MKATABA KATI YA TTCL NA BHART AIRTEL WAISHA RASMI
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,MHANDISI RAMO MAKANI AFANYA KIKAO NA VIONGOZI WA HIFADHI YA TAIFA YA KISIWA CHA RUBONDO.
Naibu
Waziri wa Maliasilili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani ,akiviishwa vazi
maalum (Boya) ambalo hutumika kujiokoa wakati uafiri wa maji unatumika.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akitia saini katika
kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika hoteli ya Asilia Lodge
iliyopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
CHADEMA KUFANYA OPERESHENI UKUTA NCHI NZIMA, MBOWE ASEMA WAPO TAYARI KWA KAZI.
Baada ya kufanya kikao cha siku mbili hatimaye Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa tarifa ya kikao hicho pamoja na kutangaza makubaliano ambayo wameyafanya kupitia kikao hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kupitia kikao hicho wamekubaliana kuanzisha operesheni ambayo itafanyika kwa nchi nzima na kuwaagiza viongozi wa wilaya zote nchini wa Chadema kuanza vikao kujiandaa na operesheni hiyo.
Alisema kuwa operesheni hiyo ina lengo kupingana na ukandamizaji wa haki na demokrasia nchini ikiwepo kuzuiwa kufanya mikutano na hivyo kupitia operesheni hiyo ambayo itaandamana na mikutano wataweza kufikisha ujumbe wao kwa serikali kuhusu masikitiko yao ukandamizwaji wa haki na demokrasia.
“Tumefanya makubaliano ya pamoja kuwa Septemba, 1 tutafanya mikutano nchi nzima na mimi kama mwenyekiti nawaagiza viongozi wa chama wa kila wilaya kuanza kujiandaa na mikutano hiyo,
“Operesheni hii imepewa jina la UKUTA ikiwa na maana ya Umoja wa Kupinga Udikteta nchini sio iwe mtu mmoja ndiyo anakuwa na sauti kila jambo anataka kuliongoza yeye hizi ni dalili za udikteta,” alisema Mbowe.
Aidha alisema kuwa katika kutimiza azma yao wamejipanga kuhakikisha operesheni hiyo inafanyika na wapo tayari hata kama vyombo vya usalama vitataka kuingilia kati na kuwazuia.
“Ukiuliza kama nimejipanga na vyombo vya usalama unadhani nimejipanga na nini? tupo tayari na kila jambo na tumeamua ukiuliza tutafanyaje, ukitaka kuvuka mto subiri ukifika mtoni, tupo serious,
“Eti kwa sababu Mwingulu Nchemba amesema kuzuia mikutano wote tutulie … hili tamko tungelitoa tangu Novemba mwaka jana tukategemea tungeona busara lakini tunaona ubabe tu,” alisema Mbowe. Kwa hisani ya Mo Blog
TANZANIA NA KOREA ZATILIANA SAINI RUZUKU NA MKOPO NAFUU WENYE THAMANI YA TSH BILIONI 650
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Hamis Shaban na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo wakibadilishana Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo baada ya kusainiwa. Hati hiyo ina thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 650. Na Benny Mwaipaja,MoFP
SERIKALI za Tanzania na Korea Kusini, zimetiliana saini Hati ya Makubaliano (Aide Memoire) kwa ajili ya Ushirikiano wa utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo wa Maji, Nishati, Kilimo, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano-TEHAMA na Viwanda itakayogharimu Dola za Marekani Milioni 300, sawa na TSh.Bilioni 650, katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka 2016 hadi 2020.
Fedha hizo ni sawa na ongezeko la Dola Milioni 100 ikilinganishwa na kiasi cha Dola Milioni 200 ambazo nchi hiyo ya Korea iliipatia Tanzania kama mkopo wenye masharti nafuu katika kipindi cha miaka miwili iliyopita (2014 hadi 2016).
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaaban, ametia saini makubaliano hayo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, huku upande wa Korea Kusini ukiwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Fedha ya Korea Bw. Weon-Kyoung Jo.
Kusainiwa kwa makubaliano hayo ni mwanzo wa matayarisho ya kuandaa Mpango kazi wa namna ya kutekeleza miradi hiyo ili iende sambamba na Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa miaka 5 uliozinduliwa hivi karibuni mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Mkakati Mbadala wa Kupunguza Umaskini Zanzibar (MKUZA Successor Strategy).
Akizungumza mara baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaaban, amesema kuwa miradi hiyo ya maendeleo iliyochaguliwa kutekelezwa katika sekta zilizotajwa zitachochea ukuaji wa uchumi wa Taifa na kupunguza umasikini kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment