Pages

Sunday, May 1, 2016

WAFANYAKAZI WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF WASHIRIKI SHEREHE ZA MEI MOSI MKOA WA DAR ES SALAAM.

index 
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakiwa katika maandamano wakipita mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (hayupo pichani) wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Mafoto Blog
index1

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, WCF, WASHIRIKI SHEREHE ZA MEI MOSI KWA MARA YA KWANZA

 Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, wakishiriki matembezi yakilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani  (May day), hapa matembezi yakiwa barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, Mei 1, 2016.

 Wafanyakazi
wa WCF wakipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuruwakati wa matembezi ya
kilele chasiku ya wafanyakazi Duniani
 Matembezi yakiwa yameingia Uwanja wa Uhuru
 Matembezi yakipita barabara ya Chang’ombe
 Matembezi yanaendelea, hapa ni barabara ya Uwanja wa Taifa  mkabala na ofisi za TAKUKURU wilaya ya Temeke
 Matembezi yakiendelea barabara ya Chang’ombe
 Matembezi yakiwa barabara ya Uwanaja wa Taifa
 Baadhi ya wafanyakazi wakiwa kwenye matembezi hayo, hapa nibarabara ya Chang’ombe
 Baadhi
ya wafanyakazi wa WCF, wakimsikiliza mwenzao aliyevaat-shirtyenye ujumbe maalum
wa Mfuko huo “WCF inatoa Fidia Stahiki kwa Wafanyakazi wote wa Sekta ya Ummana
Binafsi”.
Mkuu wa Mkoa wa Dar esSalaam, Mh. Paul Makonda, (kulia), akiteta jambo na kiongozi
wa Shirikisho la Wafanyakazi mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa kilele cha May
Day uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wafanyakazi wa WCF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha
matembezi hayo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa WCF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha
matembezi hayo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Nyuso za furaha baada ya matembezi

NCCR, CUF NA TLP VIKO ICU SHAKA ALONGA

SH1
Picha ikionyesha kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anapokea kadi ya chadema na kumkabidhi ya CCM alikuwa mgombea wa udiwani kata ya Kisimani kupitia Tiketi ya chadema Amani John  Mgonja Mara baada ya kuhamia Ccm.
SH2
Na Woinde Shizza , Kilimanjaro
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM )umesema muda mfupi ujao  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kitaifuata mahali viliko   vyama vya  NCCR-Mageuzi, TLP na Chama cha Wananchi  (CUF ) kwa sababu kimejidhuru kukubali   kukumbatia mafisadi .
Aidha umoja huo umevitaja  vyama hivyo sasa  vinachechemea, vinaishi kwa matimaini   na viko mahututi kwani  wakati wowote  , ugonjwa uliovitafuna vyama hivyo utakishambiulia  chadema.

WAHALIFU WAWEKEWA MKAKATI MZITO DODOMA.

JA6 
Na. Frank Geofray – Jeshi la Polisi, Dodoma
Katika kuhakikisha wahalifu hawapati nafasi ya kutamba nchini,  makamanda wa Polisi wa mikoa, wakuu wa upelelezi na waendesha mashtaka wameazimia kuboresha ushirikiano wao katika kufanikisha kesi za wahalifu pindi zinapofikishwa mahakamani ili waweze kupewa  adhabu kali kwa mujibu wa sheria.
Hayo yamo katika maazimio ya watendaji hao wa haki jinai nchini katika kikao kazi cha siku mbili kilichofanyika  mkoani Dodoma na kuwashirikisha makamanda wa polisi wa mikoa,  mawakili wafawidhi wa mikoa  na wakuu wa upelelezi wa mikoa.
Kikao hicho kilikuwa chini ya uenyekiti wake Mkuu wa Jeshi la Polisi,  IGP Ernest Mangu pia kilihudhuliwa na mkurugenzi wa Mashtaka nchini, DPP  Biswalo Mganga, Makamishina wa Polisi, pamoja na taasisi mbalimbali zinazohusika na upelelezi na uendeshaji wa mashtaka.
Wapelelezi hao na waendesha mashtka walisema wataendeleza  program za mafunzo ya pamoja katika ngazi ya mkoa, kufanya vikao vya mara kwa mara ili kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili  na kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano lengo likiwa kuharakisha upelelezi  na kutoa haki kwa watuhumiwa.
Aidha,  wajumbe hao wa haki jinai wameazimia pia kukabiliana na changamoto ya ucheleweshaji wa upelelezi  wa kesi ambapo wamekubaliana kwa pamoja kuzifikisha mahakamani kesi zote zenye ushahidi wa moja kwa moja ili kuondokana na kesi kuchua muda mrefu na kuleta malalamiko kwa wananchi.
 
 

Vyama Vya Siasa Vimekutana Kujadili Mapendekezo ya Mfumo Wa Utatuzi wa Migogoro Ndani na Baina ya Vyama


MS1Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini Mhe. Peter Kuga Mziray akifafanua jambo wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam  . Kulia ni Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa na Mhe. Vuai Ali Vuai, Makamu Mwenyekiti wa Baraza .
MS3 
Bw. John Cheyo  mmoja wa wajumbe wa Baraza la vyama vya siasa akichangia hoja  wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam.
MS2 
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wakifuatilia mjadala wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam.
MS4 
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wakifuatilia mjadala wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam. 
MS5 
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wakifuatilia mjadala wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam. 
MS6Picha ya Pamoja ya Wajumbe wa Baraza la vyama vya Siasa baada ya kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam. 

Wadau wa michezo waombwa kuendelea kujitokeza na kuwekeza katika mchezo wa Riadha

WAM1 
Washiriki wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20 kutoka Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mashindano hayo kufunga rasmi jana jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija,WHUSM
WAM2 
Naibu Waziriwa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akisalimiana na Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Riadha Afrika Mashariki Mhandisi Sadick Ibrahim (katikati) jana jijini Dar es Salaam wakati wa ufungaji wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20 jana jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Makamu wa Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) William Kallaghe.
WAM3
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akiwapungia mkono washiriki wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20 alipokuwa mgeni rasmi wakati wa ufungaji wa mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam.Kulia ni Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Riadha Afrika Mashariki Mhandisi Sadick Ibrahim na kushoto ni Makamu wa Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) William Kallaghe.
WAM4 
Naibu Waziriwa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akisalimiana na Makamu wa Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) William Kallaghe jana jijini Dar es Salaam wakati wa ufungaji wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20.Katikati ni Katibu wa Naibu Waziri Bibi. Anna Nkinda.
WAM5 
Makamu wa Raisi wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. William Kallaghe akisoma taarifa fupi juu ya mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20 mbele ya Naibu Waziriwa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura(kulia mwenye miwani) jana jijini Dar es Salaam.
WAM6 
Baadhi ya washiriki wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20 kutoka nchi mbalimbali wakipita mbele ya Naibu Waziriwa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura(hayupo pichani) alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufungaji wa mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam.
WAM8 
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (wapili kushoto) akiimba wimbo wa Taifa la Tanzania wakati hafla ya ufungaji wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20  jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Makamu wa Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) William Kallaghe,Raisi wa Shirikisho la Mchezo wa Riadha  Afrika Mashariki Mhandisi Sadick Ibrahim na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo upande wa Miundombinu Alex Nkenyenge.
WAM9 
Washiriki wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20 kutoka nchi mbalimbali wakiimba wimbo wa Taifa la Tanzania wakati wa  hafla ya ufungaji wa mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam.
WAM10 
Naibu Waziriwa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akimpongeza mmoja wa washiriki kutoka Tanzania ambao wamekuwa washindi wa kwanza kwa wanawake  mbio za relay mita mia nne mara nne alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufungaji wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20 jana jijini Dar es Salaam.
WAM11 
Naibu Waziriwa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akimvalisha medali mmoja wa washiriki kutoka Kenya ambao wamekuwa washindi wa kwanza kwa wanaume mbio za relay mita mia nne mara nne  alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufungaji wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20 jana jijini Dar es Salaam.
WAM13 
Mshindi wa kwanza wa mbio za mita 200 katika mashindano ya Afrika Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20 Bw. Ally Khamis Ibrahim kutoka Zanzibar ( katikati) na akiwa katika jukwaa moja na washindi wa pili na watatu ambao wate wanatokea nchini Kenya.Mshindi wa kwanza wa mbio za mita 200 katika mashindano ya Afrika Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20 Bw. Ally Khamis Ibrahim kutoka Zanzibar ( katikati) na akiwa katika jukwaa moja na washindi wa pili na watatu ambao wate wanatokea nchini Kenya.
StarTimes yawaletea wateja wake tamthiliya ya ‘Scars’
ST1 
Meneja wa Maudhui na Vipindi wa StarTimes Tanzania, Bi. Paulina Kimweri akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamthiliya ya ‘Scars’ itakayoanza kuonekana siku ya Jumatatu ya Mei 2, 2016 kupitia chaneli ya StarTimes Swahili. Akimsikiliza kwa makini katika uzinduzi huo uliofanyika katika ofisi za kampuni hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Uhusiano wa Umma, Bw. Muddy Kimwery.
ST2………………………………………………………………………………………………………….
  •      Ni tamthiliya inayohusu simulizi na visa vya kweli katika maisha ya watu.
  • ·         Itaonekana katika chaneli ya StarTimes Swahili, mahususi kwa vipindi vinavyotumia lugha ya Kiswahili inayoonekana pia nchini Kenya.
  • ·         StarTimes yahamasisha watanzania kuchangamkia fursa kwa kutengeneza filamu na tamthiliya ili ziweze kuonekana kupitia chaneli hiyo ili kupanua wigo wa mashabiki wao

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Rose Tweve AKUTANA NA WALEMAVU WA MACHO

B1 
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (kushoto) akisalimiana na mkazi wa Iringa mjini, Rebeca Mkwavi ambaye ni mlemavu wa macho jana alipokutana nao katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa mjini, mbunge huyo alitoa msaada wa Sh 1 milioni kwa wanawake walemavu 20  kwa ajili ya kuanzisha miradi ya kiujasiriamali. picha na Mpigapicha Wetu. B3Mkazi wa Iringa Mjini ambaye ni mlemavu wa macho Anna Kaheya (kulia) akipokea  kitita cha Sh 1milioni kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (kushoto) jana kwa niaba ya wanawake wenzake 20 wenye ulemavu kwa ajili ya kuanzisha miradi ya ujasiriamali. Mbunge huyo alikutana na wanawake hao Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa mjini zilizopo Sabasaba.  Picha na Mpigapicha Wetu
B2 
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (katikati) akifuhia jambo na wanawake wa Baraza la Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Iringa Mjini  baada ya kumaliza mkutano wake na wanawake hao kwa lengo la kujiwekea mikakati ya kukuza ujasiriamali kupitia Saccoss ya UWT. Picha na Mpigapicha Wetu.
Picha na mpiga picha wetu

MAMBO USIYOYAJUA KUHUSIANA NA UFOs (Unidentified Flying Objects)

bbb
 Na Benedict Liwenga (Maelezo)
…………………………………….
 
Katika Dunia tuishiyo sasa binadamu hatuko peke yetu, lakini tumejijengea dhana kuwa tunaishi peke yetu huku tukisahau kuwa Mungu kaumba viumbe kadha wa kadha vinavyoonekana na visivyoonekana.

ADOLF HITLER NA KIU YA KUTAKA KUITAWALA DUNIA.

index 
Na Benedict Liwenga, Maelezo.
…………………………………………
Kiongozi wa Chama cha Kisoshalisti kilichojulikana kama “NAZI” Adolf Hitler (1889-1945) alikuwa mmoja kati ya Madikteta dhalimu na mwenye nguvu kuwahi kutokea katika karne ya 20.

NYASA BOY ASHINDWA KUTOA VIDEO YA CHONGOROA KISA HAJAMZOEA VIDEO QUEEN WAKE

Msanii Chipukizi kutoka Jijini Mwanza, “Nyasa Boy” (Kushoto) amesema ilimchukua miezi minne hadi kuzoeana na Mlimbwende “Mwanne” (kulia) ambae ameshiriki kwenye video ya wimbo wake uitwayo “Chongoroa”.
Continue reading →

Waziri Mhagama atoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014

G1 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe Jenista Mhagama (kushoto) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini Dodoma kuhusu hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014 na jinsi dawa hizo zinavyoathiri afya na nguvu kazi ya taifa. Kulia ni Mfamasia Sehemu Elimu, Habari na Takwimu Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za kulevya nchini Amani Masami.
G2 
Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014 kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma)

Bunge lapitisha Bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora 2016/2017

J1 
Naibu Waziri wa nchini, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiingia ukumbi wa Bunge siku ya kupitishwa bajeti ya Wizara hiyo mwishoni wa wiki mjini Dodoma.
J2 
Waziri wa nchini, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akitoa hoja ili Bunge liidhinishe na kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 ya Wizara hiyo mjini Dodoma.
J3 
Naibu Waziri wa nchini, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akijibu hoja zilizoelekezwa na Wabunge kwenye Wizara hiyo kabla Bunge kuidhinisha na kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 mwishoni wa wiki mjini Dodoma.
J4 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Angellah Kairuki akitoa hoja ili Bunge liidhinishe na kupitisha bajeti ya Wizara hiyo ya mwaka 2016/2017 mwishoni wa wiki mjini Dodoma.
J5 
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip Mpango akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu fedha za Serikali wakati wa kupitisha bajeti ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora ya mwaka 2016/2017 mwishoni wa wiki mjini Dodoma.
J6 
Wabunge wakiendelea na kikao cha Bunge cha bajeti ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora ya mwaka 2016/2017 mwishoni wa wiki mjini Dodoma.

SIMIYU YAHAMASISHWA USAFI WA MAZINGIRA NA KUTUNZA MITI

1 
NA EVELYN MKOKOI
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano za Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ameshiriki usafi wa mazingira wa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi, mara hii mkoani Simiyu katika wilaya ya Meatu  jimboni Kisesa.
2 
Aliongeza kuwa, zoezi la upandaji miti mkoani simiyu katika ma shule, maeneo ya makazi ya watu na mashamba yanahitaji utunzani mkubwa kwani miti hiyo ina uwezo mkubwa wa kuboresha uoto wa asili ambao mpaka hivi sasa umetoweka
3 4

KAMBI TIBA YA GSM na MOI: Oparesheni 55 za vichwa vikubwa zafanikiwa BugandoKAMBI TIBA YA GSM na MOI: Oparesheni 55 za vichwa vikubwa zafanikiwa Bugando

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Jumla ya watoto 55 wamefanyiwa upasuaji katika kambi ya tiba ya watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi, iliyowekwa katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza siku nne mfululizo, kufuatia tatizo la kichwa kikubwa walilozaliwa nalo,  chini ya udhamini wa taasisi ya GSM Foundation. Zoezi litakalofanyika katika mikoa mitano ikiwa ni awamu ya kwanza kati ya nne zinazotarajiwa kufanyika Tanzania nzima. 
 
Akiongea wakati wa kufunga kambi hiyo rasmi jioni ya leo, Daktari Bingwa wa upasuaji na mifupa kutoka Taasisi ya Mifupa MOI, Dk Othman Kiloloma(Pichani Juu) ambaye pia ni mratibu wa kambi hiyo aliishukuru taasisi ya GSM kwa kuamua kulichukua tatizo hilo ambalo ameliita kuwa ni kubwa ukilinganisha na jinsi linavyochukuliwa na jamii ya watanzania.
 
Dk Kiloloma aliwaambia wanahabari kwamba jumla ya watoto 2000 huzaliwa na vichwa vikubwa katika kanda ya Ziwa peke yake, na mtaalamu wa kuhudumia wagonjwa wa namna hii ni mmoja tu ambapo pia kwa Tanzania nzima, wataalamu wa upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa wako tisa tu.
 
Cha kusikitisha ni kwamba kati ya hao, ni wachache sana hurudi kwa ajili ya matibabu bali wengi wao hufariki kwa kufichwa ndani na wazazi wao aidha kwa imani za kishirikina ama kushindwa kwa wazazi kumudu gharama za matibabu.
 
Mpaka jioni ya leo, ambayo ni siku ya nne tangu kuanza kwa kambi hii,  jumla ya watoto 55 walikuwa wameshafanyiwa upasuaji, ambapo siku ya kwanza, walifanyiwa watoto 16, siku ya pili wakafanyiwa watoto 17, siku ya tatu wakafanyiwa watoto 12, na leo wamefanyiwa watoto 10.
 
Mratibu huyo ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI), Dk Othman Kiloloma, amebainisha kwamba changamoto kubwa inayotokea kwa jamii linapokuja suala la watoto wenye vichwa vukubwa na mgongo wazi ni gharama za upasuaji, ambapo gharama ya upasuaji kwa mtoto mmoja ni kati ya shilingi laki saba za kitanzania mpaka Milioni moja.
 
“Watoto wengi huzaliwa katika mazingira duni na wazazi wasiokuwa na nguvu ya kiuchumi, hali inayosababisha wengi wao kuwaficha ndani huku wakiwahusisha na imani za kishirikina”, alifafanua Dk Kiloloma.
 
Dk Kiloloma amesema zaidi ya watoto 4000 huzaliwa kila mwaka wakiwa na tatizo la kichwa kikubwa, lakini wanaorudi Hospitali kwa ajili ya tiba nhawazidi laki nne, swali kubwa ambalo jamii hujiuliza ni kuhusiana na watoto ambao hawafiki hospitalini huishia wapi?
Kwa upande wake, Halfan Kiwamba, Afisa Mawasiliano wa Taasisi ya GSM Foundation ambao ndio washamini wakuu wa kambi hizo amesema, taasisi yake imeamua kuokoa maisha y watoto hao ambao ni nguvukazi ya taifa la kesho na inalifanya hilo ikiwa ni moja ya mikakati yake katika kurudisha fadhila kwa jamii ya kitanzania ambao ni wateja wakubwa wa bidhaa za GSM. 

Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano baina yaTanzania na Rwanda yafanya kikao chake Gisenyi Rwanda

gisenyi 
Gisenyi RWANDA
Kikao cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda kilichofanyika kuanzia tarehe 29 – 30 Aprili, 2016,kimekamilika Mjini Gisenyi, Rwanda,ambapo wataalam wa sekta mbalimbali wameazimia kuharakisha maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.

MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA MTANDAO WA VYAMA VYA WAZEE TANZANIA

wa1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania Ofisini kwake  bungeni mjini Dodoma  Aprili 29, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Wziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Hamis Kigwangalla .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
wa3 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania Ofisini kwake  bungeni mjini Dodoma  Aprili 29, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Wziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Hamis Kigwangalla .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)wa2 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana  na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake jijini bungeni mjini Dodoma  Aprili 29, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Wziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Hamis Kigwangalla .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Serikali kutumia shilingi bilioni 59.5 kuwezesha vijiji nchi nzima

index 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dokta Philip Mpango, amesema kuwa serikali imepanga kutumia shilingi 59.5bn kwaajili ya kuviwezesha vijiji nchi nzima katika kipindi cha mwaka fedha 2016/2017
Dokta Mpango, aliwaambia wabunge mjini Dodoma, leo tarehe 30, Machi, 2016, kwamba fedha hizo ni kwajili ya kukiwezesha kila kijiji shilingi 50m kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali.

TRA na TPA zatakiwa kufanya uchambuzi wa kina kubaini sababu za kupungua kwa shehena ya makontena bandarini

index 
SERIKALI imeziagiza Mamlaka ya Bandari-TPA, na Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kufanya uchambuzi wa kina ili kubaini sababu za kupungua kwa shehena ya kontena zinazoingia nchini kupitia Bandari ya Dar es salaam kwenda nchi jirani
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dokta Philip Mpango, ameliambia Bunge mjini Dodoma, leo tarehe 30, Machi, 2016 kwamba taarifa zilizopo zinaonesha kwamba uingiaji wa mizigo inayopelekwa nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, Malawi na Zambia kupitia bandari hiyo, umeshuka.

Dk. Philip Mpango:Serikali inaendelea kuhakiki madeni ya walimu

MP 
WAZIRI wa Fedha na Mipango Mhe. Dokta Philip Mpango, ameliambia Bunge mjini DODOMA, leo tarehe 30, Aprili, 2016, kwamba serikali inaendelea kuhakiki madeni ya walimu yaliyowasilishwa kwaajili ya malipo baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu kwenye baadhi ya madai hayo
Alisema kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015/2016, serikali ilipokea madai yenye jumla ya shilingi Bilioni 29 na Milioni 800 na imelipa  20.125bn, huku madai mengine yakizuiwa baada ya kubainika hayakuwa halali.
Alitolea mfano wa mtumishi mmoja aliyewasilisha madai ya shilingi 600m badala ya shilingi laki 6, huku madai mengine yaliyolipwa miaka ya nyuma yakiwasilishwa kama madeni mapya
Dokta Mpango alisema kuwa serikali inathamini mchango wa walimu katika maendeleo ya sekta ya elimu nchini na kwamba itaendelea kulipa madai yao na watumishi wengine wa umma baada ya kuyachambua, kuyahakiki na kujiridhisha kuwa ni halali.

Waandishi wa Habari wafundwa kuhusu kuandika masuala ya haki za binadamu.

HAK1 
Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu toka Umoja wa Mataifa (UN), Bi. Chitralekha Massey akiwapiga msasa baadhi ya waandishi wa habari kuhusu Mpango wa Kimataifa wa Kujitathmini juu ya Masuala ya Haki za Binadamu (UPR) wakati wa warsha ya siku moja 29 Aprili 2016 Mkoani Morogoro.
HAK2 
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. James Jesse akitoa mada mbele ya waandishi wa habari kuhusu Mpango wa Kimataifa wa Kujitathmini juu ya Masuala ya Haki za Binadamu (UPR) wakati wa warsha ya siku moja 29 Aprili 2016 Mkoani Morogoro.
HAK3 
Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi. Salma Ally Hassan (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu Mpango wa Kimataifa wa Kujitathmini juu ya Masuala ya Haki za Binadamu (UPR) wakati wa warsha ya siku moja 29 Aprili 2016 Mkoani Morogoro.
HAK4
Wadau wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakiwa katika picha ya pamoja na Waaandishi wa Habari waliohudhuria mafunzo ya siku moja ya warsha kuhusu Mpango wa Kimataifa wa Kujitathmini juu ya Masuala ya Haki za Binadamu (UPR) wakati wa warsha ya siku moja 29 Aprili 2016 Mkoani Morogoro.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO)
………………………………………………………………………………………………………………………..

MAPENDEKEZO YA SHERIA YA WAZEE KUWASILISHWA BUNGENI

images 
NAIBU WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amesema Serikali imekamilisha mapendekezo ya uundwaji wa Sheria ya Wazee ambayo yatawasilishwa katika mkutano wa Bunge wa Septemba.
Dk. Kigwangalla aliyasema hayo jana (Ijumaa, Aprili 29, 2016) wakati  akitoa ufafanuzi kwa Viongozi wa Mtandao wa Wazee waliomtembelea Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ofisini kwake mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment