Jenerali Taban Deng Gai
Kundi
moja la waasi wa zamani nchini Sudan Kusini limetangaza kuchukua nafasi
ya Riek Machar kama Makamu wa rais wa kwanza, baada ya kiongozi huyo
kuondoka jijini Juba baada ya kuzuka tena kwa mapigano mapya wiki mbili
zilizopita.
Hata
hivyo, Machar ambaye haifahamiki yuko wapi, ametupilia mbali taarifa
kuwa nafasi yake imechukuliwa na Jenerali Taban Deng Gai aliyeongoza
waasi katika mazungumzo ya amani mwaka uliopita nchini Ethiopia.
Jenerali Gai amesema, anashikilia wadhifa huo kwa muda tu na ikiwa Machar atarejea atamwachia.
“Nashikilia nafasi hii kwa muda tu kwa sababu ya amani, na ikiwa Riek Machar atarejea, nitamwachia nafasi hii,” amesema.
Riek Machar Makamu wa kwanza wa rais nchini Sudan Kusini
Mshirika
wa karibu wa Machar ameliambia Gazeti la kila siku nchini Kenya Daily
Nation kuwa uamuzi wa Jenerali Gai ambaye zamani alikuwa Gavana wa jimbo
la Unity halikuridhiwa na viongozi wakuu wa chama cha upinzani cha
SPLM-OI na huenda amehongwa na rais Kiir.
Wiki
iliyopita, Waziri wa Habari na msemaji wa serikali Michael Makue Lueth
alinukuliwa na Gazeti na Sudan Tribune akisema kuwa nafasi ya Machar
inaweza kuchukuliwa na mtu mwingine kutoka upande wa upinzani ikiwa
Machar kwa mujibu wa mkataba wa amani wa Addis Ababa uliokubaliwa mwaka
uliopita.
Riek Machar na rais Salva Kiir baada ya kutia saini mkataba wa amani jijini Addis Ababa mwaka jana
Wakati
hayo yakijiri, rais Salva Kiir alizuru jijini Kampala mwishoni mwa juma
lililopita kushauriana na rais Yoweri Museveni kuhusu hali inavyoendelea
katika nchi yake.
Ripoti
zinasema kuwa Kiir, amemwomba msaada wa kijeshi rais Museveni huku
kiongozi huyo wa Uganda akimtaka Kiir kukubali kutumwa kwa vikosi vya
Kimataifa vya kulinda amani. RFI
No comments:
Post a Comment