Pages

Tuesday, June 28, 2016

BENKI YA CRDB YAFADHILI UJENZI WA KITUO CHA MAWASILIANO CHA JESHI LA POLISI

Jiwe la Msingi la Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi lililowekwa na Rais Dk. John Magufuli. Kituo hicho kimefadhiliwa na Benki ya CRDB kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 300. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto) akiteta jambo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Esther Kitoka.
Brass Band ya Polisi ikitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akisalimia na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (wa kili kulia) akifurahia jambo na Naibu wake (kulia), IGP,Ernest Mangu, wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisalimia na Rais John Magufuli.

THE SILOAM CHURCH LAWATIA BARAKA WAANDSHI WA HABARI KUBARIKI KAZI ZAO ZA KILA SIKU

 
 Wakili wa Mungu wa Kanisa la The Pool of Siloam, Elisha Eliya akiendesha sala maalum ya kuuombea amani tanzania na pia kuwatia baraka Waandishi wa habari, ambao walihudhuria kwenye ibada iliyoongozwa na kiongozi huyo wa The Siloam, leo katika Kanisa hilo, Mbezi Beach, eneo la Makonde Dar es Salaam..
 Baadhi ya waumini na Waandishi wa habari wakiwa kweye ibada hiyo.
 Waumini walifanya Ingagement ya ndoa wakitekeleza nadhiri hiyo wakati wa ibada hiyo
 Waumini walifanya Ingagement ya ndoa wakitekeleza nadhiri hiyo wakati wa ibada hiyo
 Waumini walifanya Ingagement ya ndoa wakitekeleza nadhiri hiyo wakati wa ibada hiyo
 Waumini walifanya Ingagement ya ndoa wakitekeleza nadhiri hiyo wakati wa ibada hiyo
 Waumini walifanya Ingagement ya ndoa wakitekeleza nadhiri hiyo wakati wa ibada hiyo

MTANZANIA ALIYEIBUKA MSHINDI WA KWANZA AFRIKA NA WA SITA DUNIANI KATIKA MASHINDANO YA KUSOMA QUR-AN KWA NJIA YA TAJ-WEED AWASILISHA TUNZO KWA MZEE MWINYI LEO

Mwanazuoni kutoka Kondoa, Tanzania, Sheikh Rajay Ayub ambaye ameibuka mshindi wa kwanza Afrika na wa sita Duniani katika mashindano ya 37 ya Kimataifa ya usomaji Qur-an kwa njia ya Taj-weed, yaliyofanyika mwezi uliopita nchini Iran akikabidhi tuzo zake kwa Rais Mstaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, wakati wa hafla ya kumpongeza iliyofanyika leo, kwenye Viwanja vya Makao Makuu ya Baraza la Waislam Tanzania-BAKWATA, Kinondoni, Dar es Salaam. Kulia ni Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Aboubakary Bin Zubeir na Watatu kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kondoa, Alhaj Omary Kariati ambaye aliratibu hafla hiyo. KWA PICHA KEM-KEM ZA HAFLA HIYO>>BOFYA HAPA

MCHEZAJI BORA WA UMMISETA MUSA SAID KUONDOKA JUMATANO JUNI 28, 2016 KWENDA NCHINI UFARANSA

 Meneja Msaidizi wa Chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga, akizungumza na waandishi wa habari kuwaelezea juu ya safari ya mchezaji Musa Said anayetarajia kuondoka Jumatano ya Juni 28, 2016 kwenda nchini Ufaransa kwenye kambi ya kimataifa ya Copa Coca-Cola. Pembeni ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja, Mchezaji Musa Said Bakari na Mwalimu wake wa Kibasila.
Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

Na Devotha Kiwelo.
MCHEZAJI bora wa mashindano ya UMMISETA yaliyofanyika mwaka jana mkoani Mwanza, Said Musa Jumatano ya Juni 28, 2016 kuelekea Ufaransa katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca – Cola ambayo imeandaliwa na kampuni ya kinywaji cha Coca – Cola .
Akizungumza jijini Dar es Salaam katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja alisema udhamini wa kampuni ya Coca – Cola imetambua umuhimu wa michezo hivyo kukubali kudhamini michezo kupitia shule za sekondari ili kukuza vipaji vya wanamichezo chipukizi ambao wanamalengo makubwa katika kuitumikia nchini yao kupitia michezo.
“Kwetu sisi imekuwa faraja kwa kuibua kipaji kichanga ambacho kitakuwa ni mfano wa kuigwa kama ilivyo kwa Samatta ambaye amekuwa kioo kwa jamii ya wanamichezo na hivyo kuomba makampuni mengine kujitokeza kwa ajili ya kusaidiana na Coca – Cola”, alisema.
Kiganja alimtaka Musa kuzingatia nidhamu kipindi chote atakachokuwepo kwenye kambi ili kujijengea heshima katika kukuza kipaji chake kwa kipindi chote ambacho atakuwa chini ya walimu wageni ambao hajawahi kukutana nao na hiyo italeta heshima nchini.
Kwa upande wa Meneja msaidizi wa chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga, alisema wamefurahi kupata nafasi ya kudhamini mashindano hayo kwa kuwa ndiyo mara yao ya kwanza na imefanikiwa kufikia malengo ya kupata mchezaji ambaye atakuwa muwakilishi wa Tanzania katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca – Cola iliyopo jijini Paris nchini Ufaransa.
Alisema Musa ataondoka kwa kupitia Nairobi kwa kuwa kozi inaanza kesho na kumalizika Julai 4, hivyo aliwataka wanafunzi wengine kujituma ili kufikia malengo kama aliyofikia Mussa.
“Sisi kama kampuni imekuwa ni faraja kwani tutakuwa tumeitangaza nchini kwa kupitia Mussa na hii itakuwa ni muendelezo katika michezo inayoendelea,”alisema.
Mussa ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Kibasila ambaye alizaliwa Agosti 11, 2000 huku akiwa ni mchezaji tegemeo katika timu ya shule na Mkoa wa Temeke ambapo walitumia jina hilo kwa kupitia michezo.

Waziri Nape Nnauye azindua Studio ya Redio ya Jamii katika Chuo Kikuu Huria Tanzania.

N5 
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa ameongozana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda kwenda kuzindua Studio ndani ya Chuo hicho 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
N3 
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akikata utepe wakati wa Uzinduzi wa Redio ya Jamii ya ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
N1 
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akijadiliana jambo na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa toka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues wakati wa Uzinduzi wa ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
N2 
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa ndani ya Studio ya ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ akijibu baadhi ya maswali toka kwa Waandishi wa Habari mara baada ya kuizindua rasmi 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
N4 
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa ndani ya Studio ya ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari mara baada ya kuizindua rasmi 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
……………………………………………………………………………….
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Waziri wa Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amezindua studio ya redio ya jamii ya ‘Community Media Network of Tanzania’ (COMNET)   katika Chuo kuku Huria( OUT )  itakayotumika kusambaza habari maeneo yenye uhaba wa redio.
Uzinduzi huo umefanyika   leo jijini Dar es Salaam,ambapo Mhe. Waziri  amesema kuwa studio hiyo itasaidia  idadi kubwa ya wanachi wanaoishi vijijini kupata habari kutoka Serikalini na kutoa mrejesho wa kile watakachosikia kwa urahisi.
“Ni Studio muhimu kwa ajili ya kusambaza demokrasia  kwa watu hasa wale waliopo vijijini kwa vile redio nyingi bado hazijawafikia”Alisema Mhe.Nape.
Aidha amewataka wanafunzi wa taaluma ya uandishi wa habari na  mawasiliano kwa umma katika  chuo  hicho kutumia studio hiyo kujifunza zaidi kwa vitendo na kuzingatia maadili ya uandishi wa habari kwa kuandika habari zenye ukweli kutoka vyanzo sahihi ili kutoa ujumbe wenye manufaa mazuri kwa jamii.
Kwa upande wake Makamu mkuu wa Chuo hicho Prof. Elifas Bisanda amesema studio hiyo imeanzishwa kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni(UNESCO)  kwa lengo kutoa elimu kwa jamii ambayo imekuwa haipati habari kwa urahisi.
Amewataka wanahabari na wananchi kwa ujumla   kufikisha habari katika studio hizo kwa kuwa inatumia njia ya haraka na rahisi katika kufikisha ujumbe kwa kushirikiana na redio mbalimbali za jamii.
 Naye mwakilishi kutoka Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia Elimu,Sayansi,na Utamaduni(UNESCO) Bi. Zulimira Rodrigues  amesema studio ya redio ya ‘Community’ ipo kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii kuhusu maendeleo ya wanawake na vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.
Mpaka sasa Shirika hilo limefanikiwa kuanzisha redio za jamii katika baadhi ya mikoa ya Tanzania bara ambayo ni Mwanza,Arusha na Tanga na katika baadhi ya maeneo ya Unguja na Pemba.

No comments:

Post a Comment