Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua
kituo cha mawasiliano ya polisi (Call centre) katika kituo cha Kati
jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha
Mawasiliano cha Jeshi la Polisi. .Pamoja naye ni Waziri wa mambo ya
Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Ndani Meja
Jenerali Projest Rwegasira, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua
kituo cha mawasiliano ya polisi (Call centre) katika kituo cha Kati
jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha
Mawasiliano cha Jeshi la Polisi. .Pamoja naye ni Waziri wa mambo ya
Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Ndani Meja
Jenerali Projest Rwegasira, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Maguguli akisimama
wakati wa wimbo wa Taifa wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha
Mawasiliano cha Jeshi la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es
salaam leo. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,
Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe.
John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul
Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Sehemu ya wananchi na wadau waliohudhuria uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo
cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi viwanja vya Biafra jijini Dar es
salaam leo. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,
Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe.
John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul
Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Sehemu ya wananchi na wadau waliohudhuria uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo
cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi viwanja vya Biafra jijini Dar es
salaam leo. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,
Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe.
John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul
Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph akihutubia
uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi
katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi tuzo ya ufadhili Mkurugenzi Mtendaji w a
TBA Bw. Elius Mwakalinga wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha
Mawasiliano cha Jeshi la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es
salaam leo. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,
Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe.
John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul
Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi
tuzo ya ufadhili Bi. Edna Rajabu wa kwa niaba ya Shirika la Utangazaji
la TBC wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha
Jeshi la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo.
Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo
ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi,
IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na
viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata
maelezo katika mabanda mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo
cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi (Call Centre) katika viwanja vya
Bias=fra jijini Dar es salaam.. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya
Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu
Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizindua
Kituo kidogo cha Polisi kinachohamishika wakati wa uuzinduzi wa Kitaifa
wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi (Call Centre) katika
viwanja vya Biasfra jijini Dar es salaam.. Pamoja naye ni Rais Mstaafu
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba,
Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa
wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizindua
Kituo kidogo cha Polisi kinachohamishika wakati wa uuzinduzi wa Kitaifa
wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi (Call Centre) katika
viwanja vya Bias=fra jijini Dar es salaam.. Pamoja naye ni Rais Mstaafu
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba,
Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa
wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
KIKAO KAZI CHAFANIKISHA UHUISHAJI WA HAZINA BLOG
Maofisa Mawasiliano wa Wizara
ya Fedha na Mipango wakihuisha Blog ya Hazina katika kikao kazi
kilichofanyika Hazina Ndogo mjini Dodoma leo, ambapo pia
waliwashirikisha baadhi ya mablogger maarufu na watalaam wa
tehama.ambapo wadau wa mitandao John Bukuku kutoka Fullshangweblog,
Ahmed Michuzi kutoka Michuzi Media Group na Richard Mwakikenda kutoka
Kamanda wa Matukio blog wameshiriki katika kikao kazi hicho ambacho
kilikuwa maalum kwa ajili ya uhuishaji wa Hazina Blog
Mdau
wa mitandao ya kijamii kutoka Michuzi Media Group, Ahmad Michuzi
akielekeza jambo wakati kikao kazi hizo cha kuhuisha Blogu ya Wizara ya
Fedha na Mipango HAZINA BLOG leo. wa tatu kutoka kulia ni Mdau John
Bukuku wa Fullshangweblog akishiriki pamoja na maofisa habari hao
pamoja na Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na
Mipango Bw. Ben Mwaipaja
Mdau
Richard Mwaikenda wa nne kutoka kushoto waliosimama akiwa pamoja na
maofisa habari wa wizara ya fedha wakati mdau Ahmed Michuzzi akielekeza
jambo katika kikao hicho
HALMASHAURI NCHINI ZATAKIWA KUTOKUWA WABADHIRIFU WA FEDHA ZA MIRADI
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhandisi Mussa Iyombe akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi
Kukabiliana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia nchi (Decentralized
Climate Finance in Tanzania) leo mjini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Dkt. Deo Mtasiwa akizungumza wakati wa
hafla ya uzinduzi wa mradi Kukabiliana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa na
Tabia nchi (Decentralized Climate Finance in Tanzania) leo mjini Dodoma.
Meneja
Miradi wa Mfuko wa Umoja wa Taifa wa Maendeleo (UNCDF) Bw. Fakri Karim
akiwasilisha mada namna mfuko wao unavyoshiriki katika mradi wa
Kukabiliana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia nchi (Decentralized
Climate Finance in Tanzania) wakat wa uzinduzi wa mradi huo leo mjini
Dodoma.
Mwakilishi
Mshauri wa Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED) Alais
Morindat akielezea chimbuko la mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya
Hali ya Hewa na Tabia nchi (Decentralized Climate Finance in Tanzania)
wakati wa uzinduzi wa mradi huo leo mjini Dodoma.
Baadhi
ya wadu wadau wa mradi wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia nchi
akiwemo mwakilishi wa mtandao wa wanahabari watoto wanaoshughulika na
mabadiliko ya tabia nchi Bi. Getrude Clement (16) mwenye tisheti ya
kijani wakifuatilia mada wakati wa uzinduzi wa mradi huo leo mjini
Dodoma.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)
Mhandisi Mussa Iyombe (watano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya
pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo katika uzinduzi wa mradi wa
Kukabiliana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia nchi (Decentralized
Climate Finance in Tanzania) mjini Dodoma leo.
Picha na: Nasra Mwangamilo, TAMISEMI
———————————————————
Halmashauri nchini zatakiwa
kufanya kazi kwa weledi na ufanisi ili kuleta matokeo chanya na kwa
wakati, huku wakijiepusha na ufujaji rasilimali za umma wakati wa
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikaliza Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhandisi
Mussa Iyombe alipokuwa akimwakilisha Waziri wa nchi OR – TAMISEMI Mhe.
George Simbachawene katika uzinduzi rasmi wa mradi wa Kukabiliana na
Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia nchi (Decentralized Climate Finance
in Tanzania) leo mjini Dodoma.
“Niseme tu kuwa nategemea utendaji
wenye matokeo chanya kwa kufanya hiyvo kutajenga imani kwa wafadhili,
Wakurugenzi wote nchini fanyeni kazi kwa weledi,ufanisi na muepuke
kufuja mali za umma” Alisema Mhandisi Iyombe.
Mhandisi Iyombe aliongeza kuwa
mradi huu umelenga kuwajengea uwezo wanajamii katika kukabiliana na
athari za mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi ambapo juhudi
mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika kukabiliana na hilo.
Serikali kwa kushirikiana na wadau
wa maendeleo hususan Shirika la Kimataifa la Mazingira na Maendeleo
(IIED), Haki Kazi Catalyst (HKC), Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF)
chini ya ufadhili wa Serikali ya Uingereza (UK-aid) na Mfuko wa Umoja wa
Mataifa wa Maendeleo (UNCDF LoCAL) itatekeleza mradi huu katka
Halmashauri 15 nchini.
Halmashauri hizo ni pamoja na
Kondoa, Bahi, Manyoni, Mpwapwa, Kiteto, Same, Simanjiro, Kilwa, Siha,
Mbulu, Iramba na Pangani ambazo zimejumuishwa na Halmashauri za Monduli,
Ngorongoro na Longido zilizokuwa katika mradi wa majaribio.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu
anyeshughulikia Afya kutoka OR-TAMISEMI Deo Mtasiwa amesema kuwa kwakuwa
Serikali tayari imekwisha tengeneza mfumo imara ilikuhakikisha
utekelezaji wa mradi huo unafanikiwa kuanzia ngazi ya kijiji.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
mradi huu MwakilishiMshauri wa Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na
Maendeleo (IIED) Alais Morindat alisema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa
siyo kitu kipya na kuongeza kuwa historia ya mradi huo inatokana na
athari zilizojitokeza katika jamii za wafugaji katika maeneo ya
Kasikazini mwa Tanzania ambapo mifugo mingi katika maeneo ya Monduli,
Ngorongoro na Longido ilipoteza uhai.
RAIS DKT. MAGUFULI AFUTURISHA MAKUNDI MBALIMBALI YA VIONGOZI, WALEMAVU WA NGOZI, WASIOJIWEZA PAMOJA NA WAFANYAKAZI WA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.
Raiswa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana
na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ikulu jijini Dar es
Salaam. Rais Dkt. Magufuli amefuturisha makundi mbalimbali ikiwemo
viongozi wa dini, chama Serikali ya mkoa, Watoto Yatima na wenye ulemavu
wa ngozi Albino, Wavuvi wa ferry, walemavu vya viungo pamoja na
wafanyakazi wa Ikulu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir wakati wakielekea
kufuturu Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Paul Makonda na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa
Salum.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir mara baada ya
kufuturu na makundi ya watu mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na makundi mbalimbali (hawapo pichani)ikiwemo viongozi wa dini, chama
Serikali ya mkoa, Watoto Yatima na wenye ulemavu wa ngozi
(Albino),walemavu wa viungo pamoja na wafanyakazi wa Ikulu mara baada ya
kuwafuturisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir , Sheikh Mkuu wa mkoa wa
Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum pamoja Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Paul Makonda wakiwa wamesimama wakati wa dua mara baada ya kufuturu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
kwenye foleni ya kupata futari pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Paul Makonda Ikulu jijini Dar es Salaam.
Serikali yasitisha tamko la utoaji wa Chakula Muhimbili.
Na Ally Daud-Maelezo
—————–
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto , imesitisha tamko la utoaji wa vyakula kwa wagonjwa
watakaolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kupisha utafiti
wa kina kuhusu huduma hiyo ili kuweza kutoa kilicho bora kwa watanzania.
Akizungumza hayo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Bi. Ummy Mwalimu amesema kwamba wameamua kusitisha mpango
mpaka watapotangaza tena ili kufanya utafiti kujua kama kuna faida au
hasara kwa wananchi.
“Natoa tamko kwamba huduma hii
iliyotarajiwa kuanza hivi karibuni isitishwe mara moja ili kupisha
watafiti waweze kufanya uchunguzi kujua inawasaidia kwa kiasi gani
wananchi” alisisitiza Bi. Mwalimu.
Aidha Bi. Mwalimu amesema kwamba
huduma hiyo itatolewa kwa wagonjwa watakaolazwa hapo kwa kulipia
shilingi elfu 50 ikiwemo shilingi elfu kumi ya kumuona daktari , elfu
kumi ya kitanda na elfu 30 iliyobaki ni kwa malipo ya chakula kwa wiki.
“Huduma hii inalenga kuwasaidia
wananchi katika kuwaandalia chakula stahiki kwa wagonjwa na kupunguza
usumbufu kwa waangalizi wa wagonjwa wao kuleta vyakula hospitalini ili
kuimalisha afya zao kwa ujumla” aliongeza Bi.Mwalimu.
Ugonjwa wa Sumukavu wagundulika Dodoma.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Ummy Mwalimu
akiongea na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam kuhusu mlipuko wa
ugonjwa unaosababishwa na sumukavu uliotokea hivi karibuni mkoani
Dodoma.
Picha na Ally Daud-Maelezo.
———————————————
Na Ally Daud-Maelezo
Ugonjwa unaosababishwa na Sumukavu
kwenye Mahindi ya chakula umegundilika katika Wilaya za Chemba na
Kondoa Mkoani Dodoma baada ya kupeleka jopo la Wataalam waliofanya
utafiti na kugundua kuwepo kwa ugonjwa huo.
Akizungumza hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Bi. Ummy Mwalimu amesema kwamba matokeo ya awali ya watafiti
hao imeonyesha kwamba ugonjwa huo umesababishwa na ulaji wa chakula
kilichokuwa na sumukuvu na kuleta madhara.
“Hayo ni matokeo ya awali ya
watafiti wa wizara yangu hivyo basi nasubiri matokeo ya vipimo vya damu
na haja ndogo vilivyopelekwa kwa uchunguzi zaidi katika Maabara ya CDC,
Atlanta iliyopo nchini Marekani na matarajio yetu ni kupata majibu hayo
katika kipindi kisichozidi wiki moja” aliongeza Bi Mwalimu.
Aidha Bi. Mwalimu amesema kwamba
mpaka kufikia tarehe 24 Juni 2016, idadi ya wagonjwa imefikia 32, na
idadi ya vifo imebakia 7. Hii ni baada ya kuongezeka kwa wagonjwa 11
katika kipindi cha wiki moja.
“Hadi jana kulikuwa na jumla ya
wagonjwa 9 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Dodoma, na 14
wako katika Hospitali ya Wilaya ya Kondoa. Wagonjwa watatu waliolazwa
Hospitali ya Mkoa Dodoma, na wawili waliolazwa Kondoa, bado hali zao ni
tete” aliongeza Bi. Mwalimu.
Pamoja na hayo Bi. Mwalimu alisema
kwamba Serikali itaendelea kuimarisha mikakati ya kitaifa ya kupunguza
uchafuzi wa sumukuvu katika vyakula, ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo
wa kupima vimelea hivyo katika damu na mkojo miongoni mwa taasisi za
ndani ya nchi.
“ Tutaendelea kutoa matibabu kwa
wananchi walioathirika na Ugonjwa huo, kwenye Hospitali ya Mkoa wa
Dodoma na Hospitali ya Wilaya ya Kondoa ili kudhibiti na kurudisha afya
za wananchi katika kiwango kinachohitajika” aliongeza Bi. Mwalimu
Aidha Bi. Mwalimu ametoa rai kwa
wananchi na wakazi wa Dodoma kwamba wanapaswa kuchambua nafaka
zilizoharibika (zilizooza, kuvunjika, zilizobadilika rangi), kukoboa
mahindi kabla ya kusaga au kuacha kutumia nafaka zitakazoonekana
kuharibika sana ili kuepukana na kiasi kilichozidi sumukavu kwenye
nafaka.
Wizara ya Fedha na Mipango yatoa elimu ya ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi kwa wabunge
Mgeni
Rasmi, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Tulia Ackson akifungua Semina iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na
Mipango kuhusu Ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma ilifofanyika
leo Mjini Dodoma katika ukumbi wa Pius Mswekwa ikiwa na Lengo la
kuwajengea uwezo wabunge kuhusu umuhimu wa kushirikisha Sekta Binafsi
katika miradi ya maendeleo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu Bunge Vijana Kazi Ajira na
Walemavu Mhe. Jenista Mhagama(wa kwanza kushoto) akifuatilia Semina
iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango ikilenga kuwajengea uwezo
wabunge kuhusu umuhimu wa kushirikiana kati ya Sekta Binafsi na ile ya
Umma (PPP) Katika miradi ya maendeleo. Kulia ni Spika wa Bunge Mhe.
Tulia Ackson ambaye alikuwa mgeni rasmi katika semina hiyo.
Mbunge
wa Ileje Mhe. Janet Mbene akitoa maoni yake wakati wa semina ya
kuwajengea uwezo wabunge kuhusu umuhimu wa kushirikisha Sekta Binafsi
katika miradi ya maendeleo.
Mbunge
wa Viti Maalum Mhe. Sophia Simba akitoa maelezo jinsi miradi
itakayotekelezwa kwa ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi inavyoweza
kuchangia kukuza maendeleo.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson
(katikati) ambaye alikuwa mgeni rasmi wa semina ya kuwajengea uwezo
Wabunge kuhusu umuhimu wa Ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma
(PPP) akifurahia jambo mapema leo Bungeni Mjini Dodoma. Kulia ni Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na kushoto ni
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bajeti Mhe. Josephat Kandege.
MAGUFULI AWATAKA POLISI KUDHIBITI MAJAMBAZI NCHINI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akihutubia kwenye uzinduzi wa kituo cha Mawasiliano cha Polisi Call
Centre Biafra Kinondoni.
…………………………………………………………………………………………………
Jonas Kamaleki, MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka jeshi la polisi
nchini kuwadhibiti majambazi ipasavyo kwa kuwanyanganya silaha kwenye
matukio ya kiuharifu ili kukomesha vitendo viovu katika Taifa.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Usalama wa Jamii.
“Inashangaza jambazi anavamia
kituo cha polisi anaua na anaondoka wakati polisi wapo na wana silaha na
risasi wanazo lakini wanashindwa kumnyang’anya silaha,”alishangaa Rais
Magufuli.
Ameongeza kuwa ujambazi na
vitendo vya uharifu nchini inabidi vikomeshwe mara moja ili watanzania
waishi kwa amani na kufanya maendeleo kwani wananchi wanataka maendeleo.
Akiongelea kuhusu maslahi na
vitendea kazi kwa jeshi la polisi, Rais Magufuli amesema kuwa serikali
yake itafanya kila iwezalo kuliwezesha jeshi hilo ili liweze kufanya
kazi kwa ubora zaidi.
Rais Magufuli ameonyesha kuwa na
imani na jeshi la polisi licha ya kuwa na kasoro ndogo ndogo kwa baadhi
ya polisi ambao wanalichafua jeshi hilo.
Aidha ametoa agizo kwa TCRA kushirikiana na jeshi la polisi nchini ili kuweza kurekodi simu na kutoa print out mara moja tofauti na ilivyo sasa.
Kuhusu kundi la wafanyakazi
wanaofanyakazi kwenye Dawati la Taarifa la polisi, Mhe. Rais amemtaka
Mkuu wa Jeshi hilo, IGP Ernest Mangu kuwafikiria na kuwapatia posho ya
kazi kwani kazi wanayoifanya ni ngumu mno na inahitaji umakini zaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda amemwomba Mhe. Rais kuliongezea fedha jeshi
hilo ili liweze kufanya kazi kwa ustadi zaidi na kukomesha vitendo vya
uharifu nchini.
Makonda amelipongeza jeshi la polisi kwa kudhibiti matukio ya ujambazi hapa nchini hususan kwenye mabenki.
Mpango huu wa Usalama wa Jamii
umezinduliwa leo na utadumu hadi 2019 na unatarajiwa kutoa matokeo
makubwa ya kudhibiti uharifu nchini.
Media Car Wash yaanza kwa mafanikio Dodoma
Msanii
wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel (kushoto) na Mkongwe wa Bongo Fleva
Inspector Haroun na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima wakiosha
gari.
|
Mkurugenzi
wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman
Rehani (kulia) akimkabidhi fedha za kuoshewa gari Msanii wa Bongo Movie,
Aunt Ezekiel.
|
Miss
Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima (kulia) na Mkurugenzi wa Utafiti na
Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani
(kushoto) wakijitolea kuosha magari kwenye kampeni hizo.
|
Msanii
wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel na mpiga picha wa magazeti ya The Guardian
Ltd, Halima Kambi wakiosha moja ya gari katika kampeni hizo.
|
Mwenyekiti
wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For
Health’, Benjamin Thompson akishiriki zoezi la kuosha magari.
|
Mbunge
wa Kilolo Venance Mwamoto akishiriki zoezi la kuosha magari kuchangisha
fedha kwa ajili ya kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media
Car Wash For Health’ Dodoma leo.
|
SHELISHELI WAIHOFIA SERENGETI BOYS
Kocha
Mkuu wa timu ya soka ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ya
Shelisheli, Gavan Jeanne ameonesha kuihofia Serengeti Boys ya Tanzania
katika mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa
utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Jeanne alionesha hofu hiyo leo
Juni 25, 2016 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na mbele ya
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime ambao kwa pamoja walikuwa
wakmizungumzia namna walivyoandaa timu zao kwa ajili ya mchezo huo wa
kesho.
“Hatujawahi kushiriki michuano ya
vijana. Hii ni mara yetu ya kwanza. Tumekuja kujifunza kwa wenzetu
Tanzania ambao wana uzoefu,” alisema Jeanne ambaye pia alithibitisha
kuwa hawajawahi kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
Kwa upande wa Bakari Shime wa
Serengeti Boys, alisema ameindaa mechi hiyo vema kiakili na kimwili kwa
ajili ya kuikabili Shelisheli katika mchezo huo ambao hamasa yake
imekuwa kubwa kwa kuwa kikosi hicho kinaandaliwa kuwa timu ya taifa
baada ya miaka miwili.
Wachezaji wa Serengeti Boys
wamesema, watafanya vema kwenye mchezo huo. Wachezaji hao ni Anthony
Shilole ambaye alisema: “Tumejifunza mambo mengi, ushindi ni lazima kwa
sababu tutafuata maelekezo ya walimu wetu. Tutajitahidi tushinde.”
Ally Ng’anzi: Maandalizi ni
mazuri. Mechi ya Jumapili tumejiandaa vema. Tunashinda tena kwa magoli
mengi.” Ally Msengi: “Watanzania watarajie ushindi baada ya maandalizi
ya muda mrefu. Timu iko kambini kitambo.” Kennedy Nashony: Tutapambana
kadiri ya uwezo. Kila mechi kwetu ni fainali. Hatuko tayari kupoteza ili
kukosa mechi zijazo.” Shelisheli ilitua Ijumaa usiku saa 7.45 usiku
ikiwa na viongozi 25 na imefikia hoteli ya Southern Sun iliyoko katikati
ya jiji la Dar es Salaam.
Waamuzi wanne kutoka Ethiopia,
ndio watakaochezesha mchezo huo. Waamuzi hao ni Belay Tadesse Asserese
ambaye ni mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni Tigle Gizaw Belachew
upande wa kulia na Kinfe Yilma Kinfe upande wa kushoto huku mwamuzi wa
akiba atakuwa Lemma Nigussie. Kamishna wa mchezo huo atakuwa ni Bester
Kalombo.
Serengeti Boys ilikuwa kambini
tangu Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo huo wa kufuzu fainali za Kombe
la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli utakaofanyika
Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Mchezo
wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2,
2016 huko Shelisheli.
Katika kuajindaa na mchezo huo,
Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya
vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth
Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu
katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
JUMUIYA YA MUZDALIFAT YATOA MSAADA WA VIFAA MBALIMBALI KATIKA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA ZANZIBAR.
Katibu
Mkuu wa Jumuiya ya Muzdalifat Farouk Hamadi akitoa nasaha kwa mgeni
rasmi na Waalikwa katika hafla ya kukabidhi msaada wa Vifaa mbalimbali
vya Hospitali vilivyotolewa msaada na Jumuiya ya Muzdalifat
wakishirikiana na Shirika la Halping Hand kutoka marekani,katika katika
Hospitali ya Mnazi mmoja Mjini Unguja.
Muakilishi
wa Shirika la Halping Hand Muhammad Irfan Bashir akitoa hotuba katika
hafla ya kukabidhi msaada wa Vifaa mbalimbali vya Hospitali
vilivyotolewa msaada na Jumuiya ya Muzdalifat wakishirikiana na Shirika
la Halping Hand kutoka marekani,katika Hospitali ya Mnazi mmoja Mjini
Unguja.
Kaimu
Mkurugenzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Dk,Msafiri Marijani akitoa
nasaha kwa niaba ya Naibu Waziri wa Afya Baada ya kupokea Msaada wa
Vifaa mbalimbali vya Hospitali vilivyotolewa Msaada na Jumuiya ya
Muzdalifat wakishirikiana na Shirika la Halping Hand kutoka
marekani,katika Hospitali ya Mnazi mmoja Mjini Unguja.
Katibu
Mkuu wa Jumuiya ya Muzdalifat Farouk Hamadi katikati akiwa na
Muakilishi wa Shirika la Halping Hand Muhammad Irfan Bashir kushoto
wakimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Dk,Msafiri
Marijani moja kati ya Vifaa vilivyotolewa Msaada na Jumuiya ya
Muzdalifat wakishirikiana na Shirika la Halping Hand kutoka
marekani,katika Hospitali ya Mnazi mmoja Mjini Unguja.
Baadhi
ya Vifaa mbalimbali vya Hospitali ambavyo vimetolewa Msaada na Jumuiya
ya Muzdalifat wakishirikiana na Shirika la Halping Hand kutoka marekani
vikiteremshwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja Mjini Unguja.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
WACHUMI NA MAAFISA MIPANGO NCHINI WAKUTANA DODOMA KUJADILI MPANGO WA PILI WA TAIFA WA MAENDELEO
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza katika
Mkutano wa Mwaka wa Wachumi na Maafisa Mipango unaofanyika katika ukumbi
wa Hazina mjini Dodoma. Alifungua mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa
Fedha na Mipango Mge. Dkt. Philip Mpango. Kaulimbiu ya Mkutano ni
Kuelekea kwenye Utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka
Mitano 2016/17 – 2020/21.
Katibu
Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile
akimkaribisha Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe
kufungua mkutano huo. Kulia kwake ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya
Mipango, Bibi Florence Mwanri.
Kaimu
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri akizungumza
katika mkutano wa Mwaka wa Wachumi na Maafisa Mipango unaofanyika mjini
Dodoma.
Baadhi
ya washiriki wa mkutano wa Mwaka wa Wachumi na Maafisa Mipango
wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison
Mwakyembe.
Washiriki
wa Mkutano wa Mwaka wa Wachumi na Maafisa Mipango wakiwa katika picha
ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(wapili kushoto waliokaa mwenye miwani).
Picha na mpiga picha wetu
…………………………………………………………………………………………………..
Na Benny Mwaipaja, WFM
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango, Dkt. Servacius Likwelile amesema kuwa Tanzania imejipanga
kuimarisha mapato yake ya ndani ili kutekeleza kikamilifu Mpango wa Pili
wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021.
Dkt. Likwelile, amesema hayo
Mjini Dodoma, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku 2 unaowahusisha
wataalamu wa Uchumi na Mipango wapatao 170 kutoka nchi nzima.
Amesema kuwa misaada kutoka kwa
wadau wa maendeleo imekuwa ikipungua kila wakati, hatua ambayo imeifanya
Serikali kuendelea kujipanga kukabiliana na nakisi ya Bajeti yake ili
kukuza maendeleo.
“Mikopo yenye riba nafuu nayo
imepungua, sasa hivi unaenda kukopa kibiashara, kwa uchumi wetu huu
hatuwezi kumudu” alisisitiza Dkt. Likwelile
Ameeleza kuwa Tanzania
inakabiliwa na changamoto kubwa ya kuimarisha miundombinu ya barabara,
reli, bandari na mambo mengine, hali inayohitaji fedha nyingi ambazo
zitapatika kwa kukusanya kodi mbalimbali.
Amewataka wataalamu hao wa uchumi
na mipango kujadili na kuibuka na mipango itakayosaidia kufanikisha
utekelezaji wa Mpango huo wa Pili wa Maendeleo wa Taifa unaotarajiwa
kugharimu shilingi Trilioni 107.
Akifungua mkutano huo kwa niaba
ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Waziri wa Katiba na
Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wataalamu hao kutoa mapendekezo
ya kitaalamu wakizingatia changamoto mbalimbali zikiwemo za kupanda kwa
gharama za mafuta duniani.
Vilevile, amewakumbusha umuhimu
wa kutumia takwimu sahihi wakati wa kupanga namna bora ya kutekeleza
mpango huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na watanazania kuwaletea
maendeleo ya haraka
“Takwimu ndizo zinazotoa picha
halisi ya matatizo yanayowakabili watanzania ukiwemo umasikini, ambapo
zikitumika vizuri zitasaidia kupanga namna bora ya wananchi wanavyoweza
kuondokana na umasikini huo” Alisisitiza Dkt. Mwakyembe
Kwa upande wake, Kaimu Katibu
Mtendaji wa Tume ya Mipango, Florence Mwanri, amesema kuwa Tanzania
imedhamiria kuwa nchi yenye uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka
2025.
Amesema kuwa hatua hiyo itafikiwa
kwa kuelekeza nguvu kubwa katika uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda
kwa kushirikiana na sekta binafsi.
Mwanri amesema kuwa hatua hiyo
itakuza uchumi wa nchi kwa kuongeza kipato cha wananchi pamoja na ajira
na akasisitiza umuhimu wa wananchi kufanya kazi kwa bidii na kujitolea
utaalamu na nguvu zao zote kufanikisha malengo hayo.
Bodi ya Filamu yakutana na Chama cha Waigizaji Tanzania kujadili maendeleo ya sanaa nchini.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akizungumza na
viongozi wa Chama cha Waigizaji Tanzania katika kikao cha kujadili
maendeleo ya wasanii na sanaa nchini kushoto ni Mwenyekiti wa chama
hicho Bw. Eliya Mjatta.
Mwenyekiti
wa Chama cha Waigizaji Tanzania Bw. Eliya Mjatta akichangia hoja katika
kikao baina ya Chama chake na Bodi ya Filamu Tanzania katika kujadili
maendeleo ya wasanii na sanaa nchini kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya
Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akisisitiza
jambo katika kikao baina ya Bodi yake na viongozi wa Chama cha Wasanii
Tanzania katika kujadili maendeleo ya wasanii na sanaa nchini.
Afisa
Utamaduni kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Wilhadi Tairo akichangia
hoja katika kikao kati ya Bodi ya Filamu na Chama cha Wasanii Tanzania
katika kujadili maendeleo ya wasanii na sanaa nchini.
katibu
Mkuu wa chama cha Wasanii Tanzania Bw. Twiza Mbarouk akichangia hoja
katika kikao kati ya Chama cha Wasanii Tanzania na Bodi ya Filamu katika
kujadili maendeleo ya wasanii na sanaa nchini.
Afisa
Utamaduni kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Clarence Chelesi
akichangia hoja katika kikao kati ya Bodi ya Filamu na Chama cha Wasanii
Tanzania katika kujadili maendeleo ya wasanii na sanaa nchini.
katibu
Mkuu wa Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF) Bw. Mathew Bicco
(kushoto)akichangia hoja katika kikao kati ya Bodi ya Filamu na Chama
cha Wasanii Tanzania katika kujadili maendeleo ya wasanii na sanaa
nchini.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
MUHIMBILI WAFANYA USAFI LEO KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS LA KILA MWEZI
Baadhi
ya wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakifanya usafi
LEO ikiwa ni kutekeleza agizo la rais la kufanya usafi kila mwishoni mwa
mwezi.
Kutoka
kulia Chindemba Lingwana, Patrick Rogath ambaye ni Mkuu Idara ya Idara
ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwenye hospitali hiyo, Christian
Mtei na Fred Felix wakifanya usafi katika jengo la utawala LEO.
Shughuli za usafi zikiendelea
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
RIDHIWANI AKABIDHI MAGARI YA WAGONJWA KITUO CHA AFYA CHALINZE NA MIONO
MBUNGE
wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akikabidhi gari la wagonjwa
(ambulance)jana, kwa mganga mkuu wa halmashauri ya Mji wa Chalinze,dkt
Hangai ,mbunge huyo alikabidhi magari ya wagonjwa mawili ikiwa ni
pamoja na kituo cha afya Miono.
MBUNGE
wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiwasha gari la wagonjwa
(ambulance) mara baada ya kulikabidhi katika kituo cha afya cha
Chalinze, mbunge huyo alikabidhi magari ya wagonjwa mawili ikiwa ni
pamoja na kituo cha afya Miono.
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
———————————————————————-
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
MBUNGE
wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani,Ridhiwani Kikwete amekabidhi magari
ya kubebea wagonjwa (ambulance)katika kituo cha afya cha Chalinze na
Miono yote yakiwa yamegharimu zaidi ya sh.mil 200.
Ridhiwani
ametoa magari hayo kwa lengo la kupunguza adha ya usafiri kwa wagonjwa
hususan wanaotakiwa kwenda kupata matibabu zaidi katika hospital ya
rufaa ya Tumbi na Muhimbili.
Akikabidhi
magari hayo jana ,kwa mganga mkuu wa halmashauri ya Mji wa Chalinze,
dkt Rahim Hangai, mbunge huyo alisema wakati huu sio wa longolongo bali
ni wakati wa kutumikia wananchi na kutekeleza yale viongozi
waliyoyaahidi ndani ya jamii.
Ridhiwani
alisema hatotaka kuona gari hilo haliwatendei haki wananchi hivyo
aliomba litumike kwa ajili ya wagonjwa na sio vinginevyo.
Alisema
awali kituo cha afya cha Miono kilikuwa na gari la kubebea wagonjwa
lakini kwasasa limeharibika hivyo kuamua kupeleka gari jingine
lililokuwepo kituo cha afya cha Chalinze.
“Hadi sasa tumeshakabidhi magari ya wagonjwa katika hospitali ya wilaya iliyopo Msoga ambapo tumeikabidhi gari la wagonjwa tulilokabidhiwa na mh Rais John Magufuli ,nyingine ndio hizi mbili tulizokabidhi leo”alisema Ridhiwani.
“Hadi sasa tumeshakabidhi magari ya wagonjwa katika hospitali ya wilaya iliyopo Msoga ambapo tumeikabidhi gari la wagonjwa tulilokabidhiwa na mh Rais John Magufuli ,nyingine ndio hizi mbili tulizokabidhi leo”alisema Ridhiwani.
Alieleza
kuwa tatizo la ukosefu wa magari hayo lipo kwenye maeneo mengi ya jimbo
hilo hivyo amejipanga kushirikiana na wadau na wafadhili mbalimbali
kutatua changamoto hiyo hatua kwa hatua.
Aidha
Ridhiwani alisema amepokea malalamiko juu ya kulipishwa gharama za
mafuta kutoka kwa wagonjwa ambao walikuwa wakilipishwa sh.30,000 hadi
80,000 kwa wale wanaotoka Miono lakini kuanzia mwezi Julai mwaka huu
hakuna mgonjwa atakaetozwagharama hizo.
Nae
mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Chalinze, Saidi Zikatimu
alimshukuru Ridhiwani kwa niaba ya wanaChalinze na kuahidi kushirikiana
nae ili kuinua maendeleo ya jimbo hilo.
Zikatimu alisema ni jumla magari matatu ambayo yametolewa hadi sasa kutokana na juhudi za mbunge huyo iwe kwa kuomba wafadhili na jitihada zake mwenyewe.
Zikatimu alisema ni jumla magari matatu ambayo yametolewa hadi sasa kutokana na juhudi za mbunge huyo iwe kwa kuomba wafadhili na jitihada zake mwenyewe.
Diwani
wa kata ya Bwilingu ,Lucas Rufunga pamoja na diwani wa kata ya Miono
Juma Mpwimbwi walimshukuru mbunge huyo na kumuomba asichoke kushirikiana
nao kuzipatia ufumbuzi changamoto nyingine zinazowakabili kwenye sekta
ya afya.
Kwa
upande wake mganga mkuu wa halmashauri ya Mji wa Chalinze, dkt Rahim
Hangai alishukuru kupokea msaada huo na kusema atahakikisha linatumika
kwa matumizi lengwa.
Alielezea kuwa wanampongeza mbunge huyo kwa kujitoa kwake kuwatumikia wanaChalinze.
“Umekuwa
ukionyesha kwa vitendo na sio maneno, tunaamini hukutoa kwasababu ni
tajiri ama una magarii mengi bali ulitoa kwa ajili ya moyo wako wa
huruma na upendo wa kusaidia “alisema dkt Hangai.
Dkt Hangai alisema wanaamini ameguswa na changamoto iliyokuwa ikiwakabili ya kupunguza tatizo la usafiri.
Hata hivyo alisema magari hayo itaboresha huduma za wagonjwa na hasa mama wajawazito na watoto katika rufaa.
Dkt
Hangai alielezea kuwa licha ya kutatuliwa changamoto hiyo lakini bado
wanakabiliwa na changamoto ya ufunguzi wa huduma za upasuaji katika
jengo kutokana na ukosefu wa vifaa ili kupunguza rufaa za wajawazito,
upasuaji kwenda Tumbi.
Nyingine
ni uzio wa kituo, mashine ya kufulia nguo za wagonjwa, uchakavu wa
jengo la (OPD) wagonjwa wa nje, jengo la huduma ya mama na mtoto, chumba
cha maiti na majeruhi.
Dkt Hangai alimuomba Ridhiwani kubeba changamoto hizo ili aweze kuzitatua.
Kuhusiana na changamoto hizo Ridhiwani alisema ameyachukua yote na kuahidi kuyafanyiakazi kadri itakavyokuwa.
Prof. Makame Mbarawa amteua Mhandisi Deusdedit Conatus Vitalis Kakoko kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA
BANDARI TANZANIA (TPA)
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame M. Mbarawa, leo
tarehe 25 Juni, 2016 amemteua Mhandisi Deusdedit Conatus Vitalis Kakoko
kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania.
Mhandisi Kakoko amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Ephraim Mgawe ambae uteuzi wake ulitenguliwa.
Mhandisi Kakoko ni Meneja wa miradi kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Uteuzi huu unaanza mara moja.
Ramsey V. Kanyanga
KAIMU KATIBU WA WAZIRI
25/06/2016
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura alipotembelea makao makuu ya StarTimes Beijing nchini China
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
(katikati) akifanya mahojiano na mtangazaji wa StarTimes ambaye ni
Mtanzania David (kushoto) wakati alipotembelea studio hizo leo zilizopo
mjini Beijing nchini China kwa ajili ya kujionea kazi mbalimbali
zinazofanywa na studio hizo. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Prof.
Elisante Ole Gabriel.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) na Rais wa kampuni ya kimataifa ya
StarTimes Pang Xinxing (kushoto). Mhe. Naibu Waziri alitembelea studio
za StarTimes zilizopo mjini Beijing nchini China leo kwa ajili ya
kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na studio hizo.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Tanzania
na kampuni ya StarTimes walipotembelea studio za StarMedia zilizopo
mjini Beijing nchini China leo kwa ajili ya kujionea kazi mbalimbali
zinazofanywa na studio hiyo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Habari (Maelezo) Zamaradi Kawawa akifuatiwa na Erick Xue, kulia ni
Mkurugenzi Mkuu wa Star Media Tanzania Liao Lanfang akifuatiwa na
Katibu Mkuu Prof. Elisante Ole Gabriel na watatu kulia ni Mkurugenzi wa
Idara ya nchi za nje wa StarTimes William Lan.
Picha na mpigapicha wetu
LUHWAVI ATEMBELEA UHURU FM, AZUNGUMZA NA WATUMISHI KUJUA YANAYOWASIBU KATIKA UTENDAJI WAO
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akiongozwa na Mkurugezi wa
Mawasiliano Makao Makuu ya CCM, Godfrey Chongolo na Mkuu wa Chumba cha
Habari Uhuru FM, Pius Ntiga, kwenda katika Ofisi za Uhuru Fm, mtaa wa
Ukami, katika Jengo la Ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam, kuzungumza na
watumishi wa Radio hiyo ili kujua kwa undani masuala mbalimbali
wanayokabiliana nayo katika utendaji wao wa kazi za kila siku, jana.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akifurahia jambo na
Mkurugezi wa Mawasiliano Makao Makuu ya CCM, Godfrey Chongolo wakati
wakienda katika Ofisi za Uhuru Fm, mtaa wa Ukami, katika Jengo la Ofisi
ya CCM mkoa wa Dar es Salaam, kuzungumza na watumishi wa Radio hiyo ili
kujua kwa undani masuala mbalimbali wanayokabiliana nayo katika utendaji
wao wa kazi za kila siku, jana.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akisaini kitabu cha wagen baada ya kufika katika Ofisi za Uhuru FM
Mkurugenzi
wa Uhuru FM, Angel Akilimali akikabidhi taarifa ya Uhuru FM kwa Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi baada ya kumsomea
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi akimshukuru Mkurugenzo wa Uhuru FM, Ange Akilimali wakati akipokea taarifa hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akipatiwa maelezo katika chumba cha kufuatilia na kuratibu habari cha Uhuru FM
Mkurugenzi
Mtendaji wa Uhuru FM, Angel Akilimali akimpa ufafanuzi Naibu Katibu
Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi kuhusu chumba hicho cha kufuatilia na
kuratibu habari
Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru FM, Angel Akilimali akimpa ufafanuzi Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi kuhusu chumba hicho cha
kufuatilia na kuratibu habari
Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru FM, Angel Akilimali akimpa ufafanuzi Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi kuhusu chumba hicho cha
kufuatilia na kuratibu habari
UN yazindua sehemu ya pili Mpango wa Misaada ya Maendeleo (UNDAP 2)
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez akizungumza
katika halfa ya kuzindua mpango wa misaada ya maendeleo UNDAP 2
2016-2021.
Katika
kuendeleza juhudi zake za kusaidia mataifa wanachama, Umoja wa Mataifa
(UN) umezindua mpango mpya wa misaada ya maendeleo nchini (UNDAP 2)
baada ya mpango wa kwanza wa UNDAP 1 kukamilika kwa mafanikio makubwa na
hivyo kuzinduliwa mpango mpya ambao utaendeleza hatua uliyoishia mpango
wa kwanza.
Katika
mpango huu mpya UN inataraji kutoa kiasi cha Dola Bilioni 1.3 ambazo
zitatumika katika kuboresha kusaidia kukuza uchumi na upatikanaji wa
ajira, kuboresha huduma zinazopatikana katika sekta ya afya, kuboresha
demokrasia, usawa wa kijinsia na haki za binadamu na kusaidia kupambana
na mabadiliko ya tabia ya nchini.
Akizungumza
katika halfa ya kuzindua mpango huo, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez alisema utekelezaji wa mpango mpya wa
UNDAP 2 utakwenda pamoja na utekeleji na Malengo ya Maendeleo Endelevu
Duniani (SDGs).
Alisema
kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kushirikiana na Tanzania katika
kusaidia upatikanaji wa huduma bora za kijamii na ni matumaini yake kuwa
wataendelea kudumisha ushirikiano uliopo sasa katika ya UN na serikali
ya Tanzania.
“Mpango
huu utaweka mbele vipaumbele vya taifa na utahakikisha kuwa hakuna mtu
ambaye anaachwa nyuma ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa
Maendeleo Endelevu ambao unataka kila mtu ahusike,
“Umoja
wa Mataifa utaendelea kudumisha ushirikiano uliopo baina yake na
Tanzania na itaendelea kuisaidia Tanzania pamoja na wananchi wake,”
alisema Rodriguez.
Nae
mgeni rasmi katika halfa hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na
Katiba, Prof. Sifuni Mchome, alisema kuwa mpango huo umekuwa na matokeo
mazuri kwa Watanzania lakini pamoja na hilo pia serikali imekuwa
ikifanya jitihada mbalimbali zitakazoweza kukuza uchumi wa nchi na
wananchi wake.
Prof.
Mchome alisema kuwa serikali ya Tanzania inaushukuru Umoja wa Mataiffa
kwa kuwaletea mpango wa pili baada ya awali kumalizika lakini pia
serikali itahakikisha kuwa mpango huo utahusika kwa kila Mtanzania ili
na yeye aweze kufaidika na mpango wa UNDAP 2.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Prof. Sifuni Mchome akizungumza kwa niaba ya serikali katika uzinduzi wa UNDAP 2.
“Tunashukuru
baada ya ule wa kwanza mmetuletea mpango wa pili lakini pia hata pesa
imeongezeka kwa sasa kupata Dola Bilioni 1.3 kutoka ule wa kwanza ambao
ulikuwa wa Dola Bilioni 0.8 na katika mpango huu tutamshirikisha kila
mwananchi na yeye afaidike nao,
“Serikali
imekuwa ikifanya jitihada za kuleta maendeleo ya taifa na kwa mwananchi
mmoja mmoja lakini bado tunawahitaji wadau kama nyie na tunawaomba
msiondoke na tuendelee kufAnya kazi kwa kushirikiana,” alisema Prof.
Mchome.
Mpango
mpya wa misaada ya kimaendeleo ambao umetolewa na Umoja wa Mataifa (UN)
unataraji kuanza Julai, 2016 na kumalizika Juni, 2021.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima
akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dk. Juma Malik Akil akielezea jinsi UNDAP 1 ilivyosaidia sekta ya afya Zanzibar.
MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson
akijibu miongozo ya wabunge mapema leo mara baada ya Kipindi cha maswali
na majibu Bungeni Mjini Dodoma.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo akitoa maelezo wakati
wa kipindi cha maswali na majibu kuhusu mikakati ya Serikali kuhakikisha
kuwa wananchi wanapata majisafi na salama katika Halmashauri zote hapa
nchini.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki
akiteta jambo na Waziri wafedha na Mipango Dkt. Philip Mpango leo
Bungeni Mjini Dodoma.
Wanafunzi
wa Chuo Kikuucha Dodoma (UDOM) wakiongozwa na Afisa Habari wa Bunge
Bw. Deonisius Simba (wa kwanza kushoto) katika ziara ya kutembelea
maeneo mbalimbali ya Bunge kwania ya kujifunza shughulizi na zotekelezwa
na Bunge.
Walimu
na wanafunzi washule ya Marangu Hills Academy iliyopo Moshi Mkoani
Kilimanjaro wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati waziara ya kujifunza
jinsi Bunge linavyotekeleza majukumu yake.
NHC YAKUTANA NA WADAU WA SEKTA YA UJENZI KUPITIA MRADI WA ECO RESIDENCE KINONDONI HANANASIFU JIJINI DAR ES SALAAM
Mkurugenzi
wa Ubunifu wa Shirika la Nyumkba la Taifa la Tanzania (NHC), Issack
Peter akitoa mada kuhusu utendaji wa Shirika hilo jijini Dar es Salaam
wakati wa mkutano wa kujifunza utekelezaji mradi wa ECO Residence
uliojengwa na NHC Kinondoni Hananasifu na kujadili mapendekezo ya mradi
huo.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG.
Prof
Ninatubu Lema ,kutoka Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET)
akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa kujifunza utekelezaji wa mradi
ECO Residence na kujadili mapendekezo ya mradi huo.
Wadau
mbalimbali wa sekta ya ujenzi wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa
mkutano wa kujifunza utekelezaji mradi wa ECO Residence na kujadili
mapendekezo ya mradi huo.
Wafanyakazi
wa Shirika la Nyumkba la Taifa la Tanzania (NHC) wakimsikiliza
Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika hilo, Issack Peter wakati akitoa
ufafanuzi kuhusiana na malengo ya uendelezaji wa mradi huo.
BENKI KUU TANZANIA TAWI LA MBEYA (BOT) YAFUTURISHA KATIKA KUSHEREKEA MIAKA 50 YA KUANZISHWA KWA BENKI HIYO
Wageni waalikwa ,viongozi wa serikali na viongozi wa dini mbalimbali mkoani Mbeya wakipita kupata futari kwenye ukumbi wa benki kuu Tanzania( BOT) tawi la Mbeya . |
Mkurugenzi wa benki kuu Tanzania( BOT) tawi la mbeya Jovenant Rushaka akiongoza kupata futari. |
Wafanyakazi benki kuu Tanzania tawi la Mbeya wakipata futari |
wadau wakipata futari. |
Bunge limepitisha muswada wa sheriia ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Mafisadi
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju.
—————————————————-
Na: Lilian lundo – MAELEZO – Dodoma
Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha sheria ya
marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka 2016 ikiwemo kuanzishwa kwa
Mahakama ya Mafisadi.
Muswada
huo umewasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju
ambao ulikuwa na marekebisho ya sheria tano ambazo ni sheria ya mamlaka
za Mahakama ya Rufaa, sheria ya Makosa ya Uhujumi Uchumi, sheria ya
usimamiaji haki na matumizi ya sheria, sheria ya mahakama za mahakimu
pamoja na sheria ya rufaa za kodi.
“Ili
kutekeleza ahadi ya Serikali ya kuanzishwa Mahakama Maalum kwa ajili ya
kushughulikia makosa ya rushwa (ufisadi) na uhujumu uchumi, imeonekana
kuwa kuna umuhimu wa kurekebisha sheria hii kwa kuanzishwa Divisheni
Maalum ya Mahakama Kuu ambayo itakuwa na Majaji pamoja na watumishi
wengine ambao wanahusika moja kwa moja na kesi za rushwa na uhujumu
uchumi tu,” alifafanua Mhe. Masaju.
Mwanasheria
Mkuu aliendelea kwa kusema kuwa, makosa yatakayofunguliwa katika
mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ni yale ambayo
thamani yake haipungui shilingi bilioni moja, lengo la kuweka ukomo huo
kwa baadhi ya makosa ni kuiwezesha Divisheni hiyo kusikiliza makosa
makubwa ya rushwa na uhujumu uchumi na kuacha makosa madogo yasiyofikia
thamani hiyo kuendelea kusikilizwa mahakama za wilaya, hakimu mkazi au
mahakama kuu.
Aidha,
marekebisho mengine yanayopendekeza katika sheria hiyo ni pamoja na
kuboresha masharti ya kutoa dhamana pale kosa linapohusisha fedha au
mali ambayo thamani yake inazidi shilingi milioni kumi ambapo sheria ya
sasa inaeleza kuwa masharti ya dhamana kwa kosa kama hilo ni kutoa
fedha tasilimu (cash deposit) inayolingana na nusu ya thamani ya mali ya
kosa husika na thamani ya nusu inayobaki itolewe kwa njia ya bond.
Muswada
unapendekeza kwamba masharti yaboreshwe ili pale mshtakiwa anapokuwa
hana fedha inayotakiwa mahakamani basi aruhusiwe kutoa mali hiyo na kama
mali hiyo haihamishiki basi hati au ushahidi unaothibitisha umiliki wa
mali hiyo utolewe Mahakamani.
Marekebisho
mengine ni pamoja na adhabu kwa makosa ya rushwa na uhujumu uchumi iwe
ni kifungo gerezani kisichopungua miaka 20 na kisichozidi miaka 30 au
vyote kwa pamoja.
Rais Dkt. Shein AFANYA uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar .
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
———————————
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed
Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu
Mkuu Kiongozi, katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma
na Utawala Bora Nd. Bakari Khamis Muhidin ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa
Uendeshaji na Utumishi.
Mkurugenzi
wa Idara ya Mipango ya Raslimaliwatu ni ndugu Khamis Haji Juma na Ofisa
Mdhamini wa Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Pemba Nugu Masoud Ali Mohamed.
Katika
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za
Serikali Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti ni Ndugu Daima
Mohammed Mkalimoto.
Wizara
ya Fedha na Mipango alieteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uendeshaji na
Utumishi ni Ndugu Ali Bakari Ishaka, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa
Barabara ni Ndugu Mwalim Ali Mwalim na Ofisa Mdhamini wa Wizara hiyo
Pemba ni Ndugu Ibrahim Saleh Juma.
Wizara
ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Kamishana wa
Kazi ni Ndugu Fatma Iddi Ali, Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi wa wazee
Ndugu Wahida Maabad Mohamed na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya
Vijana Ndugu Mwanaidi Mohamed Ali.
Mkurugenzi
wa Idara ya Maendeleo ya Wanawake na Watoto Ndugu Nasima Haji Choum na
Ofisa Mdhamini, Wizara ya Kazi Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na
Watoto Pemba Ndugu Khadija Khamis Rajab.
Dkt.
Fadhil Mohamed Abdullah anakuwa Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya
katika Wizara ya Afya na Mkurugenzi wa Huduma za Hospitali ni Dkt.
Mohammed Dahoma.
Wizara
ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Naibu Katibu Mkuu (Mifugo na
Uvuvi) ni Dkt. Islam Seif Salum. Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti
ni Ndugu Sheha Idrissa Hamad na Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi
Ndugu Noah Saleh Said.
Mkurugenzi
wa Idara ya Kilimo ni Ndugu Mohamed Khamis Rashid, Mkurugenzi wa Idara
ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka Ndugu Yussuf Haji Kombo wakati
Dkt. Bakari Saad Assed anakuwa Mkurugenzi wa Chuo cha Kilimo, Kizimbani.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, Kizimbani ni Dkt. Suleiman Shehe
Mohammed, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Ndugu Mussa Aboud
Jumbe, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mifugo Dkt. Yussuf Haji Khamis na
Ofisa Mdhamini, Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Pemba ni
Ndugu Sihaba Haji Vuai.
Katika
Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Ndugu Hassan Abdalla
Mitawi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu (Habari), Mkurugenzi wa
Mipango, Sera na Utafiti Ndugu Mahmoud Omar Hamad.
Ndugu
Imane Duwe ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji
Zanzibar (ZBC) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa ZBC ni Nassra Mohammed Juma.
Katibu
Mtendaji wa Tume ya Utangazaji ni Ndugu Rafii Haji Makame, Mhariri
Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali Ndugu Yussuf Khamis Yussuf,
Mkurugenzi wa Habari (Maelezo) Ndugu Hassan Vuai.
Mkuu
wa Chuo cha Uandishi wa Habari ni Chande Omar Omar na Ofisa Mdhamini,
Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Pemba Ndugu Khatib Juma
Mjaja.
Wizara
ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Mkurugenzi wa Uendeshaji na
Utumishi ni Ndugu Bimkubwa Abdi Nassib. Mkurugenzi wa Mipango, Sera na
Utafiti Ndugu Khatib Mohamed Khatib na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Usafiri Baharini ni Ndugu Abdalla Hussein Kombo.
Kwa
mujibu wa Taarifa hiyo, Mkurugenzi wa Baraza la Mitihani katika Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Amali ni Ndugu Zubeir Juma Khamis.
Ofisa
Mdhamini Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Pemba ni Ndugu
Juma Bakari Alawi na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Biashara la
Taifa Zanzibar (ZSTC) ni Dkt. Said Seif Mzee.
WAZIRI MWIGULU AFUNGA MAFUNZO YA AWALI YA JESHI LA POLISI NA UHAMIAJI NAMBA 1/2015/2016, CCP MJINI MOSHI
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimkabidhi zawadi mhitimu
Irene Joji (kushoto) kwa kufanya vizuri katika masomo yake wakati wa
mafunzo ya awali ya Polisi na Uhamiaji yaliyofanyika katika Chuo Cha
Polisi (CCP) mjini Moshi. Jumla ya wahitimu 3,904 walimaliza mafunzo
hayo ambayo yamefungwa rasmi na Waziri Nchemba mjini humo leo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akikagua gadi ya wahitimu wa
Jeshi la Polisi na Uhamiaji kabla ya kuyafunga mafunzo ya wahitimu hao
wa mafunzo ya awali yaliyofanyika katika Chuo Cha Polisi (CCP) mjini
Moshi. Jumla ya wahitimu 3,904 walimaliza mafunzo.
Wahitimu
wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi na Uhamiaji wakimuonyesha Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (hayupo pichani) jinsi miili
yao ilivyokuwa imara kwa pikipiki kupita juu ya matumbo yao. Jumla ya
wahitimu 3,904 walimaliza mafunzo hayo ambayo yamefungwa rasmi na Waziri
Nchemba
Kikosi
cha gwaride la heshima kikitoa heshima mbele ya mgeni rasmi Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto jukwaa kuu) wakati wa
sherehe yao ya kumaliza mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi na Uhamiaji,
Chuo cha Polisi (CCP) mjini Moshi. Jumla ya wahitimu 3,904 walimaliza
mafunzo
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akisalimiana na
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki wakati Waziri
huyo alipokuwa anawasili katika viwanja vya Chuo Cha Polisi (CCP), mjini
Moshi kwa ajili ya kufunga mafunzo ya awali ya Polisi na Uhamiaji,
kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli na watatu
kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadick.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA BALOZI WA NORWAY, FINLAND NA MJUMBE MAALUM KUTOKA OFISI YA WAZIRI MKUU WA MALAYSIA, IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Balozi wa Norway hapa nchini Hanne-Marie Kaarstand Ikulu jijini Dar
es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Balozi wa Norway hapa nchini Hanne-Marie Kaarstand mara baada ya
kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na balozi wa Norway hapa nchini Hanne-Marie
Kaarstand watatu kutoka kushoto mara baada ya kumaliza mazungumzo yao
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma
barua ya pongezi iliyowasilishwa kwake na Waziri kutoka Ofisi ya Waziri
Mkuu wa Malaysia Dato Sri Idris Jala ambaye ni Mjumbe Maalum wa Waziri
Mkuu wa Malaysia.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Waziri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia Dato Sri Idris Jala
ambaye ni Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Malaysia mara baada ya
kumkabidhi barua hiyo ya pongezi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Waziri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia Dato Sri Idris Jala
ambaye ni Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Malaysia mara baada ya
kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Balozi wa Finland hapa nchini Pekka Hukka aliyefika
Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Balozi wa Finland hapa nchini Pekka Hukka mara baada ya kumkabidhi
Kitabu Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Balozi wa Finland hapa nchini Pekka Hukka mara baada ya kumaliza
mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment