli
ya Hyatt Kilimanjaro.
Pichani
juu na chini ni wadau mbalimbali walioshiriki kwenye Kongamano la
Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016)
lilioanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro na
kuratibiwa na Uongozi Institute.
Raisi
wa zamani wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki amezungumzia biashara ya
magendo ya madini ya Tanzanite katika Kongamano la Viongozi wastaafu wa
Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) kuzungumzia namna ya
kuzifanya biashara kuleta mabadiliko chanya barani Afrika.
Mbeki
ameyasema hayo katika kongamano hilo lililowakutanisha viongozi
mbalimbali wa Afrika kujadili jinsi biashara inavyoweza kusaidia
kubadili maisha ya Waafrika lililofanyika leo katika hoteli ya Hyatt
Regency-Kilimanjaro, Dar es salaam.
Aidha,
Mbeki amesema takribani dola milioni 800 hupatikana kila mwaka kwa
kuuza na kusafirisha madini ya Tanzanite nchi za nje, lakini kutokana na
biashara za magendo na wizi wa madini ya Tanzanite ni dola milioni mia
tano tu hupatikana kila mwaka nchini Tanzania
Ameongeza
kuwa Tanzania inasafirisha kiwango kidogo cha madini hayo ukilinganisha
na uchimbaji halisi unaoendelea kila mwaka, na hivyo kufanya sekta ya
madini pamoja na biashara kuzorota kwa hali ya juu
Tanzania
ni nchi pekee duniani inayochimba madini ya Tanzanite yenye thamani
kubwa lakini nchi za Afrika Kusini na Kenya ndiyo zimekuwa zikijulikana
kwa uuzaji wa madini hayo.
Mkutano
huo unataraji kufanyika kwa siku mbili na kudhaminiwa na mashirikia na
taasisi mbalimbali ikiwepo Taasisi ya Mo Dewji (Modewji Foundation.
Zlatan Ibrahimovic kifaa kipya cha Man U. chaanza mazoezi
Mshambualiaji mpya wa Manchester
United, Zlatan Ibrahimovic kwa mara ya kwanza ameungana na wachezaji
wenzake wa klabu hiyo ya Uingereza na kufanya mazoezi kwa pamoja.
Ibrahimovic amejiunga na Manchester United akitokea PSG ya Ufaransa baada ya mkataba na timu hiyo kumalizika.
MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI TEMEKE
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Temeke kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo jijiniDar es salam Julai
28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi
ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke wakimsikiliza Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa
Halmashauri hiyo jijini Dar es salaam Julai 28, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi wa mkoa wa Dar es salaam
baada ya kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Temeke
kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo jijini Dar es slaam Julai 28, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi wa mkoa wa Dar es salaam
baada ya kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Temeke
kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo jijini Dar es slaam Julai 28, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
BALOZI WA CANADA NCHINI AAGANA NA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO
Balozi
wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Lévêque akisaini kitabu cha
wageni kwenye Ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo. Balozi huyo alimtembelea Profesa Muhongo kwa ajili ya kumuaga
mara baada ya muda wake kumalizika hapa nchini.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimweleza Balozi
wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Lévêque (kushoto) mikakati ya
Serikali katika uboreshaji wa sekta ya nishati nchini
Naibu
Katibu Mkuu wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James
Mdoe (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini
anayeshughulikia Nishati Dk. Juliana Pallangyo (kulia) wakifuatilia
mazungumzo kati ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
na Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Lévêque (hawapo pichani)
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Balozi wa
Canada Nchini Tanzania, Alexandre Lévêque (kushoto) wakiwa katika picha
ya pamoja
No comments:
Post a Comment