Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Emmanuel Humba, (kulia), akimkaribisha Naibu Waziri wa Kazi Mhe. Anthony Mavunde alipowasilili kufungua mafunzo kwa Madaktari
yanayohusu ajali na maginjwa yanayosababishwa na kazi Jijini Arusha Leo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba
yanayohusu ajali na maginjwa yanayosababishwa na kazi Jijini Arusha Leo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba
…………………………………………………………………………………………
Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), umeendelea na kampeni
yake ya kutoa mafunzo kwa madaktari ili kujenga uelewa wa kufanya
tathmini ya ajali na magonjwa ayapatayo mfanyakazi yanayotokana na kazi
safari hii ikihusisha madaktari kutoka mikoa mitano ya ambayo ni Arusha
Tanga, Manyara, Kilimanjaro na Singida.
Mafunzo hayo yaliyofunguliwa leo
Mei 30, 2016 na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Bw. Anthony Mavunde, huko
jijini Arusha, ni muendelezo wa mafunzo mengine kama hayo yaliyotolewa
wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam, ambapo madaktari kutoka
mikoa ya Dares Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma, lindi na mtwara walihudhuria.
WCF imechukua hatua hiyo ili kujiandaa na UTOAJI WA Mafao kwa mara ya kwanza tangu uanzishwe ifikapo Julai mwaka huu wa 2016.
MISS TANZANIA USA AEESHA KAMARA ATEMBELEA, KUONGEA NA KUTOA MSAADA KENTON HIGH SCHOOL
Miss Tanzania USA 2015-2016 Aeesha
Kamara akiongea na wanafunzi wa Kenton High School ya Tabata jijini Dar
es Salaam siku alipotembelea shuleni hapo katika moja ya majukumu yake
ya kuhudumia jumuiya. Miss Kamara anadhamini wanafunzi wawili shuleni
hapo
Miss Tanzania USA Pageant Aeesha
Kamara akimkabidhi msaada mwalimu mipira siku alipotembela shule ya
Kenton High School ya Tabata jijini Dar es Salaam.
Miss Tanzania USA Aesha Kamara akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wawili anaowadhamini kwa kuwasomesha shuleni hapo.
Picha ya pamoja
MAJALIWA AWASILI ARUSHA
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii,
Profesa Jumanne Maghembe (kulia) na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix
(katikati) baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha May 30,
2016 ambako May 31, 2016 anatarajiwa kufungua mkutano wa Kimataifa wa
‘Africa World Heritage’ kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha
Arusha -AICC. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wafanyika mkoani Mtwara
Baadhi
ya wakazi wa mkoa wa mtwara waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mpango
wa kugawa bure vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito
na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki
chandarua.
Baadhi
ya watoto wa mkoani mtwara wakishindana kucheza muziki ikiwa ni sehemu
ya burudani zilizosindikiza hafla ya uzinduzi wa mpango wa kugawa bure
vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye
umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua.
Wasanii
Joe makini na Niki wa pili kutoka kundi la weusi wakitumbuiza hadhara
iliyojitokeza katika uzinduzi wa mpango wa kugawa bure vyandarua vyenye
viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya
miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Msanii
wa nyimbo za taarab isha mashauzi akiimba moja ya kibao chake wakati
akitoa burudani kwa wakazi wa mkoa wa mtwara waliohudhuria hafla
uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa
wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa
ujulikanao kama kliniki chandarua
Msanii
wa nyimbo za taarab isha mashauzi akitoa burudani kwa wakazi wa mkoa wa
mtwara waliohudhuria uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye
viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya
miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Mkuu
wa mkoa wa mtwara halima dendego akimbeba mmoja ya watoto
waliokabidhiwa chandarua chenye viuwatilifu ikiwa ni sehemu ya hafla ya
uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa
wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa
ujulikanao kama kliniki chandarua
Mkuu
wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akirusha maputo angani kuashiria
uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa
wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa
ujulikanao kama kliniki chandarua
Mkuu
wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akimkabidhi chandarua chenye
viuwatilifu mmoja ya mama wajamzito ikiwa ni sehemu ya hafla ya uzinduzi
wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama
wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama
kliniki chandarua
Mkuu
wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akimkabidhi chandarua chenye
viuwatilifu mmoja ya mama wenye watoto wa chini ya umri wa miezi sita
ikiwa ni sehemu ya hafla ya uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua
vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini
ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Serikali
ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya
Malaria wameendelea na jitihada za kupambana na ugonjwa huo ili kufikia
lengo la serikali la kupunguza vifo hadi kufikia asilimia moja ifikapo
mwaka 2020.
Katika
kutekeleza azma hiyo, serikali ya Tanzania na wadau hao wamezindua
mpango wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu vya muda mrefu kwa akina
wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa.
Akizindua
mradi huo kitaifa, mkuu wa mkoa wa Mtwara Bi Halima Dendego amewataka
wanawake kuhudhuria kliniki wakati wa ujauzito ili kupata ushauri na
kinga dhidi ya malaria ikiwa ni pamoja na kupata chandaru kitakacho
mkinga dhidi ya ugonjwa huo.Amesisitiza suala la kusafisha ameneo yote
ili kudhibiti mazalia ya mbu waenezao Malaria ikiwa ni njia moja wapo ya
kupambana na kuenea kwa ugonjwa huo unaosababisha vifo vya wakina mama
wajawazito na watoto wa chini ya miaka 5.
“kwa
mujibu wa Takwimu za ugonjwa huo kwa mkoa wa Mtwara, zimeshuka kutoka
asilimia 33 mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 17 kwa mwaka
2011/2012. Hata hivyo takwimu za kitaifa zinaonesha kushuka kwa ugonjwa
huo kutoka asilimia 33 mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 9 mwaka
2015”. Alisema Bi Dendego.“Lengo la kitaifa la mapambano dhidi ya
Malaria linaonesha kupunguza vifo hivyo hadi kufikia asilimia 5 mwaka
huu na asilimia 1 mwaka 2020 hivyo sisi mkoa wa Mtwara tuna jukumu la
kuhakikisha takwimu zetu zinaenda sambamba na takwimu za kitaifa”.
Amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa.
Kwa
upande wake Naibu Mkurugenzi wa kutoka ofisi ya Afya ya shirika la
misaada la Marekani USAID Bibi Ana Bodipo -Memba amesema, ushirikiano wa
serikila ya Marekani na Tanzania katika mapambano dhidi ya Malaria
umeonesha mafanikio makubwa kwani wamefanikiwa kupunguza kwa silimia 50
vifo vitokanavyo na malaria kwa upande wa Tanzania Bara na chini ya
asilimia moja kwa upande wa Zanzibar.
“Marekani
inafahamu umuhimu wa mapambano dhidi ya Malaria, na hivyo mfuko wa Rais
wa Kupambana na Malaria kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania
imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo hivyo nah ii ni ishara
nzuri katika kufikia malengo ya kuutokomeza kabisa ugonjwa huu.” Alisema
Bi Bodipo.
Mwakilishi
wa wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Bi Helen
Semu amesema, serikali itaendelea na uhamasishaji wa jamii kuendelea
kutumia vyandarua vyenye viuwatilifu ili asilimia 85 iliyofikiwa kwa
sasa izidi kuongezeka na kufikia lengo la kumaliza kabisa tatizo hilo
nchini.“Sisi Serikalini tutahakikisha tunaongeza jitihada za kuhamasisha
jamii kuendelea kutumia vyandarua vyenye viuwatilifu ili kila mmoja
afahamu umuhimu wa kufanya hivyo na kudhibiti maambukizi na vifo
vitokanavyo na ugonjwa huu” alisema bi Helen
Mpango
wa utoaji vyandarua vyenye viuwatilifu kwa akina mama wajawazito na
watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama CHANDARUA
KLINIKI unachukua nafasi ya mpango wa zamani wa HATIPUNGUZO na
unasimamiwa na Mradi wa VECTORWORK kwa kushirikiana na serikali ya
Tanzania na unfadhiliwa na mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na
Malaria chini ya usimamizi wa shirika la misaada la nchi hiyo – USAID.
MAANDALIZI YA UTAFITI WA VIASHIRIA NA MATOKEO YA UKIMWI TANZANIA 2016/2017 YAANZA RASMI.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akihojiwa na
waandishi wa habari katika mkutano wa wadau wa Utafiti wa Viashiria na
Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 uliofanyika leo jijini Dar
es Salaam. Utafiti huo utafanyika nchi nzima kuanzia mwezi Agosti,
2016.
Mwenyekiti
wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt. Fatuma Mrisho
akielezea umuhimu wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania
wa mwaka 2016/2017 katika mkutano wa wadau wa utafiti huo uliofanyika
leo jijini Dar es Salaam. Utafiti huo utafanyika nchi nzima kuanzia
mwezi Agosti, 2016.
Mkurugenzi
Mkazi wa ICAP Tanzania Dkt. Fernando Morales akizungumza katika Mkutano
wa Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka
2016/2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Utafiti huo utafanyika
nchi nzima kuanzia mwezi Agosti, 2016.
Baadhi
ya washiriki waliohudhuria Mkutano wa Wadau wa Utafiti wa Viashiria na
Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 wakifuatilia kwa makini
hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa
(hayupo pichani) katika Mkutano wa Wadau wa Utafiti huo uliofanyika leo
jijini Dar es Salaam. Utafiti huo utafanyika nchi nzima kuanzia mwezi
Agosti, 2016. (PICHA NA EMMANUEL GHULA).
……………………………………………………………………………………….
Na Veronica Kazimoto
Wito umetolewa kwa wadau pamoja na wananchi ili kushiriki kikamilifu katika kuwezesha upatikanaji wa takwimu rasmi nchini.
Akizungumza katika Mkutano wa
Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka
2016/2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema wananchi kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wana mchango mkubwa katika kufanikisha
upatikanaji wa takwimu rasmi nchini.
“Leo hii tumekutana na wadau
mbalimbali wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa
mwaka 2016/2017 utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu kwa ajili ya
kujadili na kushauriana namna ya kufanya utafiti huu kwa ufanisi ili
kupata takwimu bora zitakazosaidia katika kutunga sera na kupanga
mipango ya maendeleo nchini”, amesema Dkt. Chuwa.
Dkt. Chuwa amefafanua kuwa
utafiti huu unategemea sana ushiriki wa wananchi kwani wao ndio wadau na
wahusika wakuu ambao wanapaswa kutoa ushirikiano wa kutosha ili
kurahisisha upatikanaji wa takwimu rasmi zitakazosaidia Taifa katika
kuboresha huduma za afya kwa manufaa ya watanzania wote.
Dkt. Chuwa amesema Ofisi ya
Taifa ya Takwimu ipo katika harakati za kukamilisha maandalizi ya
utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania 2016/2017 ambao
utaanza kufanyika nchi nzima kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Aidha Dkt. Chuwa amesema
utafiti huu ni wa kipekee ukilinganishwa na tafiti zilizotangulia
kutokana na kuongezeka kwa viashiria vitakavyo chunguzwa ikiwemo
kuangalia kiwango cha CD4, kiwango cha maambukizi mpya, upatiakanaji wa
huduma zinazohusiana na UKIMWI pamoja na kupima watoto wadogo wenye umri
chini ya mwaka mmoja.
Amesisitiza kuwa kukamilika kwa
utafiti huu kutasaidia Serikali katika kuboresha huduma za afya nchini
hasa katika kupambana na maambukizi mapya ya UKIMWI na namna ya
kuboresha upatikanaji wa vifaa tiba.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mkazi wa ICAP nchini, Dkt. Fernando Morales amesema utafiti huu ni wa
muhimu katika kupima viashiria na matokeo ya UKIMWI kwa nchi ambazo
zimekuwa zikipata msaada wa kupambana na UKIMWI kutoka Serikali ya
Marekani.
“Lengo la Utafiti huu ni kupata
viashiria ambavyo vinasababisha maambukizi mapya pamoja na kupima jinsi
gani Taifa limeweza kupambana na ugonjwa wa UKIMWI nchini”, amesema
Dkt. Morales.
Utafiti wa Viashiria na Matokeo
ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 unafanyika katika nchi Ishirini
(20) Afrika ambapo kwa sasa nchi nane (8) zinaendelea na utafiti huu
zikiwemo Zimbabwe, Zambia, Malawi, , Lesotho, Swaziland, Uganda, Namibia
na Tanzania.
ZIARA YA LUHWAVI MANYARA LEO
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi (kulia) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Manyara Joel Bendera alipoenda ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa, mjini Babati leo Mei 30, 2016. |
Katibu wa CCM wa mkoa wa Manyara Ndekobali akishukuru baada ya mazungumzo hayo |
wakiagana baada ya mazungumzo |
Tuna kila sababu ya kulinda na kuendeleza utamaduni wetu
Benjamin Sawe
Maelezo Dar es Salaam
Watu wengi katika jamii yetu ya
Tanzania, ikiwa ni pamoja na baadhi ya viongozi, vijana na watoto hawana
uelewa mzuri kuhusu dhana ya utamaduni. Neno “Utamaduni” lina uwanda
mpana na linaelezwa kwa namna tofauti na watu mbalimbali. Wataalamu,
wanazuoni na wanajamii mbalimbali wametoa maelezo na tafsiri mbalimbali
za dhana ya utamaduni. Tafsiri hizi tofauti zinatokana na sababu za
kijiografia, kihistoria, kimazingira, kijamii na kipindi au muhula
husika.
‘Utamaduni’ ni shughuli au kazi
zote afanyazo mwanadamu na namna anavyokabiliana na mazingira
yanayomzunguka ili kukidhi mahitaji yake muhimu ya kumwezesha kuishi.
Mahitaji hayo muhimu ni Chakula, Makazi na Mavazi. Katika kumwezesha
kupata mafanikio aliyotarajia katika kupata mahitaji hayo, binadamu
alijiwekea utaratibu (nguzo) za msingi katika kutekeleza shughuli zake
za kila siku.
Utaratibu (nguzo) huo ulikuwa ni
ule wa kuandaa mazingira ambayo kila mtu alipaswa kuyafuata kila mara
anapofanya shughuli zake. Utaratibu huo ni ule wa kuwa na mila na
desturi. Mila na desturi hizi ambazo mababu zetu wamekuwa wakizifuata
kwa miaka mingi ni uridhi ambao tunapaswa kuuheshimu, kuulinda na
kuuendeleza. Kwa maneno mengine, mila na desturi hizo ambazo ni sehemu
ya utamaduni ni rasilimali muhimu sana katika maendeleo ya taifa letu.
Wahenga walinena ‘mkataa kwao mtumwa.’
Usemi huu unatufundisha mambo mengi sana ukizingatia mwenendo wa maisha
ya Watanzania katika mazingira ya sasa. Kifupi, usemi huu una maana
kwamba, mtu ambaye anadharau maisha na tamaduni ambazo amekulia nazo,
ametekwa kimawazo na yuko tayari kutumikishwa au kufuata mila na desturi
za jamii nyingine kutokana tu na tofauti ya tamaduni hizo.
Hivi sasa nchi yetu inasura
mbili. Kuna sura ambayo inaonyesha jinsi ambavyo baadhi ya Watanzania
baada ya kupata elimu yao, hususan elimu ya juu ambayo wameipata hapa
nchini au nje ya nchi, wanajiona ni tofauti kabisa na Watanzania
wengine. Wasomi hawa wanajiona wako katika nchi ngeni kabisa na sio ile
waliyozaliwa.
Kundi hili linaonekana kudharau
mila na desturi zetu na kuziona kama zimepitwa na wakati. Kundi hili
ambalo linaonekana kuongezeka hapa nchini, linaonekana kutotambua na
kutothamini kabisa utamaduni wetu na mchango wake kwa taifa. Mara nyingi
kundi hili linaonekana likitumia lugha ya kigeni (Kiingereza) zaidi
kuliko Kiswahili, kudhihirisha kuwa ni tofauti na jamii iliyopo
No comments:
Post a Comment