Pages

Monday, June 20, 2016

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA KITUO CHA UHAMIAJI HOLILI

ban1 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati), akikagua mzigo wa John Evarist ambaye ni  mfanyabiashara aliyekua akipita kutoka nchini Kenya  kupitia mpaka uliopo katika  kijiji cha Kamkunji, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yuko mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
ban2Mfanyabiashara John Evarist aliyekua akipita kutoka nchini Kenya  kupitia mpaka uliopo katika  kijiji cha Kamkunji, mkoani Kilimanjaro, akijibu maswali aliyoulizwa na Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Holili, ACI Kagimbo Hosea(wa kwanza kushoto).Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira aliyepo mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
ban3 
Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Holili, ACI Kagimbo Hosea ( aliyenyoosha mkono), akimuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto), mwisho wa mpaka unaotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya wakati wa ziara ya Katibu Mkuu kukagua njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.Wa pili kushoto ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, RPC Wilbrod Mutafungwa. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
ban4 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia), akipanda Mlima   kwenda kukagua jiwe linalotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya katika Mpaka uliopo eneo la Mlima Nyoka, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yupo  mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
ban5 
Ujumbe ulioongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(), ukishuka kutoka mlimani   baada ya ukaguzi wa mpaka uliopo Mlima Nyoka, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yupo  mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.(Picha  na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

MKURUGENZI WA MANISPAA YA ILEMELA MKOANI MWANZA AKABIDHI MADAWATI KWA AJILI YA SHULE ZA MSINGI

Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, John Wanga, akizungumza wakati wa kukabidhi madawati katika Manispaa hiyo.
…………………………………………………………………………………………………………….
Na BMG
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, imekabidhi madawati 2,600 kwa shule zote 74 za Msingi za umma zilizopo kwenye manispaa hiyo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dkt.John Pombe Magufuli la kutaka kila wilaya kumaliza tatizo la madawati ifikapo Juni 30 mwaka huu.
Madawati hayo ambayo yametengenezwa kwenye karakana ya shule ya sekondari ya wavulana ya Bwiru, ni sehemu ya mpango wa kutengeneza madawati 9,080 na hivyo kumaliza kabisa tatizo la uhaba wa madawati katika manispaa hiyo.
Akikabidhi madawati hayo hii leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilemela, John Wanga, amesema madawati hayo yametengenezwa kutokana na fedha zitokanazo na makusanyo ya ndani pamoja na michango ya wadau wengine ambapo katika mgawo wa awali, kata zote 19 za manispaa hiyo zimepewa madawati 139 kila moja.
Wanga amesema kila dawati moja lenye uwezo wa kukaliwa na wanafunzi watatu, limegharimu shilingi 98,000 ambapo manispaa ilinunua vifaa ikiwemo mbao, misumari na vyuma na kulipa gharama za ufundi zinazofikia shilingi 15,000 kwa kila dawati na kwamba madawati mengine yaliyobakia kukidhi mahitaji yanaendelea kutengenezwa kwenye karakana hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Manju Msambya, amepiga marufuku matumizi ya madawati hayo kwenye shughuli nyingine ikiwemo mikutano ya kisiasa huku akiwataka wazazi,walezi na jamii nzima kwa ujumla kutambua umuhimu wa kuchangia
juhudi za kuboresha elimu.
Renatus Mulunga ambae ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela amesema halmashauri hiyo inafanya kila jitihada kuhakikisha kwamba inatatua tatizo la upungufu wa madawati kwa shule za msingi katika manispaa hiyo, hatua ambayo itasaidia kuboresha ari ya wanafunzi kujisomea.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA

ut6TAREHE 19/06/2016 MAJIRA YA SAA 16:00HRS KATIKA BARABARA YA NYASAKA ENEO LA MADUKA TISA WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, GARI NAMBA DFP 8476 AINA YA NISSAN PICKUP LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE STANFORD KATABARO MIAKA 47 MKAZI WA KITANGIRI, LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AITWAYE ASIA ALOYCE MIAKA 66 MKAZI WA BUZURUGA NA KUSABABISHA MAJERAHA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE.
MAJERUHI ALIKIMBIZWA HOSPITALI YA MKOA WA MWANZA SEKOU TOURE KUPATIWA MATIBABU, LAKINI HALI YAKE ILIKUA SIO NZURI NA ALIFARIKI DUNIA MAJIRA YA SAA 19:00HRS WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU. MTUHUMIWA WA AJALI HIYO AMEKAMATWA YUPO CHINI YA ULINZI WA JESHI LA POLISI.
CHANZO CHA AJALI BADO KINACHUNGUZWA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MKOA WA SEKOU TOURE KWA AJILI YA UCHUNGUZI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WAKATI WOTE PINDI WANAPOKUWA BARABARA ILI KUWEZA KUZUIA AJALI NA VIFO VINAZOWEZA KUEPUKIKA, LAKINI PIA ANAWATAKA WATUMIAJIA WA VYOMBO VYA MOTO  KUZINGATIA ALAMA  NA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI.

CCM Z’BAR YAPIGA MARUFUKU UVAMIZI WA SHAMBA LAKE KILOMBERO.

images                                   
Na Is-haka Omar, Zanzibar.   
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimepiga marufuku ujenzi holela na kazi mbali mbali za kudumu zinazofanyika katika shamba la Chama hicho bila ya kujali taratibu za kisheria  lililopo Kirombero katika Wilaya ya Kaskazini “B”  Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kimesema kuna baadhi ya watu wamevamia shamba hilo na kufanya shughuli za ujenzi wa nyumba pamoja na kupanda miti ya kudumu ikiwemo minazi na miembe, na miti mingine ya kudumu  bila ya ridhaa halali ya chama hicho.
Akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,  Ndg. Vuai Ali Vuai wakati akikagua eneo na mipaka ya Shamba hilo huko Kilombero alisema CCM haitowavumilia baadhi ya watu waliofanya uvamizi wa kujimilikisha eneo halali la chama hicho bila ya kufuata taratibu za kisheria.
Alisema Shamba hilo ni urithi wa Chama cha Afro- Shiraz party (ASP), ambalo lilinunuliwa na ASP mwaka 1959 kabla ya mapinduzi matukufu ya  Januari 12, mwaka 1964 kwa ajili ya kuwapati waafrika wazalendo maeneo ya kulima na kuishi baada ya kubaguliwa  na kufukuzwa  katika mashamba ya watu wengine kwa itikadi za kisiasa.
Vuai amefafanua kwamba hakuna kiongozi yeyote ndani ya CCM mwenye mamlala ya kugawa mali yoyote ya chama bali chombo chenye mamlaka hayo ni Baraza la Wadhamini la CCM ndio linaloweza kutoa ridhaa baada ya kukaa na kujadiliana na kutoa maamuzi na siyo vinginevyo.
Ameeleza kwamba chama hicho kitaendelea kuruhusu shughuli za kijamii zifanyike katika eneo hilo zikiwemo ujenzi wa nyumba za ibada, skuli na visima vya maji kwa makubaliano na utaratibu maalum unaofaa kisheria lakini siyo kwa shughuli binafsi.
“ Watu siku hizi wamebadilika na matapeli ni wengi  tunaweza kufanya wema wa kuwaruhusu wajenge wachache baadae  na wao wakawakaribisha wengine ama kuuza maeneo hayo jambo linaloweza kuanzisha migogoro ya ardhi hali ambayo CCM haipo tayari kuona kinatokea.
Lakini pia natoa wito kwa watu wote walioanza kujenga na waliokwisha maliza ujenzi lakini hawajahamia katika nyumba zao na wanaopanda miti ya kudumu wote wasitishe zoezi hilo mpaka watakapopewa utaratibu mwingine.”, alisisitiza Vuai na kuongeza kuwa kama kuna mpango wa kubadili matumizi ya eneo hilo lazima chama kikae na kujadili kwa kina kisha kitatoa maamuzi hapo baadae.
Alitoa onyo kwa baadhi ya watu wanaofanya vitendo vya kitapeli kwa kutumia hati bandia kwa nia ya kujimilikisha mali za CCM na jumuiya zake kinyume na sheria na kuwataka kuacha kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai, na pia kwa Mwana CCM ni kosa kubwa la Kimaadili.
Aidha aliwataka viongozi na watendaji  mbali mbali wa Chama hicho nchini,   kuanza utamaduni wa kutembelea na kukagua mali zote zilizokodishwa ama kumilikishwa na taasisi ama watu ili kubaini vitendo vya udanganyifu na kuweka mali hizo katika hali ya usalama.
Alisema kwa busara na hekima za CCM itaweza kuruhusu shughuli ndogo ndogo ziendelee kufanyika katika eneo hilo zikiwemo kilimo cha mpunga, mboga mboga na mazao mengine ya muda mfupi, na kuagia viongozi wa ngazi ya mkoa Kaskazini kwa kushirikiana na viongozi wa chama na serikali katika shehia ya kilombero kuratibu vizuri shughuli zote zinazofanyika katika eneo hilo.
Aliwasihi  watu waliopewa dhamana za kulinda mali za chama kuwa makini na kuepuka kujiingiza katika vitendo vya kitapeli vinavyoweza kuhujumu mali za CCM na umma kwa ujumla.
Kwa upande wao viongozi wa CCM  katika  Shehia hiyo walisema shughuli anazotambua kufanyika katika eneo hilo ni zile za kijamii zikiwemo skuli na misima vya maji safi pamoja na baadhi ya watu wachache waliopewa kuishi katika eneo hilo kwa muda na siyo ujenzi wa nyumba za kudumu.
Viongozi hao walimuahidi  Naibu wa Katibu Mkuu huyo kutekeleza maagizo yote aliyopewa ili kuepusha migogoro ya ardhi inayoweza kutokea katika eneo hilo kwani CCM ni chama cha amani kisichotaka wananchi waishi katika matatizo.

MAAMUZI YA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) KUHUSIANA NA KUFUTA UCHAGUZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU WILAYA YA KINONDONI (KIFA)

index 
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kimesitushwa na kufadhaishwa na maamuzi yaliyofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kutangazwa kwenye vyombo mbali mbali vya habari bila ya kufuata misingi ya KATIBA na KANUNI zinazoongoza katika usimamizi wa mpira katika nchi yetu.
 
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kupitia KATIBA na KANUNI za TFF, DRFA, na KIFA kimejiridhisha kwamba maamuzi yaliyofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ya kufuta matokeo halali ya uchaguzi wa Chama Cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni uliofanyika siku ya Jumapili tarehe 12/06/2016 katika bwalo la maofisa wa polisi Oysterbay bila hayakuzingatia KATIBA na KANUNI za TFF, DRFA na KIFA.
 
Maamuzi hayo ya TFF yamevunja katiba ya TFF, DRFA na KIFA pamoja na kanuni zake ambazo ndiyo mwongozo wa mpira wetu hasa katika upatikanaji wa mamlaka za uendeshaji wa mpira katika ngazi mbalimbali za taifa, mkoa na wilaya.
 
Katiba ya TFF ibara ya 52(2) na ibara ya 52(6)(a) zinaeleza wazi kazi na majukumu ya kamati ya uchaguzi ya TFF ni kwa chaguzi za TFF na wanachama wake ambao ni vyama vya mikoa, vilabu vya ligi kuu na kusimamia uchaguzi wa Board ya ligi pamoja na kuishauri kamati ya utendaji mambo yanayo husiana na chaguzi hizo.
 
Kwa mujibu wa katiba ya TFF ya 2013 kamati yake ya uchaguzi haiwajibiki na lolote kwa vyama vya mpira wa miguu vya wilaya ambao si wanachama wa TFF. Lakini pia Ibara ya 3(i) ya kanuni za uchaguzi za TFF za 2013 inaeleza kuwa kamati ya uchaguzi ya TFF itaendesha na kusimamia uchaguzi wa TFF na Bodi ya Ligi.
Ibara ya 6 ya kanuni za uchaguzi za TFF za 2013 pia inaeleza majukumu ya kamati ya uchaguzi na katika majukumu yake hakuna popote inapoonyesha kuwa ina mamlaka ya kusimamia na kutolea maamuzi chaguzi za vyama vya mpira wa miguu vya wilaya ambao si wanachama wa TFF.
 
Kwa mujibu wa Katiba ya KIFA ibara ya 47 na kanuni za uchaguzi kipengele (b) inasema Kamati ya Uchaguzi ya KIFA itafanya kazi kwa kushirikiana na sekretarieti ya Chama na chini ya uangalizi na Miongozo ya Kamati ya Uchaguzi ya DRFA. Kwahiyo ni jukumu la kamati ya uchaguzi ya DRFA kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki.
 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kugundua kwamba Kamati yake ya Uchaguzi haina mamlaka ya KIKATIBA kuweza kusimamia chaguzi za vyama vya wilaya, miongoni mwa mapendekezo ya mabadiliko ya KATIBA waliyoleta katika Mkutano Mkuu wa TFF wa mwisho uliofanyika Tanga ni pamoja na hilo kuuomba MKUTANO MKUU wa TFF uweze kufanya hilo badiliko ili waweze kusimamia chaguzi za WILAYA lakini BAHATI mbaya marekebisho ya KATIBA hayakuweza kupitishwa na wajumbe wa MKUTANO Mkuu.
 
Katiba ya KIFA katika kanuni zake za uchaguzi 5 (h) inatamka kwamba RUFAA zote zihusuzo uchaguzi zitawasilishwa kwenye kamati ya RUFAA ya Wilaya na hatimae kama Mrufani hakuridhika basi atakata RUFAA katika kamati ya RUFAA ya Mkoa ambapo uamuzi wake utakuwa ndio wa MWISHO.
 
Baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya KIFA kutangaza matokeo ya uchaguzi huo tajwa hapo juu na kutuletea ripoti yake, mmoja wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti Bwana Thomas Mazanda aliamua kukata RUFAA katika Kamati ya uchaguzi ya Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kama katiba ya KIFA inavyoelekeza KUPINGA matokeo yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi wa KIFA. Lakini cha kushangaza wakati kamati ya uchaguzi ya DRFA ikipanga kusikiliza RUFAA hiyo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) likaitisha kikao 18/06/2016 na kuamua KUFUTA uchaguzi huo bila kufuata taratibu za KIKATIBA na KIKANUNI zinazotuongoza.
 
Kamati ya Uchaguzi ya Chama Cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni kwa mujibu wa Ibara ya 47 inaundwa na wajumbe watano. Wajumbe wa kamati hii watateuliwa na Mwenyekiti. Na Mwenyekiti wa kamati hii lazima awe ni mwanasheria na wajumbe wengine wane lazima wawe ni watu wenye ujuzi na upeo katika masuala ya michezo. Kwa mujibu wa katiba ya KIFA haina makamu mwenyekiti wala katibu wa kamati. Na maadam KATIBA inatamka wazi Mwenyekiti lazima awe mwanasheria TAFSIRI yake ni kwamba bila uwepo wa Mwenyekiti kamati haiwezi kuendelea na kazi zake kwa sababu ukiondoa Mwenyekiti wajumbe wengine waliobaki wa kamati ya KIFA hawana taaluma ya SHERIA.

WABUNGE WAJADILI MAREKEBISHO YA SHERIA MPYA YA UNUNUZI WA UMMA, DODOMA

lik2 
Kamishna wa Sera ya Ununuzi wa Umma, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, DKT. Fredrick Mwakibinga, akiwasilisha mada kwa waheshimiwa wabunge, kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410, iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa, Mjini Dodoma, jana.(Picha zote na WFM)
lik3 
Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Kushoto) na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe, wakifuatilia kwa makini mada kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410, iliyotolewa kwa waheshimiwa wabunge katika ukumbi wa Pius Msekwa, jana Bungeni Mjini Dodoma
lik4 
Baadhi wa Waheshimiwa wabunge wakifuatilia kwa makini mada iliyowasilishwa kwao kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410, iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni Mjini Dodoma Jana.
lik5 
Baadhi wa Waheshimiwa wabunge wakifuatilia kwa makini mada iliyowasilishwa kwao kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410, iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni Mjini Dodoma Jana.
lik6 
Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyaji (Prof. Maji Marefu) akichangia jambo wakati wa mjadala  kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410, wakati wa semina iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni Mjini Dodoma Jana
lik7 
Mbunge wa Nkasi, Ali Kessy, akichangia jambo wakati wa mjadala  kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410, wakati wa semina iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni, Mjini Dodoma, Jana.
lik8Mwenyekiti wa Semina ya Wabunge kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma,Sura 410, Mhe. Hawa Ghasia akiongoza mjadala kuhusu Marekebisho ya Sheria hiyo, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni, mjini Dodoma, jana.
lik9 
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchg. Peter Msigwa, akichangia jambo wakati wa mjadala  kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410, wakati wa semina iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni, Mjini Dodoma, Jana.
lik10 
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe, akifafanua jambo wakati wa semina ya waheshimiwa wabunge kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410, iliyofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni mjini Dodoma jana. Kusoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji na Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Semina hiyo, Mhe. Hawa Ghasia.
lik11 
Kamishna wa Sera ya Ununuzi wa Umma, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Fredrick Mwakibinga, akiwasilisha mada kwa waheshimiwa wabunge, kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410, iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa, Mjini Dodoma, jana.

Jamii imetakiwa kuwahamasisha vijana wa kiislamu kusoma Qurani tukufu katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani.

qr1Mwanafunzi wa madrasa AL-Mustakima Zahra Mohamedi akipokea zawadi  shilingi laki moja na thelathini na tano ( 135,000) kwa kuibuka mshindi wa kwanza  wa kusoma na kuihifadhi juzuu tano kati ya thelathini  katika kitabu cha Quaran. ( Picha na Tamimu Adam).
qr2Mwanafunzi wa Madrasa AL-Mustakima Rashid Kimweli akisoma  Quaran katika mashindano ya kusoma na kuhifadhi Quaran  yaliyofanyika  mbagala bucha, jijini Dar es salaam. Mashindano hayo yalishirikishi madrasa nne kutoka yombo dovya, mbagala bucha, na mtoni kijichi.  ( picha na Tamimu adam.)
qr3 
Mwalimu mkuu wa Madrasa AL- Mustakima Ustaadhi  Hassani Seleiman akimtunza fedha ustaadh Iddrisa wakati wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Quran  yaliyoandaliwa na Madrasa AL mustakima ya Mbagala bucha jijini  Dar es salaam. ( picha na Tamimu Adam.)
……………………………………………………………………………………….
Na. Tamimu Adam
Wazazi na walezi wa kiislamu wametakiwa  kuenzi na kuihifadhi quarani tukufu  na kuipa heshima ya aina yake kwa kuwahamasisha watoto wao kushiriki katika mashindano ya kusoma na kuifadhi Quran  ili kuwawezesha kufahamu vizuri uislamu na  kuwa muongozo katika maisha yao ya kila siku hapa dunia na kesho ahera.
 Hayo yalisemwa na Ustaadhi Iddrisa kutoka Kigoma  wakati wa mashindano ya kusoma na kuifadhi qurani yaliandaliwa na Madrasa  ya AL-Mustakima iliyopo mbagala  bucha jijini, Dar es salaam ambapo  watoto wa kiislamu takribani kumi (10) wenye umri kati ya miaka sa sita hadi kumi na tatu  wa madrasa  nne  ambavyo ni Madrasa  Tul – Mustakima  ya yombo dovya na mbagala bucha, madrassa Tul- ukutani  na madrassa Tul Ismailia ya mtoni kijichi.
Naye  Mwalimu mkuu wa Madrasa ya AL- mustakima  ambayo ndio mratibu wa mashindano hayo Ustaadhi Hassani Suleimani  alisema  mashindano hayo yalishirikisha   wanafunzi kumi ambao waligawanywa katika makundi makuu mawili  kundi la kwanza ni wanafunzi watano kutoka vyuo vyote nne ambao walisoma na kuifadhi juzuu mbili na kundi la pili ni kwa wanafunzi ambao walisoma na kuifadhi juzuu tano.
Aidha ,  aliongeza kuwa lengo kuu la mashindano hayo ni kuwafundisha vijana kusoma na kuhifadhi kitabu cha mwenyezi mungu, kuipenda qurani na kuitumia katika maisha yao yote  pamoja na kuwafundisha maadili ya kiislamu  na maamurisho yake yote kwa waislamu. Aliongeza kuwa mashindano hayo yalisimamiwa na majaji watatu kutoka mbande ambao kwa ujumla walikuwa wanaangalia  vigezo mbalimbali ikiwemo namna ya kusoma na kutamka maneno ya quaran kwa usahihi.
Kwa upande wake  Imamu wa Msikiti wa mbagala charambe  Sheikh  Adam Mikidadi  ambaye alikuwa miongoni mwa majaji wa mashindano hayo alisema kuwa mashindano yalienda vizuri  ambapo yalifanyika kwa kiwango kilichotarajiwa,  washiriki walisoma na kutamka quarani vizuri kabisa na kuweza kufikia vigezo vya mashindano kwa asilimia 85.
Sheikh aliwataka washiriki wote kuongeza bidii mwakani ili waweze kufikia asilimia 100 na kuwa mahiri katika kusoma, kuhifadhi  na kukuza uislamu ndani ya jamii.
Pia aliwataka wazazi na walezi kuhamasika  na kuisoma quaran tukufu ili iwe muongozo wao katika maisha yao yote na kwa wale wenye uwezo wawe na tabia ya kujitolewa kudhamini mashindano ya kusoma na kuhifadhi kitabu cha mwenye mungu.
Washiriki wa mashindano hayo walipewa zawadi mbalimbali ambapo mshindi wa kwanza  Zahara Mohamed alizawadiwa shilingi laki moja na thelathini kwa kusoma na kuhifadhi juzuu 5 kati ya juzuu thelathini na wa pili  alizawadiwa fedha taslimu elfu themanini, tano na watatu alizawadiwa shilingi elfu sitini na tano na wengine walipewa elfu arobaini.

BENKI YA DIAMOND TRUST YAANZISHA KAMPENI MAALUMU KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

NA Imma Matukio Blog
BENKI ya Diamond Trust Tanzania (DTBT) imeanzisha kampeni maalum kupitia mitandao ya kijamii ambayo inalenga kutoa uelewa juu ya huduma wanazotoa kwa wateja na wadau mbalimbali. Mbali na hayo kampeni hiyo iliyopewa jina la ‘miaka 70 jiunge nasi ushinde’ imedhamiria kuwapa wadau wake zawadi mbalimbali hususani wanaowafuatilia kupitia mitandao ya kijamii ukiwemo Facebook.
 Picha: MKUU wa Kitengo cha ICT kutoka Benki ya Diamond Trust Tanzania,Stella Mosha (kushoto) akitoa zawadi kwa mmoja wa washindi wa kampeni yao ya ‘miaka 70 jiunge nasi ushinde’,Said Mpanju kutoka KIBAHA mkoani Pwani,mwishoni mwa wiki.Picha na DTBT 9( Na Mpiga Picha Wetu)

No comments:

Post a Comment