MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WAANDAA ZOEZI LA UHAKIKI WA WASTAAFU WANAOLIPWA PENSHENI NA MFUKO HUO
MFUKO
WA PENSHENI WA LAPF UNAWATANGAZIA WASTAAFU WANAOLIPWA PENSHENI NA LAPF
KUWA KUTAKUWA NA ZOEZI LA UHAKIKI WA WASTAAFU NCHI NZIMA KUANZIA TAREHE
13.06.2016 HADI TAREHE 24.06.2016 KUANZIA SAA MBILI KAMILI ASUBUHI.
TAREHE KAMILI KWA KILA WILAYA INAPATIKANA KWENYA MAGAZETI YA MWANANCHI
YA TAREHE 06.06.2016, 08.06.2016 NA 10.06.2016, DAILY NEWS LA TAREHE
07.06.2016 NA 09.06.2016 NA TOVUTI YA MFUKO www.lapf.or.tz KILA MSTAAFU
ANATAKIWA KUFIKA NA PICHA MOJA NDOGO (PASSPORT SIZE) NA KITAMBULISHO
CHOCHOTE.
KILA MSTAAFU ANAYELIPWA PENSHENI NA LAPF UNAOMBWA UJITOKEZE KWENYE OFISI ZA HALMASHAURI ZILIZO KARIBU NAWE.
KWA MAELEZO ZAIDI PIGA 0767-600043 AU 0753-999991.
“STAAFU KWA UFAHARI NA LAPF”
WIZARA YA ARDHI YAKUTANA NA WADAU KUTOKA TAMISEMI KUJADILI MASUALA MBALIMBALI KUHUSU SEKTA YA ARDHI.
MADIWANI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA WAUPONGEZA MGODI WA BUZWAGI.
Meneja
Uendelevu wa Mgodi wa Buzwagi, George Mkanza akifafanua jambo kwa
madiwani wa halmshauri ya mji wa Kahama wakati ziara ya kutembelea Mgodi
huo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama Abel Shija(mwenye skafu) pamoja na
waheshimiwa madiwani na wataalamu wa halmashauri hiyo wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa wataalamu wa Mgodi huo.
waheshimiwa madiwani na wataalamu wa halmashauri hiyo wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa wataalamu wa Mgodi huo.
Afisa mazingira wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Lusajo Njobelo akifafanua jambo kwa
waheshimiwa madiwani na mbunge wa Kahama mjini Jumanne Kishimba wakati wa ziara hiyo.
waheshimiwa madiwani na mbunge wa Kahama mjini Jumanne Kishimba wakati wa ziara hiyo.
Madiwani wakipata maelezo kutoka kwa Marco Peter katika eneo la uchimbaji.
Shimo ambalo shughuli za uchimbaji hufanyika kama linavyoonekana.
Eneo maalumu la kusagia mawe kabla ya kupelekwa kiwandani kwa ajili ya uchenjuaji wa dhahabu.
TAARIFA YA UDAHILI KATIKA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII
Wizara
ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ina vyuo tisa (9)
vinavyotoa mafunzo ya taaluma ya Maendeleo ya Jamii katika ngazi ya
Cheti, “Diploma”, “Degree” na “Postgraduate Diploma” kama ifuatavyo:-
- Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru iliyoko Wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha, inatoa Shahada (Degree). katika fani ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Maendeleo na Upangaji na Uendeshaji Shirikishi wa Miradi. Aidha, Taasisi hiyo pia inatoa Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) katika Maendeleo ya Jamii.
- Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Ufundi Missungwi (Mwanza) na Mabughai (Lushoto) vinatoa Kozi ya Maendeleo ya Jamii Ufundi, kuanzia ngazi ya Cheti hadi Diploma.
- Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare kilichopo Wilaya ya Musoma Mkoani Mara, kinatoa mafunzo ya Maendeleo ya Jamii kuanzia ngazi ya Cheti hadi Diploma.
- Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Rungemba (Mafinga – Mufindi) na Monduli (Arusha) vinatoa mafunzo ya Taaluma ya Maendeleo ya Jamii katika ngazi ya Diploma.
- Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Ruaha (Iringa), Uyole (Mbeya) na Mlale (Songea) vinatoa mafunzo ya Maendeleo ya Jamii katika ngazi Cheti.
- Madhumuni ya Vyuo vya Mendeleo ya Jamii:
Madhumuni ya vyuo hivi ni pamoja na:
- Kutoa mafunzo ya taaluma ya Maendeleo ya Jamii kwa wahitimu wa kidato cha nne na sita waliotoka shuleni moja kwa moja.
- Kuendeleza Maafisa Maendeleo ya Jamii walioko kazini wenye taaluma ya Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Jamii;
- Kupata wataalamu mahiri wa Maendeleo ya Jamii wenye uwezo wa kuiwezesha jamii kujiletea maendeleo yao wenyewe.
- Kuandaa mitaala inayokidhi mahitaji ya taaluma ya maendeleo ya jamii sanjari na mabadiliko yanayotokana na utandawazi, soko la ajira pamoja na sayansi na teknolojia.
- UTOAJI WA TAALUMA YA MAENDELEO YA JAMII
Wilaya ya Monduli yazindua umezaji kingatiba ya ugonjwa wa vikope(Trakoma)
Diwani wa kata ya Meserani Mhe.Loti Naparana akimeza kingatiba ya Trakoma(Zithromax)wakati wa uzinduzi huo.
Mama
wa boma bi.Himayo Merio (aliyeshika kikombe)akipokea kingatiba toka Kwa
mhudumu wa afya ngazi ya jamii bi.Jamila Karanga.zoezi hili linafanyika
katika jamii hiyo kwa kuwatembelea kaya kwa kaya.
Wananchi
wa kijiji cha Meserani wakisikiliza hotuba toka mkuu wa wilaya (hayupo
pichani) wakati wa uzinduzi wa umezaji wa kingatiba za ugonjwa wa
trakoma uliofanyika kwenye kitongoji cha Losingirani.
……………………………………………………………………………………………………
Na.Catherine Sungura-Monduli
Wilaya ya Monduli inatarajia kutoa
kingatiba ya ugonjwa wa trakoma(vikope) wa watu wapatao 140,962 kwa
ngazi ya jamii kaya kwa kaya hadi ifikapo mwezi julai mwaka Huu
Haya yamesemwa leo Na mkuu wa wilaya ya Monduli Fransic Miti wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji dawa katika kijijo cha Losingirani wilayani hapa
Miti alisema kila mtu yupo katika hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele”napenda kusisitiza kila mwanajamii ahakikishe kila mtu katika familia anatumia dawa hizi ili tuweze kupunguza kasi ya maambukizi ambayo ni tayari katika jamii yetu
Aidha aliahidi kulisimamia zoezi hili ipasavyo katika ngazi zote kwani vifaa vyote vya utekelezaji wa zoezi hili vimeshawafikia katika wilaya Nzima
Mkuu wa Wilaya alisema kwa mwaka uliopita wilaya yake imetekeleza zoezi la ugawaji wa dawa za kudhibiti magonjwa ya kichocho na minyoo ya tumbo kwa watoto wenye umri wa kwenda shule kwa ufanisi mkubwa ambapo kati ya watoto 29,427,watoto 28,205 walipatiwa kingatiba ambayo ni sawa na asilimia 95.8
Hata hivyo alisema kwa zoezi la mwezi wa tano mwaka huu la umezaji dawa za minyoo zilitolewa kwa watoto 31,150 sawa na asilimia 97.3 kati ya watoto 32,000.
Naye Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa
Hayapewi kipaumbele toka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Upendo Mwingira alisema maambukizi ya ugonjwa wa vikope(trakoma) upo kwa kiwango cha juu kwenye maeneo ya wafugaji ambapo asilimia 57 ya watu waliofanyiwa utafiti mwaka 2004 hadi 2006 ilionesha wana tatizo la vikope hasa wilaya ya Monduli,Longido pamoja na Ngorongoro.
Inakadiliwa hadi kufikia mwaka 2020 dunia nzima iwe imetokomeza ugonjwa huu kwa kugawa dawa ambazo ni tiba na kinga

kukabiliwa na changamoto mbalimbali Tanzania imepiga hatua katika sekta ya afya-Ummy Mwalimu
Waziri
wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy
Mwalimu,akihutubia mkutano wa 69 wa afya duniani unaoendela nchini
Geneva-Uswis.
Waziri
wa afya Tanzania bara Mhe.Ummy Mwalimu kushoto akiwa na waziri wa afya
Zanzibar Mhe.Mahmoud Kombo wakifuatilia mada zinazowasilishwa kwenye
mkutano huo unaowakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi wanachama wa
shirika la afya duniani(WHO),nyuma yao ni katibu mkuu wizara ya afya
Tanzania bara dkt.Mpoki Ulisubisya.
Waziri Ummy Mwalimu wakifurahia jambo kwenye mkutano huo pamoja na viongozi wengine walioshiriki mkutano huo.
…………………………………………………………………………………………………
Mwandishi maalum-Geneva
Tanzania
imekua miongoni mwa nchi chache katika bara la Afrika kufanikiwa
kufikia lengo la nne la maendeleo ya millennia la kupunguza vifo vya
watoto chini ya miaka mitano.
Hayo
yamesemwa na waziri wa afya,maendeleo ya jamii ,.jinsia,wazee na watoto
Ummy mwalimu wakati akihutubia mkutano wa 69 wa afya duniani
unaofanyika nchini Geneva,Uswisi.
Ummy
alisema licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali Tanzania imepiga
hatua katika sekta ya afya kwa kupunguza vifo hivyo hadi kufikia vifo
54 kati ya vizazi hai 1,000 kutoka vifo 112 kati ya vizazi hai 1,000
Aidha,
mkutano huo ambao ni wa ngazi ya juu katika sekta ya afya duniani,
Tanzania imetambuliwa na kutangazwa kuwa miongoni mwa nchi
zilizotokomezwa ugonjwa wa polio kwa kufanikiwa katika utoaji wa huduma
za chanjo nchini kwa watoto.
?Ninaeleza
kwa masikitiko kuhusu tatizo la mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu
uliopo nchini Tanzania ambapo hadi kufikia tarehe 22 Mei, 2016 idadi
ya wagonjwa ilifikia 21,581,kati yao watu 338 wamepoteza maisha,naahidi
Serikali kupitia wizara ya afya itaimarisha na kuzingatia kanuni za
afya ya mazingira katika kukabiliana na ugonjwa huu?alisema
Kwa
upande wa kutokomeza malaria waziri Ummy alisema Tanzania imeweza
kupunguza maambukizi ya ugonjwa huu kutoka asilimia 18 hadi 9.5 kwa
Tanzania bara na kwa upande wa Zanzibar imefanikiwa kupunguza idadi ya
wagonjwa hadi kufikia asilimia 0.6 .
Katika
kuboresha huduma za afya nchini alisema Serikali ya Tanzania imejipanga
na kuhakikisha itaboresha huduma za afya ziweze kumfikia kila
mtanzania popote alipo, ?ili kuweza kufikia malengo haya ni wakati
muhimu sasa kuwekeza zaidi katika sekta hii kwa kuongeza uwekezaji
katika raslimali fedha,watu pamoja na kuboresha miundombinu ikiwemo
utoaji wa huduma za afya nchini?.
Waziri
Ummy alisema katika kufikia mafanikio ,wizara ya afya inatarajia
kuwasilisha muswada wa sheria katika bunge la mwezi wa Septemba,2016 wa
kila mtanzania kuwa na bima ya afya kitu ambacho kitakuwa ni mkombozi
mkubwa kwa mwananchi katika kupata huduma za matibabu wakati wowote
anapokuwa na fedha au kutokuwa na fedha kwa kuwa maradhi hayachagui
wakati.
Mkutano
mkuu wa mwaka wa Afya Duniani hufanyika nchini Geneva ?Uswis kila
mwaka mwezi mei ambao huwakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi
wanachama wa Shirika la afya Duniani {WHO} na kuhudhuriwa na
wadau,mashirika na taasisi zinazoshiriki katika kutoa huduma za afya
Duniani.Tanzania inawakilishwa na waziri wa afya Tanzania bara Mhe.Ummy
mwalimu na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Kombo.
WAKULIMA NA WAFUGAJI WA MVIWATA WATINGA BUNGENI WATATULIWE CHANGAMOTO ZINAZOWAKABI
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania
(Mviwata), Steven Ruvuga (kulia) akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Bunge
ya Kilimo, Maji, kuhusu matatizo mbalimbali wanayopata wakulima na
wafugaji nchini, wakati wa mdahalo wa kujadili changamoto
zinazowakabili kwenye Ukumbi wa Bunge wa Msekwa, Dodoma
Mfugaji ambaye ni Mjumbe wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania
(Mviwata), Trugeti Kashu kutoka Mbarali, mkoani Mbeya, akielezea mbele
ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Maji, Bungeni Dodoma jana, kuhusu migogoro
ya wafugaji na askari wa wanyamapori wa Hifadhi ya Ruaha ambapo mifugo
yao hutekwa na kuwalipisha fedha nyingi kuigomboa. Mviwata walikutana na
wajumbe wa kamati hiyo, bungeni Dodoma
Mwenyekiti wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata), Veronica Sophu(kulia)
akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji,
kuhusu matatizo mbalimbali wanayopata wakulima na wafugaji nchini,
wakati wa mdahalo wa kujadili changamoto hizo kwenye Ukumbi wa Bunge wa
Msekwa, Dodoma
Wakulima wakinyoosha mikono ili waeleze changamoto zinazowakabili mbele ya wabunge
Wajumbe wa Mviwata akisikiliza kwa makini wakati Mwenyekiti wa Kamati, Mary Nagu akifungua mjadala huo.
PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Maji
wakisikiliza kwa makini wakati wakulima wakielezea changamoto zao
MAKALA YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO NA MKAKATI WA KUWAJALI WAZEE.
Na Magreth Kinabo
…………………………………..
Bila shaka kila
mtu atakubaliana na usemi kwamba anatoka katika familia au maeneo
ambayo yenye wazee au watu wenye ulemavu na wasiojiweza. Pia waswahili
wana msemo kwamba “Utu uzima ni dawa”.
Kwa maana
nyingine ni kwamba tukiangalia suala la umri, wazee ni watu waliofikisha
umri wa miaka 50 na kuendelea. Hivyo licha ya umri wao wana mchango
katika kuendelea kuleta maendeleo katika Taifa letu.
Wazee ni watu
ambao wamechangia katika masuala mbalimbali kwenye Taifa letu kutokana
na kazi walizokuwa wakizifanya kama vile kilimo, kiutamaduni, kisiasa,
kiuchumi na kijamii.
Mara nyingi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
amekuwa akizungumzia kuhusu mkakati wake wa kuwasaidia wanyonge ili nao
waweze kujikwamua kimaisha na kuchangia pato la Taifa.
Miongoni mwa
makundi mengine ya watu wanyonge mbali na wazee, ni wajane, yatima,
watoto wanaoishi katika mazingira magumu na walemavu.
Kutokana na
umuhimu huo, hivi karibuni Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mama Janeth Magufuli ameziomba na kuzihamasisha taasisi za
Serikali na zisizo za Serikali kushirikiana na Serikali kutatua
changamoto mbalimbali zinazozikabili Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu
Walemavu cha Nungwi kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam na vingine
17 vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini.
Kauli hiyo
ilitolewa na Mama Magufuli wakati alipotembelea makazi hayo yaliyoko
Kigamboni eneo la Vijibweni jijini Dares Salaam, ambapo alisema
changamoto wanazokabiliana nazo wazee hao, amezisikia na aliwaahidi
kwamba atashirikiana na wadau wote kuzitafutia majibu yake.
Mama Magufuli
alizitaja baadhi ya changamoto hizo, ni kuwa uchakavu wa miundombinu,
uhaba wa rasilimali fedha na watu, pamoja na maslahi duni ya watoa
huduma, upungufu wa vitendea kazi na huduma za jamii, pamoja na uvamizi
wa eneo la kituo.
“Natumaini
zawadi tuliyoileta ni ndogo na haiwezi kumaliza matatizo yote mliyonayo.
Lakini ni matumaini yangu kuwa zawadi hii inaweza kuwa chachu ya
kuhamasisha watu na vikundi vingine kujitoa kusaidia watu wasiojiweza.
Aliongeza “Ni
imani yangu kuwa endapo watu wote tutajitoa kwa dhati tutaweza
kuwahudumia wazee na watu wasiojiweza na hivyo kuwapunguzia makali ya
maisha . Tukumbuke kutoa ni moyo na si utajiri na kwamba sisi sote ni
wazee na walemavu watarajiwa”.
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein atoa pongezo kwa serikali Jamhuri ya Watu wa China
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein
akizungumza na Ujumbe wa Chama cha Kikoministi cha China kutoka Kamati
ya Jimbo la Jiangsu ukiongozwa na Katibu wake Bw.Luo Zhijon,(wa tatu
kulia) mara ujumbe huo ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni,[Picha
na Ikulu.] 02/06/2016.
……………………………………………………………………………………………
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametoa pongezi kwa Serikali
ya Jamhuri ya Watu wa China kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika
kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo sekta ya afya.
Dk. Shein aliyasema hayo leo
katika mazungumzo kati yake na Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China
katika Kamati ya Jimbo la Jiangsu Bwana Luo Zhijun akiwa amefuatana na
ujumbe wake uliofika Ikulu mjini Zanzibar.
Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein
alisema kuwa azma ya Jimbo la Jiangsu kuendeleza mashirikiano yake kwa
kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo nchini ni hatua moja wapo ya
kukuza uhusiano wa kidugu uliopo kati ya pande mbili hizo.
Dk. Shein alipongeza azma ya
Kiongozi huyo katika kuimarisha uhusiano katika sekta ya afya, elimu,
viwanda, uekezaji, utalii pamoja uvuvi kati ya Zanzibar na Jimbo hilo la
Jiangsu.
Aidha, Dk. Shein alieleza kuwa
Zanzibar itaweza kufaidika kwa kiasi kikubwa na makubaliano ya awali juu
ya mafunzo kwa madaktari na wauguzi wazalendo kati yake na Jimbo hilo,
kwani ni hatua kubwa katika kuhakikisha sekta ya afya inaimarika hapa
nchini.
Dk. Shein alitumia fursa hiyo
kutoa pongezi na shukurani kwa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China
kupitia Jimbo la Jiangsu kwa utamaduni wa kuendelea kuwaleta Madaktari
bingwa kutoka Jimbo hilo tokea mwaka 1964, ambapo mbali ya wataalamu hao
pia, nchi hiyo imeweza kuleta wataalamu wake mbali mbali hapa
Zanzibar.
Aidha, Dk. Shein alitoa shukurani
kwa chama cha Kikomunisti cha China kwa kuendeleza ushirikiano wake na
chama tawala cha CCM na kuahidi kuendeleza mashirikiano hayo kwa kupanua
wigo katika nyanja mbali mbali za maendeleo.
WAZIRI WA MALIASILI PROF. JUMANNE MAGHEMBE AIOMBA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KWA VITENDO KATIKA VITA DHIDI YA UJANGILI
Waziri wa Maliasili Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kulia) akipokea
ndege maalum aina ya drones kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kimataifa wa Mfuko wa
Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF) Dkt. Marco Lambertini (wa tatu
kushoto) kwa ajili ya kusaidia doria za kiitelijensia za kupambana na ujangili
katika pori la akiba la Selous. Wengine
katika picha ni kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa WWF – Tanzania, Amani Ngusaru, Meneja
wa Pori hilo la Akiba Selous, Mabula Misungwi, Mwenyekiti wa bodi ya
WWF – Ujerumani, Dkt. Valentin Von Moscow, Mkurugenzi Mtendaji WWF – Ujerumani,
Ebenhard Brandes na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Kuzuwia Ujangili, Faustine
Ilobi Masalu.

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto), Viongozi
wa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF) na Viongozi wengine
wa Wizara wakipokea maelekezo kutoka kwa Mtaalam wa uendeshaji wa ndege maalum
aina ya drones na jinsi zinavyofanya kazi, Parmena Elisa, ndege hizo zilitolewa na Mfuko
wa WWF kusaidia doria za kiitelijensia za kupambana na ujangili katika pori la
akiba la Selous jana tarehe 1 Julai, 2016 Matambwe Selous.

Waziri wa Maliasili Prof. Jumanne Maghembe akizungumza katika hafla ya
makabidhiano ya ndege maalum aina ya drones zilizotolewa na Mfuko wa WWF kusaidia
doria za kiitelijensia za kupambana na ujangili katika pori la akiba la Selous. Wengine katika picha ni Mkurugenzi
Mkuu wa Kimataifa wa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF)
Dkt. Marco Lambertini (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji WWF – Ujerumani,
Ebenhard Brandes (kushoto).

Mkurugenzi Mkuu wa Kimataifa wa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na
Mazingira Duniani (WWF) Dkt. Marco Lambertini (wa pili kushoto) akimkabidhi, Namsifu
Johannes Marwa (Mhifadhi Wanyamapori), Tuzo ya WWF ya Mhifadhi Bora kwa mchango
wake alioutoa katika kupambana na ujangili katika pori la akiba la Selous. Wanaoshuhudia
ni Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto), Mkurugenzi
Mtendaji WWF – Ujerumani, Ebenhard Brandes na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya
Kuzuwia Ujangili Wizara ya Maliasili, Faustine Ilobi Masalu (wa nne kushoto),
tuzo hiyo ilitolewa Matambwe Selous tarehe 1 Julai, 2016.

Picha ya pamoja.
………………………………………………………………………………………..
………………………………………………………………………………………..
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Prof.
Jumanne Maghembe ameiomba Jumuiya ya Kimataifa kuunga mkono juhudi za
Serikali katika kupiga vita ujangili kwa vitendo katika kuimarisha uhifadhi
nchini.
Jumanne Maghembe ameiomba Jumuiya ya Kimataifa kuunga mkono juhudi za
Serikali katika kupiga vita ujangili kwa vitendo katika kuimarisha uhifadhi
nchini.
Prof. Maghembe alisema hayo jana, Matambwe Selous, katika hafla fupi
ya makabidhiano ya ndege maalum 8 zilizotolewa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na
Mazingira Duniani (WWF) kwa Wizara ya Maliasili na Utalii.
ya makabidhiano ya ndege maalum 8 zilizotolewa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na
Mazingira Duniani (WWF) kwa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Ndege hizo ndogo aina ya drones ambazo hazitumii rubani na huongozwa na mitambo
maalum zitatumika katika pori la akiba la Selous kwa ajili ya kuimarisha ulinzi
wa Wanyamapori kwa kukusanya taarifa za kiitelijensia zitakazosaidia kukamatwa
majangili. Ndege hizo zina thamani ya dola za kimarekani 80,000 sawa na zaidi
ya Tsh milioni 172.

“Msaada huu umekuja wakati muafaka ambapo Pori la Akiba la Selous linahitaji teknolojia
za kisasa katika kuimarisha mapambano dhidi ya ujangili ndani na kuzunguka
hifadhi hii” alisema Prof. Maghembe.
za kisasa katika kuimarisha mapambano dhidi ya ujangili ndani na kuzunguka
hifadhi hii” alisema Prof. Maghembe.
Alieleza kuwa changamoto kubwa inayoikabidili hifadhi ya Selous ni ujangili ambao kwa
kiasi kikubwa umesababisha idadi ya Wanyamapori hususani tembo kupungua kwa kasi
kubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma.
kiasi kikubwa umesababisha idadi ya Wanyamapori hususani tembo kupungua kwa kasi
kubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Alisema kuwa takwimu zinaonesha kuwa mwaka 1986 idadi ya tembo katika pori hilo ilikuwa
50,000, idadi ambayo iliongezeka mwaka 2003 na kufikia 70,000 baada ya
Serikali ya Ujerumani kusaidia kuanzishwa kwa Mpango wa Kuendeleza Selous
(Selous Conservation Program) na Serikali ya Tanzania kukubali aslimia 50 ya
makusanyo yanayotokana na utalii yabaki kuendeleza uhifadhi katika pori hilo.

Alisema kuwa baada ya mradi huo kuisha na mfumo wa “retention” kuondolewa na Serikali
hali ilibadilika na kuwa mbaya zaidi ambapo kati ya mwaka 2008 na 2011 vitendo
vya ujangili viliongezeka maradufu, sensa ya mwaka 2013 ilionesha idadi ya
tembo hao kupungua hadi kufikia 13,000.
hali ilibadilika na kuwa mbaya zaidi ambapo kati ya mwaka 2008 na 2011 vitendo
vya ujangili viliongezeka maradufu, sensa ya mwaka 2013 ilionesha idadi ya
tembo hao kupungua hadi kufikia 13,000.
Prof. Maghembe aliongeza kuwa pamoja na hayo Serikali imejipanga kuhakikisha
Wanyamapori wanalindwa usiku na mchana na kwamba wale wote wanaojihusisha na
vitendo vya ujangili watakamatwa na kufikishwa mahamani ili sheria ichukue
mkondo wake.
Wanyamapori wanalindwa usiku na mchana na kwamba wale wote wanaojihusisha na
vitendo vya ujangili watakamatwa na kufikishwa mahamani ili sheria ichukue
mkondo wake.
“Hatutawavumilia hawa watu wamalize wanyamapori wetu wote tulionao, tunawafuatilia usiku na
mchana na lazima tutawakamata” alisisitiza Prof. Maghembe
mchana na lazima tutawakamata” alisisitiza Prof. Maghembe
Aliongeza kuwa Serikali kwa kushirikiana na washirika wa uhifadhi imechukua hatua za
makusudi za kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo kuanzishwa kwa mpango wa Kitaifa
wa Kukabiliana na Ujangili na Biashara Haramu ya Wanyamapori, mpango ambao
umekuwa na matokeo mazuri baada ya kuungwa mkono na washirika hao kwa kusaidia
fedha, vifaa na misaada mbalimbali ya kiufundi.

Aliongeza kuwa sehemu ya mpango wa Serikali wa kukabiliana tatizo hilo ni kuanzishwa kwa
Jeshi Usu (Paramilitary) ambapo maeneo yote ya hifadhi nchini yatalindwa
kijeshi.
Jeshi Usu (Paramilitary) ambapo maeneo yote ya hifadhi nchini yatalindwa
kijeshi.
Prof. Maghembe ameeleza kuwa pamoja na mambo mengine ili kukomesha ujangili ni lazima
mataifa yaliyoendelea ambayo ndiko yaliko masoko makubwa ya meno ya tembo na
bidhaa zake kusitisha kabisa uingizwaji wa meno hayo katika nchi zao ili
kukomesha biashara hii haramu.
mataifa yaliyoendelea ambayo ndiko yaliko masoko makubwa ya meno ya tembo na
bidhaa zake kusitisha kabisa uingizwaji wa meno hayo katika nchi zao ili
kukomesha biashara hii haramu.
“Kuna nchi ambazo tayari zimechukua hatua ya kukataza kabisa uingizwaji wa meno ya
tembo nchini mwao, mfano Marekani, tunaiomba sana jumuiya ya kimataifa wakiwemo
marafiki zetu China na nchi nyingine wakatae kabisa uingizwaji wa meno haya
nchini mwao, hii itasaidia sana kukomesha biashara hii haramu” Alisema.

Katika hatua nyingine Prof. Maghembe aliwataka wafugaji walioingiza mifugo katika
maeneo yote ya hifadhi nchini waondoe mifugo yao kwa hiari kabla ya
kushinikizwa kufanya hivyo na Serikali kwa mujibu wa sheria.
maeneo yote ya hifadhi nchini waondoe mifugo yao kwa hiari kabla ya
kushinikizwa kufanya hivyo na Serikali kwa mujibu wa sheria.
Sheria ya Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 Ibara ya 18 (2) inasema “Si ruhusa mtu yeyote
kuingia na kulisha mifugo ndani ya Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu na Ardhioevu”
kuingia na kulisha mifugo ndani ya Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu na Ardhioevu”
Prof. Maghembe alisema kuwa “mtandao wa ujangili unaanzia na watu wanaoingiza mifugo
ndani ya hifadhi, hivyo ni lazima sheria zifuatwe na waondoke mara moja,
watakaokaidi sheria itafuata mkondo wake na mifugo itakayokamatwa itataifishwa
na Serikali kwa mujibu wa sheria za nchi, sheria hizi hazina tofauti na sheria
zinazokataza watu wasijenge mabondeni au kwenye hifadhi za barabara”

Awali
akitoa taarifa, Meneja wa Pori hilo la Akiba la Selous Mabula Misungwi
alieleza baadhi ya changamoto kuu zinazoikabili hifadhi hiyo kuwa ni
pamoja na ujangili, miundombinu mibovu ya barabara kwa ajili ya doria na
vifaa ikiwemo magari ya doria na nyumba za watumishi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kimataifa
wa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF) Dkt. Marco
Lambertini alisema kuwa ili kuimarisha Uhifadhi nchini ni lazima wananchi
waishi karibu na maeneo hayo na pia washirikishwe juu ya umuhimu wake ili wasaidie
kuyalinda kwa faida yao na taifa kwa ujumla.

(Na Hamza Temba – Wizara ya Maliasili na Utalii # www.wizarayamaliasilinautalii.blogspot.com)
Afrika yatakiwa kuimarisha Utawala wa Sheria: Balozi Mahiga
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki Balozi Augustine
Maiga akitoa maelezo kwa wadau waliohudhuria mkutano wa Utawala wa
Sheria na Utawala Bora (hawapo pichani) uliofanyika leo jijini Dar es
salaam.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine
Maiga akiongea jambo na Balozi wa Italia Nchini Mhe. Luigi Scotto baada
ya kumaliza mkutano wa Utawala wa Sheria na Utawala Bora uliofanyika leo
jijini Dar es salaam.
Wadau
wa Mkutano wa Utawala wa Sheria kutoka nchi mbalimbali duniani
wakifatilia kwa makini mkutano wa Utawala wa Sheria na Utawala Bora ili
kufikia agenda ya mwaka 2030 na 2063 ya malengo ya millennia
uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Picha na Ally Daud- Maelezo
………………………………………………………………………………………………………………….
Na: Immaculate Makilika- MAELEZO, Tarehe
Dar es Salaam
BARA la Afrika limetakiwa
kuimarisha Utawala wa Sheria kupitia vyombo vya dola ikiwemo mahakama na
polisi ili kuisaidia mfumo huo kutetea maslahi ya wanyonge.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Augustine Mahiga wakati alipokuwa akifunga Mkutano wa siku
mbili wa Kimataifa kuhusu Utawala wa Sheria na Utawala bora.
“Lazima Afrika iimarishe vyombo
vyake vinavyosimamia Utawala wa sheria na Utawala bora kama Polisi na
Mahakama pamoja na kuwa na msimamo wa Bara katika kuzungumzia masuala
mbalimbali” alisema Balozi Mahiga
Balozi Maiga alisisitiza kuwa
rushwa imekua adui mkubwa katika Utawala wa Sheria, hivyo ni lazima
suala hilo lipatiwe ufumbuzi ili haki iweze kutendeka kwa watu wote.
Aidha, Balozi Maiga amemshukuru
Balozi wa Italia nchini Mhe. Luigi Scott kwa kufanikisha mkutano huo
pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Sheria
(IDLO) Bibi. Irene Khani kwa uamuzi wa wake wa kuichagua Tanzania kuwa
mwenyeji wa mkutano huo.
“Mkutano huu ni wa kihistoria
utasaidia kuleta mageuzi katika Taasisi ama Vyombo vinavyosimamia
masuala ya Sera na Sheria ambayo yatachochea maendeleo mazuri katika
nchi za Afrika” alisema Balozi Mahiga.
Mkutano huo unaomalizika leo
ulikua na kauli mbiu isemayo “Kufikia agenda ya 2030 na agenda ya 2063:
Utawala wa Sheria kwa Maendeleo Endelevu ya Afrika”, umehusisha wadau
mbalimbali wakiwemo Mawaziri, kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Mabalozi
kutoka ndani na nje ya Afrika pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya
kutetea Haki za Binadamu ulimwenguni.
No comments:
Post a Comment