Pages

Monday, June 20, 2016

Wakulima wa zao la Shahiri wanaoshirikiana na TBL Group waadhimisha siku yao

Wakulima wa zao la Shahiri kanda ya Kaskazini mwa Tanzania wanaoshirikiana na kampuni ya TBL Group wameadhimisha siku yao wilayani Karatu ambapo mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha wakiwemo wadau wao kutoka SABMiller,na makampuni mengine yanayouza  madawa na pembejeo za kilimo.
Wakulima waliweza kufanya maonyesho mbalimbali  ya kazi zao pia walielezea mafanikio walioweza kuyapata kutokana na kilimo cha zao la Shahiri
SHAI1 
Maofisa wa SABMiller na wafanyakazi wa TBL wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho hayo ambapo pia TBL Group ilitunukiwa tuzo kwa kendeleza kilimo cha zao la Shahiri nchini
SHAI2Mkuu wa  Uendelezaji Kilimo cha Shahiri wa SABMiller kanda ya Afrika Thinus  Van Schoor akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakulima wa Shahiri
SHAI3 SHAI4 
Wakulima wa Shahiri wakitembeza wageni mashambani
SHAI5 
Naibu Waziri wa Kilimo,Chakula na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha (kulia) akimpongeza mkulima aliyejishindia zawadi ya kabati 2/4-Wakulima wa Shahiri wakitembeza wageni mashambani
SHAI6 
Naibu Waziri wa Kilimo,Chakula na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha (kushoto) akimpongeza mkulima wa Shayiri kutoka Kijiji cha Lendikinya wilaya ya Monduli,Masiaya Oloshuda aliyeshinda kwenye bahati nasibu ya kupata vifaa vya usalama shambani
SHAI7 
Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha akihutubia wananchi

KUPANDA MABASI YA MWENDO WA HARAKA JIJINI DAR ES SALAAM SASA NI KWA KADI HUDUMA HIYO KUANZA RASMI KESHO

 Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Udart),  David Mgwasa (kushoto),akionesha kipeperushi chenye maelezo ya matumizi ya kadi zitakazotumika katika mabasi hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Udart Jangwani jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart  katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart  katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Ofisa Habari UDART, Deus Bugaywa.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabar ukiendelea.
 
Na Dotto Mwaibale
 
MRADI wa Mabasi Yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (UDART) imeanzisha huduma kwa wateja wao za kutumia kadi maalumu wakati wa kupanda mabasi hayo itakayoanza rasmi leo.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa UDART,  David Mgwasa alisema wameanza kutoa huduma hiyo ya kadi ili kuwarahisishia wateja wao na kuondoa changamoto ya kusubiri tiketi kwa muda mrefu kabla ya kuondoka.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart  katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu alisema kwamba kwa kuanzia wametoa kadi 200,000 ambapo kila kadi itauzwa kwa shilingi 5000 ingawa bei halisi kwa kadi moja ni shilingi 500 na sh.4500 inayobaki itakuwa ni malipo ya mteja wao.
 
“Shilingi 4500 zitatumika kama malipo ya nauli kwa siku saba hadi nane kwa kwenda eneo lolote na kuwa kadi hizo zitapatikana katika vituo vya Kimara, Mbezi, Morocco, Gerezani, Posta na kuwa zitakuwa ni endelevu” alisema Rajabu
 
Aliongeza kuwa katika nchi nyingi zimekuwa zikitumia kadi hizo katika kusafirisha abiria na kuwa kwa hapa nchini ni huduma mpya ambayo itakuwa na changamoto zake kabla ya kuzoeleka.
Alisema licha ya kuanzisha huduma ya kadi bado ile ya risiti itaenelea kama kawaida ambapo alisema namna ya kujiunga na hu duma hiyo unatakiwa kupiga *152*22#

MTUMISHI WA MUNGU MASANJA MKANDAMIZAJI ARINDIMA KATIKA MKUTANO WA OYES 2016 JIJINI MWANZA.

Mhubiri na Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji, akihudumu katika Mkutano Mkubwa wa Injili wa Open Your Eyes and See OYES 2016 wenye lengo la kuwafungua watu wote kiroho na hivyo kuondokana na vifungo mbalimbali vinavyowakabiri, uliofanyika katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.
 
Mkutano huo ulianza June 12,2016 na kufikia tamati jana June 19,2016 katika viwanja vya Kanisa hilo. Wahubiri na waimbaji mbalimbali walihudumu katika mkutano huo akiwemo Mchungaji wa Kimataifa kutoka nchini Canada Mama Domitila Nabibone ambae amewahi kufariki na kufufuka siku ya nne, Mwimbaji na Mhubiri Joseph Rwiza pamoja na Mwimbaji Chamwenyewe Jembe ambapo watu wengi walifunguliwa kiroho na kuokoka katika mkutano huo.
Na George Binagi-GB Pazzo
 
Mhubiri na Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji, akihudumu katika Mkutano Mkubwa wa Injili wa Open Your Eyes and See OYES 2016, uliofanyika katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.
Mhubiri na Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji, akiimba katika Mkutano wa OYES 2016
Mhubiri na Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji, akiimba katika Mkutano wa OYES 2016
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola (Kushoto), akiwa na Mama Mchungaji, Mercy Kulola (Kulia) katika Mkutano wa OYES 2016
Mama Mchungaji, Mercy Kulola (kushoto) akiwa katika Mkutano wa OYES 2016
Mwimbaji Chamwenyewe Jembe (Kushoto) pamoja na Mhubiri na Mwimbaji Joseph Rwiza (Kulia) wote kutoka mkoani Morogoro wakiwa katika Mkutano wa Injili wa OYES 2016
Wazee wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakiwa katika Mkutano wa OYES 2016
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakiwa katika Mkutano wa OYES 2016
Ni katika Mkutano wa OYES 2016 ambao umewafungua watu wengi kiroho
Wakazi wa Jiji la Mwanza pamoja na Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakiwa katika Mkutano wa OYES 2016
Wakazi wa Jiji la Mwanza pamoja na Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakiwa katika Mkutano wa OYES 2016.

Ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari Prof Elisante Ole Grabriel katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.

dat1 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, kijiji cha Mtama  (hawapo pichani) wakati wa ziara yake katika Halmashauri Mkoa wa Lindi na Mtwara kuangalia usikivu wa vituo vya Redio na Televisheni vya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).dat2 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel( wa pili kulia) akizungumza na wawakilishi Kutoka Star Times wakati wa ziara yake katika Halmashauri Mkoa wa Lindi na Mtwara kuangalia usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kulia ni Mkurugenzi wa Shirika  hilo Dkt Ayoub Riyoba.
dat3 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja wawakilishi kutoka kampuni ya Star Times na wanakijijji wa kijiji cha Mtama wakati wa ziara yake katika Halmashauri Mkoa wa Lindi na Mtwara kuangalia usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashuri ya Lindi Bw. Matei Makwinya.
 
PICHA NA WHUSM

Serikali yaboresha matumizi ya kuandaa ramani kwa kutumia Drone

index 
Picha ya Angani zilizopigwa na Ndege Isiyo na Rubani (Drone) ambazo zinaaminika kuwa ni bora zaidi ya zile za awali.
…………………………………………………………………………………
Serikali imeanza hatua za awali za kufanyia utafiti wa ubora wa picha zinazopigwa na ndege isiyo na rubani katika matumizi ya kuandaa ramani.
Hadi sasa picha zilizopigwa zinaonyesha kuwa nzuri ambapo mafunzo zaidi juu ya matumizi ya picha hizo na jinsi ya kuandaa ramani yanahitajika.
Serikali ya Tanzania na ile ya Korea Kusini zinaendelea na mazungumzo ili Korea iweze kutoa mafunzo na ushauri wa kitaalam kuhusu matumizi ya drones katika kuchora ramani na kuhuisha ramani za siku nyingi.
Kwa kuanzia utaangaliwa uwezekano wa picha hizo kutumiwa kupanga ukuaji wa miji midogo kama Kibaigwa, Uvinza, Chanika na mingineyo ili ikue kimpangilio.

TANZANIA KUSHIRIKI MIAKA 65 YA JUNDOKAN KARATE 2018, NAHA CITY, OKINAWA, JAPAN.

 Mwalimu wa Karate wa kimataifa Sensei Rumadha 
 Magwiji wa karate duniani wakiwa katika picha ya pamoja katika kongamano la Karate European Jundokan Gasshuku.
………………………………………………………………………………….
Sensei Rumadha Fundi mwalimu wa karate mtanzania anatambuliwa na baraza
la OKINAWA
BODOKAN & KARATE FEDERATION” lenya makao Okinawa,Japan,juzi katika
alikuwa ni mwakilishi pekee kutoka Afrika katika kongamano la walimu
magwiji wa karate lilifanyika Lisabon,Ureno.
Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu ni chimbuko la  dojo iliyo
jengwa na Master Eiichi Miyazato miaka 63 iliyo pita huko mjini Naha,
Okinawa baada ya  kifo cha mwanzilishi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu ,
Master Chijun  Miyagi , ambayo hivi sasa  inaendeshwa na mtoto wake
Yoshihiro Kancho Miyazato.
Sensei Rumadha Fundi, amepokea na kukubali mwaliko kama
mwakilishi wa “JUNDOKAN SO HONBU” Tanzania ikiwa natumaini la usajiri wa
chama hicho hapa Tanzania ambao kwa sasa bado unalegalega.
Sensei Rumadha yupo nchi Ureno hivi sasa akishiriki katika kongamano la Karate ” European Jundokan  Gasshuku 2016″.
Na wakati huohuo, kitengo kinachisimamia ubora na uthabiti wa
sanaa asili ya mitindo ya  karate toka Okinawa kiitwacho ” OKINAWA
BODOKAN & KARATE FEDERATION” imefanya mabadiliko hivi karibuni
yatakayo tofautisha  karate asilia na ile ya  kimichezo itayo kuwa
katika michezo ya  Olympics.
Kutokana na mabadiliko ya  kimbinu na ufasaha yanayo onekana
katika michezo, shirikisho hilo limeamua kutofautisha kabisa jinsi
karate asilia izidi kuimarika na kutochujwa na kuwa sanaa nyepesi.
Pia, kuhakikisha kwa kiundani zaidi kwamba  mbinu halisi,
zinazingatiwa na ma- Sensei wote wa mitindo ya  karate toka visiwani
Okinawa duniania kote.
Hivyo ime teuwa timu ya Karate ya Okinawa ( Masters) toka
mitindo mbalimbali inayo tambulika na ” BUDOKAN” kusambaza uadilifu wa
mitindo hiyo kama jinsi ilivyokuwa  inafundisha na waasisi wake asilia.
Semina hii inayoendelea nchini Ureno inawawezesha walimu (
Sensei) kuwa na mabadiliko au kuendana sambamba na jinsi sanaa inavyo
jadiliwa katika chimbuko lake chini ya shirikisho hilo huko
Okinawa,Japan.
Tunatumaini kwamba chama cha “JUNDOKAN SO HONBU” kitapata
usajili wake nchini Tanzania pasipo fika mwaka 2018, chini ya Sensei
Rumadha Fundi mwakilishi wa “JUNDOKAN SO HONBU” Afrika mashariki na
Kati. Endapo usajili utaleta kulegalega na kuvuta muda zaidi, basi chama
hicho hakitakuwa na budi, bali kitajisajili visiwa vya Zanzibar kwanza.
Alimalizia hivyo; sensei Rumadha

MAKAMU WA RAIS AHIMIZA WATOTO KUPEWA ELIMU KATIKA MASHINDANO YA KUHIFADHI QURAN

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwasili kwenye ukmbi wa Diamond Jubilee ambapo kulikuwa na mashindano ya kuhifadhi Quran yalioandaliwa na Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Aisha Sururu.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akizungumza na Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Aisha Sururu  Bi. Aisha Sururu (kushoto) na Katibu wa Taasisi hiyo Bi. Joha Lemky wakati wa mashishindano ya kuhifadhi Quran yaliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
 Sehemu ya Viongozi waliohidhuria mashindano hayo ya kuhifadhi Quran
 Majaji wa Mashindano ya kuhifadhi Quran yalioandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya  Aisha Sururu kwenye ukumbi wa Diamond.
 Sheikh Muharami Mziwanda akitoa elimu juu ya umuhimu wa kuijua Quran kwenye mashindano ya Kuhifadhi Quran yaliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
 Kijana mwenye ulemavu wa macho Ali Hamisi Mpemba akisoma Juzuu 30 wakati wa mashindano hayo.

IGP Mangu -AKAGUA UJENZI WA KITUO KIPYA CHA KUPOKELEA SIMU ZA DHARURA (CALL CENTRE)

G1 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa kituo kipya cha kupokelea simu za dharura (CallCentre) wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo  ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kitazinduliwa hivi karibuni ikiwa ni hatua mojawapo  ya utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha usalama wa Jamii, unaotekelezwa na Jeshi la Polisi kwakushirikiana na Ofisi ya Rais, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi(PDB) katika mkoa wa Kipolisi Kinondoni ambapo kupitia kituo hicho wananchi wataweza kuripoti matukio na kupokelewa mapema tofauti na ilivyo hivi sasa.
G2 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa kituo kipya cha kupokelea simu za dharura (CallCentre) wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo  ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kitazinduliwa hivi karibuni ikiwa ni hatua mojawapo  ya utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha usalama wa Jamii, unaotekelezwa na Jeshi la Polisi kwakushirikiana na Ofisi ya Rais, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi(PDB) katika mkoa wa Kipolisi Kinondoni ambapo kupitia kituo hicho wananchi wataweza kuripoti matukio na kupokelewa mapema tofauti na ilivyo hivi sasa.
G3 
Askari Polisi wakiwa katika mafunzo maalumu ya kupokea simu katika kituo kipya cha kupokelea simu za dharura (CallCentre) ambacho kitazinduliwa hivi karibuni ikiwa ni hatua mojawapo  ya utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha usalama wa Jamii, unaotekelezwa na Jeshi la Polisi kwakushirikiana na Ofisi ya Rais, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi(PDB) katika mkoa wa Kipolisi Kinondoni  ambapo kupitia kituo hicho wananchi wataweza kuripoti matukio na kupokelewa mapema tofauti na ilivyo hivi sasa.
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

Watanzania waaswa kujifunza mchezo wa YOGA

Y5 
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza katika Siku ya Kimataifa ya Yoga iliyofanyika katika viwanja vya Coco kushiriki Siku ya kimataifa ya Yoga leo June 19, 2016 katikati ni Balozi wa  nchini Mhe. Sandip Aryan na kulia ni Mkuu wa Mkoa  wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda.
……………………………………………………………………………………………………………
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Watanzania wameaswa kujifunza mchezo wa Yoga ili kuimarisha miili yao na kujikinga dhidi ya matatizo mengi yanayosababishwa na mfumo wa maisha.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye mara baada ya kushiriki katika mahadhimisho ya  Siku ya Kimataifa ya Yoga yaliyofanyika katika viwanja vya Coco.
Mhe. Nape Nnauye alisema kuwa mchezo huo unatoa fursa kwa watu wa kabila, dini na mataifa mbalimbali kujumuika pamoja na kujifunza utamaduni na michezo mbalimbali.
“ Yoga sio kwa jamii ya kihindi peke yake ila ni kwa ajili ya watu wote Duniani na nawashauri watanzania wenzangu tujifunze mchezo huu kwa manufaa ya afya zetu na maendeleo ya michezo nchini”.Alisema Mhe. Nnauye.
Kwa upande wake Balozi wa India nchini Mhe. Sandip Arya ameshukuru Serikali kupitia Wizara ya abariHhhhhhahahahahwjvuajdsdhAISDUHDWWFUFWEGUA Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kutoa ushirikiano mkubwa  katika kufanikisha Siku ya kimataifa ya Yoga na kuahidi kuendelea kushirikiana zaidi katika kuendeleza michezo nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la Mchezo wa  Kabaddi ambao ni wasimamizi wa mchezo wa Yoga nchini Bw. Abdallah Nyoni amesema Siku ya kimataifa ya Yoga ni fursa kwa watanzania kujifunza mchezo huo hasa vijana ili kujenga uwezo kwa watanzania kushiriki katika michezo mbalimbali ikiwa ni juhudi za kuendeleza michezo na na kuongeza ajira nchini.
Yoga ni mazoezi ya kiroho na kimwili yenye asili katika falsafa ya Uhindi, hujumuisha umoja wa roho na mwili, mawazo na matendo na uelewa kati ya mwanadamu na mazingira yanayomzunguka pamoja na mtazamo wa kuijumla wa afya ya binadamu.
Desemba 11,2014,Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha mapendekezo na kukubali azimio ambalo lilitambua Juni 21 kila mwaka iwe siku ya Kimataifa ya Yoga kwa kusambaza taarifa zaidi kuhusu faidi za Yoga duniani.

THE POOL OF SILOAM CHURCH WAUOMBEA AMANI MKOA WA DAR ES SAALM NA TANZANIA KWA JUMLA, LEO


Wakili wa Mungu wa Kanisa la The Pool of Siloam, Elisha Eliya akiendesha sala maalum ya kuuombea amani mkoa wa Dar es Salaam na Tanzania kwa jumla wakati wa Ibada iliyofanyika leo, katika Kanisa hilo, Mbezi Makonde, jijini Dar es Salaam. 
 Wakili wa Mungu wa Kanisa la The Pool of Siloam  Church, Elisha Eliya akiendesha sala maalum ya kuuombea amani mkoa wa Dar es Salaam na Tanzania kwa jumla wakati wa Ibada iliyofanyika leo, katika Kanisa hilo, Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Bashir Nkoromo

MKOA wa Arusha, umefanikiwa kupata madawati 22, 756

ARUSHA 
Ahmed Mahmoud Arusha
………………………………………………..
MKOA wa Arusha, umefanikiwa kupata madawati 22, 756 na bado una upungufu wa madawati 2577 ili kukamilisha madawati 24,373 ambayo yanahitajika kwa ajili ya shule za msingi za mkoa ambazo hazina madawati.
Hayo yameelezwa jana na Katibu tawala  wa mkoa wa Arusha, Richard Kwitega, wakati wa kuwatunuku vyeti vya madaraja  matatu tofauti ya wadau waliochangia madawati kwa kutambua mchango wao katika kuboresha elimu kwenye hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa..
Kwitega, ambae ametunuku vyeti hivyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa, Daud Felix  Ntibenda, amesema mkoa huo una jumla ya wanafunzi 285,844 kuanzi darasa la kwanza hadi la saba mwaka 2016, na mahitaji ya Madawati  ni 119,765, yaliyokuwepo ni 95,394 .
Amewapongeza fanyabiashara  kwa moyo wao huo na lengo ni kuhakikisha ifikapo julai mosi hakuna mwanafunzi anae kaa chini
Akikabidhi hati hizo kulingana na mchango uliotolewa na kampuni,Kwitega, amesema  serikali inatambua na kuthamini moyo wao wa uzalendo wa kujitolea sehemu ya mapato yao kuchangia madawati kwenye shule za msingi mkoa wa Arusha.
Vyeti hivyo ni vya Fedha, Shaba na Dhahabu, ambapo waliochangia madawati 1 hadi 10,ambao ni 20,wametunukiwa hati a Fedha, waliochangia madawati 11 hadi 19 ,ambao ni 15 wametunukiwa hati za shaba na waliochangia madawati kuanzia 101, na kuendelea ambao ni 5 wametunukiwa hati za dhahabu.
Akizungumza kwenye hafla hiyo mkuu wa mkoa wa Arusha,Daud Felix  Ntibenda, amewaomba wafanyabiashara hao kuendelea kuchangia madawati 2577 yanayohitajika ili kukamilisha mahitaji ya mkoa ambayo ni 24,337.
Amesema katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa ameunda timu ya wataalamu kwendalaya zote na shule zote ili kujiridhisha kama madawati yanatosheleza au bado kuna upungufu.
Ntibenda, amesema Juni 18 ,2016, anaanzisha zoezi la kupita kwenye maduka makubwa na viwanda kwa ajili ya kukusanya madawati yaliyopungua.
Amesema wapo baadhi ya wafanya biashara wakubwa hawajaitikia wito huo hivyo kutumia utaratibu huo wa kuwapitia wataweza kuchangia madawati.
Ntibenda, amesema Julai mosi mwaka huu anaenda kuwsilisha taarifa ya madawati kwa Rais, hivyo hayuko tayari kufukuzwa vkazi kwa kushindwa kufikia malengo ya madawati katika mkoa  wakati wapo watu wenye uwezo hawajatoa michango yao.
Ameongeza kuwa ameshakutana na watumishi wa serikali waliopo chini ya ofisi ya Katibu tawala wa mkoa ili nao kila mmoja achangie dawati moja  kwa kuwa nao wana watoto waliopo shuleni na tayari amechangia madawati 692.

Waziri wa michezo Nape nnauye ashiriki Siku ya Kimataifa ya YOGA.

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimia na Balozi wa India nchini Mhe. Sandip Arya mara
baada ya kuwasili katika viwanja vya Coco kushiriki Siku ya kimataifa ya Yoga leo June 19, 2016.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na Balozi Peter Kallaghe kutoka Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika viwanja vya Coco kwenye hafla ya
 kuadhimisha  Siku ya kimataifa ya  Yoga leo June 19, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza katika Siku ya Kimataifa ya Yoga iliyofanyika katika viwanja vya Coco
leo June 19, 2016 kushoto ni Balozi wa India nchini Mhe. Sandip Arya .
 Balozi wa India nchini Mhe. Sandip Arya akizungumza katika Siku ya Kimataifa ya Yoga iliyofanyika katika viwanja vya Coco leo June
19, 2016 kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza katika Siku ya Kimataifa ya Yoga
iliyofanyika katika viwanja vya Coco kushiriki Siku ya kimataifa ya Yoga leo June 19, 2016 katikati ni Balozi wa
 nchini
Mhe. Sandip Aryan na kulia ni Mkuu wa Mkoa
 wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akifanya mazoezi mbalimbali katika kuadhimisha Siku ya kimataifa ya Yoga iliyofanyika Leo June 19, 2016 Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akifanya mazoezi katika kuadhimisha Siku ya kimataifa ya Yoga iliyofanyika Leo
June 19, 2016 Jijini Dar es salaam kulia ni Balozi Peter Kallaghe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI ATEMBELEA KITUO CHA UHAMIAJI CHA HOROHORO

1 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto), akisalimiana na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama, mara baada ya kuwasili katika kituo cha Uhamiaji Horohoro,wilayani Mkinga mpakani mwa Kenya na Tanzania, barabara kuu ya Mombasa-Tanga.Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
2 
 Katibu Mkuu  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akiweka saini katika kitabu cha wageni, mara baada ya kuwasili katika kituo cha Uhamiaji Horohoro, wilayani Mkinga mpakani mwa Kenya na Tanzania, barabara kuu ya Mombasa-Tanga.Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti  njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
3 
Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Horohoro, DCI Deogratius  Magoma, akimuelekeza jamboKatibu Mkuu  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira mara baada ya ukaguzi wa ofisi za jengo la kituo hicho zinazotumika katika utoaji huduma za uingiaji na utokaji wa raia wa kigeni na raia wa Tanzania wanaopitia mpaka wa horohoro , wilayani Mkinga, jijini Tanga. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi.
4 
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga,DCI Andrew Kalengo, akimuelekeza jambo  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira,mara baada ya kutembelea daraja la Mwakijembe, linalotumiwa na wakazi wa nchi za Tanzania na Kenya. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi.
5 
Katibu Mkuu  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (aliyevaa kiraia), akifafanua jambo kwa viongozi wa Idara ya Uhamiaji Wilayani Nkinga, mara baada ya kutembelea jiwe linaloonyesha mpaka kati ya Tanzania na Kenya katika kijiji cha Jasini kilichopo Kaunti ya Kwale. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua  na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
6 
Katibu Mkuu  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto), akionyeshwa namba za jiwe la mpaka unaotenganisha nchi za Kenya na Tanzania mara baada ya kutembelea kituo cha Uhamiaji Horohoro. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua  na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

MAKAMU WA RAIS KUSOMESHA WATOTO 100

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye Tamasha Fadhili Mtoto Asome pamoja na Binti Clubs iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Binti Foundation ambapo aliahidi kuwasomesha watoto 100 na  aliwasihi Wanawake wanapoweka mipango ya kimaendeleo kuwashirikisha pia wanaume.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwa pamoja na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa mara baada ya uzinduzi wa Binti Clubs jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya watu waliojitokeza kwenye Tamasha Fadhili Mtoto Asome pamoja na Binti Clubs iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Binti Foundation ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akipitia kitabu cha Binti Foundation wakati wa Tamasha Fadhili Mtoto Asome.

TAIFA LINAZALISHA WAHANDISI WENGI KULIKO MAFUNDI SANIFU HIVYO KUKOSA MAENDELEO

Arusha.. 
Na Mahmoud Ahmad Arusha
—————————-
Taifa letu linahitajia kuangalia kwa mapana takwimu za wahitimu wahandisi ni wengi kuliko wahitimu mafundi sanifu kutokana na hali hiyo huduma za kihandisi na za ufundi hazitakidhi matakwa ya maendeleo yanayotarajiwa na itakuwa vigumu kufikia malengo makuu ya dira ya maendeleo ya Tanzania 2025 na pia ya MKUKUTA awamu ya pili.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu mkuu wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi Maimuna Tarishi kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo Prof Joyce Ndalichako wakati wa uzinduzi wa maabara ya skimu ya umwagiliaji (Hydraulics Engineering) iliyojengwa na shirika la misaada la Japan(JAICA)kwenye chuo cha ufundi Arusha jijini Arusha.
Alitanabaisha kuwa Mashirika ya kimataifa yamekuwa kupendekeza kuwa na uwiano kwa kila mhandisi mmoja pawepo na mafundi watano na mchundo 25 ilikuweza kuleta maendeleo ipasavyoi katika nchi yetu.
Tarishi alisema kuwa kasi ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji nchini ni ndogo kwa sababu ya uhaba wa maofisa ugani na wataalamu mbali mbali wa umwagiliaji wenye uwezo wa kusimamia utekelezaji hasa kwenye ngazi ya halmashauri zetu hapa nchini,chuo kama sehemu inatakiwa kubuni mbinu mbadala za kuweza kutowa na kuandaa mipango ya masomo yatakayosaidi upatikanaji wa ajira kwenye soko la ajira.
“Changamoto ya kupata ajira kwa baadhi ya waajiri hawajajumuisha hii kada ya uhandisi ujenzi na umwagiliaji katika(Scheme of service) zao hivyo basi tunaomba waajiri wote kujumuisha kada hii muhimu katika(Scheme of service)zao ili kutatua changamoto hii na kuongeza tija katika kazi zetu za kilimo cha umwagiliaji”alisema Tarishi
Aidha katibu mkuu huyo alitanabaisha kuwa kutokana na hali hiyo tunaomba kuwa program za ufundi sanifu zipewe kipaumbele kwani taifa lenye rasilimali nyingi litanufaidika na rasilimali hizo tu iwapo litaziongezea thamani(processing and value addition)kabla ya kuuzwa vinginevyo taifa hilo litachuuza hizo rasilimali na halitaendelea.kwani mafundi saniu mahiri ni mhimili mkuu wa kuongeza thamani ya rasilimali zetu.
Kwa upande wake balozi wa japani hapa nchini Masaharu Yoshinda wakati akikabidhi mradi huo kwa serikali ya Tanzania alisema kuwa mradi huo wa mashine ya umwagiliaji ni mkubwa na mashine ya aina hiyo haipo katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati na itasaidia nchi ya Tanzania kuwajenga wataalamu wa masuala ya umwagiliaji na kukuza kilimo cha umwagiliaji nchini kwenu.
Alisema kuwa serikali ya Japan itaendelea kutoa wataalam katika kuhakikisha utaalamu huo unawafikia watanzania wote ilikukuza uchumi wa nchi yenu kwa kuweza kukuza uzalishaji na hatimaye viwanda.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Ufundi Arusha dkta Richard Masika alisema kuwa mradi huo utasaidia chuo na vyuo vyengine kuweza kuinua taaluma kwani mashine hiyo itasaidia kukuza na kuweka mezania kwa wahitimi na kwenda kufanya vizuri katika kukuza kilimo cha umwagiliaji hapa nchini.
Alisema kuwa serikali ya Japan imekuwa mstari wa mbele katika kujengea uwezo chuo kupitia ufadhili wa mfuko wa chakula wa pamoja kati ya Tanzania na Japan(TJFACF) Kwa wanachuo na chuo wamejengewa uwezo wa kufundisha program ya uhandisi ujenzi na umwagiliaji kupitia mradi”kujenga uwezo wa wanataaluma katika kutoa mafunzo ya uhandisi Umwagiliaji yaani (ATC irrigation human Resoursces Development Programme AIHRDP)Unaofadhiliwa na serikali hiyo.

MAJALAIWA AKUTANA NA WADAU WA ZAO LA PAMBA.

TAM1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na wadau wa  zao la pamba kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni 17, 2016. Kulia kwake ni Wazieri wa Kilimo,  Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mku)
TAM2

KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM JIJINI DAR

KAMA01Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akifungua Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM kwenye Ofisi Ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Juni 18, 26. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM , Abdulrahman Kinana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu))
KAMA1 
Makamu wa Rais Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi  wakifuatilia kikao cha Kamati  Kuu ya CCM kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwenye Ofisi ndogo ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Juni 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KAMA2 
Baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Rais Mstaafu Jakaya Kikwete wakati alipofungua kikao chao kwenye Ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Juni 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KAMA3Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto) pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Dk. Tulia Ackson mara baada ya kumaliza kikao maalum kwenye ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es salaam ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
KAMA4 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Dk. Tulia Ackson mara baada ya kumaliza kikao maalum cha Kamati Kuu ya CCM  kilichofanyika , Makao makuu ya CCM, Ofisi Ndogo Lumumba(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
SENDE

MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU MAKATIBU WAKUU WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR WAPATIWA MAFUNZO YA UONGOZI

KIT01 
Wakufunzi wa mafunzo ya Uongozi kutoka Chuo cha Uongozi Institute Dkt. Jochen Lohmeier (kushoto) na Nathaniel Mjema wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza mafunzo ya siku tatu kwa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wa Serikali ya Zanzibar yaliyofanyika katika Ofisi Mdhibiti na  Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Maisara Mjini Zanzibar.
KIT1 
Mkufunzi Nathaniel Mjema akiwasilisha mada ya  kujitathmini kwa viongozi wanaoshiriki mafunzo ya uongozi yaliyowashirikisha Makatibu wakuu na wasaidizi wao.
KIT2 
Waratibu wa Mafunzo hayo wakifuatilia kwa kina uwashilishwaji wa mada mbali mbali zilizowasilishwa katika mafunzo hayo.
KIT4 
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum akitoa mchango katika mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya  Maendeleo endelevu yaliyowashirikisha Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu wa Serikali ya Zanzibar.
KIT6Dkt. Jochen Lohmeier kutoka Uongozi Institute akitoa mada kuhusu kuitathmini Jamii katika mafunzo ya Makatibu wakuu na Wasaidizi wao yanayofanyika Ofisi ya CAG Maisara, Mjini Zanzibar.
KIT7 
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Ali Khalil Mirza (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Juma Ali Juma wakinakili mafunzo hayo.
KIT8 
Washiriki wa mafunzo hayo wakibadilishana mawazo na kujadiliana kutokana na kazi waliyopewa na wakufunzi wao.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

MFUKO WA PENSHENI WA PPF WAANDAA FUTARI KWA WAFANYAZI WAKE, DAR

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (kushoto) akiongozana na mgeni Ramsi Kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA, Sheikh Ali Hamis, wakati alipofika kwenye Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam jana Juni 17, 2016 kwa ajili ya kumwakilisha Mufti  Mkuu wa Tanzania katika Hafla ya Futari
iliyoandaliwa na Mfuko huo. Picha na Mafoto Blog
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (katikati) mgeni Ramsi Kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA, Sheikh Ali Hamis, wakiwaongoza wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, kuchukua Futari wakati wa hafla Futari iliyoandaliwa na Mfuko huo katika Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam jana Juni 17, 2016.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla
hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla
hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla
hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla
hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akizungumza na wafanyakazi wa mfuko wake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na mfuko huo  kwenye Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam, jana Juni 18, 2016. Kushoto ni mgeni rasmi, Sheikh Ali Hamis. 
 Mgeni rasmi Sheikh Ali Hamis, akizungumza na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF,(hawapopichani)  wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na mfuko huo  kwenye Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam, jana Juni 17, 2016. Katikati ni Mkurugenzi mkuu wa Mfuko huo, William Erio.
*********************************************
Na Mwandishi Wetu, Dar
JAMII imetakiwa kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwani mfuko huo ni faraja kwa Watanzania na unaofanya mambo makubwa kwa lengo la kuwasaidia wananchi.
Wito huo umetolewa na mwakilishi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Ali Hamis wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na uongozi wa mfuko huo kwa wafanyakazi wake.
Alisema kuna faida kubwa kwa wananchi kujiunga na mfuko huo kwani watafaidika na mafao mbalimbali yanayotolewa na PPF. Aidha Sheikh Hamis alisema kuwa ipo haja kwa watendaji wa mfuko huo kuendelea kuwaelimisha wananchi ili waendelee kujiunga na PPF.
Alifurahishwa na namna uongozi wa mfuko huo ulivyoandaa hafla ya futari hiyo maalum kwa kuwafuturisha wafanyakazi wake na kwamba hilo ni jambo jema kwani wafanyakazi wanafahamiana na kubadilishana mawazo.
Sheikh Hamis aliitaka jamii kuwaenzi waasisi wa taifa hili kwa kuendelea kudumisha Amani na umoja kwani wamefanya jambo jema la kuwafanya wananchi wote kuwa kitu kimoja bila kujali dini wala kabila.
Kwa mujibu wa Sheikh Hamis,  PPF ni aina ya mfuko unaowawezesha wananchi kujikomboa.

Hivyo ameuomba uongozi wa mfuko huo uendelee na jitihada za kuwafikia wananchi kwenye maeneo mbalimbali hapa nchi na hasa maeneo ya vijijini.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa PPF, William Erio aliwashukuru wafanyakazi kwa kushiriki futari hiyo,ambayo imekuwa ikiandaliwa kika mwaka na kuwashirikisha wafanyakazi wake wote. Naye mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi TUICO aliushukuru uongozi wa mfuko huo kwa kuwaandalia futari hiyo.
Futari hiyo ilihudhuriwa na wafanyakazi wa PPF kutoka makao
makuu, kanda za Ilala, Temeke na Kinondoni.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko huo wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi katika hafla hiyo, Sheikh, Ali Hamis, wakati wa hafla hiyo. 
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko huo wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi katika hafla hiyo, Sheikh, Ali Hamis, wakati wa hafla hiyo. 
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, Tawi la Tuico, akiwashukuru wafanyakazi wa mfuko huo kwa kushiriki kikamilifu katika hafla hiyo.
 Sheikh Mohamed Ali, kutoka Baraza Kuu la Waislam Tanzania
BAKWATA, akiomba dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MOR

MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI AKABIDHI VYAKULA VYA FUTARI KWA VITUO VINNE VYA KULEA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM

JAM1 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akikabidhi sehemu ya vyakula hivyo kwa Mwenyekiti wa Kituo cha Charambe Islamic Center Dkt. Haruni Kondo aliyepokea kwa niaba ya vikundi vigine vinne. Mke wa Rais amekabidhi mchele kilo 500, sukari kilo 500 na tende kilo 28, tukio hilo limefanyika katika ofisi ya Mke wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam.
JAM2 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akikabidhi sehemu ya vyakula hivyo kwa Mwenyekiti wa Kituo cha Charambe Islamic Center Dkt. Haruni Kondo aliyepokea kwa niaba ya vikundi vigine vinne. Mke wa Rais amekabidhi mchele kilo 500, sukari kilo 500 na tende kilo 28, tukio hilo limefanyika katika ofisi ya Mke wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam.
JAM3 
Khalifa wa Zawiyatul lqadiria, Abas Hamdan watatu kutoka kulia akiongoza dua ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na viongozi wengine wakuu wa serikali mara baada ya tukio la kukabidhi vyakula hivyo. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri mkuu Mama Marry Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali vya vikundi vya kulea watoto yatima na watu waishio kwenye mazingira magumu.
JAM4 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa na  mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa vikundi vya kulea watoto yatima na watu waishio kwenye mazingira magumu. Tukio hilo limefanyika katika Ofisi za Mke wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam.
JAM5 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Mama Mlezi wa Kituo cha Charambe Islamic Center Asile Zahali mara baada ya kukamilika zoezi la utoaji wa vyakula mbalimbali kwa vituo vinne vya kulea watoto na watu waishio kwenye mazingira magumu.
JAM6
JAM7 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa na mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa vituo hivyo kabla ya kuwakabidhi vyakula hivyo katika Ofisi yake Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
……………………………………………………………………………………………………………………….
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli amekabidhi chakula kwa ajili ya futari wakati huu wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa vituo vinne vya kulea watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu Jijini Dar es salaam.
Vyakula hivyo vimekabidhiwa leo tarehe 18 Juni, 2016 katika ofisi ya Mke wa Rais Ikulu Jijini Dar es salaam vimejumuisha Mchele kilogramu 500, Sukari kilogram 500 na Tende kilogramu 28.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vyakula hivyo, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli aliyeongozana na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewatakia heri Waislamu wote katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuwasihi waendelee kuliombea Taifa amani na utulivu.
 (“Tunawatakia mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, katika kipindi hiki tunawaomba mzidi kuiombea nchi yetu amani, viongozi wetu wa nchi na watanzania wote kwa ujumla, nchi ikiwa na amani ndio mambo mengi mazuri yanaweza kufanyika”)
Kwa niaba ya vituo vilivyopatiwa vyakula hivyo, Mwenyekiti wa Kituo cha Charambe Islamic Center Dkt. Haruni Kondo amemshukuru Mke wa Rais kwa kutoa vyakula hivyo na ameeleza kuwa kitendo hicho kinaonesha mshikamano na ushirikiano walionao watanzania wote bila kujali tofauti ya dini, kabila wala maeneo wanayotoka.
 (“Kwa hiyo ndugu zangu mna imani ya kikristo lakini mnatambua waislamu ni ndugu zenu, wote tunajenga nyumba moja, mshikamano ndio tunu tuliyoachiwa na Baba yetu wa Taifa, leo mmeguswa kuona wenzenu tunafanya ibada na nyinyi mmeingia kwenye ibada, sasa ibada ya kutoa ni ibada kubwa sana, sio nchi nyingi katika Afrika zinafanya kitendo hiki, watu hawaelewi, ni nchi chache sana ambazo imani moja inaunga mkono imani nyingine, lakini sisi waislamu tunalitambua hili hata toka kipindi ambacho mtume wetu SWA anapigana kusimika dini hii kwa waumini alipata nusura kwa wakristo”) 
Vituo vilivyokabidhiwa vyakula hivyo ni Charambe Islamic Center, Tasofe Lqadiria, Nur Twarigatu Lqadiria na Zawiyatul Lqadiria.

Wanachama wa Chama cha waajiri wafanya ziara ya mafunzo TBL

JE1 
Meneja usalama ,afya na mazingira wa TBL Group Renatus Nyanda,akitoa mafunzo kwa wanachama wa Chama cha waajiri Tanzania( ATE) wakati walipokwenda kujifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na usalama sehemu za kazi kwenye kiwanda cha  TBL Ilala jijini Dar es Salaam.
JE2Wanachama wa Chama Cha Waajiri Tanzania(ATE) wakimsikiliza kwa makini mtaalam wa upishi wa TBL Group  Castor Masawe, kuhusiana na  uzalishaji wa bia unavyofanyika.
JE3Wanachama wa Chama cha Waajiri (ATE) wakipewa maelekezo na Meneja usalama ,afya na mazingira wa TBL Group Renatus Nyanda wakati walipotembelea chumba cha maabara cha TBL Ilala jijini Dar es Salaam
JE4Wanachama wa Chama cha Waajiri (ATE) wakipewa maelekezo na Meneja usalama ,afya na mazingira wa TBL Group Renatus Nyanda wakati walipotembelea chumba cha maabara cha TBL Ilala jijini Dar es Salaam
JE5 
Baadhi ya wanachama cha Waajiri Nchini (ATE) wakiangalia vikombe vya tuzo mbalimbali ambavyo TBL Group ilishinda
………………………………………………………………………………………………
Kutokana na kampuni  ya TBL Group kuonyesha mafanikio ya kuwa mwekezaji bora nchini na mchango wake kutambuliwa na taasisi mbalimbali kwa kuitunukia tuzo ,imekuwa kivutio kikubwa kwa taasisi zinazotaka kupata mafanikio  kwa kutembelea viwanda vyake kwa ajili ya kupata mafunzo na uzoefu na kujua siri ya mafanikio.
Wanachama wa Chama cha Waajiri nchini (ATE) wamefanya ziara katika kiwanda cha TBL cha Ilala ambako wamepatiwa mafunzo ya usalama kazini ikiwemo kuona uzalishaji unavyofanyika kiwandani hapo.
Meneja Usalama,Afya na Mazingira wa TBL Group,Renatus Nyanda aliwapatia somo la kanuni za usalama zinazotekelezwa na kampuni hiyo ambazo zinalenga kulinda usalama wa wafanyakazi wanapokuwa kazini na nje ya kazi ikiwemo wageni mbalimbali wanaofika kiwandani hapo.
Wanachama hao walifurahishwa na mafunzo hao ikiwemo mkakati wa  kampuni hiyo kuendelea kufanya uwekezaji unaozingatia utunzaji wa mazingira,kuchangia kuendeleza uchumi wa taifa,kupunguza tatizo la ajira na kubadilisha maisha ya jamii kuwa bora.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI ZA UCHANGIAJI WA UJENZI BWENI LA MWANACHUO WA KIKE KATIKA CHUO KIKUU CHA MZUMBE

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika Siku ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Uzinduzi wa Kampeni za Uchangiaji wa Ujenzi wa Bweni la Wanachuo wa Kike.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika Siku ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Uzinduzi wa Kampeni za Uchangiaji wa Ujenzi wa Bweni la Wanachuo wa Kike ambapo aliwashi mabinti kuzingatia masomo kwanza kabla ya kuingia kwenye mambo mengi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua rasmi kampeni za uchangiaji wa ujenzi wa bweni la wanachuo wa Kike.
 Wanafunzi wa Chuo Cha Mzumbe wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Siku ya Wahitimu wa Chuo Kikuuu cha Mzumbe na uzinduzi wa kampeni za uchangiaji wa ujenzi wa bweni la wanachuo wa kike.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Bernadetha Msigwa mwanafunzi wa chuo cha Mzumbe ambaye amepoteza uwezo wake wa kuona na anasubiri kwenda nje kwa matibabu.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kitabu chenye orodha ya majina ya wanachuo waliohitimu katika chuo cha Mzumbe
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Msanii maarufu wa kuigiza sauti za Viongozi anayejulikana kwa jina la JK Komedian
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali wakati wa sherehe ya Siku ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Uzinduzi wa Kampeni za Uchangiaji wa Ujenzi wa Bweni la Wanachuo wa Kike Kampasi Kuu mjini Morogoro, Waliokaa kutoka kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako na Mkuu wa Chuo cha Mzumbe,Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Barnabas Samatta, kulia ni Mkuu wa mkoa wa Moro Mhe. Steven Kebwe na Rais wa Baraza la la Masajili,chuo kikuuu Mzumbe Bw. Ludovick Utouh

TANGAZO LA SHULE

index

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE CHAFANYA KONGAMANO KUHUSU UADILIFU NA UTAWALA BORA KATIKA KUSIMAMIA RASILIMALI ZETU

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dk.Lenard Akwilapo akikabidhiwa picha na Mwakilishi Makazi wa Shirika la KAS, Daniel El-Noshokaty ya waasisi wa ushirikiano kati ya Tanzania na Shirika lisilo la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) la nchini Ujerumani, Hayati Mwalimu Julius Nyerere (kushoto pichani) na Konrad Adenauer (kulia), wakati wa Kongamano la la kitaifa na kimataifa lililokuwa na mada yake kuu uadilifu wa viongozi na utawala bora katika usimamizi wa maliasili kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Tanzania lililofanyija  katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Dar es Salaam juzi.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Bara, Philip Mangula akichangia jambo kwenye kongamano hilo.
Taswira katika ukumbi wakati wa kongamano hilo

NAIBU SPIKA AKUTANA NA UJUMBE WA WABUNGE KUTOKA BUNGE LA CHINA

 Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akisalimiana na Kiongozi wa Msafara wa Ujumbe wa Wabunge wa Kamati ya Mambo ya  Nje kutoka Bunge la China ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe  Zhang Haiyang wakati alipofanya mazungumzo na Kamati hiyo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akizungumza na Ujumbe wa Wabunge wa Kamati ya Mambo ya  Nje
kutoka Bunge la China
  kushoto  ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe  Zhang Haiyang ambaye pia ni Kiongozi wa
Msafara huo.
 Kiongozi wa Msafara wa Ujumbe wa Wabunge wa Kamati ya Mambo ya  Nje kutoka Bunge la China ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe  Zhang Haiyang (katikati) akisanini Kitabu cha Wageni alipomtembelea Naibu Spika Dkt Tulia Ackson ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.
 Kiongozi wa Msafara Ujumbe wa Wabunge wa Kamati ya Mambo ya  Nje kutoka Bunge la China ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe  Zhang Haiyang  akimkabidhi Naibu Spika Dkt Tulia Ackson zawadi mara baada ya kuzungumza nae ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.
Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akiangalia zawadi aliyopewa na  na Kiongozi wa Msafara Ujumbe wa Wabunge wa Kamati ya Mambo ya  Nje kutoka Bunge la China ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe  Zhang Haiyang
mara baada ya kuzungumza nao ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.
(Picha na Ofisi ya Bunge)

WAFANYAKAZI WA HOTELI YA SOUTHERN SUN WAFANYA USAFI KWENYE FUKWE ZA BAHARI YA HINDI

WAFANYAKAZI  wa Hoteli ya Southern Sun ya jijini Dar es Salaam leo wameadhimisha Siku ya Usafi wa Fukwe za Bahari Duniani kwa kufanya usafi wa kwenye fukwe za maeneo ya Salender Bridge jijini Dar es Salaam.
 
Wafanyakazi hao wamesema wamechukua hatua hiyo ili kuthamini siku hiyo inayoadhimishwa duniani kote na kuionesha dunia kwamba Tanzania ni moja ya nchi zinazojali hatua hiyo ya kuziweka fukwe za bahari katika hali ya usafi kwa ajili ya kuviokoa viumbe mbalimbali vinavyoishi baharini.
Aidha akizungumza na Blog ya Bayana Mratibu wa shughuli hiyo, Halima Nneka, alisema kuwa hiyo wao imekuwa ni tabia yao ya kufanya usafi kwenye sehemu mbalimbali za fukwe za bahari kwa kuwa wanathamini sana mazingira hayo kuwa katika hali ya usafi kwani inasaidia hata vijana na watu wanaotembelea maeneo hayo kujali na kuiga mfano wao huo.
“Kwakweli huwezi ukaenda pahala ambako ni safi, halafu wewe uitumie sehemu hiyo na kisha  uiwache ikiwa katika hali ya uchafu. Kwa mtu mstaarabu lazima naye atafanya usafi katika sehemu hiyo, aliyoikuta ikiwa safi kabla ya kuitumia,”alisema Mneka.
Aidha amezitaka Taasisi mbalimbali jijini Dar es Salaam, zilizoko kwenye maeneo ya Bahari kutenga walau hata siku moja katika mwezi kwa ajili ya kufanya usafi wa mazingira kwenye sehemu za fukwe za bahari, kwani ni sehemu ambazo jamii na wageni mbalimbali wanaoingia nchini hupenda kutembelea kwa ajili ya kupumzika na kupata hewa safi.
Wafanyakazi wa Hoteli ya Southern Sun ya jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kufanya usafi kwenye fukwe za maeneo ya Salender Bridge jijini Dar es Salaam, katika kuadhimisha Siku ya Usafi wa Fukwe za Bahari Duniani leo. 

KAMPUNI YA TING YATOA MAGETI YA CHUMA KUDHIBITI WEZI WA KOKI ZA MAJI UWANJA WA TAIFA

Naibu Waziri wa Habari, Uramaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia James Wambura (wane kushoto), akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ting, Father Fernandez, wakati akipokea msaada wa mageti kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Juni 17, 2016. Kampuni hiyoimetoa mageti 27 yenye thamani ya shilingi milioni 44.


NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID KAMPUNI
———————————————————————-
YA kusambaza ving’amuzi vya televisheni ya Ting ya jijini Darves Salaam, imekabidhi mageti ya chuma  27 kwa
uongozi wa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam ili kuwadhibiti “wakora” wanaoingia kwenye vyoo na kuiba koki za maji.
Akipokea msaada huo leo Juni 17, 2016 kwenye hafla fupi iliyofanyika uwanjanin hapo,
Naibu Waziri wa Habri, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia James Wambura, ameishukuru
kampuni hiyo kwa msaada huo ambao utakomesha vitendo vya wizi na uharibifu wa miundo mbinu ya uwanja huo wa soka wa kisasa kabisa hapa nchini “Mwanzoni mwa mwezi wa tatu mwaka huu, nilifanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya
uwanja huu na kujionea uharibifu mkubwa kwenye vyoo ambapo koki za maji zimeibiwa na hivyo kusababisha baadhi ya vyoo kufungwa na kupelekea usumbufu mkubwa kwa mashambiki was ok.” Alisema Naibu waziri. Naye Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Ting, Mchungungaji Dkt. Veron Fernandos, alisema kampuni yake ambayo inajishughulisha na uagizaji na usambazaji wa ving’amuzi, imeona inao wajibu mkubwa wa kusaidia sekta ya michezo kwenye eneo hilo la kutunza
miundombinu ya uwanja wa Taifa.
Alisema, Ting imetoa jumla ya mageti 27 yenye thamani ya shilingi milioni 44 ambayo
yatasaidia kudhibiti wezi wanaoingia kwenye vyoo na kuiba koki na kuharibu miundombinu mingine.
K-VIS
MEDIA imeshuhudia koki za maji kwenye baadhi ya vyoo zikiwa zimeng’olewa.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Ting, Mchungaji Dkt. Vernon Fernados, akimuonyesha moja ya mageti hayo Naibu Waziri Anastazia James Wambura
 Mkazi wa jijini Dar es Salaam, akitoka kwenye vyoo vya juu vya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambavyo vimeathirika sana na wizi huo, Mageti hayo yatafungwa kwenye vyoo hivyo vya juu uwanja mzim

Serikali kuongeza muda wa kufunga maduka makubwa (Shop Malls) Dar es salaam

p.txt 
Na: Frank Shija, MAELEZO
Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam inakusudia kuruhusu baadhi ya maduka makubwa kutoa huduma zaidi ya muda wa kawaida wa maduka kufungwa ili kutoa fursa kwa wafanyakazi kupata huduma hiyo pindi wanapotoka makazini.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda  alipomwakilisha Makamu wa Rais kwenye hafla ya Futali iliyoandaliwa na Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam.
Makonda alisema kuwa kusudio hilo linatokana na changamoto ya upatikanaji wa nafasi ya kupata huduma hiyo kwa wafanyakazi  kwani uchelewa kutoka maofisini jambo lilalosababisha baadhi ya wafanyabiashara kupeleka bidhaa zao huko huko ofisini.
Aliongeza kuwa amekusudia kufanya mambo muhimu matatu katika kipindi hiki cha mwenzi mtukufu wa ramadhani ambapo aliyataja mambo hayo kuwa ni kuongeza muda wa kufunga maduka hasa yale makubwa (malls), kupiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo ya umma na kupambana na watumiaji wa usafiri wa pikipiki wanaokiuka sheria ya matumizi ya Kofia ngumu (helmet).
“Nimekusudia kufanya mambo muhimu matatu ndani ya mwezi huu mtukufu wa ramadhan, niwadokeze tu kuwa mambo hayo ni pamoja na kuongeza muda wa kufanya biashara kwa maduka makubwa (shopping malls), kupiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo ya umma na kupambana na wavunjifu wa sheria ya matumizi ya helmet.” Alisema Makonda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania Bibi. Ineke Bussemaker alisema kuwa wao kama Taasisi ya Kifedha imekuwa na desturi ya kuwajali wateja wao hivyo wanatumia fursa hii kushiriki pamoja na wateja wao walio katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ili kuwatia moyo wakustahilifunga hiyo muhimu katika uislamu.
Aidha aliongeza kuwa NMB itaendelea kushirikiana na jamii mbalimbali katika kuhakikisha inasaidia pale panapohitajika msaada wao kama ambavyo wamekuwa wakitoa misaada katika kuchangia huduma za kijamii kama vile madawati.

No comments:

Post a Comment