Pages

Friday, June 24, 2016

Bunge limepitisha muswada wa sheriia ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Mafisadi

12243064_1016356178428376_4208274545155299439_n 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju.
—————————————————-
Na: Lilian lundo – MAELEZO – Dodoma
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka 2016 ikiwemo kuanzishwa kwa Mahakama ya Mafisadi.
Muswada huo umewasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju ambao ulikuwa na marekebisho ya sheria tano ambazo ni sheria ya mamlaka za Mahakama ya Rufaa, sheria ya Makosa ya Uhujumi Uchumi, sheria ya usimamiaji haki na matumizi ya sheria, sheria ya mahakama za mahakimu pamoja na sheria ya rufaa za kodi.
“Ili kutekeleza ahadi ya Serikali ya kuanzishwa Mahakama Maalum kwa ajili ya kushughulikia makosa ya rushwa (ufisadi) na uhujumu uchumi, imeonekana kuwa kuna umuhimu wa kurekebisha sheria hii kwa kuanzishwa  Divisheni Maalum ya Mahakama Kuu ambayo itakuwa na Majaji pamoja na watumishi wengine ambao wanahusika moja kwa moja na kesi za rushwa na uhujumu uchumi tu,” alifafanua Mhe. Masaju.
Mwanasheria Mkuu aliendelea kwa kusema kuwa, makosa yatakayofunguliwa katika mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ni yale ambayo thamani yake haipungui shilingi bilioni moja, lengo la kuweka ukomo huo kwa baadhi ya makosa ni kuiwezesha Divisheni hiyo kusikiliza makosa makubwa ya rushwa na uhujumu uchumi na kuacha makosa madogo yasiyofikia thamani hiyo kuendelea kusikilizwa mahakama za wilaya, hakimu mkazi au mahakama kuu.
Aidha, marekebisho mengine yanayopendekeza katika sheria hiyo ni pamoja na kuboresha masharti ya kutoa dhamana pale kosa linapohusisha fedha au mali ambayo thamani yake inazidi shilingi milioni kumi ambapo sheria ya sasa  inaeleza kuwa masharti ya dhamana kwa kosa kama hilo ni kutoa fedha tasilimu (cash deposit) inayolingana na nusu ya thamani ya mali ya kosa husika na thamani ya nusu inayobaki itolewe kwa njia ya bond.
Muswada unapendekeza kwamba masharti yaboreshwe ili pale mshtakiwa anapokuwa hana fedha inayotakiwa mahakamani basi aruhusiwe kutoa mali hiyo na kama mali hiyo haihamishiki basi hati au ushahidi unaothibitisha umiliki wa mali hiyo utolewe Mahakamani.
Marekebisho mengine ni pamoja na adhabu kwa makosa ya rushwa na uhujumu uchumi iwe ni kifungo gerezani kisichopungua miaka 20 na kisichozidi miaka 30 au vyote kwa pamoja.
b3 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akijibu miongozo ya wabunge mapema leo mara baada ya Kipindi cha maswali na majibu Bungeni Mjini Dodoma.
b4 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo akitoa maelezo wakati wa kipindi cha maswali na majibu kuhusu mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa wananchi wanapata majisafi na salama katika Halmashauri zote hapa nchini.
b2 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki akiteta jambo na Waziri wafedha na Mipango Dkt. Philip Mpango leo Bungeni Mjini Dodoma.
b6 
Wanafunzi wa Chuo Kikuucha Dodoma (UDOM) wakiongozwa na Afisa Habari wa Bunge  Bw. Deonisius Simba (wa kwanza kushoto) katika ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Bunge kwania ya kujifunza shughulizi na zotekelezwa na Bunge.
b5 
Walimu na wanafunzi washule ya Marangu Hills Academy iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati waziara ya kujifunza jinsi Bunge linavyotekeleza majukumu yake.

NHC YAKUTANA NA WADAU WA SEKTA YA UJENZI KUPITIA MRADI WA ECO RESIDENCE KINONDONI HANANASIFU JIJINI DAR ES SALAAM

1Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumkba la Taifa la Tanzania (NHC), Issack Peter  akitoa mada kuhusu utendaji wa Shirika hilo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa  kujifunza utekelezaji  mradi wa ECO Residence uliojengwa na NHC Kinondoni Hananasifu na kujadili mapendekezo ya mradi huo.
2 
Prof  Ninatubu  Lema ,kutoka Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa  kujifunza  utekelezaji wa  mradi ECO Residence na kujadili mapendekezo ya mradi huo.
3 4 
Wadau mbalimbali wa sekta ya ujenzi wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano wa  kujifunza utekelezaji  mradi wa ECO Residence na kujadili mapendekezo ya mradi huo.
5Wafanyakazi wa Shirika la Nyumkba la Taifa la Tanzania (NHC) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika hilo, Issack Peter  wakati akitoa ufafanuzi kuhusiana na malengo ya uendelezaji wa mradi huo.
6Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumkba la Taifa la Tanzania (NHC), Issack Peter akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kujifunza utekelezaji  mradi wa ECO Residence na kujadili mapendekezo ya mradi huo.
7Muonekano wa Jengo  linavyoonekana kwa nje
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG.

BENKI KUU TANZANIA TAWI LA MBEYA (BOT) YAFUTURISHA KATIKA KUSHEREKEA MIAKA 50 YA KUANZISHWA KWA BENKI HIYO

Waumini wa dini ya kiislamu Mkoa wa Mbeya pamoja na wadau mbalimbali wakifuturu futali iliyoandaliwa na benki Kuu ya Tanzania (BOT)Tawi la Mbeya ambapo benki hiyo ipo katika kuadhimisha miaka ya hamsini ya kuanzishwa kwake.Picha E.Madafa na D.Nyembe
Wageni waalikwa ,viongozi wa serikali na viongozi wa dini mbalimbali mkoani Mbeya  wakipita kupata  futari kwenye ukumbi wa benki kuu Tanzania( BOT) tawi la Mbeya .
Mkurugenzi wa benki kuu Tanzania( BOT) tawi la mbeya  Jovenant Rushaka akiongoza kupata futari.
Wafanyakazi benki kuu Tanzania tawi la Mbeya wakipata futari
Wageni waalikwa Viongozi wa serikali na wadau mbalimbali  wakibadilishana mawazo pamoja na kupata futari iliyoandaliwa na benki kuu Tanzania(BOT) kama sehemu ya kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwa benki hiyo.
wadau wakipata futari.

No comments:

Post a Comment