Pages

Wednesday, June 1, 2016

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI ATEMBELEA MRADI WA UZALISHAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA GEREZA MTEGO WA SIMBA NA GEREZA KUU LA WANAWAKE KINGOLWIRA

kat1 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akipokea salaam kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Magereza, ACP. Shaban Kitolo mara tu baada ya kuwasili katika Gereza Mtego wa Simba katika ziara yake ya kikazi Mei 31, 2016, Mkoani Morogoro(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, CGP, John Casmir Minja.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, CGP, John Casmir Minja(kulia) akiongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Projest Rwegasira kuelekea katika Shamba la uzalishaji wa ng’ombe wa maziwa la Gereza Mtego wa Simba.
kat3 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akiangalia kundi la ng’ombe wa maziwa katika shamba la uzalishaji wa ng’ombe wa maziwa Gereza Mtego wa Simba, Mkoani Morogoro. Gereza hilo hivi sasa linafuga ng’ombe wa maziwa 496.
kat4 
Kundi la ng’ombe wa maziwa wanaofugwa katika shamba la uzalishaji Mifugo Gereza Mtego wa Simba, Kingolwira Mkoani Morogoro wakiwa malishoni kama wanavyoonekana katika picha.
kat5 
Wafungwa wa Kike katika Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira(walioketi) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(meza Kuu) alipofanya ziara ya kikazi gerezani hapo ili kujionea uendeshaji wa Magereza hapa nchini.
kat6 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akionja chakula cha Wafungwa katika Jiko la Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira, Mkoani Morogoro alipofanya ziara ya kikazi ili kujionea Uendeshaji wa Magereza hapa nchini(kulia) ni Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira, ACP. Loyce Ruhembe(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP. John Casmir Minja.
kat7 
Sajini Taji wa Jeshi la Magereza, Sarah Kabunda ambaye ni Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Ufugaji Kuku katika Gereza Kuu la Wanawake Kongolwira akitoa maelezo ya Kitaalam kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira namna Ufugaji kuku unavyofanyika(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Serikali kushirikiana na kampuni ya TING kuboresha mapato ya Uwanja wa Taifa.

tin1 
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge akizungumza na wawakilishi kutoka Kampuni ya TING(hawapo pichani) kuhusu kushirikiana na Serikali kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
tin2 
Afisa Mtendaji Mkuu kutoka TING Mch. Dkt. Veron Fernandos akifafnua jambo katika kikao kati ya kampuni yake na Serikali kilicholenga kushirikiana katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
tin3 
Mkuu wa Masoko kutoka TING Bi. Bernice Hannah akionesha jinsi kampuni yake itakavyoweka miundombinu ya kuweka matangazo ndani ya uwanja wa taifa katika kikao baina ya Serikali na kampuni ya TING kushirikiana katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
tin4 
Baadhi ya maafisa wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakifatilia kikao baina ya Serikali na kampuni ya TING kushirikiana katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
…………………………………………………………………………………………………………….
(Picha na Raymond Mushumbusi WHUSM)
Serikali imeanza majadiliano na kampuni ya TING katika kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa kupitia matangazo uwanjani hapo.
Akizungumza hapo jana wakati wa kikao kati ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na kampuni hiyo, Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge amesema kuwa Serikali imefarijika kupata maombi hayo kutoka kampuni ya TING ya kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa kupitia matangazo ambayo yatawekwa katika maeneo ya uwanja huo.
“Ndugu zetu TING wamekuja na wazo zuri sana na tumelipokea na tunaahidi kuliangalia kwa jicho la tatu kwani ni fursa ya pekee kwetu, sio kuboresha mapato tu bali kutangaza uwanja wetu na kuendeleza michezo kwa ujumla” alisema Bw. Nkenyenge.
Aliongeza kuwa ni wakati sasa wa Serikali pamoja na Wananchi kufaidika na uwanja wao ambao ni wa kipekee katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwani fursa hiyo itasaidia pia kuendeleza Kijiji cha Michezo Changamani ambao pia ni mpango wa Serikali katika kuendeleza sekta ya michezo nchini.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu kutoka TING Mch. Dkt. Veron Fernandos amesema kuwa kampuni yake itatoa ushirikiano kwa Serikali kupitia Wizara na ni azma yao kuona wananchi wanaona faida ya kuwa na uwanja wa kisasa ambao utawaletea mafanikio katika maendeleo ya michezo nchini.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Esther Yonael ameipongeza kampuni ya TING kwa kuona fursa na kuitumia kwani kuna kampuni nyingi zinaweza kuwa ziliona hiyo fursa hii lakini sikakosa uthubutu wa kuleta maombi Wizarani kushirikiana katika suala hilo ambalo linafaida kwa pande zote mbili.
Aidha, Mkuu wa Masoko kutoka TING Bi. Bernice Hannah ameihakikishia Serikali kuwa wamejipanga vizuri na wamefanya utafiti wa kina wa mradi huo na kuona kuwa unawezeka ukafanyika na kuleta mabadiliko katika sekta ya michezo nchini.
Kampuni ya TING imedhamiria kushirikiana na Serikali katika kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa na imejipanga kuwekeza Shilingi Billioni moja kwa miaka minne katika miundombinu na wataalam.

WASHIRIKI MISS ILEMELA 2016 WATEMBELEA KITUO CHA UTAMADUNI BUJORA KILICHOPO MAGU MKOANI MWANZA.

Washiriki wa Shindano la kumsaka mlimbwende katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza la MISS ILEMELA 2016 (pichani), wakionyesha upendo wao kwa 102.5 Lake Fm Mwanza, walipotembelea Kituo cha Utamaduni Bujora kilichopo katika Wilaya ya Magu mkoani Mwanza siku ya jana. 
……………………………………………………………………………………………
Walimbwende hao wamepiga kambi katika hotel ya “New Bujora Point” iliyopo Magu ili kujinoa na fainali za shindano hilo linalotarajiwa kufanyika jumamosi ijayo June 4, 2016 katika viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza, ambapo kiingilio itakuwa shilingi 10,000 kawaida na shilingi 30,000 kwa VIP huku wasanii mbalimbali wakiongozwa na Ney Wa Mitego wakitarajiwa kudondosha burudani kali.

Pamoja na mambo mengine, lengo la washiriki hao wa shindano la Miss Ilemela 2016 ambao mwaka huu ni 16, ni kutembelea kituo hicho ni kujifunza masuala mbalimbali kuhusiana na utamaduni wa kabila la Kisukuma.

NAPE AWASHA UMEME KATA YA NACHUNYU

Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Nachunyu kwenye mkutano maalum wa kuwasha umeme kijijini hapo ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kila jambo aliloliahidi litakamilika mapema.
Wakazi wa kijiji cha Nachunyu jimbo la Mtama wakiwa wamejitokeza kwa wingi kushuhudia uwashaji wa umeme kijijini hapo uliofanywa na Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikata utepe kuashiria uwashaji wa umeme katika kata ya Nachunyu.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akifungua kitambaa kama ishala ya uwashaji wa umeme katikakata ya Nachunyu.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwasha taa kuashilia kuwashwa umeme katika kata ya Nachunyu.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wananchi wa Nachunyu mara baada ya kuwasha umeme katika kata ya Nachunyu.

No comments:

Post a Comment