Pages

Tuesday, June 21, 2016

Meneja wa Huduma kwa wateja wa PSPF Bi. Laila Maghimbi

Mamia wajitokeza Usaili wa Maisha Plus Dar es salaam

677A0614
Akitaja vigezo vya kushiriki Maisha Plus, Kaka Bonda, miongoni mwa majaji na waanzilishi wa Maisha Plus alisema, “Tunachukua washiriki wenye umri wa miaka 18 hadi 26, walio na elimu na ambao hawajasoma kabisa, wawe raia kutoka nchi za Afrika Mashariki”
677A0389
677A0646
677A0422
Maisha Plus kwa mwaka huu wa 2016 inatarajia kuchukua washiriki 30 kutoka nchi tano ambazo ni Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda na Tanzania ambapo mshindi atafadhiliwa wazo la biashara lenye thamani ya fedha ya kitanzania Milioni 30. Kauli mbiu ya mashindano haya kwa mwaka huu ni ‘Vijana Ndio Ngazi’.
677A0857
677A0262
677A0763
Usaili unaendelea katika mikoa mingine na nchi nyingine nje ya Tanzania. Vijana wametakiwa kusikiliza matangazo ya ratiba kupitia redio mbalimbali katika nchi shiriki, runinga ya Azam Two, mitandao mbalimbali ya kijamii pamoja na tovuti maalum ya mashindano hayo ya www.maishaplus.tv
677A0946

BENKI YA CRDB YAKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA KAMPENI YA “Shinda na TemboCard”

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa hafala ya kukabidhi zawadi kwa kwa washindi wa Kampeni ya “Shinda na TemboCard” iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akitoa hotuba yake wakati wa hafala ya kukabidhi zawadi kwa kwa washindi wa Kampeni ya “Shinda na TemboCard” iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza wakati wa hafla hiyo. 
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (kushoto), ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa Kampeni ya “Shinda na TemboCard” akiwa katikapicha ya pamoja na mshindi aliyejishindia simu aina ya iphone 6, Barbara Hassan (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia).
Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay (kushoto), akimkabidhi mfano wa tiketi ya ndege ya kwenda Dubai mshindi wa kwanza wa Kampeni ya “Shinda na TemboCard” kwa upande wa wateja, Ismail Jimroger wakati wa hafla ya utoaji zawadi kwa washindi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB  wakiwa katika hafla hiyo.
 Baadhi ya wakurugenzi na Mameneja wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

Mwakilishi wa Katibu Tawalawa mkoa wa Manyara Bw.Longino Kazimoto (katikati), akifungua kikao cha pamoja kati ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na wanachama wake wa mkoa wa Manyara. Mkutano huo ambao uliandaliwa na PSPF katika utaratibu wake wa kukutana na wanachama wake katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa lengo la kujadiliana namna bora ya kuboresha huduma na bidhaa ambazo PSPF inazitoa kwa wateja ulifanyiki mjini Babati.
p3 
Afisa Mfadhiwi wa PSPF mkoa wa Manyara Bw. Said Ismail, akitoa hotuba wakati wa kikao cha pamoja kati ya PSPF na wanachama wake wa mkoani Manyara kilichofanyika mjini Babati. PSPF inautaratibu wa kukutana na wanachama wake katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa lengo la kujadiliana namna bora ya kuboresha huduma na bidhaa ambazo PSPF inazitoa kwa wateja.Wengine pichani ni Mwakilishi wa Katibu Tawalawa mkoa wa Manyara Bw.Longino Kazimoto (katikati) na na Meneja wa Huduma kwa wateja wa PSPF Bi. Laila Maghimbi
p4
Baadhi ya washiriki wa kikao cha pamoja  wakifuatilia kwa karibu.p5 
Meneja wa Huduma kwa wateja wa PSPF Bi. Laila Maghimbi akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na  wanachama hao wakati wa semina hiyo.

UTEKELEZAJI WA MJI KABAMBE KATIKA JIJI LA ARUSHA KUKAMILIKA AGOSTI MWAKA HUU

index 
Na Mahmoud Ahmad,  Arusha.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mpango Kabambe kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Amulike Mahenge amesema kuwa utekelezaji wa mpango kabambe wa Jiji la Arusha na viunga vyake unatarajia kukamilika Agosti mwaka huu.
Mahenge alisema mpango huo wa rasimu ya mwisho ya mpango kabambe wa Jiji la Arusha umewakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo madiwani ili kuwezesha kupitisha kwenye vikao vya Baraza la Madiwani na hatimaye kupitiwa na Mkurugenzi wa Miji Wizarani kwaajili ya kuanza kujengwa Mji wa kisasa Jijini Arusha na viunga vyake.
Mahenge aliyasema hayo Jana Jijini hapa wakati alipokuwa akizungumza na wadau wa  maendeleo walikutana kwa pamoja kwaajili ya kuchangia mada na kuona jinsi Mji huo wa Arusha utakavyokuwa wa kisasa.
Alisema Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi itapitia mpango huo mara baada ya madiwani kupitisha kwenye vikao vyao vya mabaraza kisha utekelezaji wake utaanza rasmi Agosti mwaka huu kwaajili ya kuhakikisha Arusha inakuwa ya kisasa.
“Mpango huu ni mpango kabambe utakaobadilisha taswira ya Jiji la Arusha na halmashauri zake hivyo ni vyema wadau wa maendeleo wakapitia mpango huu na kujadili kwa kina ili kuona Arusha itakayobadilika kwa kupimwa kisasa ili kuleta madhari mazuri ndani na nje ya nchi”.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega akifungua mkutano huo wa wadau aliwasihi kuhakukisha wanajadili kwa kina jinsi ya kupanga mji pamoja na kutoa mawazo yao pale wanapoona kunamahali pakurekebishwa kabla ya kupelekwa kwenye baraza la madiwani ili kupitishwa kabla ya kuanza kazi rasmi
Alisema eneo lilioandaliwa kwaajili ya Utekelezaji wa mpango huo ni kilomita za mraba 608 ambapo Halmashauri ya Jiji la Arusha  ni kilomita za mraba 272,huku Halmashauri za Arusha Dc na Meru mpango huo utachukua kilomita za mraba 187.
Aliongeza kuwa mpango huo umelenga kuboresha Jiji la Arusha na serikali imetumia zaidi ya Sh, bilioni 8 kwaajili ya kuhakikisha majiji mawili ya Arusha na Mwanza yanapangwa vizuri  kwani ni mojawapo ya miji inayokua kwa kasi.
Awali   Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ilisaini mkataba wa makubaliano (memorandum of Understanding) na  Kampuni ya Subrana International Pte Ltd ya Nchini Singapore kwaajili ya kuendeleza majiji mawili ya Arusha na Mwanza pamoja na viunga vyake.
Makubaliano hayo zilisainiwa mwaka juzi   Jijini Arusha na mkataba huo wa makubaliano unatakiwa ukamilike Julai 2016 huku kazi kubwa ikiwa ni kupanga  Mji wa Arusha kuwa wa kisasa zaidi.
Lengo la makubaliano hayo ni kwaajili ya kuwezesha majiji hayo mawili kuwa ya kisasa pamoja na kusaidia wananchi  kuendesha shughuli zao za kiuchumi bila shida kutokana na miji kupangiliwa kisasa zaidi

China and African countries agreed to strengthen Mass Media Cooperation.

images 
By Zamaradi Kawawa, Maelezo, Beijing, China.
African countries and China have agreed to strengthen Africa – China Media Cooperation to improve media quality through experience sharing of implementation of media policies, capacity building programs for journalists, digitalization and development of new media.
Sharing  Tanzanian experience in digital migration at the Third Forum on China – Africa Media Cooperation in Beijing today, Deputy Minister for Information, Culture, Arts and Sports Mrs Annastazia Wambura said Tanzania is now commemorating one year of migration from analogue to digital terrestrial television (DTT). She said although the process was challenging it was accomplished due to sound policies, regulatory framework and Government Commitment.
She told the forum that as of now, close to two million Tanzanians are enjoying quality television programmes from locally and foreign produced content enriching the people’s choice and diversity.
Mrs Wambura pointed out a digital migration road map, political will, consultation with stakeholders, a communication strategy , public private partnership (PPP) in the area of cost sharing and  consumer consideration in the purchase of affordable services and equipment contributed to the smooth analogue to digital migration in broadcasting ahead of ITU deadline of 17th June, 2015.
She said the achievement was contributed largely by the Public Private Partnership between Star  Communication Network Technology (Star Times ) from China which in May 2009 formed a joint venture company – Star Media (Tanzania)  Limited  with the Tanzania Broadcasting Corporation (TBC), the Country’s public broadcaster.
However,  the Zimbabwe Minister for Media, Information and Broadcasting Mr. Christopher Chindoti Mushohwe said efforts that strengthen African Media to fight against negative  media coverage of African countries and China by Western countries should be applauded.
” The establishment of strong indigenous media in African countries will reduce dependence  of western global media which is negative to African countries and China. Zimbabwe is ready to cooperate with China in fighting western media negative coverage”, he said.
A total of 350 participants including Government Ministers, Vice Chairperson of the African Union Commission, Chief Executive Officer of the AU Broadcasting, Chief Executive Officers  of Radio and Television stations from 45 African Countries and China attended the meeting.
China Deputy Minister responsible for Press, Publication, Radio, Film and Television Mr Tong Gang told the conference that China is ready to support African Countries in strengthening broadcasting digitalization, Training of media personnel,  improvement of Television and Radio program production  and quality of film production.
He said Chinese Government has set aside a total of 10 billion U.S. Dollars for China Africa cooperation in the areas of human resources development, media exchange programs , healthy and food security for three years.
He said  his government would like to promote China Africa media cooperation and a total of 1,000 journalists from African countries would be trained at a newly established media centers in China.
Press Minister from Chad Mr Ali Ali Fei said African countries  are in the transition period from analogy to digital broadcasting hence need China support in the installation of infrastructure for the digitalization process of broadcasting .
” we are in a critical stage of revolution. All African countries have to go through digitalization. New economy is built by digitalization” he said.
Deputy Chairperson of the African Union Mr Erastus Mwencha said African Countries need to safeguard their culture since they are now facing globalization culture that threatens to impose a new era of digital colonization.
He requested Chinese Government to assist African countries in facing the challenges in the areas of cyber security,  technology transfer especially infrastructure and capacity building.
On his part, Professor LI Anshan from Peking University said the media in China and African countries should contribute to the development of their countries by broadcasting and publishing objective information and encourage exchange programs  of training in the areas of information.
A two day forum was jointly organized by State Administration of Press, Publication, Radio, Film and Television of the people’s Republic of China and the African Union of Broadcasting.
The forum is the implementation of the Johannesburg China- Africa cooperation Summit of 2015 action plan (2016-18) to serve the need for development of China- Africa comprehensive strategic and cooperative partnership  in a new era of China- Africa win win cooperation and common development.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO

ut6 
TAREHE 20/06/2016 MAJIRA YA SAA 07:30HRS KATIKA MSITU WA BUHINDI ULIOPO KIJIJI CHA MAJENGO KATA YA IRENZA TARAFA BUCHOSA WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA, MARIAM MATHIAS MIAKA [35] MKAZI WA KIJIJI CHA NYANGALAMILA ALIKUTWA AKIWA AMEKUFA KIFO CHA MASHAKA KATIKA MSITU TAJWA HAPO JUU HUKU UCHUNGUZI WA AWALI UKIONYESHA MWILI WAKE UKIWA NA MIKWARUZO KWENYE BEGA LA KULIA PAMOJA NA SHINGO.
AIDHA INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIONDOKA NYUMBANI KWAKE SIKU YA IJUMAA YA TAREHE 17.06.2016 MAJIRA YA ASUBUHI NA KWENDA KATIKA MSITU TAJWA HAPO JUU KUTAFUTA KUNI NA NDIPO MAUTI YALIPO MKUTA HUKO, HADI TAREHE 20.06.2016 MAJIRA YA SAA 07:30HRS AMBAPO MWILI WAKE ULIWEZA KUOKOTWA KATIKA MSITU HUO.
JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA MUME WA MAREHEMU AITWAYE PONYIWA JEREMIA MIAKA [37], MKAZI WA NYANGALAMILA KWA MAHOJIANO ZAIDI DHIDI YA TUKIO HILO KWANI ALISHINDWA KUTOA TAARIFA POLISI NA KWA MAJIRANI ANAOISHI NAO KWA KIPINDI CHOTE AMBACHO MKEWE HAKUONEKANA NYUMBANI KWAKE HIVYO KUPELEKEA KUTILIWA SHAKA KATIKA TUKIO HILO.
CHANZO CHA KIFO HICHO BADO HAKIJAJULIKANA, JESHI LA POLISI BADO LINAENDELEA NA UCHUNGUZI PAMOJA NA UPELELEZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI AKIWATAKA WAONGEZE USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI WAKATI WOTE PANAPOTOKEA JAMBO AU TATIZO WASISITE KUTAARIFU ILI KUWAZA KUZUI VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA PILI
KWAMBA TAREHE 20.06.2016 MAJIRA YA SAA 13:20HRS NA KUENDELEA KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA WILAYA YA ILEMELA MKOANI MWANZA, ASKARI WALIFANYA DORIA PAMOJA NA MISAKO KATIKA MITAA MBALIMBALI YA WILAYA TAJWA HAPO JUU NA KUFANIKIWA KUWAKATA WATU WA NNE WAKITUHUMIWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA BHANGI PAMOJA NA POMBE AINA YA GONGO KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI
WATUHUMIWA WALIOKAMATWA 1.JANETH MASOLE MIAKA [30], MKAZI WA KISEKE ALIYEKAMATWA AKIWA NA BHANGI MISOKOTO 83, 2. SUZANA DOTTO MIAKA [50], MKAZI WA IGOMBE ALIYEKAMTWA AKIWA NA POMBE YA GONGO LITA 60, 3. MADURU MATHIAS MIAKA [35], MKAZI WA IGOMBE ALIYEKAMATWA AKIWA NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA POMBE YA GONGO NA, 4. BUSHESHE FAIDA MIAKA [20], PIA MKAZI WA IGOMBE ALIYEKAMATWA NA BHANGI MISOKOTO MIWILI KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.
AIDHA WATUHUMIWA WOTE WA NNE WAPO CHINI YA ULINZI WA JESHI LA POLISI HUKU MAHOJIANO DHIDI YA TUHUMA ZA UHALIFU WANAOJIHUSISHA NAO YAKIENDELEA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU TUHUMA ZA UHALIFU ZINAZO WAKABILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANAWATAKA WANANCHI WAENDELEE KUTULIA LAKINI WAKIENDELEA KUTO USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLSI ILI LIWEZE KUFANYA KAZI VIZURI NA KUTOKOMEZA UHALIFU WA AINA ZOTE KATIKA MKOA WA MWANZA.
IMESAINIWA NA:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

TBS YATAKIWA KUSHUGHULIKIA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NCHINI ZISIZO KIDHI VIWANGO

index 
Na Mahmoud Ahmad  Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Filex Ntibenda amelitaka shirika la viwango(TBS) kushughulikia vipasavyo bidhaa  zinazozalishwa hapa nchini zisizo kidhi viwango vinavyotakiwa ili kuondoa bidhaa  zisizo na ubora.
Ameyasema hayo Jana wakati akifungua Mkutano wa 22 wa maonesho ya viwango barani Afrika yaliyoanza jijini Arusha na kushirikisha nchi zaidi ya 15.
Ntibenda alisema kuwa kumekuwepo na tatizo la nchini katika suala la uzalishaji wa bidhaa  hivyo ili kuhakikisha   bidhaa  hafifu hazitengenezwi kwa mashirika hayo kuongeza juhudi katika usimamizi.
“Ili kuandokana na bidhaa  zisizokidhi viwango hapa nchini mnatakiwa  kuwajibika ipasavyo katika kuhakikisha bidhaa  hizo hazizalishwa” Alisema Ntibenda.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa shirika la viwango Tanzania Joseph Masikitiko alieleza kuwa pasipo viwango huwezi kufanya biashara yoyote iyostahili kwa kuwa itakuwa  haijathibitishwa  .
Alisema lengo la Mkutano huo ni kuboresha viwango kuwa katika hali ya ubora zaidi na   kwa kiwango kimoja Afrika.

BENKI YA NBC YANDAA FUTARI KWA WATEJA WAKE WA DAR NA MTWARA

G1 
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya NBC Tanzania, James Kinyanyi (wa pili kushoto), Mkuu wa Huduma Rejereja za Kibenki wa benki hiyo, Musa Jallow (wa pili kulia), pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo wakishiriki mlo wa futari iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
G2 
Mjumbe wa Bodi ya Benki ya NBC, Dk. Kassim Hussein (kushoto), akisalimiana na mmoja wa wateja wao, Ibrahim Shaddad katika hafla ya futari iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wao jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Huduma Rejareja za Kibenki wa benki hiyo, Musa Jallow.
G3 G4
G6 
Baadhi ya wateja wa Benki ya NBC jijini Dar es Salaam na wafanyakazi wa benki hiyo, wakishiriki mlo wa futari iliyoandaliwa na NBC jijini Dar es Salaam.
G5Mkuu wa Kitengo cha Islamic Banking cha Benki ya NBC, Yassir Masoud (kulia) akishikana mikono na Sheikh wa mkoa huo na Naibu Kadhi wa Mtwara,  sheikh Nurdin Mangochi

Wananchi wa Chasimba kuweni wavumilivu mtakula mbivu

indexmm 
Na Jacquiline Mrisho-MAELEZO
———————————–
Baada ya mtafaruku mkubwa kutokea katika Kijiji cha Chasimba kilichopo katika Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam na kuwaacha wakazi wa eneo hilo katika hali ya sintofahamu juu ya maisha yao ya siku zijazo, wakazi wa eneo hilo wamepata ahueni baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Willium Lukuvi kuingilia kati na kutoa suluhu ya mtafaruku huo.
Mgogoro huu baina ya wananchi wa Kijiji cha Chasimba na mwekezaji wa Kiwanda cha Saruji cha Twiga, Bw. Alfonso Rodriguez kilichopo Wazo Hill ambao ulianza takribani miaka 15 iliyopita baada ya Mkurugenzi huyo kugundua kuwa wananchi wamevamia eneo lake na kujenga makazi yao.
Hayo yalitokea baada ya kiwanda hicho kushindwa kuilinda mipaka yake kwa muda mrefu na kusababisha wananchi kujenga maeneo hayo na kukaa kwa muda mrefu sana hali iliyowapelekea kujiona kama wana haki na eneo hilo na kukataa kuhama.
Mkurugenzi Msaidizi Usanifu wa Miji na Uendelezaji Upya Maeneo wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Immaculata Senje alisema kuwa eneo hilo ni mali ya mwekezaji wa Kiwanda hicho.
“Ni ukweli usiofichika kuwa eneo hili la Chasimba ni mali ya mwekezaji na ana hati ya mwaka 1957 aliyopewa na Wizara yetu inayoonyesha ukubwa na mipaka ya eneo lake kwahiyo wananchi ndio wavamizi wa eneo hilo”.anakiri Bi. Senje.
Mgogoro huo ulileta tafrani kubwa baada ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kutoa agizo kuwa wananchi waliojenga katika eneo hilo wahame mara moja na kwenda eneo ambalo wamepangiwa na Wizara ambapo takribani wakazi 30 waligoma kuondoka katika eneo hilo na kuamua kwenda mahakamani kudai haki yao, hatua ambayo haiukupata suluhu ya mgogoro.
Ili kuwasaidia wakazi wa Chasimba, Waziri Lukuvi aliamua kuingilia kati kwa kufanya mazungumzo ya amani na muwekezaji wa kiwanda hicho ambapo alimuomba Mkurugenzi huyo kuwaachia wakazi wa Chasimba sehemu hiyo kwa makubaliano maalumu watakayoafikiana.

UCHAGUZI JUDO KUFANYIKA AGOSTI 6.

imagesG 
Na Mwandishi wetu
——————–
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) linatarajia kusimamia uchaguzi wa viongozi wa Chama cha mchezo wa Judo Tanzania (JATA) unaotarajiwa kufanyika  tarehe 06 Agosti mwaka huu jijini Dar es salaam.
Fomu zitaanza kutolewa na kurudishwa kuanzia tarehe 30 June katika Ofisi za Baraza la michezo la Taifa na mwisho  ni tarehe 01 Agosti mwaka huu.
Akieleza  BMT  jana alipowasilisha taarifa ya uchaguzi,  Katibu Mkuu JATA  Innocent Mallya alisema,  uchaguzi utatanguliwa na Mkutano wa mabadiliko ya Katiba ya chama hicho unaotarajiwa kufanyika tarehe 05 saa nne asubuhi katika ukumbi wa Baraza ambao utawakilishwa na wajumbe watatu kutoka katika kila klabu na ndiyo wapiga kura.
“Kila klabu inataarifawa siku ya uchaguzi kuwapa barua za kuwatambulisha wajumbe wake  watakaokuja kupiga kura pamoja na kila klabu kuja na cheti cha usajili wa klabu (club registration certificate)” alieleza Mallya.
Nafasi za uongozi zinazogombewa ni,  nafasi ya Raisi, Makamu wa Raisi, Katibu Mkuu, Katibu  Mkuu Msaidizi, na Mhasibu ambapo,  gharama ya fomu kwa nafasi hizo ni shilingi za Kitanzania elfu ishirini (20,000).
Wengine ni, Mkurugenzi wa ufundi,  Kamishna  wa waamuzi, Kamati ya kujitolea na ustawi, Kamati ya fedha na masoko pamoja na Kamati ya elimu na michezo ambao watalipia fomu shilingi elfu kumi  (10,000).
Baraza linatoa wito kwa wenye sifa na wapenda maendeleo ya mchezo huo kujitokeza kuchukua fomu ili kugombea nafasi tofauti  kwa maendeleo ya JUDO Tanzania.

RAIS Dk.Shein akutana na Balozi wa Afrika Kusini

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Afrika ya  Kusini katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Thamsanga Dennis Msekelu leo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Afrika ya  Kusini katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Thamsanga Dennis Msekelu leo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akifuatana na Balozi wa Afrika ya  Kusini katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Thamsanga Dennis Msekelu baada ya mazunguzo yao leo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar.
[Picha na Ikulu.]

MAFUNZO KWA ASKARI WA CHUO CHA MAFUNZO ZANZIBAR

 Kaimu Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Zanzibar
Dkt. Mahmoud Ibrahim Mussa akitoa mafunzo juu ya kuwasaidia watumiaji wa madawa
ya kulevya kwa Askari wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar katika ukumbi wa Chuo hicho Kilimani
Mjini Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuwasaidia watumiaji wa madawa ya kulevya wakimsikiliza
Kaimu Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Zanzibar
Dkt. Mahmoud Ibrahim (hayupo pichani) katika mafunzo ya siku moja yaliyofanyika
ukumbi wa Chuo hicho.
Picha na Haji Ramadhan Suweid.
———————————————————————————————————————-
Na Miza kona – Maelezo Zanzibar                 
Matumizi ya dawa za kulevya ni janga linaloathiri vijana na kupoteza mwelekeo ambao hupelekea kufanya maamuzi yasiyo sahihi na kupoteza kumbukumbu jambo ambalo linarejesha nyuma maendeleo ya Taifa. 
Akitoa mafunzo kwa watendaji wa Chuo cha Mafunzo  Kaimu Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya
Kulevya Dkt Mahmoud Ibrahim Mussa katika shamra shamra za kuadhimisha siku ya kudhibiti madawa ya kulevya.
Amesema mtumiaji wa madawa ya kulevya huathirika ubongo ambao hawezi kuacha kutumia madawa hayo kwa kuongeza kiwango hali ambayo inayopelekea kutoweza kufanya shughuli za kimaendeleo.
Ameeleza kuwa maambukizi makubwa ya virusi vya ukimwi yanasababishwa zaidi na watumiaji wa madaya ya kulevya kwa njia ya kujidunga sindano ambayo yanaathiri jamii na kupoteza nguvu ya taifa.
“Sigara ina madhara makubwa nacho pia ni kilevi  ina kemikali 4000 ambayo huleta madhara kwa binadamu na kuharibu viungo,
husababisha maradhi ya moyo, kansa pia hupelekea ugonjwa wa akili,” alitanabahisha Dkt Mahamoud. 
Amefahamisha jamii itanabahishwe zaidi juu ya madhara ya matumizi dawa za kulevya pamoja na
uvutaji wa sigara jinsi ya kuyaepuka na  na kuwasaidia watumiaji wa madawa ya kulevya ili  kuweza kuyaacha madawa hayo.
Dkt Mahamoud amefahamisha kuwa kinga ya msingi ya kuachana matumizi ya dawa za kulevya imo ndani ya familia ambayo iweze kumkubali muathirika ili aweze kuachana na kilevi kwa kumpa huduma nzuri bila ya kunyanyapaa.
Aidha wameshauri kutafuta njia ya kuweza kudhibiti utumiaji wa dawa za kulevya katika Vyuo vya mafunzo kwa wafungwa kwani imebainika kuwa baadhi yao hutumia dawa hizo wakati wanatumia kifungo.    
Nao washiriki wa mafunzo hayo wameiomba jamii kutoa mashiriakiano makubwa na vyombo vya kudhibiti madawa ya kulevya ili kuweza   kuwafichua na kuwadhibiti wale wote wanaoingiza, wanaosambaza na watumiaji pamoja na kutoa elimu hiyo kupitia skuli mbali mbali ili kuhakikisha kuwa jambo hilo linadhibitiwa nchini.
Aidha wameitaka Tume ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya kuwa huru katika kutoa huduma zake ii iweze kufanyakazi kwa uwazi pamoja na wazazi kuwafundisha watoto wao maadili mema na kukua katika misingi mizuri kwani vishawishi vya madhara hayo ni vijana.
Mafunzo hayo ni ya siku moja ambayo yaliyowashirikisha watendaji wa Chuo cha Mafunzo ambapo
kilele chake kinatarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu. 

WATENDAJI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI WAKUTANA KUPITISHA MPANGO KAZI 2016/17

indexKatibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto meza kuu) akizungumza katika Kikao cha kupitisha Mpango Kazi na Mpango wa Manunuzi kwa Mwaka wa Fedha 2016/17 wa Wizara hiyo kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Kikao hicho kimehudhuriwa na Wakuu wa Idara na Taasisi za Wizara hiyo. Kulia meza kuu ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TZTAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI, PAMOJA NA MLIPUKO WA UGONJWA WILAYANI CHEMBA NA KONDOA, MKOANI DODOMA,  LILILOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU (MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, TAREHE 20 JUNI, 2016
———————————————————————————————————————
Ndugu wanahabari,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto inaendelea na utaratibu wa kutoa tahadhari kwa wananchi na maelekezo ya hatua za kuchukua katika kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu. Huu ni mwendelezo wa utoaji wa taarifa ya kila wiki, kuhusu mwenendo wa ugonjwa huu kama tulivyoahidi. Hadi kufikia tarehe 19 Juni 2016, jumla ya wagonjwa 21,820 wametolewa taarifa, na kati yao, watu wapatao 344 wamepoteza maisha, tangu ugonjwa huu uliporipotiwa mnamo mwezi Agosti 2015.
Ndugu wanahabari,
Takwimu zinaonyesha kuwa, katika wiki hii inayoishia   tarehe 19 Juni 2016, idadi ya wagonjwa wa Kipindupindu walioripotiwa ni 46 na kati yao wawili walipoteza maisha.  Takwimu hizi zinaonesha kuwa wagonjwa wamepungua wiki hii ikilinganishwa na wiki iliyotangulia, ambapo kulikuwa na wagonjwa 78 na kifo kimoja. Mikoa iliyoripoti ugonjwa wa Kipindupindu wiki hii ni Morogoro (Morogoro mjini 13, Morogoro vijijini 4, Kilosa 3 na Mvomero 3), Shinyanga (Msalala wagonjwa 13 na vifo 2), Mara (Tarime vijijini 7) na Mwanza (Nyamagana 3).
Ndugu wanahabari,
Mkoa wa Shinyanga ambao haukuwa na wagonjwa wiki iliyotangulia, umeripoti wagonjwa katika wiki hii. Aidha, mikoa ya Lindi na Manyara ambayo ilikuwa na wagonjwa wiki iliyotangulia, haikuripoti wagonjwa katika wiki hii. Mikoa mingine ambayo haikuwa na wagonjwa katika wiki hii ni Pwani, Dar-es-Salaam, Kigoma, Dodoma, Geita, Singida, Arusha, Tanga, Tabora, Lindi, Manyara, Kagera, Rukwa, Katavi, Mbeya, Simiyu, Iringa, Kilimanjaro na Mtwara. Hadi sasa bado mikoa ya Njombe na Ruvuma haijaripoti mgonjwa yeyote wa Kipindupindu tangu mlipuko huu uanze mnamo mwezi Agosti mwaka 2015.
Continue reading →

WACHAWI WAVAMIA MKUTANO WA INJILI JIJINI MWANZA.

Na Binagi Blog_BMG
Katika hali ya kushangaza, binti mmoja (pichani katikati) ametoa ushuhuda mbele ya waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza na kueleza jinsi alivyoshindwa kumtoa kafara mchungaji wa kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola.

Ilikuwa katika Mkutano wa Open Your Eyes and See OYES 2016 uliomalizika jumapili iliyopita katika Viwanja vya Kanisa hilo, ambapo binti huyo anasema alitumwa na shangazi yake ili akamtoe mchungaji wa Kanisa hilo kafara lakini alipofika alishindwa kutekeleza adhma yake hiyo ovu.
“Baada ya kujipaka damu ya mnyama (hakutaja ni mnyama gani) nilibeba kitovu cha binadamu na kuja katika mkutano. Nilipojaribu kukukamata nilishangaa moto unatoka mdomoni mwako na kunichoma hivyo nikashindwa kukushika”. Alisema binti huyo na kueleza kuwa walifikia maamuzi hayo kutokana na mchungaji huyo kukemea wachawi kila anapokuwa akihubiri.
Alisema baada ya kushindwa kumkamata mchungaji, Shangazi yake nae alifika katika mkutano huo na kujaribu kumshika mchungaji bila mafanikio na hivyo wakaamua kuhamishia mashambulizi kwa waumini wengine wawili wa kanisa hilo lakini nao wakaanza kutoa moto kama ilivyokuwa kwa mchungaji na hivyo zoezi lao kukwama.
Kutokana na maombi yaliyokuwa yakiendelea katika mkutano huo, nguvu za Mungu zilimzidia binti huyo na kushindwa kurudi nyumbani kwa njia ya kichawi (kupaa), ambapo alianguka chini na alipoamka akaanza kutoa ushuhuda wa adhima aliyokuwa nayo.

SERIKALI YAAGIZA WAKIMBIZI WANAJESHI, WENYE SILAHA WAJISALIMISHE

Serikali ya Tanzania imewataka wakimbizi wote ambao walikuwa wanajeshi kutoka nchi walizokuwepo, kuripoti kwenye mamlaka husika ili waweze kupewa uangalizi maalum (special protection) kama wanajeshi.
Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali (Mstaafu) Emmanuel Maganga, wakati wa maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani yaliyofanyika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
Alisisitiza kuwa wakimbizi ambao wako nchini wakijua ni wanajeshi ni lazima wasajiliwe na mamlaka husika.
Aidha Maganga aliwataka vile vile wakimbizi wote ambao wanamiliki silaha wazisalimishe kwa hiari yao wenyewe.
Alisema kumekuwa na matukio mengi ya ujambazi wa kutumia silaha na hivyo kuhatarisha amani na kuwaamuru wenye silaha kuzisalimisha mara moja ili waende sawa na sheria za nchi walikopata hifadhi.
Maandamano ya wakimbizi yakiingia uwanjani katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani yaliyofanyika katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
(Picha na story Modewjiblog)
……………………………………..
Mkuu huyo wa mkoa pia alitoa wito kwa mashirika ya misaada duniani kutoa misaada inayoowana na misaada inayotolewa kwa nchi zilizoendelea na kuongeza kuwa mahitaji ya binadamu ya msingi hayatofautiani iwe nchi zilizoendelea au zinazoendelea.
Alisema kuwa wakimbizi waliopo kwenye nchi zilizoendelea hupewa makazi ya kudumu na vyakula tofauti tofauti wakati waliopo kwenye nchi zinazoendelea hupewa mahema na chakula aina moja ambayo ni mahindi.
“Mwaka jana tulishindwa kuadhimisha siku ya wakimbizi duniani kwa kuwa tulikuwa tunawapokea wakimbizi kutoka Burundi,” alisema.
Alisema wakimbizi wameongezeka sana nchini na sasa hivi kuna makambi matatu yanayowahifadhi wakimbizi nchini.
Wakati huo huo Tanzania imepongezwa kwa ukarimu wake kwa kuwahifadhi wakimbizi kwa zaidi ya miongo minne sio tu kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na hata duniani.
Mwakilishi mkazi wa shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR , Chansa Kapaya alisema hayo katika sherehe za kuadhimisha siku ya wakimbizi duniani yenye kauli mbiu kuwa “Tupo Pamoja na Wakimbizi, Tafadhali ungana nasi”.
“Tanzania ni mfano wa kuigwa kwa mfano mzuri wa kuwahifadhi wakimbizi wengi duniani na pia kuwatafutia suluhu,” alisema.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akizungumza na hadhira iliyokusanyika katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani yaliyofanyika katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
Alisema mwaka 2014 Tanzania iliwapa uraia wakimbizi zaidia ya 162,000 baada ya kuishi nchini kwa zaidi ya miaka 40.
Aliongeza kuwa, wakimbizi wanapaswa kuthaminiwa kama binadamu wengine kwa kuwa hakuna mtu anayechagua kuwa mkimbizi.
Kapaya alisema kuwa kwa sasa kambi ya Nyarugusu ina wakimbizi zaidi ya 131,733 ambao ni wengi zaidi na kusababisha msongamano unaohatarisha maisha yao.
Mwakilishi wa Shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa Kapaya akisoma risala wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani yaliyofanyika katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa, wafanyakazi wa Shirika la UNHCR na wadau wa maendeleo waliohudhuria sherehe hizo wakifuatilia hotuba mbalimbali.
Mwakilishi wa Shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa Kapaya akipitia ratiba ya maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani ambapo kitaifa yamefanyika mkoani Kigoma katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu. Kulia kwake ni mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita.

TIGO YAKABIDHI KOMPYUTA NA PRINTA KWA JESHI LA POLISI MWANZA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi,akipokea kompyuta na printa kutoka kwa Mkurugenzi wa Kanda ya ziwa wa mtandao wa tigo Ali Maswanya(kushoto), wakati wa hafla ya makabidhiano jijini Mwanza jana,kulia ni Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Mwanza ACP Augustino Senga akishuhudia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi,akizungumza na Mkurugenzi wa Kanda ya ziwa wa mtandao wa tigo Ali Maswanya(kushoto) jijini Mwanza jana,baada ya kupokea kompyuta na printa wakati wa hafla ya makabidhiano ,kulia ni Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Mwanza ACP Augustino Senga akishuhudia.

Mahojiano na Makala Jasper kuhusu Tuzo ya National Geographic Society for Leadership

Makala Jasper ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Shirika lisilo la kiserikali la Mpingo Conservation & Development Initiative (MCDI).
Juni 16, 2016, alitunukiwa tuzo ya National Geographic Society/Buffett Award for Leadership in African Conservation, akiwa ni mshindi miongoni ma washiriki 30 kutoka barani Afrika.
Tuzo hiyo imetokana na kazi anayofanya pamoja na wananchi katika Vijiji mbalimbali mkoani Lindi.
MCDI huwezesha wanakijiji kutumia rasilimali za misitu kujenga uchumi na kutunza mazingira.
Katika miradi inayofanyika chini ya MCDI, wananchi wameweza kujiendeleza na kujenga shule, hospitali, kununua chakula cha dharura na kutoa misaada kwa vijiji vingine.
Tuzo ya National Geographic Society/Buffet Award ni ya pili kupokelewa na Bw. Jasper.
Ya kwanza ilikuwa Whitley Fund for Nature Award aliyopokea nchini Uingiereza tarehe 27 Aprili, 2016.
Karibu umsikilize

Mchezo wa Shuga wabadilisha tabia za vijana

Mratibu wa mradi wa Shuga akijibu maswali yaliyokua yanaulizwa na kikundi cha wasikilizaji cha Iwawa- Makete mkoani Njombe
Wakionyesha furaha zao baada ya kuelewa mada ya siku ukihusianisha na maisha yao ya kila siku
Mwezeshaji wa kikundi cha wasikilizaji wa Kihesa, Manispaa ya Iringa mjini akitimiza jukumu lake la kuelimisha wenzake na kuwawezesha kushiriki katika majadiliano baada ya kusikiliza kipindi
Vijana wa Iringa wakionyesha nyuso zenye furaha baada ya kuongeza uelewa kupitia majadiliano baada ya kipindi cha saba cha mfululizo wa vipindi vya Shuga
 Kikundi cha wasikilizaji kutoka kijiji cha Kabanga, Kyela wakifurahia uelewa walioupata juu ya kukabiliana na changamoto zinazowakumba katika maisha yao
Kikundi cha wasikilizaji Jitambue 1 kutoka wilaya ya Kyela mkoani Mbeya wakijadiliana sehemu ya saba ya mfululizo wa vipindi vya mchezo wa redio wa Shuga.
Wakina mama wakifuatilia mjadala kuhusu kujitambua na namna ya kujikinga na Virusi vya UKIMWI pamoja 

NOAH YAACHA NJIA NA KUPARAMIA DALADALA, BUZA JIJINI DAR ES SALAAM WANAJESHI WANUSURIKA KIFO

 Wananchi wakiangalia ajali ya Noah yenye namba za usajili T 359 DFQ iliyodaiwa kuacha njia na kuparamia daladala namba T 797 DEW eneo la Buza Njia Panda ya Kitunda jijini Dar es Salaam leo jioni. Katika ajali hiyo watu wawili waliokuwa kwenye Noah hiyo waliotajwa kuwa ni Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), walijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya Temeke kwa matibabu.
 Noah hiyo ikiwa kwenye mtaro baada ya kutokea ajali hiyo.
 Daladala lililogongana na Noah hiyo likiwa eneo la tukio.
Wananchi wakiwa eneo la ajali hiyo.

Shule za Msingi katika Manispaa ya TEMEKE zaanza Kupokea Madawati

Mkuu wa Wilaya ya TEMEKE, Bi Sophia Mjema akikabidhi Dawati kwa Mwakilishi wa Shule ya Msingi ya  Mtoni kama Ishara ya kuanza Kupokea Madawati ndani ya Manispaa ya Temeke, ambapo Madawati mengine 50  yatatolewa na Kampuni ya African.
Mkuu wa Wilaya ya TEMEKE, Bi Sophia Mjema akipeana Mkono na Mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mtoni, mara Baada ya kukabidhi Madawati 200 kwenye Shule hiyo, ambapo Madawati mengine 50  yatatolewa na Kampuni ya African.
Mkuu wa Wilaya ya TEMEKE, Bi Sophia Mjema akiwa ameketi kwenye Dawati akiwa pamoja na Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mtoni, Baada ya Kukamilisha Zoezi la Kukabidhi Madawati 200 kwenye Shule hiyo ikiwa ni Ishara ya Kuanza kupokea Madawati ndani ya Manispaa Hiyo.

Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Bajeti ya Trilioni 29.5 ya mwaka wa fedha 2016/17.

jia1 
Mawaziri  na Wabunge wakimpongeza  Waziri wa Fedha  na Mipango Dkt. Philip Mpango  pamoja na Naibu Waziri wake Dkt. Ashatu Kijaju mara baada ya kupitishwa kwa bajeti Kuu ya Serikali ya Trilioni 29.5 kwa mwaka wa fedha 2016/17 leo Bungeni mjini Dodoma.
jia2 
Wabunge wakifurahia  mara baada ya kupitisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
jia3 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akipongezana na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaju nje ya ukumbi wa Bunge, leo mjini Dodoma mara baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17.
jia4 
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako  akimpongeza Waziri wa fedha na Mipango Dkt . Philip Mpango nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma mara baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17.
index Waziri wa fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango watano kutoka kushoto akiwa na baadhi ya watendaji wa Wizara ya fedha na Mipango  nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kupitishwa kwa bajeti Kuu ya Serikali, leo mjini Dodoma.
……………………………………………………………………………………………………
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – DODOMA
Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha bajeti ya shilingi Trilioni 29.5 ya mwaka wa fedha 2016/17 ambayo iliwasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango June 08, 2016.
Bajeti hiyo ilipigiwa kura na wabunge waliokuwepo bungeni, ambapo jumla ya wabunge 251 walipiga kura za ndio za kuipitisha bajeti hiyo kati ya wabunge 252 waliokuwepo ukumbini wakati  kura hizo zikipigwa.
Katika kupiga kura  Hakukuwa na kura yoyote ya hapana au kutokuamua kati ya wabunge waliopiga kura. Jumla ya wabunge 137 hawakuwepo wakati kura zinapigwa.
 “Naipongeza Serikali kwa kutoa hoja ya bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17 na kupitishwa  na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, namtakia Waziri wa Fedha kila la heri katika hatua zinazofuata katika utekelezaji wa bajezi hii,” alisema Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson.
Aidha bunge hilo, lilipitisha muswada wa sheria za Serikali kuidhinisha Trilioni 29.5 kwa matumizi ya Serikali kutoka mfuko wa hazina kwa mwaka unaoishia June 30, 2016.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango  amewataka watanzania kulipa kodi na wale wote wanaotakiwa kusimamia ukusanyaji wa kufanya kazi hiyo kwa ukamilifu ili fedha zilizopitishwa katika bajeti ya mwaka 2016/17.
Sheria hiyo ya bajeti ya mwaka 2016/17 inasubiri kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo utekelezaji wake utaanza Julai 01, 2017.

Mamia wajitokeza Usaili wa Maisha Plus Dar es salaam

677A0614
Akitaja vigezo vya kushiriki Maisha Plus, Kaka Bonda, miongoni mwa majaji na waanzilishi wa Maisha Plus alisema, “Tunachukua washiriki wenye umri wa miaka 18 hadi 26, walio na elimu na ambao hawajasoma kabisa, wawe raia kutoka nchi za Afrika Mashariki”
677A0389
677A0646
677A0422
Maisha Plus kwa mwaka huu wa 2016 inatarajia kuchukua washiriki 30 kutoka nchi tano ambazo ni Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda na Tanzania ambapo mshindi atafadhiliwa wazo la biashara lenye thamani ya fedha ya kitanzania Milioni 30. Kauli mbiu ya mashindano haya kwa mwaka huu ni ‘Vijana Ndio Ngazi’.
677A0857
677A0262
677A0763
Usaili unaendelea katika mikoa mingine na nchi nyingine nje ya Tanzania. Vijana wametakiwa kusikiliza matangazo ya ratiba kupitia redio mbalimbali katika nchi shiriki, runinga ya Azam Two, mitandao mbalimbali ya kijamii pamoja na tovuti maalum ya mashindano hayo ya www.maishaplus.tv

No comments:

Post a Comment