Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Katibu wa Chama cha Kikoministi cha China kutoka Kamati
ya Jimbo la Jiangsu Bw.Luo Zhijon,(kulia) akiwa na ujumbe wake
walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni,[Picha na Ikulu.] 02/06/2016.

akizungumza na Ujumbe wa Chama cha Kikoministi cha China kutoka Kamati
ya Jimbo la Jiangsu ukiongozwa na Katibu wake Bw.Luo Zhijon,(kushoto)
mara ujumbe huo ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni,[Picha na
Ikulu.] 02/06/2016.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein
akizungumza na Ujumbe wa Chama cha Kikoministi cha China kutoka Kamati
ya Jimbo la Jiangsu ukiongozwa na Katibu wake Bw.Luo Zhijon,(wa tatu
kulia) mara ujumbe huo ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni,[Picha
na Ikulu.] 02/06/2016.
Wadau wa watakiwa kutoa mchango wa kuboresha kanuni za upatikanaji wa mbolea nchini.
Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka akifungua
warsha ya wadau wa mbolea iliyofanyika leo jiji Dar es Salaam kujadili
na kuboresha sheria na kanuni zinazosimia sekta ya mbolea nchini ili
kuwa na kilimo chenye tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla.

Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka (katikati
aliyekaa )akiwa picha ya pamoja na wadau wa mbolea mara baada ya
kufungua warsha ya wadau ha oleo jijini Dar es salaam.
…………………………………………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Wadau wa mbolea wameaswa
kuangalia namna ya kuboresha sheria na kanuni za kusimamia sekta ya
mbolea kwa manufaa ya wananchi wanaojishughulisha na kilimo ili kiwe na
tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa leo na
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka
alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa mbolea uliofanyika leo jiji Dar
es Slaam.
Dkt. Turuka amesema kuwa maeneo
ya kuzingatiwa katika warsha hiyo ni pamoja na kuboresha sheria na
kanuni zinazosimamia sekta ya mbolea ili kuwezesha sekta binafsi
kushiriki katika kuinua kilimo kwa manufaa ya Watanzania.
Gharama hizo zinahusisha
kufanyiwa majaribio mbolea zinazotoka nje ya nchi kabla ya kuanza
kutumiwa na wakulima ambapo majaribio hayo yanafanyika kwa misimu mitatu
ya kilimo.
Maeneo mengine ya kurekebisha ni pamoja na mlolongo wa tozo ambazo zimekuwa zikitozwa kwenye mbolea inayoingizwa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika linalojishughulisha na matumizi ya mbolea Bara la Afrika
anayesimamia eneo la Tanzania Dkt. Mshindo Msolla amesema kuwa kazi
kubwa waliyonayo wajumbe katika warsha hiyo ni kuhakikisha sheria na
kanuni wanazozifanyia kazi zitasaidia kuboresha upatikanaji wa mbolea
zenye ubora unaotakiwa kulingana na mahitaji ya wakulima na waipate kwa
wakati.
“Wakulima hapa nchini
wananufaika na huduma zetu ambazo tunatoa ikiwemo kuwaunganisha na
mawakala wakubwa wa pembejeo na makampuni yanayozalisha au kuingiza
mbolea nchini” alisema Dkt. Msolla.
Kuhusu hali ya upatikanaji wa
mbolea nchini, Dkt. Msolla amesema kuwa shirika hilo linatoa huduma
katika mikoa 12 nchini ambapo wapo mawakala 30 wanahudumia mawakala
wadogo 500.
Mikoa hiyo ni Arusha,Kilimanjaro,Manyara, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma, Rukwa, Katavi na Kigoma.
Mawakala hao msimu wa mwaka
2014/2015 wamefanikiwa kuuza kwa wakulima mbolea tani 60,000 na mbegu
tani 3000 ambazo zimekuwa na manufaa katika kuhakikisha upatikanaji wa
mazao ya chakula na biashara nchini.
Aidha, shirika hilo
limefanikiwa kuwaunganisha wakulima na makampuni ya mbolea sita ikiwemo
YARA, Extra Trading, Premium Agrochemical pamoja na Minjingu.
Vile vile, Dkt. Msolla amesema
kuwa wakulima wamenufaika na kujengewa maghala 14 hadi sasa yameanza
kutumika ambayo yanauwezo wa kuhifadhi tani 50,000 kwa wakati moja hatua
ambayo inasaidia kusogeza huduma karibu na wakulima wanapozihitaji.
Dkt. Msolla amesema kuwa
Shirika hilo lenye makao yake makuu Afrika Kusini linatoa huduma kwa
sekta ya mbolea katika nchi mbalimbali Barani Afrika ikiwemo nchi tatu
za kipaumbele ambazo ni Tanzania, Msumbiji na Ghana, nchi nyingine
ambazo shirika hilo linafanya kazi ni Ethiopia, Senegal, Ivory Coast na
Nigeria.
KATIBU WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA JIMBO LA JIANGSU AFANYA ZIARA YA SIKU MBILI ZANZIBAR.
KATIBU
wa Chama cha Kikomunisti cha China katika Jimbo la Jiangsu Luo Zhijun,
akivishwa shada la mauwa mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Ussi
Gavu, akisalimiana na Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China katika
Jimbo la Jiangsu Luo Zhijun wakati mgeni huyo alipowasili katika uwanja
wa ndege mjini Zanzibar.
Katibu
wa Chama cha Kikomunisti cha China (aliyevaa shati jeupe) Luo Zhijun,
akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Issa Ussi Gavu (wa kwanza kushoto).
WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Ussi
Gavu, akizungumza na Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China Jiangsu
Luo Zhijun katika ukumbi wa watu mashuhuri (VIP) uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Abeid Abeid Karume Zanzibar. Picha na Makame Mshenga
Maelezo Zanzibar.
Zaidi ya Bilioni 4 kutumika kuwezesha wajasiriamali Kinondoni
Afisa
uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Sebastian Mhowera akizungumza na
Waandishi wa Habari kuhusu mikakati ya Manispaa hiyo kuwawezesha
wanawake na vijana kupitia mfuko maalum ulioanzishwa na Serikali ili
kutoa mikopo kwa wajasiriamali hao ili kuwajengea uwezo kushiriki
kujenga uchumi.kulia ni AfisaUhusiano wa Manispaa hiyo Bw.Bornwell
Kapinga.
…………………………………………………………………………………………………………….
Frank Mvungi-Maelezo
Serikali kutumia zaidi ya bilioni
4 kuwawezesha wajasiriamali wadogo katika Manispaa ya Kinondoni katika
Kipindi cha mwaka 2016/2017 ili kuchochea kasi ya ukuachi wa uchumi.
Kauli hiyo imetolewa Leo Jijini
Dar es salaam na Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Sebvastian
Mhowera wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.
Akifafanua Mhowera amesema fedha
hizo zitatolewa kupitia Mfuko wa wanawake na Vijana unaolenga
kuwawezesha kishiriki katika shughuli za uzalishaji hali itakayachangia
kukuza uchumi.
Kwa Sasa manispaa ya Kinondoni
inajumla ya Vikundi 546 vya wanawake na vijana vyenye jumla ya
wajasiriamali 2729 ikilinganishwa na vikundi 40 na wanufaika 200
waliokuwepo mwaka 2013.
Wajasiriamali wanaonufaika na
fedha za mfuko huo ni wale wanajishughuisha na shughuli za Kiuchumi
ikiwemo kilimo,Biasharandogondogo,Ushonaji,Ufugaji,Uvuvi,Mafundi
seremala,wasusi.
Pia Mhowera alitoa wito kwa
wajasiriamali wa Wilaya ya Kinondoni kujitokeza kuchangamkia fursa
zinazotokana na mfuko wa wanawake na vijana.
Kuanzishwa kwa mfuko huu katika
manispaa ya Kinondoni ni utekelezaji wa agizo la Serikali Kuu
lililoagiza Halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 ya mapato yake
kwa ajili ya mfuko wa kuwawezesha wanawake na vijana.
Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni inaandaa maonesho kwa ajili ya wajasiriamali wadowadogo
wanaonufaika na Mikopo ya Mfuko wa wanawake na vijana inayotolewa na
Manispaa hiyo ambapo maonesho hayo yatafanyika mwishoni mwa wiki ijayo.

No comments:
Post a Comment