Pages

Saturday, June 4, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI, AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KIONGOZI WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA LUO ZHIJUN IKULU

ib1

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Gerson John Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ikulu jijini Dar es Salaam.
ib2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi  Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gerson John Mdemu mara baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
ib3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gerson John Mdemu mara baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
ib4 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gerson John Mdemu wa pili kutoka kushoto. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga mara baada ya tukio la uapisho kukamilika.
ib5 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Kiongozi  wa Chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun  kutoka jimbo la Jiangsu nchini China.
ib6 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Kiongozi  wa Chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun  kutoka jimbo la Jiangsu nchini China, ikulu jijini Dar es Salaam.
ib7 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini lu youqing aliyeambatana na Kiongozi huyo wa chama cha Kikomunisti cha China, Ikulu jijini Dar es Salaam.
ib8 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda Ikulu jijini Dar es Salaam.
ib9 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kiongozi  wa Chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun  kutoka jimbo la Jiangsu nchini China mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
ib10 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa kiongozi huyo wa chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun  pamoja na Balozi wa China hapa nchini lu youqing mara baada ya kumaliza Mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi pamoja na Mkuu wa mkoa wa dar es Salaam Paul Makonda. PICHA NA IKULU

Serikali imewataka wanamichezo kujiepusha na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini au matumizi ya dawa

index 
Na Anna Nkinda – Dodoma
 Serikali imewataka wanamichezo kujiepusha na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini au matumizi ya dawa zisiruhusiwa kwa wanamichezo kwa kufanya hivyo wanaweza kupata madhara ya kiafya na  kufungiwa kushiriki katika mashindano ya kitaifa na kimataifa.
Mwito huo umetolewa leo na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakati akifunga mashindano ya michezo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Dodoma yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri uliopo mkoani humo.
Mashindano hayo yaliyojumusha wanafunzi kutoa vyuo vikuu vya Dodoma, Mipango, St. John na Chuo cha Biashara (CBE) yaliandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Pensheni wa PSPF .
Mhe. Wambura alisema kwa kipindi cha mwaka 2015/16 wanamichezo 14 walichukuliwa vipimo vyao na kupelekwa katika maabara za Kimataifa na wote kukutwa salama na hivyo kuwapongeza  wanamichezo hao ambao wameweza kujilinda kwa kutotumia dawa hizo.
Alisema, “Viongozi wote wa Vyama vya Michezo, waalimu na madaktari wa wanamichezo tuungane  kwa pamoja kupiga vita matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni.  Msisite kuchukua hatua kali pale inapothibitika bila shaka yeyote kuwa mwanamichezo ametumia dawa za kuongeza nguvu mwilini”.
Mhe. Naibu Waziri pia aliwasisitiza wanafunzi wa vyuo vyote nchini kushiriki katika michezo na kusoma kwa bidii ili waweze kujikwamua kiuchumi na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa.
“Vijana wakitumia muda wao wa ziada kushiriki katika Michezo watajiepusha na mazingira hatarishi  yatakayowapelekea kuwa wazurulaji, kupata maambukizi ya VVU, kutumia dawa za kulevya na kushiriki katika vitendo vya uhalifu”, alisisitiza Mhe. Wambura.
Aidha Mhe. Naibu Waziri huyo aliwakumbusha Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa PSPF waendelee kudhamini michezo kama hiyo ili kuweza kuhamasisha vijana kushiriki katika michezo kwani Michezo ni ajira, afya na inaimarisha umoja.

Dk. Shein azipamba timu za UMISSETA

UMI1 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Omar Hassan (King) akizungumza na wanamichezo watakaoshiriki mashindao ya UMISETA wa Kanda ya Unguja na Pemba katika Uwanja wa Amani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar wakati alipowakabidhi vifaa vya michezo  timu  zitakazoshiriki mashindano hayo Mjini  Mwanza kuanzia tarehe 13 mwezi huu.
UMI2 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Omar King  kwa niaba ya Rais wa Zanzibar akimkabidhi  vifaa vya michezo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Elimu Khadija Bakari Juma kwa ajili ya wanafunzi watakaoshiriki mashindano ya UMISETA kuanzia tarehe 13 mwezi huu Mkoani Mwanza. Picha na Makame Mshenga /Maelezo Zanzibar.
………………………………………………………………………………………
Na Kijakazi Abdalla-Maelezo
WANAMICHEZO wamekumbushwa kuzingatia nidhamu na uvumilivu wanapokuwa viwanjani.
Wito huo umetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu za skuli za Zanzibar  zitakazoshiriki mashindano ya UMISSETA inayotarajiwa kufanyika jijini Mwanza baadae mwezi huu.
Akiwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Omar Hassan ‘King’ katika uwanja wa Amaan leo, Dk. Shein amesema mambo hayo ndio msingi wa mafanikio kwa wanamichezo wakiwa kwenye mashindano au nje ya viwanja.
Aliwataka wanamichezo hao Mwanza, kushirikiana na kuunganisha nguvu wakiwa jijini Mwanza ili waweze kurudi na ushindi utakaoinua jina la Zanzibar katika medani ya michezo nchini Tanzania.
Hata hivyo, Mhe. Rais hakuacha kueleza jinsi anavyosikitishwa na kudorora kwa michezo humu visiwani, ambako alisema kunasababishwa na utitiri wa timu nyingi.
“Jambo hili la kuwepo utitiri wa timu ndilo linalodumaza michezo hapa Zanzibar na kuifanya baadhi yao isipewe kipaumbele,” alisema.
Lakini amewasisitiza wanamichezo hao kuelewa kwamba wana wajibu wa kushindana kadiri ya uwezo wao kwani serikali inajitahidi kuwanjengea mazingira mazuri kwa kuwa inatarajia kupata ushindi hasa katika michezo inayopendwa na mashabiki wengi ikiwemo mpira wa miguu.
Mapema, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Khadija Bakari Juma,  akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo, alitoa shukurani zake kwa Rais wa Zanzibar kutokana na msaada huo wa vifaa.
Alieleza matumaini yake kwamba vifaa hivyo vitawapa hamasa zaidi washiriki wa mashindano hayo ili wapate ushindi na kuweza kutembea kifua mbele.
Vifaa vilivyotolewa ni vya mpira wa miguu,  mpira wa wavu (volleyball) na mikono (handball), riadha pamoja na mpira wa meza (table tennis).
Michuano ya UMISSETA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi jijini Mwanza Juni 13 na kufikia tamati Juni 25, mwaka huu.
Katika mashindano hayo, Zanzibar  itawakiliishwa na timu mbili ambazo ni kanda ya Unguja na ile ya Pemba.

MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI AZINDUA MAONYESHO YA MRADI WA MJI MPYA WA ZANZIBAR UJULIKANAO KWA JINA LA NG’AMBO TUITAKAYO’

SAD1 
Katibu Mtendaji Kamisheni ya Ardhi Zanzibar Ahmed Abdulrahman Rashid akitoa maelezo juu ya Mpango Mkuu wa matumizi ya Ardhi wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Mradi wa Mji mpya wa Zanzibar uliofanyika Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge Mjini Zanzibar.
SAD2 
Mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Tanzania Eugen Gies akizungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho ya Mradi wa Ngambo tuitakayo katika viwanja vya Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi Mjini Zanzibar.
SAD3Mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Tanzania Eugen Gies akizungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho ya Mradi wa Ngambo tuitakayo katika viwanja vya Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi Mjini Zanzibar.
SAD4 
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud akitoa maelezo namna Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilivyojiandaa katika kuwapatia wananchi nyumba bora za kuishi wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Ngambo Tuitakayo.
SAD5Mkurugenzi wa mipango Miji na Vijiji Dkt. Mouhammed Juma akimunyesha Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud namna ya Mji mpya utakavyokuwa mara baada ya kukamilika kwake katika sherehe za uzinduzi zilizofanyika viwanja vya Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi Mjini Zanzibar.
SAD6 
Watoto wakiangalia na kufurahia mji mpya wa Zanzibar utakavyokuwa kupitia Mradi wa Ngambo tuitakayo wakati wa uzinduzi wa maonyesho katika viwanja vya Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi. Picha na Makame Mshenga /Maelezo Zanzibar.

RAIS DK SHEIN KATIKA MKUTANO WA VIONGOZI KASKAZINI A UNGUJA LEO

ZA1 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni leo alipofika katika mkutano wa Mabalozi,Wenyeviti wa Matawi,Makatibu na Maskani za CCM wa Wilaya ya Kaskazini “A” kwa ajili ya kuwashukuru na kuwapongeza  kwa ushindi uliopatikana katika Uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 04/06/2016.
ZA2Wanachama Viongozi wa Wilaya ya Dimani CCM wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza katika mkutano wa  Mabalozi,Wenyeviti wa Matawi,Makatibu na Maskani za CCM wa Wilaya ya Kaskazini “A” uliofanyika leo katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni  kwa ajili ya kuwashukuru na kuwapongeza  kwa ushindi uliopatikana katika Uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 04/06/2016.
ZA3Risala ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya kaskazini “A”Unguja ikiomwa na Yussuf Shaaban Shaibu wakati wa mkutano wa Viongozi wa wilaya hiyo wakiwemo Mabalozi,Wenyeviti wa Matawi,Maskani na Makatibu,uliofanyika leo katika Ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,ambapo aliwashukuru na kuwapongeza kwa ushindi wa uchaguzi Mkuu wa marudio ulifanyika mwezi machi mwaka huu. [Picha na Ikulu.] 04/06/2016.
ZA4Mwenyekiti wa Wilaya ya Kaskazini “A” CCM Ali Makame Khamis alipokuwa akimakaribisha Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo wakati wa mkutano wa  Mabalozi,Wenyeviti wa Matawi,Makatibu na Maskani za CCM wa Wilaya ya Kaskazini “A” uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,leo katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni  kwa ajili ya kuwashukuru na kuwapongeza  kwa ushindi uliopatikana katika Uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 04/06/2016.
ZA6Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na Viongozi wa CCM wakiwemo Mabalozi,Wenyeviti wa Matawi,Makatibu na Maskani za CCM wa Wilaya ya Kaskazini “A” uliofanyika leo katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni kwa ajili ya kuwashukuru na kuwapongeza  kwa ushindi uliopatikana katika Uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi machi mwaka huu, [Picha na Ikulu.] 04/06/2016.

WAWEKEZAJI KUTOKA CHINA AWAALIKA NCHINI

IKULU TENA

RAIS DKT MAGUFULI AMUAPISHA NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

IMG-20160604-WA0018

VISIMA VINGI DAR VIMECHIMBWA BILA KUFUATA UTARATIBU.

index 
Na Fatma Salum- MAELEZO, Dodoma.
……………………………………
Serikali imesema  kuwa visima vingi Jijini Dar es Salaam vimechimbwa bila ya kufuata kanuni na taratibu za uchimbaji hivyo maji yake si salama kwa matumizi ya binadamu.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge aliyasema hayo  wakati  akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake Bungeni mjini Dodoma.
 Mhe. Lwenge alibainisha kuwa katika kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu uliotokea mwezi Agosti 2015 Jijini Dar es Salaam na kuenea nchini, Serikali ilifanya uchunguzi wa sampuli za maji ya visima 108 vya jijini humo na matokeo  ya uchunguzi huo  yalionesha kuwa visima 66 maji yake si salama.
“Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na wadau wengine ilifanya ukaguzi na kupima uwepo wa vimelea vya vijidudu vya ugonjwa huo katika visima vya maji vinavyotumika jijini Dar es Salaam na sampuli za maji ya visima 108 zilichukuliwa, kati ya hivyo visima 20 vifupi na visima 46 virefu maji yake yaligundulika kuwa si salama. Kwa ujumla visima vingi vilivyopo kwenye maeneo ya watu vimechimbwa bila ya kufuata kanuni na taratibu.” Alisema Mhe. Lwenge.
Aidha, Waziri Lwenge alisema kuwa Serikali pia ilifanya ukaguzi wa ubora wa maji kwenye vyanzo vya maji katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Mara, Manyara, Kagera, Kigoma, Morogoro na Dodoma ambapo vyanzo vya maji vipatavyo 600 vilikaguliwa na kubaini kuwa  maji yaliyo salama ni chini ya asilimia 40.
Mhe. Lwenge alieleza kuwa Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) imekamilisha uandaaji wa miongozo ya utekelezaji wa Mpango wa Usalama wa Maji (Water Safety Plan) kwa Vyombo vya Watumiaji wa Maji na Mamlaka za Maji.
“Miongozo hiyo inakusudia kuboresha huduma za upatikanaji wa maji safi na salama kwa Mamlaka za Maji na Vyombo vya Watumiaji wa Maji Vijijini (COWSOs) kuanzia kwenye chanzo cha maji hadi kwa mtumiaji.” Alifafanua Mhe. Lwenge.
Kutekelezwa kwa mpango huo kutaboresha usimamizi wa usalama wa maji katika vyombo hivyo na kuwaepusha wananchi kutumia maji yasiyo salama pamoja na kupunguza upotevu wa maji katika mifumo ya kusambaza maji kote nchini.

SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI MKUU WA WILAYA AHIMIZA VYANZO VYA MAJI VILINDWE

Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Wilson Nkambaku aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Arusha akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira duniani ambayo kimkoa yamefanyika leo katika Shule ya Msingi Kiranyi.Ameagiza wananchi wote walijenga kwenye eneo lilitengwa kwaajili ya chanzo cha maji wabomoe wenyewe.                

Mtendaji Mkuu wa Mamkala ya Mji Mdogo wa Ngaramtoni,Sophia Shoko akizungumza jambo katika maadhimisho hayo.

Diwani wa Kata ya Kiranyi ,halmashauri ya wilaya Arusha DC,John Seneu alikiwataka wananchi kutii sheria ili kulinda vyanzo vya maji.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Wilson Nkambaku(katikati) aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Arusha akifurahia jambo na Katibu Tawala mkoa(RAS),Richard Kwitega(kulia) kushoto Katibu Tawala Msaidizi huduma za Afya,Hargeney Chitukulo.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Serikali ya mchepuo wa Kiingereza ya Arusha School wakiimba Shairi lao lenye kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kupanda miti.

Baadhi ya viongozi kutoka halmashauri ya Arusha DC wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa wilaya.

Baadhi ya viongozi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha wadau wa taasisi binafsi na wananchi kwa pamoja wameshiriki kikamilifu Siku ya mazingira duniani.
SEMAJI WA CCM, OLE SENDEKA AFANYA ZIARA KUKAGUA NA KUIMARISHA UHAI WA CHAMA WILAYANI KILWA MKOANI LINDI LEO
Kijana wa Umoja wa Vijana wa CCM, Kibibi Duka akimvalisha skafu Msemaji wa CCM, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Christopher Ole Sendeka, alipowasili Ofisi ya CCM y Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama wilayani humo leo.
Kijana wa Umoja wa Vijana wa CCM, Ali Njonzi akitokwa na jasho jembemba wakati wa Vijana wa umoja huo walipokuwa wakimpokea msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka katika Ofisi ya CCM wilaya ya Kilwa leo akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama
Msemaji wa CCM, Cheristopher Ole Sendeka akimsalimia Katibu wa CCM Wilaya ya Liwale Raphael Maumba, alipokuwa akisalimia viongozi mbalimbali wa CCM mkoa wa Lindi, baada ya kuwasili ofisi ya CCM wilaya ya Kilwa leo akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa akimuongoza Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka kuingia Ofisi ya CCM wilaya ya Kilwa, alipowasili akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama leo
Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Ofisi ya CCM wilaya ya Kilwa, akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarsiha uhai wa Chama wilayani humo leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa
Baadhi ya wageni waliofuatana na semaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka wakiwa ukumbi wa Ofisi ya CCM, wakati Sendeka alipokuwa akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Kilwa mkoani Lindi leo.
Katibu wa CCM mkoa wa Lindi Adelina Geffi akisoma taarifa ya Chama, Msemaji wa CCM alipowasili Ofisi ya CCM wilaya ya Kilwa mkoani humo leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa huo wa Lindi Ali Mtopa.
Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka akizungumza na viongozi wa CCM, alipowasili katika Ofisi ya CCM wilaya ya Kilwa mkoani Lindi leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa.
Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akiselebuka na Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM waliofika kumpokea katika Ofisi ya CCm wilaya ya Kilwa mkoani Lindi leo kukagua na kuimarisha uhai wa Chama
Wazee wa Kilwa mkoani Lindi wakimpokea kwa shamrashamra Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka, alipowasili katika ukumbi wa Hall Fair, kuzungumza nao leo akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama wilayani Kilwa mkoani Lindi
Wazee wa Kilwa mkoani Lindi wakimpokea kwa shamrashamra Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka, alipowasili katika ukumbi wa Hall Fair, kuzungumza nao leo akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama wilayani Kilwa mkoani Lindi
Mwenyekiti wa Wazee wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, Mohammed Msinjepi akimkaribisha Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka (katikati), kuzungumza na wazee wa wilaya ya Kilwa, katika ukumbi wa Hall Fair leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa.
Hakim Mstaafu Mzee Zuberi Liengama akisoma risala, kabla ya Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka kuzungumza na wazee wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi leo
Hakim Mstaafu Mzee Zuberi Liengama akimkabidhi risala baada ya kuisoma, kabla ya Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka kuzungumza na wazee wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi leo
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa akimtambulisha kwa wazee wa wilaya ya Kilwa, Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka, leo katika Ukumbi wa Hall Fair
Msemaji wa CCM, Cheristopher Ole Sendeka akizungumza na Wazee wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi alipokuwatana nao katika ukumbi wa Hall Fair, wilayani humo leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

WAZIRI JANUARI MAKAMBA APANDA MITI UFUKWE WA BAHARI YA HINDI

mam1 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akitia saini kitabu cha Wageni alipotembelea Kata ya Mbweni iliyopo Manispaa ya Kinondoni kwa ajili ya shughuli za upandaji mikoko katika eneo hilo.
mam2 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akipanda mti aina ya mkoko katika fukwe za bahari ya hindi katika eneo la Mbweni jijini Dar es Salaam. Upandaji huo wa mikoko ni katika kuadhimisha wiki ya mazingira duniani, ambayo kilele chake ni kesho
mam3 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba  akishirikiana kupanda miti ya mikoko na wakazi wa kata ya  Mbweni jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha siku ya mazingira hapo tarehe 5 juni.
mam4 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akifurahia jambo na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbweni ambao walijumuika pamoja naye kupanda mikoko katika fukwe za Mbweni jijini Dar es salaam.
mam5 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza kupanda mikoko katika fukwe za bahari ya Hindi katika kata ya Mbweni.
……………………………………………………………………………………………………………
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba Ametoa wito kwa Wananchi  wa Kata ya Mbweni kutunza mazingira na kutoa kipaumbele kwa mazingira. Aliyasema hayo wakati wa zoez la upandaji mikoko lilifanyika katika fukwe za bahari ya Hindi zilizoko Mbweni.
Akiongoza Wananchi wa Kata hiyo kupanda miche 5,000 ya mikoko , Waziri Mkamba alisititiza pia Wanafunzi wa shule waliopo katika eneo hilo kupenda mazingira yao na kuyatunza ili yawafae baadaye.
Wakisoma Risala yao , Wanawake wa Mbweni walimuomba Waziri awasaidie kuwapatia vitendea kazi  kwa ajili ya kuhudumia mikoko pamoja na kumuomba awasaide kuwatatulia changamoto wanazokutana nazo. Ikiwamo ya maafisa wa TRA kukata hovyo mikoko wanapokua wanafanya doria katika fukwe zaMbweni.
Mwisho Waziri aliwahukuru Wananchi wa Mbweni waliojitypkeza kujumuika naye katika zoezi hilo la upandaji mikoko. Shuhuli za upandaji mikoko ni kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira ambayo kilele chake ni tarehe 5 juni kila mwaka.

POLISI KUZIDI KUIMARISHA ULINZI KWA KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA DINI, MADIWANI

mad1
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP)  Charles Mkumbo akifungua kikao cha kujadili amani katika mkoa wa Arusha ambacho  kilifanyika katika bwalo la Maofisa wa Polisi Arusha (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha) mad2 
Meya wa halmashauri ya Jiji la Arusha Calist Lazaro akitoa mchango wake wakati akichangia mada ya uimarishaji wa amani katika Mkoa wa Arusha (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha) mad3 
Sheikh wa wilaya ya Arusha Abraham Salum akisisitiza jambo wakati  akitoa mchango wake juu ya uimarishaji wa amani katika mkoa wa Arusha  ( Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
index 
Padre Festus Mangwangi wa Parokia ya Mtakatifu Theresia akielezea umuhimu wa amani ndani ya Jamii yetu wakati akichangia mada katika kikao kilichofanyika jana ukumbi wa bwalo la Maofisa wa Polisi Arusha ( Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha) mad4 
Baadhi ya viongozi wa dini, madiwani na askari Polisi waliohudhuria kikao cha kujadili amani ya Mkoa wa Arusha kilichofanyika jana katika ukumbi wa bwalo la Maofisa wa Polisi Arusha (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
……………………………………………………………………………………………………………………………..
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Jeshi la Polisi Mkoani hapa limefanya kikao ambacho kiliwashirikisha viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali pamoja na Madiwani wa halmashauri ya jiji la Arusha kwa nia ya kuimarisha amani na usalama.
Kikao hicho kilichofanyika jana katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi kiliwajumuisha watu zaidi ya mia mbili; Maofisa wa Mkoa wa Jeshi hilo, viongozi wa dini wa madhehebu yote, Madiwani, Wakaguzi wa Polisi wa Tarafa na Polisi wa kata.
Akizungumza katika kikao hicho Kamanda wa Polisi mkoani hapa Naibu Kamishna Charles Mkumbo ambaye alikuwa mwenyeji wa kikao hicho alifungua kwa kusema kwamba Jeshi la Polisi pekee haliwezi kukabiliana na uhalifu bali kwa kushirikiana na viongozi wa dini na wa kisiasa wataweza kuushinda uhalifu.
Alisema makundi hayo ni wadau wakubwa wa kuimarisha amani kutokana na ushawishi walionao kwa waumini wao na wananchi wanawaongoza huku Jeshi hilo likiahidi kuwa bega kwa bega hasa katika upokeaji wa taarifa za uhalifu na kuzifanyia kazi kwa haraka. 
Kamanda Mkumbo alisema kwamba bila amani hakutakuwa na shughuli zozote za maendeleo ikiwemo uwezekaji na hata waumini hawataweza kwenda Misikitini na Makanisani kutokana na hofu ya kiusalama.
“Sote tunajukumu la kufichua uhalifu na wahalifu kupitia taarifa za waumini wetu hasa kwa viongozi wetu wa dini kuendelea kuhubiri na kutoa mawaidha katika Makanisa na Misikiti huku Madiwani waendelee kufanya hivyo katika maeneo yao ya kiutawala hasa wanapokutana na wananchi kwenye mikutano mbalimbali”. Alisisitiza Kamanda Mkumbo.
Kwa upande wake Meya wa jiji la Arusha Calist Lazaro alisema kwamba wananchi pamoja na viongozi wote wasiwe na hofu kwa kuwa Jiji la Arusha linaongozwa na CHADEMA kwani wao kama viongozi wa Siasa wanahitaji amani na wanalitambua jukumu hilo na wataendelea kutoa ushirikiano na Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vyote vya usalama huku akiwataka baadhi ya askari wa Jeshi hilo kufuata haki katika utendaji wa kazi zao. 
Sheikh wa wilaya ya Arusha Abraham Salum alisema kwamba kikao hicho kimekuja wakati muafaka kwani mikoa ya Tanga na Mwanza kumejitokeza vitendo vya uvunjifu wa amani matukio ambayo hapo awali hayakuwepo katika nchi yetu na kulishauri jeshi hilo kuongeza weredi katika kupambana na uhalifu huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo.
Akichangia mjadala huo Padre Festus Mangwangi wa Parokia ya Mtakatifu Theresia, alisema kwamba wao kama viongozi wa dini wana dhamana kubwa ya kulisaidia Jeshi la Polisi katika kuhubiri amani kupitia waumini wao. Alisema amani iliyopo idumishwe kwani baadhi ya nchi zinavurugu na zinatamani amani iliyopo hapa nchini.
Akihitimisha kikao hicho kamanda Mkumbo aliwashukuru viongozi wote waliohudhuria kwa michango yao yenye tija kwa mustakabali wa uimarishaji wa amani ndani ya mkoa wa Arusha na kusema kwamba ana matumaini makubwa ya kupata ushirikiano toka kwao naye kuahidi kutatua kero zilizowasilishwa na washiriki ambazo zipo ndani ya uwezo wake.

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI DK. JULIANA PALLANGYO AFANYA ZIARA KATIKA KAMPUNI YA PUMA ENERGY

nai1 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati,  Dk. Juliana Pallangyo (kushoto) akiwa ameambatana na  Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali  wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA),Michael Mjinja (kulia) mara alipowasili katika ofisi za Puma  Energy jijini  Dar es Salaam kwa ajili ya kukagua shughuli zake.
nai2 
Meneja  Afya, Usalama na Mazingira  kutoka katika kampuni ya  Puma  Energy Blasio Menchi (kulia) akielezea shughuli za kampuni hiyo mbele ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati,  Dk. Juliana Pallangyo pamoja na ujumbe wake.
nai3 
Kutoka kushoto Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati  Dk. Juliana Pallangyo, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo  ya Petroli Nchini  James Andelile, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali  wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA),Michael Mjinja,na  Kaimu Kamishna wa Petroli ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya   Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Mwanamani Kidaya wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Meneja  Afya, Usalama na Mazingira  kutoka katika kampuni ya  Puma  Energy Blasio Menchi (hayupo pichani) kwenye ofisi za Puma Energy jijini Dar es Salaam.
nai4 
Meneja Uendeshaji  kutoka   Kampuni ya  Puma  Energy Lameck Hiliyai (katikati)  akielekeza  jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati  Dk. Juliana Pallangyo (kushoto) Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo  ya Petroli Nchini  James Andelile (aliyekaa katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali  wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA),Michael Mjinja (kulia) katika kikao hicho kwenye ofisi za Puma Energy jijini Dar es Salaam.
nai5 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati  Dk. Juliana Pallangyo (kushoto) na Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo  ya Petroli Nchini  James Andelile (kulia) wakibadilishana mawazo katika  kikao hicho.
nai6 
Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo  ya Petroli Nchini  James Andelile,(kulia) akielezea  jambo katika kikao hicho. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati  Dk. Juliana Pallangyo
nai7 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dk. Juliana Pallangyo akitoa maelekezo kwa kampuni ya Puma Energy katika kikao hicho

No comments:

Post a Comment