Pages

Friday, June 24, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AKUTANA NA WAZIRI KUTOKA MALAYSIA NA MAKAMU WA RAIS WA TIGO AFRIKA



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na Waziri asiye na Wizara Maalum katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia na Mkurugenzi Mtendaji wa kitengo kinachoshughulikia masuala ya utendaji Na utekelezaji wa miradi ya serikali Dk. Sri Idris Jala ,Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri asiye na Wizara Maalum katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia na Mkurugenzi Mtendaji wa kitengo kinachoshughulikia masuala ya utendaji Na utekelezaji wa miradi ya serikali Dk. Sri Idris Jala (kushoto) mara baada ya mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri asiye na Wizara Maalum katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia na Mkurugenzi Mtendaji wa kitengo kinachoshughulikia masuala ya utendaji
Na utekelezaji wa miradi ya serikali Dk. Sri Idris Jala na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais wa Tigo Afrika Bi. Rachel Samren (Kushoto) wakati Bi. Rachel Samren alipomtembelea Makamu wa Rais  ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo tarehe 24 Juni 2016.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Makamu wa Rais wa Tigo Afrika Bi. Rachel Samren wengine pichani kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masuala ya Kisheria Bi. Sylvia Balwire na Bi. Halima Okash Afisa Uhusiano (wa kwanza kushoto)  Ikulu jijini Dar es salaam leo tarehe 24 Juni 2016.
——————————————————–
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN ameiomba serikali ya MALAYSIA kujenga ofisi za ubalozi wake hapa
nchini ili kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili. 
Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo leo Juni 24, 2016 alipokutana na kufanya mazungumzo Waziri asiye na Wizara Maalum Dkt SRI IDRIS JALA ambaye
aliongozana na Balozi wa MALAYSIA aliye na makazi yake jijini Nairobi Kenya, ISMAIL SALAM walipomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar Salaam.
Makamu wa Rais amesema ujenzi wa ofisi za ubalozi huo hapa nchini utarahisisha kwa kiasi kikubwa Watanzania wanaotaka kusafiri kwenda nchini
MALAYASIA kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwemo za masomo na biashara kuliko hali ilivyo sasa ambapo ofisi za balozi hizo zipo Nairobi – Nchini KENYA.
Kwa upande wake Waziri asiye na Wizara Maalum Dkt SRI IDRIS JALA amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa nchi yake itaendelea kuimarisha,kukuza
na kuendeleza mahusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Malaysia hasa uanzishaji wa ubalozi wake hapa nchini.
Hata hivyo, Waziri huyo amesisitiza umuhimu wa kuanzishwa kwa Makubaliano ya pamoja ya ushirikiano kati ya Tanzania na Malaysia ambayo
yatajikita  katika sekta mbalimbali zikiwemo za elimu, uchukuzi na biashara.
Wakati huo huo, Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN pia amekutana Makamu wa Rais wa TIGO – Afrika RACHEL SAMREN ambapo wamezungumzia masuala
mbalimbali ikiwemo namna kampuni hiyo itakavyosadia katika kuwawezesha wanawake kuondokana na umaskini hapa nchini.
Katika kuhakikisha taifa linaongeza ukusanyaji wa mapato,
Makamu wa Rais ameuhimiza uongozi wa kampuni ya Simu ya Tigo hapa nchini kuhakikisha
unalipa kodi kwa uwazi ili fedha hizo ziweze kusaidia serikali katika kuimarisha
utoaji wa huduma za kijamii hapa nchini.

MSWADA WA SHERIA YA MANUNUZI YA UMMA WA MWAKA 2106

IMG_20160624_151157_421

Watanzania waaswa kuzingatia umri katika kuangalia filamu na maigizo.

index2 
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fisso akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani) kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo tasnia ya filamu nchini katika kuazimisha wiki ya Utumishi wa Umma.
————————————————————
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Watanzania wameaswa kuzingatia umri katika kungalia filamu katika majumba ya sinema na sehemu mbalimbali.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fisso wakati akifafanua masuala mbalimbali kuhusu tasnia ya filamu nchini  kwa  waandishi wa habari.
Bibi Joyce Fisso amesema kuwa Bodi yake inafanya kazi ya kuzipa kiwango kazi za filamu na maigizo ikiwemo umri sahihi wa kuangalia filamu  na hili linapaswa kuzingatiwa na waoneshaji na waangaliaji wa Filamu.
“ Natoa wito kwa watanzania hasa wazazi kuzingatia umri katika kuangalia filamu, ukiona imeandikwa umri wa miaka 18 ujue ni maalum kwa ajili ya umri huo na mtoto chini ya hapo hatakiwa kuangalia kwasababu maudhui ya filamu au maigizo hayo hayamuhusu alisisitiza Bibi. Joyce.
Bibi Joyce Fisso ameongeza kuwa jukumu la kujenga maadili kwa watanzania hasa watoto lipo mikononi mwa wazazi wao na kuwaasa wazazi kuzingatia umri katika kuangali filamu na maigizo mbalimbali ili kupunguza wimbi la mmomonyoko wa maadili nchini.
Aidha Bibi Joyce Fisso ameshauri waandaaji wa filamu na maigizo nchini kuandaa filamu na maagizo yenye maudhui ya watoto  ya kuwajenga katika Mila, Desturi na Tamaduni za kitanzania kwa kuwa ndio kizazi cha baadae na kinatakiwa kulelewa katika maadili mema.
Bodi ya Filamu inapokea filamu na maigizo mbalimbali kwa ajili ya kupata kibali cha kusambazwa na zaidi ya asilimia 70 ya filamu hizo maudhui yake ni mapenzi  hivyo basi jamii inatahadharishwa kuzingatia umri uliowekwa katika filamu na maigizo hayo ili kuepukana na mmomonyoko wa maadili kwa watoto uanaozidi kuongezeka siku hadi siku kwa kuangalia filamu na maigizo yenye maudhui yasiyowahusu.

TAA YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI KWA IDARA YAKE YA RASILIMALI WATU


 Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Fatma Matimba, akichapa kazi ofisini kwake jijini Dar es Salaam, wakati wa kilele cha siku ya Utumishi wa Umma ambapo mwaka huu, maadhimisho hayo yamefanyika mahala pa kazi ambapo wananchi pamoja na wafanyakazi wa taasisi husika walipata fursa ya kujipatia elimu ya shughuli mbalimbali zifanywazo na taasisi husika. 
Meneja Rasilimali Watu Mafunzo wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Abdul Mkwizu (kulia) akimpa maelezo kuhusu mafunzo Ally Zongo, mfanyakazi wa taasisi hiyo, kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.
Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Fatma Matimba (kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya upandishaji vyeo kwa wafanyakazi Omari Hazaa (katikati) na Yusuph Mahadhi (kulia), ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, 2016. 

(PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)

Zaidi ya wilaya 81 kuongezewa usikivu wa redio ya Taifa

napeeee 
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
————————–
Zaidi ya Wilaya 81 ambazo zimekuwa hazipati usikivu wa redio ya Taifa nchini kuongezewa usikivu kwa mwaka wa fedha 2016/17 na kuendelea.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye leo Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nachingwea Mhe. Hasani Eliasi Masala juu ya kutokusikika redio ya Taifa katika jimbo lake.
Aidha Mhe. Nape amesema kuwa kutosikika kwa redio ya Taifa katika Wilaya hiyo kumetokana na uchakavu wa mitambo, lakini kwa hivi sasa eneo la Nachingwea Mjini linapata matangazo ya redio ya Taifa kwa kutumia mitambo miwili midogo ya Redio-FM ya TBC-FM na mtambo wa TBC-Taifa.
“Nia ya Serikali ni kufunga mitambo mipya na ya kisasa ya FM yenye nguvu kubwa ya kilowati 2 ambao utakuwa na uwezo wa kurusha matangazo yatakayowafikia wananchi sehemu mbali mbali nchi nzima,” alifafanua Mhe. Nape.
Aliendelea kwa kusema kuwa, tathmini iliyofanyika kubaini usikivu wa redio ya Taifa nchini umeonyesha kuwa jumla ya wilaya 81 hazina usikivu mzuri wa redio ya Taifa kutokana na uchakavu wa mitambo.
Aidha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imejipanga kufunga mitambo mipya, sambamba na ukarabati wa majengo ya mitambo, ofisi na miundo mbinu mbalimbali kuanzia mwaka wa fedha 2016/2017 na kuendelea kwa kuanza na Mikoa iliyopo pembezoni ili kuboresha usikivu ikiwezekana isikike mpaka nchi jirani.

MAHAFALI YA CHUO CHA Shanghai International Studies University.

Y1 Y2 Y3 
Juma Mohammed Salum wa Idara ya Habari (MAELEZO Zanzibar) akiwa na wahitimu wenzake wa PhD ambao wametunukiwa vyeti vyao jana na Chuo Kikuu cha Shanghai International Studies University. 

WAZIRI WA AFYA (SMZ) AFUNGUA MASHINDANO YA MASAUNI-JAZEERA JIMBONI KIKWAJUNI

Z1 
Waziri wa Afya(SMZ), ambaye pia ni mgeni Rasmi, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni mchezaji wa timu ya maveterani ya Kikwajuni,  Mhe. Nassor Salim Jazeera, muda mfupi kabla ya mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya Masauni-Jazeera, iliyofanyika katika Uwanja wa Mnazi Mmoja, Zanzibar.
Z2 
Waziri wa Afya(SMZ), ambaye pia ni mgeni Rasmi, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, akisalimiana na wachezaji wa timu ya kundi la G1, muda mfupi kabla ya mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya Masauni-Jazeera, iliyofanyika katika Uwanja wa Mnazi Mmoja, Zanzibar.
Z3 
Waziri wa Afya(SMZ), ambaye pia ni mgeni Rasmi, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kikwajuni juu, wakati wa ufunguzi wa Ligi ya Masauni-Jazeera, iliyofanyika katika Uwanja wa Mnazi Mmoja, Zanzibar.
Z4 
Waziri wa Afya(SMZ), ambaye pia ni mgeni Rasmi, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Ligi ya Masauni-Jazeera, iliyofanyika katika Uwanja wa Mnazi Mmoja, Zanzibar.
Z5 
Waziri wa Afya(SMZ), ambaye pia ni mgeni Rasmi, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (wa pili kulia), na waalikwa wengine wakifuatilia mchezo wa Ligi ya Masauni- Jazeera katika Uwanja wa Mnazi Mmoja.
Z6
Watazamaji wakifuatilia mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya Masauni-Jazeera, kati ya Timu ya Maveterani na Timu ya Kundi la G1, uliofanyika katika Viwanja wa Mnazi Mmoja,Zanzibar.
(Picha na Mpiga Picha Wetu)

BHARTI AIRTEL COMMITS TO TANZANIA AS IT EXITS TTCL

 R2TREASURY Registrar, Mr Lawrence Mafuru (left) and Bharti Airtel Africa CEO, Christian De Faria signing an agreement to exit its shareholding in Tanzania Telecommunications Company Limited (TTCL) where it had 35% Equity together with the Government of Tanzania holding 65%. Looking on center is the Deputy Permanent Secretary Ministry of Construction Work and Communication Dr. Maria Sasabo, and other government officials. The Signing ceremony took place today at TTCL Head Office Samora Street Dar es Salaam.
R3TREASURY Registrar, Mr Lawrence Mafuru (left) display  Bharti Airtel shareholding certificate soon after Bharti Airtel Africa CEO, Christian De Faria (right) signed an agreement to exit its shareholding in Tanzania Telecommunications Company Limited (TTCL) where Bharti Airtel had 35%.
R1 
Airtel  Africa team with Tanzania Government delegates  soon after  signing an agreement for Bharti Airtel  to exit its 35% shareholding in Tanzania Telecommunications Company  Limited (TTCL )were Government  of Tanzania will own 100% equity.
————————————————————–
Dar es salaam, 24th June, 2016  : Airtel Tanzania (Airtel)  announced that it has signed an agreement with Tanzania Telecommunications Company Limited (TTCL) to complete the sale of its 35% shareholding in the fixed line business to the Government of Tanzania.
Airtel Africa’s Executive Chairman, Christian de Faria said, “The completion of the sale of Bharti Airtel’s shareholding in TTCL to the Government marks the end of a long and mutually beneficial journey in fixed line telecommunications. Airtel remains committed to Tanzania as it continues its strategic partnership with the Government through the mobile business – Airtel Tanzania, and will continue to invest to grow the business further.”

WAZIRI KAIRUKI AFUNGA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2016 MKOANI DODOMA

M1 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa ufafanuzi kuhusu hoja zilizowasilishwa na Watumishi wa Umma mkoani Dodoma wakati wwa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016
M2 M3 
KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2016 -MATUKIO,-DODOMA. Watumishi wa Umma mkoani Dodoma wakisikiliza Hotuba ya Waziri wa Nchi-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb)
M4 
KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2016 -MATUKIO,-DODOMA. Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb), katikati akisikiliza hoja za Watumishi wa Umma mkoani Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Jordan Rugimbana na kushoto, Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi. Rehema Madenge.
M5 
Mmoja wa watumishi akiwasilisha hoja kuhusu madai mbalimbali ya watumishi.
M6 
Katibu wa Chama Cha Walimu (CWT)-Chunya Mbeya Bw.Sauli George akiwasilisha hoja.
M7 
Bw. Richard Kasogoto akiwasilisha hoja kuhusu watumishi kuonewa maeneo ya kazi.

MEDIA CAR WASH UWANJA WA JAMUHURI DODOMA JUNI 25, 2016

index

Waziri wa afya Ummy Mwalimu afungua mkutano wa 12 wa baraza la mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

u1 
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jobs is,Wazee na watoto Ummy Mwalimu (katikati) akiwa na waziri wa afya toka Uganda(kulia)wakifuatilia mada zinazowasilishwa Kenney mkutano huo.
u3 
Katibu Mkuu,Wizara ya Afya Tanzania,Dkt.Mpoki Ulisubyisya akiwasilisha mada kwenye mkutano huo.
u2 
Baadhi ya mawaziri wa baraza hilo wakiwa Kenney picha ya pamoja.
u4 
Mawaziri wa  afya za nchi za  Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa pamoja wa majadiliano kuhusu maendeleo endelevu ya kupunguza kiwango cha juu cha maambukizi ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza unaofanyika jijini Arusha.
(Picha zote na Wizara ya Afya)

WAZEE JIMBO LA KIWAJUNI ZANZIBAR KUPATA HUDUMA YA MATIBABU BURE

J1 
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza  na wananchi wa Jimbo hilo wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Jimbo ambapo alitoa taarifa juu ya watu wazima kuanzia umri wa miaka 70 kupata huduma ya matibabu bure.
J5 
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia), akimsikiliza mmoja wa wananchi wa Jimbo hilo mara baada ya kutoa muda wa kusikiliza kero mbalimbali za wananchi  wakati wa mkutano uliofanyika Ofisi ya Jimbo hilo, Zanzibar.
J3 
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Tawi la Zanzibar, Ismail Kangeta, akitoa ufafanuzi juu ya huduma ya matibabu itakayoanza kutolewa bure kwa wananchi wa Jimbo la Kikwajuni, wakati wa mkutano uliofanyika Ofisi ya Jimbo.Wapili ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
J6 
Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Nassor Salim Jazeera (kulia), akimsikiliza mwananchi wa Jimbo hilo mara baada ya kutoa muda wa kusikiliza kero mbalimbali za wananchi  wakati wa mkutano uliofanyika Ofisi ya Jimbo hilo, Zanzibar.
J2 
Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar  wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati  akizungumza  katika  mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Jimbo ambapo alitoa taarifa juu ya watu wazima kuanzia umri wa miaka 70 kupata huduma ya matibabu bure.J4 Mwananchi wa Jimbo la Kikwajuni akisoma kipeperushi kilichotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambacho kina majina ya Hospitali ambazo wafaidika wa huduma ya matibabu bure wanaweza kwenda kupata huduma hiyo wakati wa mkutano uliofanyika Ofisi ya Jimbo hilo Kikwajuni Zanzibar.
(Picha na Mpiga Picha Wetu)

Bodi ya Filamu yakutana na wadau wa filamu katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma

1 
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi Joyce Fisso (kushoto) akizungumza na wadau wa filamu (hawapo pichani) kujadili changamoto na namna ya kuendeleza tasnia ya filamu nchini ikiwa ni utaratibu wa kukutana na wadau hao kusikiliza changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi ikiwa ni  maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma, kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Genofeva Matemu.
2Mwanasheria wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Patrick Kipangula (kulia) akifafanua hoja za kisheria katika kikao kati ya Bodi ya Filamu Tanzania  na wadau wa filamu nchini ikiwa ni utaratibu wa kukutana na wadau hao kusikiliza changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi ikiwa ni  maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma.
3 
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Bw.Simon Mwakifwamba akichangia hoja katika kikao kati ya Bodi ya Filamu Tanzania  na wadau wa filamu nchini ikiwa ni utaratibu wa kukutana na wadau hao kusikiliza changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi ikiwa ni  maadhimisho ya wiki ya Utumishi.
4 
Muandaaji na msanii wa filamu nchini Bw. William Mtitu akichangia hoja katika kikao kati ya Bodi ya Filamu Tanzania  na wadau wa filamu nchini ikiwa ni utaratibu wa kukutana na wadau hao kusikiliza changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi ikiwa ni  maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma.
5 
Mmoja ya wadau wa filamu Bw. Hussein Kimu akichangia hoja katika kikao kati ya Bodi ya Filamu Tanzania  na wadau wa filamu nchini ikiwa ni utaratibu wa kukutana na wadau hao kusikiliza changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi ikiwa ni  maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma.
Picha zote na Shamimu Nyaki WHUSM

No comments:

Post a Comment