Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na wanachama cha
Mapinduzi CCM Wilaya ya Mfenesini Kichama, Mkoa wa Magharibi wakati
alipokua akiwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio
uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,mkutano ulifanyika leo katika
ukumbi wa Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu,[Picha na Ikulu.]
03/06/2016
Baadhiya
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM wakiwa katika mkutano wa
kuwapongeza na kuwashukuru Wananchi na Viongozi wa Chama Wilaya ya
Mfenesini Kichama wakiwemo Mabalozi,Wenyeviti wa matawi,Maskani na
Makatibu katika ukumbi wa tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere leo mgeni
rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,[Picha na
Ikulu.]03/06/2016.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akimkaribisha Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa
CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein kuzungumza na Viongozi wa CCM
wakiwemo Mabalozi,Makatibu wa Matawi,Maskani na Wenyeviti katika Wilaya
ya Mfenesini katika ukumbi wa Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere,Bububu
Mkoa wa Magaharibi Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 03/06/2016.
Mwanachama
wa Umoja wa Vijana UVCCM Rashid Mohamed Othman alipokuwa akitoa
mchango wake uliogusia zaidi uendelezaji wa Matawi ya Chama yaendane na
hadhi mchango huo aliutoa leo katika ukumbi wa Chuo cha Tawi la Mwalimi
Nyerere Bububu Mkoa wa Magharibi Unguja wakati wa Mkutano wa Kuwashukuru
Viongozi wa Mashina,wenyeviyi wa Matawi na Maskani uliofanywa na Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein, [Picha na Ikulu.] 03/06/2016.
Balozi
kutoka Koani Mwanahamis Iddi Mwanachama cha Mapinduzi wa Jimbo la
Mfenesini Wilaya ya Mfenesini alipokuwa akichangia kuhusu wanachama
wanaokiuwa Chama wachukuliwe hatua wakati Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar
Dkt.Ali Mohamed Shein,alipofanya mkutano wa kuwashukuru na kuwapongeza
wanachama Viongozi wa Wilaya ya Mfenesini kwa ushindi wa Uchaguzi
marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika
leo katika ukumbi wa Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere,Bububu Mkoa wa
Magharibi,[Picha na Ikulu.] 03/06/2016.
Mwanachama
cha Mapinduzi wa Jimbo la Mfenesini Wilaya ya Mfenesini Mkoa wa
Magharibi Mashaka Petro alipokuwa akichangia kukushu matengenezo ya
Barabara ya Mwachealale wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed
Shein,alipokua akizungumza na wanachama hao alipowashukuru na
kuwapongeza kwa ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi
mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa
Amani,[Picha na Ikulu.] 01/06/2016.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Mfenesini Bw. Mjumbe Msuri wakati wa mkutano wa kuwashukuru
na kuwapongeza wanachama cha Mapinduzi Wilaya hiyo uliofanyika leo
katika ukumbi wa taCCM Mkoa Amani, [Picha na Ikulu.] 01/06/2016.
KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA BENKI KUU YA TANZANIA (1966 – 2016) KUFANYIKA JUNI 22, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha sherehe za
kuadhimisha miaka 50 tangu Benki Kuu ya Tanzania ilipoanzishwa.
Sherehe hizi zitafanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam tarehe
22/06/2016 ambapo mgeni rasmi atazindua vitabu viwili na kufuatiwa na
kongamano litakaloshirikisha wataalam mbalimbali wa uchumi wakiwemo
magavana 20 wa benki kuu kutoka nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Mada kuu katika Kongamano hilo
itakuwa: “Beyond Aid and Concessional Borrowing: New Ways of Financing
Development in Africa and its Implications”, (yaani namna ya kupata
fedha za miradi ya maendeleo zaidi ya misaada na mikopo nafuu na athari
zake) itakayowasilishwa na Prof. Justin Lin wa Chuo Kikuu cha Peiking,
China. Mada hii imechaguliwa kwa kuzingatia changamoto ambazo serikali
za Afrika zinakumbana nazo katika kugharamia miradi ya maendeleo wakati
ambapo misaada na mikopo nafuu imekuwa ikipungua kwa kiasi kikubwa.
Wachumi waliobobea wa ndani na
nje ya nchi, wakiwemo magavana 20 kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika
mashariki (EAC) na wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika
(SADC) watashiriki katika kongamano hilo.
Vitabu vitakavyozinduliwa siku
hiyo ni (i) “Tanzania: The Path to Prosperity” kinachoelezea masuala
yanayohusu sera za uchumi nchini Tanzania ambacho kimeandikwa na wachumi
waliobobea wa ndani na nje ya nchi, na kimechapishwa na Oxford
University Press. (ii) Kitabu cha pili ni cha miaka 50 ya Benki Kuu ya
Tanzania kiitwacho “50th Anniversary of the Bank of Tanzania:
Evolution of the Bank of Tanzania’s Role and Functions”, ambacho
kinaelezea historia, majukumu, mafanikio na changamoto za Benki Kuu
katika kipindi cha miaka 50 na matarajio ya Taasisi hii ya Umma katika
maendeleo ya taifa katika kipindi cha miaka 50 ijayo.
Aidha, Tarehe 11/6/16 Mheshimiwa
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa atakuwa Mgeni Rasmi kwenye
matembezi ya hisani ya wafanyakazi wa Benki Kuu kutoka makao makuu ya
Benki hadi viwanja vya Mnazi Mmoja kuchangia ununuzi wa madawati ya
shule za msingi kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki.
Wafanyakazi wa Benki Kuu walioko matawini Mtwara, Mwanza, Dodoma,
Arusha, Mbeya, Zanzibar na Chuo cha Benki Mwanza nao pia watafanya
matembezi ya hisani kwenye mikoa yao.
Pamoja na matembezi kutakuwa na
maonesho yaliyoandaliwa na Benki Kuu katika viwanja vya Mnazi Mmoja
yenye lengo la kuwapa wananchi historia ya taasisi hii, ilikotoka, ilipo
na inakoelekea katika kutekeleza majukumu yake.
Benki Kuu ingependa kuwakaribisha
wananchi kufika kwa wingi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja siku hiyo ya
tarehe 11/6/16 kujifunza mengi kuhusu taasisi hii ya umma.
Aidha, tunawaomba wananchi
kufuatilia vipindi mbalimbali vya redio na makala kwenye magazeti ambapo
mengi kuhusu historia, changamoto, mafanikio na matarajio ya Benki
yataelezwa na viongozi mbalimbali wa Benki wa sasa na waliopita.
Benki Kuu ilianzishwa kwa mujibu
wa Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 1965 na kuanza kutoa huduma rasmi tarehe
14 mwezi Juni mwaka 1966. Katika kipindi cha uhai wake, Benki Kuu ya
Tanzania imetimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kulingana na
mahitaji ya taifa yalivyojitokeza mwaka hadi mwaka.
Imetolewa na:
Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki
03/06/2016
Cosmas Cheka kuwania ubingwa wa dunia dhidi ya Mmalawi Jumamosi June 4
Na Mwandishi wetu
Bondia nyota wa ngumi za
kulipwa nchini, Cosmass Cheka Jumamosi June 4 anapanda jukwaani kwenye
uwaja wa Ndani wa Taifa kupambana na bondia wa Malawi, Chrispin Moliyati
katika pambano la kuwania ubingwa wa Dunia wa Universal Boxing Union
(UBO) wa uzito wa Super feather.
Pambano hilo la raundi 12
limeandaliwa na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Advanced Security,
Juma Ndambile kwa lengo la kuendeleza mchezo wa ngumi za kulipwa nchini.
Ndambile ambaye ni meneja wa
Cheka alisema kuwa ameaua kumtuafutia mpinzani wa nje bondia wake kwa
lengo la kumpandisha kiwango ili aweze kucheza mapambano makubwa
duniani.
Alisema kuwa ameamua kuondokana
na kuwaandalia mabondia wake mapambano dhidi ya mabondia wa hapa hapa
kwani hawapati uzoefu wa kimataifa.
Kwa upande wake, Cheka alisema
kuwa amejiandaa vyema kwa pambano hilo na anataka kuonyesh ubora wake
katika mchezo wa ngumi za kulipwa.
Cheka alisema kuwa anatarajia kushinda katika pambano hilo ili kuendeleza rekodi yake katika ngumi za kulipwa.
“Moliyati ni bondia mzuri na
najua atanipa upinzani mkali, lakini sitakubali kupoteza katika ardhi ya
Tanzania, nimejiandaa vizuri kwa ajili ya pambano hilo,” alisema.
Mbali ya mapambano hayo, leo pia kutakuwa na ‘mawe’ ya aina yake katika mapambano ya utangulizi.
Bondia nyota, Japhet Kaseba
atawania ubingwa wa Taifa wa TPBC Limited dhidi ya bondia nyota kutoka
Zanzibar, Amour Mzungu katika pambano la uzito wa juu, Pia Alphonce
Mchumiatumbo atazipiga na bondia Mussa Ajibu kutoka Malawi katika
pambano la uzito wa juu kabla ya Ashraf Suleiman kuonyeshana kazi na
Aliki Gogodo wa Malawi katika pambano la uzito wa juu pia.
Pambano lingine la ubingwa
litakuwa kati ya bondia Shabani Kaoneka dhidi ya Zumba Kukwe la uzito wa
middle raundi 10 ambapo Yonas Segu atazichapa na bondia wa Malawi,
Wilson Masamba katika pambano la uzito wa Light-Welter la raundi nane.
Mabondia wa kike, LuluKayage atazichapa na Enelesi Nkwanthi katika pambano la uzito wa bantam la raundi sita.
“Serikali haitamvumilia mtumishi wa afya anayefanya kazi bila kuzingatia weledi na maadili ya kazi yake”
Mganga
Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi, akizungumza na waandishi
wa habari nje ya Ukumbi unaofanyika Mkutano wa Pili wa Neuroradiolojia
jijini Dar es Salaam, unaojadili Jukumu la Neuroradiolojia katika
kukapambana na Magonjwa Yasiyoambukiza.
Msajili
Mstaafu wa Baraza la Wataalamu wa Radiolojia (MRIPC) Euniace Bandio,
akizungumza kuwakaribisha Wataalamu na Washiriki wa Mkutano wa Pili wa
Neuroradiolojia unaofanyika jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa siku
mbili unajadili Jukumu la Neuroradiolojia katika kukapambana na Magonjwa
Yasiyoambukiza.
Katibu
wa Jukwaa la Neuro-rad Dkt. Mboka Jacob akizungumza na washiriki wa
mkutano wa Pili wa Neuroradiolojia unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watalaamu wa Radiolojia na washiriiki wa mkutano huo wakimsikiliza mgeni rasmi.
……………………………………………………………………………………………………………………………………….
Hussein Makame-MAELEZO
SERIKALI imesema haitamvumilia
mtumishi yeyote wa sekta ya afya atakayefanya kazi zake bila kuzingatia
weledi na maadili ya taaluma za sekta hiyo.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa
Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi, wakati akifungua Mkutano wa Pili
wa Neuroradiolojia ulioanza jijini Dar es Salaam leo, kujadli Jukumu la
Neuroradiolojia katika kukapambana na Magonjwa Yasiyoambukiza.
Prof. Kambi alisema ametoa
msimamo huo kutokana na ukweli kwamba wataalamu wa sekta hiyo
wanashughulikia afya ya binadamu kwa hiyo ni lazima wafanye kazi zao kwa
kuzingatia weledi na maadili.
“Mtu yeyote ambaye ni mtumishi
katika sekta ya afya ni lazima afanye kazi zake kwa kuzingatia weledi na
maadili ya taaluma, hivyo ndivyo taaluma zetu kwenye sekta ya afya
zinavyotaka” alisema Prof. Kambi na kuongeza kuwa:
“Kwa hiyo mtu ambaye hatafuata
weledi na maadili sisi kama Serikali hatutaweza kumvumilia kwa sababu
tunashughulikia afya ya binadamu kwa hiyo ni lazima kazi hizi tuzifanye
kwa kuzingatia weledi na maadili”
Kuhusu mkutano huo, Mganga Mkuu
huyo wa Serikali, aliwaomba washiriki wa mkutano huo kuangalia na
kujadili changamoto mbalimbali za taaluma ya Neuroradiolojia ili
waisaidie Serikali kupata mawazo na ushauri wa jinsi ya kuzitafutia
ufumbuzi changamoto hizo.
Akizungumzia vifaa muhimu katika
hospitali za Kanda nchini, Prof. Kambi alisema Serikali inafanya
jitihada za kuhakikisha hospitali zote za Kanda angalau zihakikishe
zinapata vifaa vya Ultrasound, CT Scan na MRI ambazo ni muhimu katika
kutoa huduma za afya.
Aliongeza kuwa hali si mbaya
katika vituo vya afya kuhusu masuala ya vipimo kwa sababu hospitali
nyingi za Serikali zina vipimo vikubwa muhimu kwa utoaji wa huduma ya
afya kwenye hospitali hizo.
“Kwa mfano kwenye Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili tuna Ultrasound, tuna CT Scan, tuna MRI.Ukienda
hospitali ya Bugando baadhi ya vipimo vipo vingine havipo, ukienda
kwenye Hospitali ya Kanda ya Mbeya nako kuna baadhi vipo na vingine
havipo” alisema na kufafanua kuwa:
“Lakini sisi kama Serikali
tunafanya jitihada za kuhakikisha hospitali zote za Kanda angalau
zihakikishe zinapata vifaa vyote hivi ambavyo ni muhimu katika kutoa
huduma za afya”.
Kwa upande wake Mkufunzi
Muandamizi wa Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili na Mwenyekiti wa Baraza la
Walaamu wa Radiolojia Nchini (MRIPC) Dkt. Ramadhani Kazema alisema
jukumu la baraza hilo ni kuangalia kama wataalum wa Radiolojia wanakidhi
mahitaji katika mafunzo na wanafanya kazi zao kwa weledi.
“Changamoto zinazoikabili tasnia
hii katika nchi hasa za Afrika ni uhaba wa fedha na kuna jitihada
zimefanywa ili kuboresha upatikanaji wa fedha kama unavyojua bajeti za
hospitali ni kidogo ziko finyu kwa hiyo inakua na athari kwenye utendaji
wetu wa kazi” alisema Dkt. Kazema.
Alifafanua kuwa pamoja na
wataalamu wa Radiolojia kuwa si wa kutosha lakini wanaridhisha na
vitendea kazi vipo vinaridhisha ,ingawa changamoto ni jinsi ya kuvifanya
vitendea kazi hivyo viendelee kufanya kazi kwa muda wote.
Mkutano huo wa siku mbili wa
Wataalamu wa Nuerolojia unajadili Mada kuu inayosema “Jukumu la
Neuroradiolojia katika kukabialiana na Magonjwa Yasiyoambukiza na
kushirikisha wataalamu kutoka Kenya, Marekani, Uganda, Korea Kusini,
Uingereza na Tanzania.
Hata hivyo, mkutano huo pia
unatarajia kushirikisha wataalamu hao kubadilishana uzoefu na utaalaamu
katika masuala ya Neuroradiolojia na kujadili masuala ya ugonjwa ya
kansa ya matiti.
KUAHIRISHWA KWA USAILI WA NAFASI ZA KAZI KWA TANGAZO LILILOTOLEWA TAREHE 1 JUNI, 2016
Katibu
wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Tanzania
Metrological Agency (TMA), Tanzania Meat Board (TMB), The Local
Government Training Institute (LGTI) na Registration, Insolvency And
Trusteeship Agency (RITA) alitoa tangazo katika tovuti ya Sekretarieti
ya Ajira la kuita kwenye usaili tarehe 1 Juni, 2016 waombaji wa kazi
waliowasilisha maombi na kukidhi vigezo kwa taasisi zilizoanishwa hapo
juu.
Kupitia tangazo hili Waombaji
kazi wote waliotangaziwa kuitwa kwenye usaili kwa tangazo hilo
wanafahamishwa kuwa usaili huo umeahirishwa mpaka watakapotangaziwa tena
hapo baadaye.
Kwa Matangazo ya nafasi za kazi
yaliyotolewa mnamo tarehe 6 Mei, 2016, 11 Mei, 2016, 18 Mei, 2016 na
tarehe 26 Mei, 2016 nayo waombaji kazi watakaokidhi vigezo watataarifiwa
hapo baadae kuhusu mchakato wake unavyoendelea.
Aidha, Kupitia tangazo hili,
Sekretarieti ya Ajira kwa niaba ya Serikali inaomba radhi waombaji kazi
wote waliowasilisha maombi na wale waliokuwa wamejiandaa kuhudhuria
usaili huo kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na
X.M. DAUDI
KATIBU
Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma.
Mama Janeth Magufuli aahidi kuendelea kusaidia Jamii ya Wazee na walemavu nchini.
Wananchi wa Kijiji cha Nandagwa Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi wakimlaki Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli aliwapowasili eneo hilo kwa ajili ya kutoa Msaada wa Vyakula, Mafuta pamoja na Dawa kwa ajili ya Kambi ya Wazee ya Nandanga iliyopo katika kijiji hicho.
Mratibu
wa kambi ya Kulea wazee na watu wenye ulemavu ya Nandanga Bw. Agnerus
Chiamba akimpa maelezo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mama Janeth Magufuli kuhusu nyumba za malazi katika kambi hiyo,
aliwapowasili eneo hilo kwa ajili ya kutoa Msaada wa Vyakula, Mafuta
pamoja na Dawa.
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
akifungua kitambaa kwenye jiwe la msingi cha zahanati ya kijiji cha
Nandanga itakayorahisisha upatikanaji wa huduma ya afya kwa wakazi wa
eneo hilo waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo.
Baadhi ya Vitu vilivyotolewa kwa ajili msaada katika kambi ya kulea Wazee na watu wenye ulemavu ya Nandanga.
Mratibu
wa kambi ya Kulea wazee na watu wenye ulemavu ya Nandangwa Bw. Agnerus
Chiamba akimkabidhi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama
Janeth Magufuli taarifa ya kambi ya Kulea Wazee ya Nandanga
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi akitoa taarifa ya utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mama Janeth Magufuli wakati wa hafla ya utoaji misaada katika
kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mke
wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
Wakicheza Ngoma na kikundi cha Vijana wakati wa hafla ya utoaji misaada
katika kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani
Lindi.
Mke
wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
akiongea na wananchi wa Kijiji cha Nandanga na kumshukuru Mke wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli kwa kutoa msaada
katika kambi ya Wazee na watu wenye ulemavu iliyopo katika kijiji hicho.
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth
Magufuli(kushoto) akikabidhi misaada kwa wawakilishi wa kambi ya kulea
wazee ya Nandanga iliyopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi, Katikati ni
Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary
Majaliwa.
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
akiongea na wananchi wa Kijiji cha Nandanga kilichopo Wilayani Ruangwa
Mkoani Lindi na kuahidi kuendelea kusaidia kambi hizo za wazee na watu
wenye ulemavu wa ukoma ambapo mpaka sasa meshatoa msaada katika kambi 4
katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Lindi na Mtwara yenye thamani ya
Takribani shilingi 250.
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
akipokea zawadi kutoka wawakilishi wa kijiji cha Nandanga kilichopo
Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
akiagana na wananchi wa Kijiji cha Nandanga kilichopo Wilaya ya Ruangwa
Mkoani Lindi baada ya kutoa msaada katika kambi ya kulea wazee ya
Nandanga iliyopo eneo hilo.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
No comments:
Post a Comment