Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Chama cha watu wenye Ulemavu wa
Ngozi Mkoa wa Lindi walipomtembelea leo asubuhi kwa ajili ya kupokea
msaada wa mafuta ya kujikinga na mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa
ngozi.
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mke
wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
wakifurahia jambo na mtoto mwenye ulemavu wa ngozi walipomtembelea leo
asubuhi Ikulu ndogo Mkoani Lindi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta
ya kujikinga na mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi..
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
akiongea na jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi walipomtembelea leo
asubuhi Ikulu ndogo Mkoani Lindi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta
ya kuzia mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ambapo aliiasa
jamii kujali kundi hili na kuacha imani potofu dhidi yao. Kulia ni Mke
wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa na
kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
akiongea na jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi walipomtembelea leo
asubuhi Ikulu ndogo Mkoani Lindi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta
ya kuzia mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ambapo aliiasa
jamii kujali kundi hili na kuacha imani potofu dhidi yao. Kulia ni Mke
wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa na
kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ulemavu wa Ngozi Mkoa wa
Lindi Bw. Hemed Said mafuta ya kuzuia mionzi ya jua kwa watu wenye
ulemavu wa ngozi leo Ikulu ndogo ya Mkoa wa Lindi.Katikati ni Mke wa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
akikabidhi zawadi ya mbuzi na kuku kwa Mwenyekiti wa Chama cha watu
wenye Ulemavu wa Ngozi Mkoa wa Lindi Bw. Hemed Said walipomtembelea leo
asubuhi Ikulu ndogo Mkoani Lindi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta
ya ngozi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
akikabidhi zawadi ya kuku kwa Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ulemavu
wa Ngozi Mkoa wa Lindi Bw. Hemed Said walipomtembelea leo asubuhi Ikulu
ndogo Mkoani Lindi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta ya ngozi kwa
watu wenye ulemavu wa ngozi.Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli, Mke wa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa na
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi wakiwa katika picha ya Pamoja na
jamii ya watu wenye ulemavu leo asubuhi Ikulu ndogo Mkoani Lindi.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
TANZANIA YATEULIWA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUU WA 37 WA SHIRIKA LA MAKAZI AFRIKA
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline
Mabula akiwa na viongozi wa Taifa la Nigeria na Shirika la Makazi la
Afrika Jijini Abuja wakati ukipigwa wimbo wa Taifa la Nigeria katika
ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika.
………………………………………………………………………………………………………………………
Katika kutambua mchango wa
Tanzania katika uendelezaji wa makazi ya watu na kuweka mbele utu wa
binadamu wa mahitaji ya msingi ikiwemo nyumba, wajumbe kutoka nchi 44 za
kiafrika waliohudhuria Mkutano wa 35 wa Shirika la Makazi la Afrika
Jijini Abuja Nigeria, kwa pamoja wameiteua na kuiidhinisha Tanzania kuwa
mwenyeji wa Mkutano wa 37 wa Shirika hilo utakaofanyika mwaka 2018.
Katika Mkutano Mkuu wa Abuja
changamoto iliyojitokeza ni uwezo wa nchi za kiafrika wa kuwapatia
wananchi wake nyumba za gharama nafuu, huku wajumbe wakitoa rai kwa
serikali zao kuainisha vigezo vya kutambua nyumba ya gharama nafuu.
Aidha, wajumbe wa Mkutano huo wanaona changamoto kubwa ya wananchi wengi
wa Afrika kuweza kumiliki nyumba ya gharama nafuu ni uwezo mdogo
unaotokana na vipato vidogo, kutokuwepo sera ya kuwezesha raia kumiliki
nyumba za gharama nafuu, kukosekana kwa miundombinu katika makazi ya
gharama nafuu, riba kubwa za mikopo ya ujenzi wa nyumba nafuu na
ukosefu wa ardhi ya kujenga nyumba hizo.
Kwa ujumla changamoto za nchi za
kiafrika katika kuwapatia wananchi wa kawaida makazi nafuu zinafanana
na kilio kikubwa katika nchi hizo ni kuwepo makazi holela hata baada ya
nchi hizo kujikomboa kutoka ukoloni mkongwe. Hivyo, Mkutano Mkuu huu
umeazimia nchi wanachama kuweka juhudi katika kuipa kipaumbele sekta ya
nyumba kwa kuwa ni sekta mtambuka katika kuharakisha ukuaji wa uchumi na
maisha bora ya watu.(Habari za mkutano huo katika picha na Muungano
Saguya, Abuja, Nigeria)
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline
Mabula (wan ne kulia) akifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa
katika Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika (Shelter Afrique).
Wengine ni Waziri wa Nishati, Ujenzi na Nyumba wa Nigeria Mh. Babatunde
Fashiola (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shelter Afrique Bw. James
Mugerwa (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shelter
Afrique Bw. Jean-Paul Missi (wa kwanza kulia).
Mkurugenzi Msaidizi wa Usanifu wa Miji na Uendelezaji Upya Maeneo, kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi Immaculata Senje (wa pili kushoto) akiwa miongoni mwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shelter Afrique uliofanyika Jijini Abuja wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa.
Mkurugenzi Msaidizi wa Usanifu wa Miji na Uendelezaji Upya Maeneo, kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi Immaculata Senje (wa pili kushoto) akiwa miongoni mwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shelter Afrique uliofanyika Jijini Abuja wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline
Mabula akiwa meza kuu baada ya Tanzania kuteuliwa na kuidhinishwa na
Mkutano Mkuu wa 35 wa Shelter Afrique Jijini Abuja kuwa mwenyeji wa
Mkutano wa 37 utakaofanyika nchini Tanzania mwaka 2018.Kulia kwa Naibu
Waziri ni Waziri wa NIshati, Ujenzi na Nyumba wa Nigeria Mh. Babatunde
Raji Fashola ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo.
Wajumbe
kutoka nchi 44 za Afrika na wageni waalikwa kutoka nchi na mashirika
mbalimbali ya Kimataifa wakiendelea na Mkutano wa 35 wa Shirika la
Makazi la Afrika uliofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton Jijini
Abuja, Nigeria. Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline
Mabula akiwa katika kilima cha Katampe Jijini Abuja, ambacho ni
katikati ya nchi ya Nigeria alipotembelea maeneo mbalimbali ya
kihistoria mara baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la
Makazi Afrika (Shelter Afrique). Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkurugenzi
Msaidizi wa Usanifu wa Miji na Uendelezaji Upya Maeneo, kutoka Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi Immaculata Senje.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline
Mabula akiwa katika kilima cha Katampe Jijini Abuja, ambacho ni
katikati ya nchi ya Nigeria alipotembelea maeneo mbalimbali ya
kihistoria mara baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la
Makazi Afrika (Shelter Afrique). Kutokana na hali ya amani katika nchi
hiyo, Naibu Waziri alipata ulinzi wa kutosha kama inavyoonekana
alipopiga picha ya pamoja na walinzi walioandamana na wageni kutoka nchi
mbalimbali katika ziara hiyo. Tudumishe amani yetu Tanzania
Mchoro
huu juu na chini unaonyesha taswira ya mji wa kisasa unaotabiriwa kuwa
Dubai ya Nigeria unaojengwa nje kidogo ya Jiji la Abuja ujulikanao kama
Centenary City Abuja ambao wajumbe wa nchi mbalimbali za Afrika
waliohudhuria Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika waliweza
kuutembelea na kujionea ndoto ambayo wanigeria wameamua kuitekeleza.
Wajumbe
wa Mkutano wa 35 wa Shelter Afrique wakiwa katika eneo la centenary
city unaotarajiwa kuwa mji wa kibiashara Jijini Abuja mji ambao
unajengwa na serikali ya Nigeria kwa kushirikiana na sekta binafsi.
TUME YA KUREKEBISHA SHERIA YASHIRIKI KUFANYA USAFI ENEO LA FERI KATIKA KUADHIMISHA WIKI YA MAZINGIRA
Katibu
Mtendaji wa Tume Bw. Casmir Kyuki (katikati) akiwa na mkuu wa Wilaya ya
Ilala Bw. Raymond Mushi (Kulia) na Kamishna wa Tume Bw. Albert Msangi
wakishiriki zoezi la Usafi katika eneo la Feri.
Katibu Mtendaji wa Tume Bw. Kyuki akiwa na Kamishna wa Tume Bw. Albert Msangi wakizoa taka katika eneo la Fer
Watumishi wa Tume wakiwa wamebeba taka wakati wa zoezi la kufanya usafi eneo la Feri.
Mkurugenzi
wa Halmshauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Isaya Mngurumi (kushoto) na Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi anayemfuatia wakishiriki kufanya
usafi.
Katibu
Mtendaji wa Tume Bw. Casmir Kyuki (kushoto ) akiwa pamoja na Mkuu wa
Wialaya ya Ilala pamoja na Makamishana wa Tume wakishiriki kufanya
usafi.
Kamishana wa Tume Profesa Sufian Bukurura (kulia) akiwa na mtumishi wa Tume Bw. Ally Msengi wakishiriki kufanya usafi.
Katibu Mtendaji wa Tume Bw. Casmir Kyuki akihojiwa na chombo cha habari wakati wa zoezi la kufanya usafi.
Watumishi
wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja
mara baada ya zoezi la kufanya usafi katika eneo la Feri.
Madereva TBL Mwanza wapigwa msasa kuhusu udereva wa kujihami
Mkufunzi,
Herbert Kubo akitoa elimu kwa madereva wa Kiwanda cha Bia TBL mkoani
Mwanza katika mafunzo ya wafanyakazi hao yaliyofanyika kiwandani hapo
jana.
Madereva wa Kiwanda cha Bia TBL mkoani Mwanza wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na Herbert Kubo kiwandani hapo jana
Madereva wa Kiwanda cha Bia TBL mkoani Mwanza wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na Herbert Kubo kiwandani hapo jana.
Boxing legend Muhammad Ali dies aged 74
The former world heavyweight
boxing champion, one of the world’s best-known sportsmen, died at a
hospital in the US city of Phoenix in Arizona state after being admitted
on Thursday.
He was suffering from a respiratory illness, a condition that was complicated by Parkinson’s disease.
The funeral will take place in Ali’s hometown of Louisville, Kentucky, his family said in a statement.
Born Cassius Marcellus Clay, Ali shot to fame by winning light-heavyweight gold at the 1960 Rome Olympics.
Nicknamed “The Greatest”, the
American beat Sonny Liston in 1964 to win his first world title and
became the first boxer to capture a world heavyweight title on three
separate occasions.
He eventually retired in 1981, having won 56 of his 61 fights.
TaGLA na TBA wakamilisha Mafunzo ya Siku Tano kwa njia ya Mtandao(Video Conferencing).
Wadau
kutoka Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) pamoja na Wakala
wa Majengo Tanzania (TBA) wakimsikiliza mtoa mada kwa njia ya video
(Tele Conference) wakati wa Mafunzo ya Siku Tano yaliyolengwa kwa ajili
ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuhusiana na masuala mbalimbali
yanayaohusu majengo 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO)
Wadau
kutoka Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) pamoja na Wakala
wa Majengo Tanzania (TBA) wakimsikiliza mtoa mada kwa njia ya video
(Tele Conference) wakati wa Mafunzo ya Siku Tano yaliyolengwa kwa ajili
ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuhusiana na masuala mbalimbali
yanayaohusu majengo 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
Meneja
Mafunzo toka Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Dickson
Mwanyika akiwashukuru wadau waliohudhuria mafunzo hayo wakati wa
ufungaji jan 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
Mdau
kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi Mtapuli Juma
akichangia mada kuhusiana na mafunzo ya siku tano waliyopatiwa na Wakala
wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) wakati wa ufungaji wa mafunzo
hayo 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA), Bw. Elius Mwakalinga
akitoa neno la sukurani kwa mtoa mada (hayupo pichani) mara baada ya
kumalizika kwa mafunzo ya siku tano yaliyoaratibiwa na Wakala wa Mafunzo
kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Washiriki wa Mafunzo ya siku tano kwa njia ya mtandao akipokea cheti chake toka kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Charles
Senkondo (katikati) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo
(TBA), Bw. Elius Mwakalinga (kushoto) mara baada
ya kumalizika kwa mafunzo hayo yaliyoaratibiwa na Ofisi ya Wakala wa
Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles Senkondo akiwashukuru
wateja wake mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku tano
yaliyoaratibiwa na Ofisi yake 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Washiriki wa Mafunzo ya siku tano kwa njia ya mtandao akipokea cheti chake toka kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Charles
Senkondo (katikati) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo
(TBA), Bw. Elius Mwakalinga (kushoto) mara baada
ya kumalizika kwa mafunzo hayo yaliyoaratibiwa na Ofisi ya Wakala wa
Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
PROF.MBARAWA:BARABARA YA IRINGA- DODOMA KILOMITA 260 KUFUFUA UCHUMI WA MIKOA HIYO
Waziri
Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza
Meneja wa wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Iringa Eng.
Daniel Kindole wakati wa ukaguzi wa barabara ya Dodoma –Iringa KM 260
ambapo ujenzi wake umekamilika kwa kiwango cha lami.
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza akitoa taarifa ya hali ya
Miundombinu kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa wakati wa ziara ya waziri huyo katika mkoani Iringa.
Waziri
Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa watendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mkoani Iringa. Kulia ni Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi na Kushoto Mkuu wa mkoa wa
Iringa Bi Amina Masenza.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi akifafanua
jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa mara baada ya kuanza ziara ya siku nne mkoani Iringa.
………………………………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wakazi wa mikoa ya Dodoma
na Iringa kutumia fursa ya kukamilika kwa kiwango cha lami barabara ya
Dodoma Iringa kufanya shughuli za uzalishaji ili kujiletea maendeleo.
Akizungumza wakati akikagua
barabara ya Dodoma Iringa KM 260 Profesa Mbarawa amesema Barabara hiyo
imelenga kufufua uchumi wa mikoa ya Iringa na Dodoma hususani hifadhi ya
Ruaha na Vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Iringa.
“Barabara hii tuIiigawa katika
sehemu tatu Iringa-Migori KM 95.2, Migori- Fufu KM 93.8 na Fufu –Dodoma
Km 70,9 ili ikamilike kwa haraka na hivyo kuharakisha maendeleo ya watu
wa Dodoma na Iringa “. Amesema Profesa Mbarawa.
Profesa Mbarawa amesema kiasi cha
sh. bil 4.6 itatolewa na Serikali ili kulipa fidia kwa wananchi
watakaopisha ujenzi wa barabara ya Iringa mchepuo KM 7.3 itakayoanzia
Kihesa –Kilolo kupitia Chuo Kikuu cha Iringa hadi Igumbilo ili kuondoa
msongamano wa magari katikati ya Mji wa Iringa.
Waziri Mbarawa amesisitiza nia ya
Serikali ya kuukarabati uwanja wa Ndege wa Nduli mkoani Iringa ili
kuwawezesha watalii wanaokwenda katika hifadhi ya Ruaha na Vivutio
vingine vya Utalii Mkoani Iringa kutumia uwanja huo ili kuhamasisha
uchumi wa mkoa wa Iringa.
Naye Mbunge wa Isimani Mhe.
Wiliam Lukuvi ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
akizungumza kwa niaba ya wabunge wa Mkoa wa Iringa amemshukuru Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Mbarawa kwa kukubali kujenga
barabara ya Mchepuo ya Iringa na kumuomba aangalie uwezekano wa kujenga
kwa kiwango cha lami barabara ya Iringa-Kalenga hadi katika hifadhi ya
Taifa Ruaha yenye urefu wa KM 104.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina
Masenza amemuomba Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupanua
barabara ya TANZAM eneo la Mlima kitonga na kumalizia ujenzi wa barabara
ya Tosamaganga –Ugwachanya kwa kiwango cha lami na Ujenzi wa daraja la
Tosamaganga ili kupunguza changamoto za usafiri kwa wakazi wa Iringa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano yupo katika Ziara ya siku nne mkoani Iringa kukagua
maendeleo ya Ujenzi wa Miundombinu mkoani humo.
KIPINDI CHA UNYAYO WANGU: DAVID MANOTI AZUNGUMZIA ADHABU YA WABUNGE WA UPINZANI BUNGENI
Unyayo
wangu ni kipindi kipya kabisa kinachokujia kupita Tone Tv, ambacho
kinaletwa kwenu na Mtangazaji wetu Eddie Nyota , kinacholenga shabaha ya
watu waliothubutu kufanya jambo fulani katika jamii na wanauelewa na
jamii husika. Utajifunza mengina kuburudika pia kupitia kipindi hiki
Kinacholenga rika zote.
RC TANGA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA WILAYA YA PANGANI,AZINDUA JENGO LA UPASUAJI KITUO CHA AFYA MWERA WILAYANI HUMO
KULIA NI MGANGA MFAWIDI WA KITUO CHA AFYA CHA MWERA WILAYANI PANGANI
DR.MADARAKA RAPHAEL AKISISITIZA JAMBO KWA MKUU WA MKOA WA
TANGA,MH.,MARTINE SHIGELLA WAKATI ALIPOTEMBELE UJENZI HUO KUSHOTO NI
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA PANGANI,
DR.MADARAKA RAPHAEL AKISISITIZA JAMBO KWA MKUU WA MKOA WA
TANGA,MH.,MARTINE SHIGELLA WAKATI ALIPOTEMBELE UJENZI HUO KUSHOTO NI
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA PANGANI,
MH.MKUU WA MKOA WA TANGA,MARTINE SHIGELLA AKISOMA JIWE LA MSINGI WA PILI KULIA NI KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA MHANDISI ZENA SAID |
MKUU WA MKOA WA TANGA,MH MARTINE SHIGELLA AKIZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI WAKATI ALIPOFANYA ZIARA |
BAADHI YA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI WAKIMSIKILIZA KWA UMAKINI MKUU WA MKOA WA TANGA,MH,MARTINE SHIGELLA ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NAO LEO |
No comments:
Post a Comment