Pages

Thursday, July 28, 2016

DKT. KIGWANGALLA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA VIONGOZI WA MFUKO WA ABBOTT (ABBOTT FUND) KUTOKA MAREKANI.

kg1 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na viongozi wa mfuko wa Abbott (Abbott Fund) kutoka Marekani na Tanzania waliomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya uboreshaji wa huduma za Afya na Elimu kupitia program mbalimbali zinazofanywa na Mfuko huo nchini. Kutoka Kulia ni Makamu Mtendaji wa Rais wa Mfuko wa Abbott, Stephen Fussell na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund Bi.Elaine Leavenworth (katikati).
kg2 
Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund) Bi.Elaine Leavenworth (kulia) akimweleza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) juu ya namna Mfuko wa Abbott ulivyojipanga kuendelea kutekeleza Program mbalimbali nchini Tanzania zikiwemo za Matumizi ya Teknolojia ya kisasa katika utoaji wa Tiba, maabara za kisasa, dawa na vifaa vya mafunzo kwa wanafunzi wa masomo ya Sayansi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akifurahia jambo na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund) Bi.Elaine Leavenworth (kulia) leo jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelewa na  ujumbe  wa viongozi wa mfuko huo kutoka nchini Marekani.
kg4 
Ujumbe  wa viongozi wa mfuko wa Abbott (Abbott Fund) kutoka Marekani ukimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla mara baada ya kumtembelea Ofisini kwake leo.
kg5 
Makamu wa Rais wa  Mfuko wa Abbott (Abbot Fund) nchini Tanzania Andy Wilson akielezea utayari wa Mfuko huo katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazoikabili sekta ya Afya na Elimu nchini kupitia ufadhili wa Programu mbalimbali zinazofanywa na Mfuko huo kwa niaba ya Watu wa Marekani.
PICHA/ Aron Msigwa –MAELEZO.

NAIBU WAZIRI HAMAD MASAUNI AONGOZA KIKAO CHA KUJADILI MKAKATI WA KUPUNGUZA AJALI NCHINI

suf1 
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika kikao cha Baraza hilo cha kujadili Mkakati wa Kupunguza Ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
suf2 
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto meza kuu) akimsikiliza Mjumbe wa Kikao hicho, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dk. Zakaria Mganilwa (kulia) alipokuwa anachangia mawazo katika Kikao cha kujadili Mkakati wa Kupunguza Ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
suf3 
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika kikao cha Baraza hilo cha kujadili Mkakati wa Kupunguza Ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali wa Baraza hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
suf4 
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto meza kuu) akimsikiliza Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga (kulia meza kuu) alipokuwa akizungumza katika Kikao cha kujadili Mkakati wa Kupunguza Ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MRADI WA HARAMBEE NI MKOMBOZI WA WANANCHI WA KIJIJI CHA CHOLE, MAFIA – PWANI

Mwenyekiti wa Kijiji cha Chole, Shehari Ahmadi akielezea waandishi wa habari maendeleo ya kijiji cha Chole ikiwa ni pamoja na kutolea ufafanuzi suala la kauli iliyoleta mkanganyiko hivi karibuni ya kuwa mwekezaji amemilikishwa mapango ya kale kinyume cha sheria jambo ambalo si halina ukweli wowote kwa vile linachafua sura ya kijiji chao. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog – CHOLE, MAFIA.
Wananchi wa kijiji cha Chole, wilayani Mafia – Pwani wameusifia mradi wa Harambee unaowapatia elimu watoto wao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Kajunason Blog iliyoweka kambi kijijini hapo kujionea hali halisi ya kisiwa hicho, wananchi hao walisema ujio wa mwekezaji umekuwa mkombozi wa wanachi kwa vile ni mambo mengi waliyofaidika kwa muda wote ambao amekuwepo mwekezaji kijijini hapo.
Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee, Hamis Musa Athuman alisema mpaka sasa zaidi ya Sh. milioni 500 zimetumika kugharimia ada na mahitaji muhimu ya wanafunzi shuleni wa kijiji cha Chole, kupitia mradi huo.
Aliongeza kuwa pesa hiyo imeweza kuwafikia jumla ya wanafunzi wapatao 300.
Mwenyekiti mstaafu wa kijiji cha Chole (kulia) ambaye alianza kazi yake 1999 – 2014, Bw. Maburuki Sadiki aliishukuru kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development kwa kuweza kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kuwajengea shule ya msingi, Zahanati, shule ya ChekeChea, Darasa la watu wazima kujifunza kingereza, watoto kwenda sekondari na mengine mengi. Pembeni ni mwenyekiti wa sasa Shehari Ahmadi.

Mkazi wa kijiji cha Chole, Bi. Riziki Hassan Selenge ambaye anasomeshewa watoto wake wawili na Mfuko wa maendeleo wa Harambee.

 Mkazi wa Chole, Bw. Johari Rajabu Fadhil ambaye ndiye mmoja ya waasisi waliompokea mwekezaji, na aliweza kupata ufadhili wa kwenda kusoma masomo ya kufundisha watoto ya miaka 2.
 Mkazi wa kwanza wa kijiji cha Chole wilayani Mafia kijiji cha Chole Mjini kupata digrii ya chuo kikuu, Zubeda Bhai akiwaelezea waandishi wa habari abato Kasika na Florence Mugarula waliotembelea eneo hilo la kihistoria jinsi ambavyo taasisi ya Chole Mjini Conservation and Development ilivyomsaidia gharama zote za kupata elimu ya juu.

Alisema kuwa miaka ya nyuma wakazi wa Chole hawakuwa na mwamko wa elimu, lakini baadaye wakapata mwekezaji ambaye amechangia shughuli mbalimbali za maendeleo na kuwafanya wakazi wa kisiwa hicho kuwa nma mwamko wa elimu.
“Tuna mwekezaji ambaye ni kampuni ya Chole Conservation & Development inayosimamia na kutunza magofu ya Kijerumani, ametusaidia sana kutuamsha na sasa hapa Chole kuna mwamko mkubwa wa elimu,” alisema Kingi.
Alisema kuwa mwekezaji huyo aliwahamasisha kuanzia kamati hiyo ndipo ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba ukaanza kuongezeka kuanzia mwaka 2007 na umekuwa ukizidi kupanda kadri miaka inavyokwenda.
 Wanafunzi wa Chekechea wakifundishwa.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari wanaonufaika na mfuko wa maendeleo wa Harambee. wakiwa pamoja na mkurugenzi wa Kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development Bi. Anne K. de Villiers.
Moja ya usafiri wa boti unaotumika kuwavusha wakazi wa Chole kwenda Mafia Mjini.
Wageni waliofika kutembelea kisiwa cha Chole kujionea majumba ya kizamani yenye histori za mababu zetu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee, Hamis Musa Athuman akielezea maendeleo ya kijiji cha Chole katika upande wa elimu akiwa na  katibu wa kamati hiyo Mohamed Kingi (kulia).
Shule ya msingi ya Chole iliyojengwa na Mwekezaji wa Kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development.
Majengo ya kale yanayosimamiwa na kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development yakionekana katika sura nzuri ya utunzaji wa hali ya juu.

Mkazi wa Kijiji Cha Chole Mjini kilichopo Mafia mkoani Pwani, Faharani Shomari, akiwaonyesha picha ya magofu ya kihistoria yalivyokuwa yameharibika na yalivyo sasa baada ya kufanyiwa ukarabati na kampuni ya Chole Mjini Conservation & Development wakati waandishi hao walipoenda kutembelea eneo hilo. 
Picha zikionyesha jinsi majengo ya kale yalivyoonekana kabla hayajakarabatiwa na kufanyiwa usafi.
Katibu wa Harambee wa Kijiji Cha Chole Mjini kilichopo Mafia Mkoa wa Pwani, Mohammed Kingi akiwafundisha wanafunzi wa Shule ya Msingi Chole. Shule hiyo pamoja na masomo hayo yanafadhiliwa na kampuni ya Chole Conservation and Development
Kituo cha elimu ya watu wazima, hapa ndipo hujifunza kingereza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Chole Mjini Conservation & Development, Anne K. de Villiers, alisema kuwa wafadhili wa Kamati ya Harambee wako nchini Uingereza.
Alisema kuwa aliwatafuta baada ya kubaini kwamba wakazi wa kijiji hicho hawana mwamko wa elimu na wamekuwa wakifadhili hata ujenzi wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa nyumba za walimu na mambo mengine ya muhimu kwa ajili ya elimu.
“Mbali na hilo kwa sasa tuna shule ya chekechea, kituo cha wanawake cha kujufunza kusoma, kituo cha kujifunza kompyuta na kituo cha wanafunzi na watu wengine kujifunza lugha ya Kiingereza na maktaba,” alisema mkurugenzi huyo na kuendelea:
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chole, Shehari Ahmad alisema kuwa serikali imekuwa ikifaidika kwa kupata dola 10 kwa kila mgeni anayeingia na kulala katika hoteli ya Chole mjini inayosimamiwa na kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development sambamba na dola 5 kwa kila mgeni anayetembelea majengo ya kale ya mapango ya Chole ambayo yakikuwa yakitumika katika biashara ya watumwa.
Nae Bi. Riziki Hassan Selenge alisema kuwa hapo mwanzo mambo yalikuwa magumu tokea kuingia kwa mwekezaji huyo ndiye amekuwa mwasisi wa maendeleo kijijini kwao kwa vile asilimia 99 wakazi wa Chole hali zao ni masikini na hawakuweza kupeleka shule watoto wao.
Upande wake Mwenyekiti mstaafu, 1999 – 2014, Bw. Maburuki Sadiki aliishukuru kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development kwa kuweza kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kuwajengea shule ya msingi, Zahanati, shule ya ChekeChea, Darasa la watu wazima kujifunza kingereza, watoto kwenda sekondari na mengine mengi.
Akitoa historia fupi Bw. Sadiki alisema mchakato wa kumpokea mwekezaji huyo ulifanyika Desemba 4, 1993 kwa kueleza dhamila yake na tulimkubalia kwa kufuata sheria zote na makubaliano tuliwekeana nae tokea kipindi hicho ambapo tokea ameingia mwekezaji huyo amekuwa akitekeleza mkataba aliyopewa na kijiji.  

TAMWA kupambana na ajali za barabarani kuokoa vifo vya akinamama na watoto

Mgeni rasmi katika hafla ya TAMWA wakizinduwa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga akizungumza kabla ya kuzindua mradi huo. TAMWA wamezindua mradi huo ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali hizo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wanawake, watoto pamoja na jamii nzima.
Mgeni rasmi katika hafla ya TAMWA wakizinduwa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga akizungumza kabla ya kuzindua mradi huo. TAMWA wamezindua mradi huo ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali hizo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wanawake, watoto pamoja na jamii nzima.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga (kushoto) akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali hizo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wanawake, watoto pamoja na jamii nzima.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga (kushoto) akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali hizo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wanawake, watoto pamoja na jamii nzima.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali hizo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wanawake, watoto pamoja na jamii nzima.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali hizo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wanawake, watoto pamoja na jamii nzima.
Ofisa Miradi Mkuu, TAMWA, Bi. Gradness Munuo (kulia) akitambulisha mradi huo kwa washiriki wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani.
Ofisa Miradi Mkuu, TAMWA, Bi. Gradness Munuo (kulia) akitambulisha mradi huo kwa washiriki wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani.
Baadhi ya maofisa kutoka TAMWA wakifuatilia mijadala anuai katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani.
Baadhi ya maofisa kutoka TAMWA (wa kwanza na wa pili kulia) wakifuatilia mijadala anuai pamoja na washiriki wengine katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga (kushoto) akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali hizo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wanawake, watoto pamoja na jamii nzima.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga (kushoto) akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali hizo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wanawake, watoto pamoja na jamii nzima.
Baadhi ya washiriki wa hafla ya TAMWA wakizinduwa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wadau anuai.
Baadhi ya washiriki wa hafla ya TAMWA wakizinduwa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wadau anuai.
Baadhi ya washiriki wa hafla ya TAMWA wakizinduwa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wadau anuai.
Baadhi ya washiriki wa hafla ya TAMWA wakizinduwa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wadau anuai.
Baadhi ya washiriki wa hafla ya TAMWA wakizinduwa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wadau anuai.
Baadhi ya washiriki wa hafla ya TAMWA wakizinduwa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wadau anuai.
Baadhi ya washiriki wa hafla ya TAMWA wakizinduwa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wadau anuai.
Baadhi ya washiriki wa hafla ya TAMWA wakizinduwa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wadau anuai.
Baadhi ya washiriki wa hafla ya TAMWA wakizinduwa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wadau anuai.
Baadhi ya washiriki wa hafla ya TAMWA wakizinduwa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wadau anuai.
………………………………………………………………………………………………………………
CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimezindua mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali za vyombo hivyo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wanawake, watoto pamoja na jamii nzima. Akizindua mradi huo Makao Makuu ya Ofisi za TAMWA, Sinza jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga amepongeza jitihada hizo kwani zitasaidia kuongeza elimu juu ya masuala ya usalama barabarani na namna ya kukabiliana na ajali.
Akizungumza awali Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga alisema chama hicho kimeguswa kushiriki katika mapambano ya ajali za barabarani kutokana na kuona ipo idadi ya wanawake wengi na watoto wamekuwa wakiathiriwa na ajali hizo kila uchao. Alisema ujio wa usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda watumiaji wengi wa usafiri huo ni wanawake wanapokuwa katika shughuli zao za kila siku na ndio wanaoguswa na ajali hizo.
Alisema wapo wakina mama ambao wamekuwa wakifanya biashara zao pembezoni wa barabara kundi ambalo nalo limekuwa likiathiriwa kwa kiasi kikubwa na ajali za barabarani zinapotokea. Akifafanua zaidi alisema chama hicho kitajikita katika kutoa elimu ya usalama barabarani; ikiwa ni pamoja kupinga ulevi wakati wa uendeshaji vyombo vya moto, kuhamasisha uvaaji wa kofia ngumu (helment) kwa waendesha pikipiki pamoja na abiria wao, kuhamasisha ufungaji mikanda kwenye magari pamoja na kuelimisha jamii kuwa mwendo wa kasi barabarani ni hatari.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika tukio hilo, Kamanda Mohammed Mpinga alisema kuna kila sababu ya wadau kama TAMWA kujitokeza kupambana na ajali za barabarani kwani zinamguza kila mmoja. Alisema licha ya idadi ya ajali kuendelea kupungua mwaka hadi mwaka ukilinganisha, lakini bado kuna roho na mali za raia zinapotea kila wakati hivyo kuna kila sababu ya elimu ya usalama barabarani na mapambano yakafanywa kwa ushirikiano wa wadau wote.
Alitolea mfano kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari 2016, jumla ya ajali za barabarani zilizotokea ni 5,152, ambapo vifo vilikuwa 1,580 na majeruhi ni 4,659 huku vifo hivyo vikigharimu maisha ya wanawake 301. Uzinduzi huo ambao uliambatana na kutoa mada mbalimbali juu ya mikakati na mapambani katika mradi huo, wakiwemo viongozi wa Serikali, madereva na mashirika anuai yasiyo ya kiserikali pamoja na waandishi wa habari.

Mwenyekiti wa Bodi ya JKCI , Profesa William Mahalu apongeza utendaji wa JKCI.

jki1Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete-JKCI- Profesa William Mahalu( katikati) akiwasili ndani  taasisi hiyo kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe na Rais John Magufuli  , kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI , Profesa Mohamed Janabi  na  kulia ni Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Maulid Kikondo.
jki2 
Profesa William Mahalu akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
jki3Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Profesa Mohamed Janabi akielezea utendaji kazi wa taasisi hiyo .
jki4Mwenyekiti wa Bodi ya JKCI Profesa William  Mahalu akijitambulisha kwa viongozi wa taasisi hiyo .
jki5 
Baadhi ya viongozi wa Taasisi ya JKCI wakimsikiliza Profesa Mahalu wakati akizungumza nao mara baada ya kujitambulisha .
……………………………………………………………………………………………….
Dar es salaam,
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakay Kikwete JKCI- Profesa William Mahalu kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe na Rais John Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi hiyo  ametembelea JKCI kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na viongozi.
Katika mazungumzo hayo amewataka viongozi wa taasisi hiyo kuwa mfano na  kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya Rais John Magufuli  ya hapa kazi tu.
Pia amewapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuhakikisha watanzania wenye magonjwa ya Moyo wanapatiwa matibabu hapa hapa nchini hatua ambayo imepunguza gharama kubwa ya kugharamia matibabu nje ya nchi.

SAYONA FRUITS LTD YAMPIGA TAFU RIDHIWANI KIKWETE

index 
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa  na mwakilishi wa kampuni ya sayona fruits ltd Abubakary Mlawa kwenye moja ya meza na kiti ambavyo alikabidhiwa kutoka kwa kampuni hiyo kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari tano jimboni humo.(Picha na Mwamvua Mwinyi)index 
Mbunge wa jimbo la  Chalinze Ridhiwani Kikwete akikabidhiwa  viti na meza kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari tano za jimbo hilo  ,kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya Sayona  fruits ltd ,Abubakary Mlawa huko katika shule ya sekondari ya Lugoba .Kampuni hiyo imetoa viti 724 na meza 724 vyote vikiwa na gharama ya mil.80.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
………………………………………………………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
MBUNGE wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ,amepokea msaada wa viti 724  na meza 724 kwa ajili ya wanafunzi wa  shule ya sekondari tano jimboni humo.
Msaada huo umetolewa na kampuni ya Sayona fruits ltd ambapo viti na meza hizo zimegharimu kiasi cha sh.mil 80.
Aidha mdau huyo wa maendeleo ametoa madawati 1,200 yaliyogharimu sh.mil 90 ,katika shule za msingi wilayani Bagamoyo ambapo kati ya madawati hayo 600 ni ya jimbo la Chalinze na 600 ni jimbo la Bagamoyo.
Akipokea msaada huo,kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya sayona fruits na kampuni mama ya MMI ,Abubakary Mlawa,mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani alisema walimfuata mkurugenzi mtendaji  wa kampuni hizo Shubash Patel ambae amewatatulia tatizo lao.
Alieleza kuwa ufadhili huo ni mkubwa kwani awali halmashauri hiyo ilikuwa ikikabiliwa na mapungufu ya meza na viti 1,500 katika shule za sekondari lakini kwasa itabaki upungufu wa meza na viti 120.
Ridhiwani alisema wanaelekeza nguvu zao kuhakikisha wanamaliza tatizo hilo ifikapo mwezi octoba mwaka huu.
Alisema jitihada hizo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais John Magufuli na ya mikakati yake ya kukabiliana na changamoto katika sekta ya elimu hivyo halmashauri ya Chalinze inafanya kwa vitendo kuunga mkono mikakati hiyo.
Hata hivyo Ridhiwani alisema kuwa amejipanga na halmashauri ya Mji wa Chalinze kuendelea kutatua tatizo la meza,viti na madawati ili hali kumaliza hali hiyo na kubaki historia.
Alieleza kwasasa wanajielekeza katika kutatua tatizo la upungufu wa madarasa ambalo limejitokeza kutokana na mpango wa elimu bure.
“Tumejipanga kujielekeza katika tatizo lililoibuka la mahitaji mapya la madarasa ,maeneo mengine madawati sio tatizo lakini sasa yamejaa hadi walimu hawana nafasi ya kuandika kutokana na wingi wa wanafunzi “
“Tumetenga fedha kuanza ujenzi katika baadhi ya shule lakini pia tunaomba wahisani wajitokeza kuungana nasi kuboresha sekta ya elimu ili wanafunzi waweze kusoma kwenye manzingira mazuri”alisema Ridhiwani.
Ridhiwani alisema kuwa program hiyo inatarajia kumalizika ndani ya miaka mitatu kutokana na halmashauri yao kuwa bado changa .
Awali akikabidhi viti na meza kwa mbunge huyo, mwakilishi wa kampuni ya Sayona fruits ambae pia ni afisa mahusinao wa kampuni ya MMI  ,Abubakary Mlawa alisema wataendelea kushirikiana na jamii ili kutatua changamoto mbalimbali.
Alisema lengo la kusaidia vitu hivyo ni kuhakikisha wanafunzi wanakaa kwenye viti ,meza na madawati na kuondokana na kero ya kukaa chini.
Mlawa alisema wanatarajia kujenga kiwanda eneo la Mboga jimbo la Chalinze kutokana na hilo ni sehemu yao kushirikiana na jamii inayowazunguka ili kuinua maendeleo .
Nae mkuu wa shule ya sekondari ya Lugoba Abdallah Sakasa aliishukuru kampuni hiyo na kuueleza bado wana changamoto nyingi hivyo wasichoke kuwasaidia.
Sakasa alimuomba mwakilishi  huyo amfikishie salamu za shukrani mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Shubash Patel  ambapo walikabidhiwa choroko kilo 50 kama zawadi yao.

MWENYEKITI WA CCM DK MAGUFULI AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA CCM MJINI DODOMA

New Picture (3) 
Mwenyekitib wa CCM Dk JohnMagufuli akizunguza na wafanyakazi wa CCM Makao Makiiu yaCCM mjini
Dodoma leo.
……………………………………………………………………………..

Bashir Nkoromo

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa mara ya kwanza amekutana na kuzungumza na wajumbe wa Sekretarieti ya chama hicho na baadaye wafanyakazi wa CCM Makao Makuu katika Ofisi za Chama hicho Mjini Dodoma ikiwa ni siku tano tangu achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa Tano wa Chama hicho.
Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amekutana na watendaji hao wa CCM kwa lengo la kuwasalimia, kupokea maoni na ushauri wao juu ya utendaji kazi ndani ya Chama.
Katika mazungumzo hayo, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewapongeza watendaji wote wa Chama Cha Mapinduzi kwa kazi kubwa wanayoifanya na kwa namna ya pekee kwa jinsi walivyotoa mchango mkubwa kuhakikisha CCM inapata ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Pia amewataka kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa lengo la kuendelea kukiimarisha Chama hicho ambacho kimebeba dhamana ya kuongoza Serikali kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Dkt. Magufuli amewahakikishia kuwa chini ya uongozi wake atafanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi wa CCM ikiwemo maslahi duni, vitendea kazi na kuondoa utegemezi.
Aidha, Dkt. Magufuli amewataka watumishi wa chama kutoa ushirikiano katika zoezi la uhakiki wa mali za Chama litakalosimamiwa na sekretarieti ya chama na ameahidi kuwa atahakikisha mapato yatokanayo na vyanzo vya mapato vya chama yanatumika ipasavyo.
Kwa upande wao watumishi wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndugu Abdulrahaman Kinana wamempongeza Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa kwa asilimia mia moja na wajumbe wa Mkutano Mkuu uliofanyika tarehe 23 Julai, 2016 Mjini Dodoma kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa.
Watumishi hao wamemuahidi kuendeleza utumishi uliotukuka na wameelezea matumaini yao ya kuboreshewa maslahi.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.

SIHABA NKINGA: JITOKEZENI KUSAIDIA MAKAZI YA WAZEE NA WATU WENYE ULEMAVU NCHINI.

V1 V2 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akisalimiana na wazee alipotembelea Makazi ya kulea wazee ya Kolandoto leo Mkoani Shinyanga.
V3 
Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe akimkabidhi taarifa ya kituo hicho Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga wazee alipotembelea Mkazi hayo leo Mkoani Shinyanga.
V4 
Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe akimuleza Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga (kulia) changamoto za Makazi hayo na kumuomba kusaidia kusimamia utatuliwaji wa matatizo hayo ikiwemo ujenzi wa majengo kwa ajili ya malazi ya wazee hao, Katikati ni Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Amina.
V5 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongea na Wazee wanaoishi katika Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto leo Mkoani Shinyanga na kuwahakikishia serikali kuendelea kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili ili kuwawezesha kuishi katika mazingira rafiki. Katikati ni Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara hiyo Bi. Amina… na kushoto ni Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe
V6 
Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga sehemu ya nyumba zinazohitaji ujenzi kwa ajili ya Makazi ya Wazee hao. Wakati wa Ziara ya Kutembelea Makazi ya Wazee na kuona hali halisi ya makazi hao.

Simulizi Kambi ya Wazee ya Kolandoto mkoani Shinyanga, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Atoa Rai kwa Wadau.

MPIGA CHAPA MKUU WA SERIKALI ATOA TAMKO JUU YA MATUMIZI YA ALAMA ZA TAIFA.

C1Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.Cassian Chibogoyo akizungumza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano na waandishi hao katika kueleza jamii umuhimu wa kuzingatia matumizi sahihi ya vielelezo vya Taifa walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Julai 27, 2016 kulia kwake ni Afisa Habari Ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Nyamagory Omary.
C2Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.Cassian Chibogoyo akiwaonesha wanahabari (hawapo pichani) muonekano sahihi wa Nembo ya Taifa wakati wa mkutano wake na wanahabari Juali 27, 2016, wa kwanza kulia ni Afisa Habari Idara ya Habari Maelezo Bw.Frank Shijja.
C3Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.Cassian Chibogoyo akionesha baadhi ya Vielelezo muhimu vya Taifa wakati wa Mkutano wake na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi yake Julai 27, 2016.
C4Mtangazaji wa Televisheni ya Taifa Bw.Elisha Elia akiuliza swali kwa Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.Cassian Chibogoyo (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wake na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………………………………………
Na.MWANDISHI WETU
Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Cassian Chibogoyo amewataka wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya vielelezo vya Taifa kama njia ya kuheshimu Taifa na kuonesha uzalendo.
Chibogoyo ameyasema hayo hii leo katika kipindi cha pili cha ‘TUJITAMBUE’ ambacho kimewakutanisha waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari Jijini Dar es salaam kwa lengo la kutoa muendelezo wa  elimu sahihi ya vielelezo vya taifa kwa jamii.
Akitaja alama tatu muhimu za Taifa ambazo ni Bendera ya Taifa, Wimbo wa Taifa na Ngao ya Taifa, Chibogoyo amesema kila kimoja kinasimamiwa na sheria ili kuhakikisha matumizi yake yanaliletea heshima Taifa la Tanzania hivyo, wananchi ni vyema wakawa sehemu ya kutunza tunu hizo na kujiepusha na matumizi yasiyo sahihi.
Katika ufafanuzi wake ameeleza kuwa, Wimbo wa taifa una Tone Maalum na maneno maalum yaliyowekwa hivyo uimbaji unaoongeza vibwagizo kinyume cha uhalisia wake ni kosa kisheria.
Akielezea matumizi ya Bendera ya Taifa amesema ni kinyume cha sheria kubadili rangi zilizoainishwa kisheria kwani kila rangi ina maana yake na kuwa matumizi ya bendera serikalini yana utaratibu maalum kuanzia Ofisi ya Rais hadi kwa viongozi wa ngazi za chini.
“Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pekee ndiye anayeweza kufanya mabadiliko ya Bendera ya Taifa na Ngao ya Taifa kama kinavyoagiza kifungu cha 5 cha sheria ya vielelezo vya Taifa Na. 15 ya mwaka 1971.” Alisema Chibogoyo.
Kuhusu Nembo ya Taifa amesema ziko nembo nyingi feki mtaani ambazo pia zinatumiwa na wananchi katika matangazo au shughuli za kibiashara kinyume na matakwa ya sheria huku akitumia kipindi hicho kuonesha tofauti zilizopo katika alama sahihi na zile ambazo si, sahihi.
Bwana Chibogoyo alihitimisha kikao hicho kwa kuwashukuru wadau wote na kusema kuwa tarehe ya kikao kingine itatolewa kupitia Kitengo cha Mawasiliano Serikalini  Ofisi ya Waziri Mkuu.

MARAIS WASTAAFU NCHI ZA AFRIKA WAWASILI JIJINI DAR KUHUDHURIA MKUTANO MKUU WA UONGOZI WA MWAKA 2016


Rais mstaafu wa Afrika Kusini Mheshimiwa Thabo Mbeki (pichani kulia) akiwasili leo jijini Dar Es Salaam akiwa na Mwenyeji wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja,kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 utakoanza kesho hapa jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.Mkutano huo utakaodumu kwa siku mbili utawajumuisha wadau mbalimbali.
PICHA NA MICHUZI JR.MMG.

Raisi mstaafu wa Afrika Kusini Mheshimiwa Thabo Mbeki akisalimiana na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Mh. Thamsanga Dennis Msekelu baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 utakoanza kesho hapa jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro wa siku mbili.Pichani kati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa
Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja .

Raisi mstaafu wa Afrika Kusini Mheshimiwa Thabo Mbeki akizungumza na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Thamsanga Dennis Msekelu baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 utakoanza kesho hapa jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya
Hyatt Kilimanjaro.

Rais mstaafu wa Msumbiji, Armando Emilio Guebuza akikaribishwa na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya UONGOZI mara baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam kuhudhuria mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 unaotarajiwa kuanza hapo kesho jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro kwa siku mbili.

Rais mstaafu wa Msumbiji, Armando Emilio Guebuza akikaribishwa na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya UONGOZI mara baada ya kuwasili jioni ya leo jijini Dar Es Salaam kuhudhuria mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 unaotarajiwa kuanza hapo kesho jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya
Hyatt Kilimanjaro kwa siku mbili.

Rais Mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano akikaribishwa na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya UONGOZI mara baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam jioni ya leo kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 wa siku mbili,utakoanza hapo kesho jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.Pichani shoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya
UONGOZI Profesa Joseph Semboja .

PSPTB YAHITIMISHA MAFUNZO KWA WAKURUGENZI NA WAKUU WA IDARA MNH

01Mtoa mada Kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania  Meneja  Manunuzi  Fredy Mbeyella akitoa mada katika mafunzo  ya siku tatu juu ya  sheria ya manunuzi , mafunzo hayo yametolewa kwa wakurugenzi  na Wakuu wa Idara wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .
02 
Baadhi ya washiriki wa m

No comments:

Post a Comment