Pages

Tuesday, May 3, 2016

WAKAZI WA TEMEKE WAMIMINIKA KUJIUNGA NA MFUKO WA TAIFA WA HIFADHI YA JAMII ‘NSSF’


 
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye
foleni kwa katika banda la NSSF kwa ajili ya kujiunga na mfuko huo katika kampeni
maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya
ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam. (Picha na John Dande)
 Afisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango (kulia), akiwajazia fomu baadhi ya wanachama wapya katika
kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia
Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi.
Jumla ya wanachama 214 walijiunga na NSSF.
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye
foleni katika banda la NSSF kwa ajili ya kujiunga na NSSF katika kampeni
maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya
ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
Afisa Masoko na Uhusiano wa NSSF, Amani Marcel (kushoto) akiwakabidhi fulana wanachama wapya, Emmanuel
Joseph na Prisca Mwamsojo katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama
wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini
Dar es Salaam juzi. Jumla ya wanachama 214 waliandikishwa.
 
Ofisa Msajili wa Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Grace Mutegeki (kushoto) akiwaelekeza jambo baadhi
ya wanachama wapya waliojiunga na mfuko huo katika kampeni maalumu ya kuelimisha
na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia
  Wilayaya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga
jijini Dar es Salaam.
Afisa
Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango
akimjazia fomu ya kujiunga na NSSF mchuuzi wa mayai wakati wa  kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha
wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya
Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi. Jumla ya wanachama wapya 214 walijiunga
na NSSF.
 
Baadhi ya wananchi wakisoma fomu
kabla ya kujiunga na NSSF katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama
wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Jijini
Dar es Salaam.
 Watu mbalimbali wakisubiri kujiandikisha.
Afisa Uandikishaji wa NSSF, Amina Kisawaga, kushoto akiwaelekeza jambo baadhi ya wananchi waliotembelea banda lao katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachamawa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi. Zaidi ya wanachama 20 walijiandikisha.

RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI TAREHE 03 MEI 2016 MKOANI DODOMA

J1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri tarehe 03 Mei, 2016 katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma.
J2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kutoka kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri tarehe 03 Mei, 2016 katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma.
PICHA NA IKULU

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM MKOANI DODOMA

4Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakielekea kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma.
3Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipowasili mkoani Dodoma kwa ajili ya kikao hicho cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa.
2Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa kikao cha cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma.
1Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kushoto ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein.
PICHA NA IKULU

TAARIFA KWA WANACHAMA WA TANZANIA BLOGGERS NETWORK (TBN)

index 
Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini ‘Tanzania Bloggers Network’ – TBN inawaomba wanachama wake wote kutotumia taarifa ama habari au picha yoyote kutoka katika mkutano wa maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari (WPFD) unaofanyika kitaifa mkoani Mwanza.
Kamati Kuu ya Uongozi TBN imefikia hatua hiyo leo baada ya kujadiliana na kujiridhisha kuwa kumekuwepo na taasisi za tasnia ya habari ambazo zimekuwa zikiwatenga wanahabari wa mitandao ya kijamii (bloggers) na kutotambua umuhimu wao wakati sehemu kubwa ya taarifa mbalimbali nchini husambazwa na mitandao hiyo.
TBN iliyosajiliwa rasmi serikalini Aprili 2015 na kupewa namba ya usajili; S. A 20008 inawataka wanachama wake kutotoa ushirikiano wa aina yoyote kwa taasisi ambazo zinawatenga bloggers.
Tunasikitika kufikia hatua hii ila hamna jinsi.
TBN itasikitika na kumshangaa mwanachama wake au blogger asiye mwanachama kutounga mkono agizo hili, na kwenda kinyume na agizo hili. Muda umefika ‘Bloggers’ kudai heshima, kutambulika na kuthaminika kama tasnia ya habari ingine yoyote.
Imetolewa na;-
Mwenyekiti wa Muda wa TBN
Joachim E. Mushi
03/05/2016

KATIBU WA BUNGE AKUTANA NA VIONGOZI WA JESHI LA MAGEREZA NA SUMA – JKT, JIJINI DAR, UTENGENEZAJI WA MADAWATI YA SHULE NCHINI KUANZA MUDA WOWOTE

mg1
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashilila akiongea na Viongozi wa Jeshi la Magereza pamoja na SUMA – JKT kwenye Ofisi za Bunge, Jijini Dar es Salaam kuhusiana na namna walivyojipanga katika kutekeleza jukumu la utengenezaji wa Madawati ya shule hapa nchini. 
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashilila akiongoza mazungumzo na Viongozi wa Jeshi la Magereza pamoja na SUMA – JKT(hawapo pichani).
mg3 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Casmir Minja(wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo wakifuatilia kwa makini mazungumzo na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashilila(hayupo pichani).
mg4 
Mtendaji Mkuu wa SUMA – JKT, Bregedia Jenerali C. Yateri akifuatilia mazungumzo hayo na Maofisa Watendaji wa Shirika hilo la SUMA – JKT.
mg5 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Casmir Minja akiteta jambo na Mtendaji Mkuu wa SUMA – JKT, Bregedia Jenerali C. Yateri walipokutana leo Mei 3, 2016 katika Ofisi za Bunge, Jijini Dar es Salaam(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

WANAHABARI SHIRIKIANENI NA WADAU WA AFYA KUELIMISHA JAMII KUHUSU MABADILIKO YA TABIANCHI.

05 
Dkt. Azma Simba wa Kitengo cha Epidemolojia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambaye alimwakilisha mgeni rasmi katika ufunguzi wa Semina kwa Waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko ya tabianchi akisoma taarifa ya Mkurugenzi toka Wizarani leo 3 Mei, 2016 Jijini Dar es Salaam.
DSC_5757
02
03 Msimamizi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabia Nchi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Geofrey Mchau akitoa mada mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko ya tabianchi nchini wakati wa Semina Maalum kwa Waandishi hao leo 3 Mei, 2016 Jijini Dar es Salaam.

JAJI WA SHINDANO LA TUZO ZA EJAT 2015, NATHAN MPANGALA ALIPONGEZA BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT)

1 
Baadhi ya majaji wa Shindano la Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT) 2015, wakifuatilia utoaji tuzo wa shindano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam wiki iliyopita. Kutoka kushoto ni Bw. Nathan Mpangala, Bw. Juma Dihule, Bw. Kiondo Mshana, Bi. Valerie Msoka (Mwenyekiti), Bw. Ndimara Tegambwage na Dkt. Joyce Bazira Ntobi.
2 
Jaji wa Shindano la Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT) 2015, Nathan Mpangala (kushoto) akimkabidhi tuzo Bw. Mansour Jumanne wa SAUT FM ya Mwanza katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.
……………………………………………………………………………………
MMOJA wa majaji wa Shindano la Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT) 2015, ambaye pia ni mchoraji vibonzo maarufu nchini, Nathan Mpangala amelipongeza Baraza la Habari Tanzania (MCT), kwa kumpa heshima ya kuwa mmoja wa majaji wa tuzo hizo zilizofanyika wiki iliyopita Jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia ushiriki wake katika shindano hilo, alisema toka kinyang’anyiro hiko kianze mwaka 2009 hakijawahi kuwa na jaji mchora vibonzo. Safari hii MCT wameliona hilo. Ni jambo zuri na la kupongezwa.
“Yanapofanyika mashindano ya aina yeyote yale, ni vema yakahusisha watu waliobobea katika eneo husika ili waweze kusaidia kutoa miongozo,” alisema Mpangala.
Jopo hilo la majaji liliongozwa na Bi. Valerie Msoka, wajumbe wengine ni  Bw. Ndimara Tegambwage, Dkt. Joyce Bazira Ntobi, Bw. Ali  Uki, Bw. Jesse  Kwayu, Bw. Kiondo Mshana,  Bw. Juma Dihule, Bw. Godfrey  Nago na  Bi. Pili Mtambalike.

UINGEREZA YAIFAGILIA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE, JKCI

 Kaimu Muuguzi Mkuu wa taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), Flora Kasembe, (wapili kulia), akitoa maelezo ya namna wanavyohudumia wagonjwa waliolazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi cha JKCI, wakati Naibu Balozi wa Uingereza hapa nchini, Matt Sutherland, (wapili kushoto), alipotembelea kambi ya upasuaji wa moyo iliyoendeshwa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na taasisi ya hiari ya Uinegereza ya Muntada Aid, Mei 3, 2016. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Profesa Mohammed Y.Janabi, Meneja Mradi wa Muntada Aid, Kabir Miah, Mkuu wa Upasuaji wa JKCI, Dkt.Peter Kisenge, na Daktari Bingwa wa Moyo wa JKCI, Dkt.Tulizo Shem
Profesa Janabi (kushoto) na Balozi Sutherland baada ya kutembelea chumba cha Coronary care unit
NA K-VIE MEDIA/Khalfan Said
NAIBU balozi wa Uingereza hapa nchini, Matt Sutherland, (pichani wapili kushoto), ameisifu
taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), kwa kuratibu kambi ya upasuaji wa
moyo kwa kushirikiana na madaktari kutoka nje kwa mafanikio makubwa.
Pongezi hizo amezitoa leo May 3, 2016, baada ya kutembelea kambi
hiyo maalum iliyoko kwenye taasisi hiyo, na kujionea madaktari wakiendelea na
kazi ya kuwafanyia upasuaji watoto wa Kitanzania kutoka sehemu mbalimbali
nchini.
“Nimefurahishwa sana na uamuzi wa JKCI wa kuratibu zoezi hili
kwa ushirikiano na wataalamu wa magonjwa ya moyo kutoka nje ya nchi, najua
taasisi ya hiari kutoka Uingereza imekusanya fedha na kwa kushirikiana na
madaktari wengine, wamewezesha zoezi hili kufanyika kwa mafanikio.” Alisema
Balozi Sutherland.
Taasisi ya Muntada Aid, ni taasisi ya Kiislamu yenye makazi yake
nchini Uingereza, ambayo ndiyo iliyowezwesha kuwaleta madaktari na vifaa, na
hatimaye kwa kushirikiana na madaktari na wataalamu wengine kutoka JKCI
wameweza kufanya upasuaji wa watoto 20 hadi sasa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Profesa Janabi alisema, chini ya
uratibu wa taasisi yake, wataalamu kutoka Australia kupitia Open Heart
International, wakishirikiana na wataalamu kutoka JKCI waliendesha kambi  ya upasuaji wa moyo kwa watoto 15 kuanzia
Aprili 25 hadi Aprili 30.
“Kambi hii ya sasa, inaundwa na wataalamu kutoka Saudi Arabia
chini ya uratibu wa taasisi ya hiari ya Muntada Aid, yenye makazi yake nchini
Uingereza, na hadi leo hii Mei 3, 2016, tayari watoto 20 wameshafanyiwa
upasuaji na hivyo kufanya jumla ya watoto 40 wamefanyiwa upasuaji tangu kambi
hizi mbili zianze.” Alifafanua Profesa Janabi kwenye mkutano na waandishi wa
habari.
Profesa Janabi alisema, malengo yao ni kuwafanyia upasuaji
watoto 70 Ifikapo Mei 7. “Tunawashukuru wenzetu hawa kwa kuja kutshirikiana
nasi kwani upasuaji unaofanyika ni huu wa kisasa, ambapo hakuna kumpasua kifua
mgonjwa bali tunafanya upasuaji kwa kutumia matundu na hili ni jambo muhimu kwa
wataalamu wetu ambao wamepata fursa ya kujifunza kutoka kwao.” Alisema.
 Profesa Janabi (wapili kulia), wengine kutoka kulia, ni Balozi Sutherland, Dkt. Shem, na Dkt.Delila Kimambo
 Wataalamu wa JKCI wakiwa kazini kwenye mojaya vyumba vya upasuaji
 Balozi Sutherland, katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka JKCI na wale wa Muntada Aid
 Profesa Janabi, akimsikiliza mgeni wake, Balozi Sutherland
 Dkt.StellaMongella. (kushoto, akimpatia maelezo Balozi Sutherland, alipotembelea wodi ya watoto waliofanyiwa upasuaji (Post Operative Recovery Word), Kulia ni Profesa Janabi
 Balozi Sutherland, akiwapongeza wataalamu wa moyo kutoka Muntada Aid, wanaoshuhudia ni Profesa Janabi (kulia na Dkt. Tulizo Shem kutoka JKCI.
 Baadhi ya Watanzania wakisubiri huduma ya matibabu ya moyo
 Kiongozi wa timu ya madaktari kutoka Muntada Aid, (katikati)
 Dkt. Tulizo Shem akiongea
Balozi Sutherland akipokewa kwenye taasisi alipowasili

Uswahilini Bingwa Mama Shija Cup

 shi1 
Mchezaji Sultani Kasikasi wa Uswahilini wa pili kushoto akipongezwa na wenzake kupiga picha na mpira aliozawadiwa baada ya kufunga mabao matatu Hat Trick katika mchezo huo.
shi2Mwenyekiti wa timu ya Bodaboda ya Mbagala,Ali Omari akipokea jezi seti mbili na mpira mmoja kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilungule baada ya klushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Mama Shija Cup juzi Dar es Salaam.
shi3 
Muaandaji wa mashindano ya Mama Shija Cup, Fatuma Shija akikabidhi mpira kwa waamuzi wa mashindano yake baada ya kumaliza fainali za Kombe la Shija zilizofanyika uwanja wa Shule ya Msingi Kingunge, Mbagala na Uswahilini kuibuka mabingwa.
…………………………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Soka ya Uswahilini FC imeibuka mabingwa wa Kombe la Mama Shija baada ya kuichapa Wamangati zote za Mbagala katika fainali ilijaa ushindani mkubwa iliyofanyika uwanja wa Shule ya Msingi Kingunge, Mbagala Dar es Salaam.
Katika fainali hizo ambazo zilidhaminiwa na Kampuni ya Simu ya Vodacoma, mshambuliaji Sultani Kasikasi wa Uswahilini aliibuka mchezaji bora wa mchezo huo baada ya kuifungia timu yake mabao 3 yaliyoipatia timu yake ubingwa na kuzawadiwa mpira “hat Trick”.
Mabao ya Kasikasi yalipatikana dakika ya 32 , dakika ya 41 na 59 na mabao ya WAmangati yaliyungwa na Salum Gava dakika ya 39 na bao la pili lilifungwa na Musa Madebe aliyeunganisha krosi safi ya Shaaban Pazi.
Muandaaji wa mashindano hayo, Fatuma Shija akizipongeza timu zote 20 zilizoshiriki Kombe hilo aliwataka vijana kutumia muda wao mwingi kwenye michezo ambayo itachukua muda wao mwingi kujenga miili yao badala ya kuvuta bangi na kufanya vitendo vya kihuni mitaani.
Mashindano hayo yalishirikisha timu kuoka Mkuranga mkoa wa Pwani, Wilaya Mpya ya Kigamboni na Temeke, Mshindi wa nne ilikuwa timu ya  Kisemvule FC iliyezawadiwa mpira mmoja, mshindi wa tatu ni Bodabdoda iliyopata  jezi seti moja na mpira mmoja na mshindi wa pili alipata medali 15 za shaba, jezi seti mbili na mpira mmoja.
Ilikuwa furaha kubwa kwa mashabiki wa Uswahili baada ya kuzawadiwa Kombe na medali 15 za dhahabu kwa wachezaji wake, jezi seti mbili na mpira mmoja walishangilia na kucheza uwanja mzima  huku kuimba nyimbo za ushindi na kuwavutia mashabiki wake na wapita njia.

Mv Magogoni yasitisha huduma zake kwa ajili ya matengenezo

tem1 
Mtendaji Mkuu wa Temesa Mhandisi Manase Ole-Kujan akitoa taarifa juu ya kusimamia kwa huduma za Mv Magogoni inayofanyiwa Matengenzo makubwa.
tem2 
Wananchi wakipita katika daraja la Nyerere lilopo Kigamboani Jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli hivi karibuni.
tem3 
Kivuko cha Mv Magogoni kikiwa katika shughuli zake za kila siku za kutoa huduma kwa wananchi.
(Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO)
…………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Kivuko cha Mv Magogoni kinachotoa huduma kwa wananchi kutoka upande wa bahari eneo la Magogoni kuelekea  Kigamboni Jiji la Dar es Salaam kimesitisha kutoa huduma kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo makubwa.
Katika taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) Mhandisi Manase Ole Kujan kwa niaba ya Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano imesema kuwa kuanzia Mei 5 2016 kivuko hicho kitakuwa katika matengenezo makubwa ambayo yatafanya kusitisha huduma zake kwa muda.
Taarifa hiyo imesema kuwa huduma za kivuko zitaendelea kama kawaida kwani wananchi watatumia huduma ya kivuko cha Mv Kigamboni pamoja na kivuko kilichokodishwa na Serikali kutoka kampuni ya Azam Marine vitavyokuwa vinasaidia kutoa huduma kwa wananchi kwa muda wote ambao Mv Magogoni itakuwa katika matengenezo.
“ Muda wake wa matengenezo umefika na ni wakati muafaka kwa kivuko kwenda kwenye matengenezo ni muda mrefu kimetumika na kusimama kwa kivuko hiki hakutaleta madhara makubwa kwani mara baada ya kuzinduliwa kwa daraja la Nyerere hivi karibuni tuna imani wananchi watatumia daraja hili  ili kendelea na shughuli zao za kila siku” imesema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo wananchi wenye magari wanaotumia vivuko hivyo wameshauriwa kutumia daraja jipya la Nyerere ili kuepukana na usumbufu wa kusubiri kivuko pekee cha Mv Kigamboni chenye uwezo wa kubeba magari na kufafanua kuwa kivuko kutoka Azam Marine kina uwezo wa kubeba watu peke yake.
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa matengenezo ya kivuko cha Mv Magogoni yatafanyika  Jijini Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Temesa katika matengenezo ya mitambo na ukarabati na ujenzi  utafanywa na kampuni ya kizawa ya na Songoro Marine Transport Yard yenye makao makuu yake Jijini Mwanza.
Aidha kivuko cha Mv Magogoni kitakabidhiwa kesho kwa kampuni ya Songoro Marine Transport Yard kwa ajili ya matengenzo hayo na mara baada ya mkandarasi kuangalia hali ya kivuko atatoa muda kamili wa kumalizika kwa matengenezo ya kivuko hicho.
Serikali katika katika  jitihada za kupunguza msongamano katika vivuko hivyo imeamua kwenda kukifanyia ukarabati mkubwa ili kukiongezea uwezo na ufanisi wa kuhudumia wananchi kwa kusaidiana na daraja jipya la Nyerere lililozinduliwa na Mhe. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt john Pombe Magufuli hivi karibuni ili kuondoka na tatizo la msongamono kwenye vivuko vya Kigamboni.

RATIBA YA KUWASILI NA MAZISHI YA MPENDWA WETU ANDREW NICKY SANGA HAPA TANZANIA.


 RATIBA YA KUWASILI NA MAZISHI YA MPENDWA
WETU
ANDREW NICKY SANGA
Ndugu zetu pamoja na Marafiki; Kwa niaba ya Familia ya
Bwana Nicky Amon Sanga, Kamati ya Maandalizi inapenda kuwajulisha Ratiba ya
Safari ya Mpendwa wetu ANDREW NICKY SANGA hapa Tanzania kuanzia kuwasili kwa
mwili wa Marehemu hadi tutakapomweka kwenye nyumba yake ya Milele
Muda
Tukio
Mahali
Wahusika
DAR ES SALAAM
Jumanne 3 Mei 2016
3:55 Usiku
Mwili kuwasili
Uwanja wa Ndege: Julius Nyerere
Familia, Ndugu, Marafiki na Jamaa Wote
4:30-5:30 Usiku
Kuelekea Kuhifadhi Mwili
Hospitali ya Taifa Muhimbili
Familia, Ndugu na Marafiki na Jamaa Wote
Jumatano 4 Mei 2016
4:00-6:00 Asubuhi
Ibada ya Kuaga
Kanisa la Kilutheri Ubungo (Nyuma ya Ubungo Plaza)
Familia, Ndugu, Marafiki na Jamaa Wote.
6:30 Mchana
Safari ya Kuelekea Dodoma
Kanisa la Kilutheri Ubungo
Wote Waliojiandaa.
DODOMA
5:00:-6:00 Asubuhi
Chakula
Nyumbani- Kizota
Waombolezaji Wote
6:00
Kuelekea Uwanja wa Mashujaa
Waombolezaji Wote
6:30-7:20 Mchana
IBADA
Uwanja wa Mashujaa
Waombolezaji Wote
7:30-8:45 Mchana
Heshima za Mwisho
Uwanja wa Mashujaa
Waombolezaji Wote
8:46 Mchana
Kuelekea Makaburini
Waombolezaji Wote
9:20 Mchana
Mazishi
Makaburi ya Hijra Chinangali
Waombolezaji Wote

Kamati ya maandalizi siku ya Utamaduni Duniani yaanza maandalizi

ut1Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Hajjat Shani Kitogo (aliyesimama) akiongoza majadiliano jana Jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha kamati ya maandalizi ya siku ya Utamaduni Duniani inayoadhimishwa kila tarehe  ya 21 Mei.
ut2Afisa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Sefania Motela (aliyesimama) akichangia wakati wa kikao cha kamati ya maandalizi ya siku ya Utamaduni Duniani inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 21 Mei mwaka huu.
ut3Mwenyekiti wa Tamasha la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo Bw. John Mponda (kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao cha kamati ya maandalizi ya siku ya Utamaduni Duniani inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 21 Mei mwaka huu.
ut4 
Afisa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Fransis Songoro (aliyesimama) akiwasilisha mchango ulitolewa katika kamati ndogo ndogo zilizoundwa wakati wa  kikao cha kamati ya maandalizi ya siku ya Utamaduni Duniani inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 21 Mei mwaka huu.
ut5 
Baadhi ya Maafisa Utamaduni na Wadau wa Utamaduni wakifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokua yakiendelea wakati wa kikao cha kamati ya maandalizi ya siku ya Utamaduni Duniani inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 21 Mei mwaka huu.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo

Tume ya Kurekebisha Sheria Yakutana na Wataalamu Kutoka Marekani

mw1Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe. Jaji Aloysius Mujulizi akiongoza kikao cha pamoja baina ya Tume na Wataalamu kutoka Marekani kujadili Mfumo wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Tanzania.
mw2 
Kamishna wa Tume Prof. Sufian Bukurura akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja baina ya Tume na Wataalamu kutoka Marekani wakiongozwa na Prof Allen kujadili Mfumo wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Tanzania.
mw3 
Sehemu wa washiriki wa kikao cha pamoja baina ya Tume na Wataalamu kutoka Marekani kujadili Mfumo wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Tanzania.
mw4 
Mmoja wa washiriki kutoka Marekani akijitambulishwa wakati wa kikao cha pamoja  baina ya Tume na Wataalamu kutoka Marekani kujadili Mfumo wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Tanzania.
mw5Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe. Jaji Aloysius Mujulizi ( wan ne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka Marekani wakioongozwa na Prof Allen ( kulia kwa Mwenyekiti) wakati wa kikao cha pamoja baina ya Tume na Wataalamu kutoka Marekani wakiongozwa na Prof Allen kujadili Mfumo wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Tanzania. (Picha na Munir Shemweta, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania)

MBUNGE ABDALLAH ULEGA ADHAMIRIA KULIKOMBOA JIMBO LA MKURANGA KIMAENDELEO

ul001 
Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akichangia Bajeti ya Serikai katika Mpango pili  wa wa miaka mitano ijayo wakati wa vikao vya bunge la bajeti linaloendelea mjini Dodoma hivi karibuni.
ul01 
Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akiendelea na uchangiaji wa hoja katika Mpango huo wa pili  wa Maendeleo wa miaka mitano ijayo.
ul1 
Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akizindua kisima cha maji Mkamba katika jimbo lake  la Mkuranga mkoani Pwani.
…………………………………………………………………………………………………….
SERIKALI ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli imedhamiria kuwa Serikali ya mageuzi ya Viwanda ukilinganisha na zilizotangulia.
  Rais Dkt.Magufuli hata katika kampeni zake za uchaguzi 2015 wakati akipita kuomba kura alisisitiza dhamira ya Serikali ya kujenga uchumi wa Viwanda.
  Wakati Serikali ikisisitiza kujenga uchumi wa Viwanda huku ikipata sapoti kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi wabunge nao katika kuunga mkono hilo kila mmoja amekuwa na kiu ya Jimbo lake kuwa la mfano katika eneo hilo.
Abdallah Ulega ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga  lililopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani kwa upande wake tangu achaguliwe na wananchi wake ameonesha dhamira na kiu ya kutaka kuwakomboa wananchi wake Kwa kutaka jimbo hilo kuwa na viwanda.
  Anasema kuwa lazima wao kama wawakilishi wa wananchi Kwa maana ya wabunge wanaotokana na Chama cha Mapinduzi CCM wapokee Kwa mikono miwili mageuzi haya kwani wameahidi hivyo lazima watende.
  Ulega anasema kuwa Jimbo la Mkuranga ni kubwa na  linarutuba ya kutosha hivyo anakaribisha wawekezaji kuingia na kukubali Kuwekeza viwanda vidogovidogo na vikubwa katika kilimo hasa cha mazao mbalimbali  Kwa ajili ya maendeleo ya watu wake.
  Anasema kuwa kuna jitihada kama Mbunge amekuwa akizifanya za kuhakikisha kwamba jimbo lake ni miongoni mwa majimbo ambayo yanafaidika na mikakati ya Serikali ya kutaka mageuzi ya viwanda.
  “Kimsingi jimbo langu la Mkuranga ni kubwa kama nilivyosema na uzuri zaidi lina ardhi nzuri sana na ndiyo maana naomba wahisani na wawekezaji wa ndani kujitokeza kuja Kuwekeza na zaidi kijenga viwanda.”anasema ulega
Anasema kuwa kutokana na utajili wa Ardhi yenye rutuba wanaweza kujenga viwanda vya kusindika mazao lakini pia kwa sababu eneo lao ni kubwa basi hata viwanda vya kubangua korosho na kujengwa Kwa viwanda hivyo kutasaidia kuleta ajira katika eneo hilo.
  Anasisitiza kuwa  ndio maana wakati akichangia mpango wa wa maendeleo wa Serikali Kwa miaka mitano ameomba Serikali na wahisani kujitokeza Mkuranga lakini Kwa upande wa Serikali kuiweka Mkuranga kuwa sehemu yenye hitaji la ujenzi wa viwanda.
  Anasema amebainisha wazi kiu ya wananchi wa jimbo lake la kutaka maendeleo na ajira hivyo bila kuwepo na viwanda hakuna ajira inayoweza kuwepo na zaidi vijana watazidi kulaumu serikali yao.
  “Nimesema wazi kuwa Mkuranga kuna matatizo ya miundombinu mbalimbali ikiwamo barabara.Maji .kilimo na mambo mengine na katika baadhi ya maeneo haya nashukuru baadhi ya marafiki wameitikia mwito wangu na wameweza kusaidia katika kichimba visima ambapo wananchi wangu wameaza kupata Maji safi na salama.”anasema Ulega
  Anasema kuwa anawashukuru African Foundation Reflection Kwa kuonesha moyo wa kusaidia na juhudi  hizo zote zimetokana na jitihada zake za kutaka kuona siku moja Mkuranga inakuwa ya kutolea mfano tofauti na ilivyo sasa.
  Aidha katika mpango huo wa maendeleo Kwa miaka mitano Kwa Serikali ameomba kujengewa barabara Kutoka Kisiju hadi Mkuranga Kwa kiwango cha lami kwani barabara hiyo ni muhimu Kwa wananchi wa wilaya hiyo lakini hata wale wanaotoka Mafia.
  Pia anasema katika mpango  mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano Kuhusu maendeleo ya miundombinu nchini na hapo aliangalia  wilaya ya Mafia kwa sababu pale kuna bandari na watu wake pia ndiyo wazalishaji wakubwa wa korosho na samaki.
  Anasema kuwa  pia kwenye kata yake ya  mbezi kwaniaba ya wananchi wake wa Mkuranga wangeishauri Serikali kuwa  eneo la viwanda ili wananchi wake wawe sehemu ya uzalishaji wake.
  Aidha Ulega anazungumzia suala la kuondoa kero ya uhaba wa upatikani wa Maji katika jimbo hilo ambapo Serikali ingefanya bidii ya kutoa maji hayo kutoka katika mto rufiji kupitia kibiti hadi kufika Mkuranga na hatimaye Dar es Salaam.
  Anasema haiwezekani Kwa miaka nenda rudi tatizo la Maji halipatiwi ufumbuzi wakati Mkuranga inapitiwa kwa karibu  na Mto Rufiji ambapo mikakati madhubuti ya kuleta Maji ikifanyika tatizo hilo litabaki kuwa historia katika eneo hilo.
  Anasema tatizo la ajira Kwa vijana ni kubwa mno hivyo wanashukuru Serikali Kwa kutambua umuhimu wa kutilia mkazo uazishwaji na ufufuaji wa viwanda kwani eneo hilo ndilo linaweza kuwa.msaada Kwa vijana kuweza kupata ajira.
  “Mimi kama Mbunge wao kama nilivyosema awali nitaendelea kupambana na kufanya kila linalowezekana Kwa kuhakikisha Mkuranga inakuwa sehemu ya viwanda na naendelea kitoa rai Kwa wawekezaji kuchangamkia Ardhi yetu Kwa kujenga viwanda vingi ili vijana wangu wapate ajira.”anasema
  Anaongeza kuwa mkuranga ilisahaulika mno pamoja kwamba ni miongoni mwa wilaya za siku nyingi lakini imekuwa nyuma kimaendeleo hivyo niwakati mwafaka wa kushirikiana Kwa pamoja Kwa ajili ya maendeleo.
  Anasema kuwa wananchi wake waendelee kumuombea Kwa Mungu na wazidi kudumisha Umoja na mshikamano ili Kwa pamoja wapambane Kwa lengo la kuona jimbo la mkuranga linakuwa la mfano.
Akizungumzia kilimo cha korosho anasema kuwa pamoja na zao hilo kuwa ndio zao linalotegemewa kuendesha maisha ya wananchi wake lakini bado kwasababu ya ukosefu wa kuwepo Kwa viwanda hususani vya ubanguaji kunafanya pasiwepo na tija sana wanayoipata wananchi wake katika kilimo hicho.
  Anasema kuwa kutokana na hali hiyo ana kazi kubwa ya kuendelea kuzungumza na watu mbalimbali ili kuleta ushawishi wa kukubali Kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda hivyo.
  Pia akizungumzia Elimu anasema  anatambua changamoto zilizopo katika eneo hilo hivyo amedhamiria Kwa dhati Kwa kushirikiana na Halmashauri wanaongeza hamasa Kwa wanafunzi ili waweze kufanya vema katika masomo yao na hatimaye kuweza kupata wataalamu wa baadae.
  “Najua kuna Changamoto ya madawati na hili tunalishugulikia Kwa kushirikiana na kamati mbalimbali za Shule,wazazi,pamoja na walimu ili kuona namna ya kukabiliana na tatizo hilo na hata uchakavu wa majengo .”anasema Ulega.
  Anahitimisha Kwa kuwataka wananchi wa Mkuranga kila mmoja kujielekeza katika kuzalisha Mali huku wakienda na Kauli mbiu ya Rais Dkt.Magufuli ya Hapa Kazi Tu.

MAAZIMISHO YA SIKU YA MUZIKI WA JAZZ DUNIANI YAFANA

jaz1 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza akizungumza na wadau wa Sanaa kwenye maadhimisho ya Siku ya Muziki wa Jazz duniani yaliyofanyika mapema wiki hii katika Ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ilala Sharif Shamba jijinI Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Msanii mkongwe John Kitime na Mkuu wa Kitengo cha Matukio kutoka BASATA Kurwijira Mareges.
jaz2 
Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Maximilan Chami akitoa elimu kwa wasanii na wadau wa Sanaa kuhusu maadhimisho ya siku ya Muziki wa Jazz duniani yaliyofanyika mapema wiki hii kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ulioko ofisi za Baraza hilo Ilala Sharif Shamba. Kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza.
jaz3 
Msanii mkongwe na mchambuzi wa masuala ya Sanaa John Kitime akifafanua juu ya kwa nini bendi nyingi nchini zilitumia jina la jazz wakati akiwasilisha mada kwenye maadhimisho ya siku ya muziki wa Jazz duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Wengine kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza, Mwakilishi kutoka UNESCO Maximilan Chami na Afisa Habari wa BASATA Aristides Kwizela
jaz4Msanii Mkongwe wa muziki wa reggae na mchambuzi wa masuala ya Sanaa Innocent Nganyagwa (Katikati) akiimba sambamba na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza (Kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Matukio kutoka BASATA Kurwijira Mareges kwenye maadhimisho ya siku ya Muziki wa Jazz duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa BASATA ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewaongoza zaidi ya wasanii na wadau wa Sanaa mia moja katika maadhimisho ya siku ya Jazz duniani yaliyofanyika makao makuu ya Baraza hilo yaliyoko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.
Maazimisho hayo ambayo yameazimishwa kwa mara ya kwanza nchini yalipambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa Bendi ya muziki wa Jazz huku wataalam na wasanii wakongwe wakiwasilisha mada mbalimbali katika kongamano maalum lililobeba mijadala na hoja mbalimbali kuhusu muziki huo.
Akizungumza kwenye kongamano hilo Msanii Mkongwe John Kitime alisema kuwa muziki wa jazz una historia ya aina yake duniani hasa katika kujenga diplomasia baina ya mataifa, kuunganisha tamaduni mbalimbali duniani na kushiriki katika ukombozi dhidi ya ukandamizaji na utumwa.
“Sifa kubwa ya muziki huu wa jazz ni namna ulivyopokelewa na kuvuka mipaka katika tamaduni mbalimbali. Ni muziki unaoeleza hisia na matukio ya kweli yanayotokea. Ni aina ya muziki ambao ni urithi wa Dunia kwani una mchango wa pekee” alisema Kitime.
Awali akielezea historia ya muziki huu, Mtaalam wa muziki ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Matukio kutoka BASATA Kurwijira Mareges alieleza kwamba muziki wa jazz una mizizi yake barani Afrika kabla baadaye kupitia biashara ya utumwa haujasambaa sehemu mbalimbali duniani na kugeuka urithi wa Dunia nzima.
“Watumwa waliotoka Afrika ndiyo waliusambaza muziki wa jazz duniani. Walitoka nao Afrika ukachanganywa na tamaduni za Marekani na baadaye kuzalika jazz tunayoisikia leo. Waliutumia muziki huu katika kujiliwaza, kutetea haki zao, kupinga dhuluma na manyanyaso yaliyotokana na utumwa” alisisitiza Mareges
Akizungumza katika maadhimisho hayo, mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bw. Maximilan Chami alisema shirika hilo limetenga siku maalum kwa ajili ya kuadhimisha muziki wa jazz kutokana na mchango wake katika diplomasia ya utamaduni (cultural diplomacy), kutetea usawa miongoni mwa jamii na kuwa alama ya urithi wa tamaduni mbalimbali duniani.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza aliwapongeza wasanii na wadau wa Sanaa kwa kujitokeza kwa wingi katika kuadhimisha siku hiyo huku akisisitiza kwamba BASATA kwa kushirikiana na wadau litaendelea kuadhimisha tukio hilo muhimu kila mwaka na kuahidi kuboresha zaidi.
“Nawapongeza sana kwa kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho haya. Huu ni mwanzo mzuri. Tunaahidi kuendelea kuadhimisha siku hii kila mwaka na kwa ubora zaidi” alisema Mngereza.
Siku ya muziki wa jazz duniani imekuwa ikiazimishwa kila mwaka tarehe 30 mwezi Aprili kutokana na muziki huu kutambuliwa rasmi na Shirika la Umoja wa mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kama urithi wa dunia na ni kwa mara ya kwanza imeazimishwa nchini Tanzania. 

NEC YAKAMILISHA RASIMU YA KWANZA YA TAARIFA YA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2015

lubuva 
Na Benedict Liwenga-Maelezo.
Kamati Maalum iliyoundwa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kuandaa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika nchini Oktoba 25, 2015 imekamilisha Rasimu ya kwanza ya Taarifa hiyo na kuiwasilisha kwa Tume.
Akizungumza Katika kikao cha Tume mara baada ya kupokea Rasimu hiyo ya kwanza, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Mstaafu Damian Lubuva kwa niaba ya Wajumbe wa Tume amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na Kamati hiyo licha ya majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na Tume hiyo kwa sasa.
Jaji Lubuva ameeleza kuwa Tume imeridhishwa na kazi nzuri iliyofanywa ya kuandaa Rasimu hiyo ikiwa ni pamoja na muda mfupi uliotumika katika kukamilisha kazi hiyo.
Aidha, ameongeza kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa taarifa hiyo inakamilika na kukabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mapema mwezi Julai mwaka huu.
Pongezi hizo pia zimetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bwana Ramadhan Kailima wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa Tume akieleza kufurahishwa kwake na namna ambavyo dhana ya ushirikishwaji ilivyotumika katika kuandaa Rasimu hiyo.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliratibu na kuendesha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kuanzia Otoba 25 mwaka jana na kuhitimisha rasmi zoezi hilo Machi 20 mwaka huu kwa Uchaguzi wa Jimbo la Kijitoupele mkoa wa Kaskazini Unguja.  

MAPOROMOKO YA ARDHI WILAYA YA MOSHI YAMSHTUA MBUNGE WA JIMBO LA VUNJO ,JAMES MBATIA.

Mbunge wa Jimbo la Vunjo akisalimiana na mmoja wa waathirika wa mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni na kusababisha kufusi kilichokuwa kando ya nyumba yake kuporomoka na kuhatarisha maisha yake katika kijiji cha Iwa ,Kirua Vunjo katika wilaya ya Moshi.
Mbunge wa jimbo la Vunjo James Mbatia akizungumza jambo mara baada ya kutembelea familia ambazo nyumba zao zimeathirika na mvua zilizonyesha hivi karibuni baada ya kuangukiwa na vifusi na kunusulika vifo.
Mbunge wa jimbo la Vunjo akitizama zoezi la uondoaji wa Vifusi vilivyo poromoka kutoka na mvua zinazoendelea kunyesha.
Sehemu ya Kifusi kilichoporomoka kando ya nyumba .
Mkazi wa kijiji cha Iwa ambaye nyumba yake iliathirika na maporomoko ya udongo yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha akimuonesha maeneo yaliyoathirika kuzunguka nyumba hiyo.
Continue reading →

MRADI WA KUKUZA TEKNOLOJIA KUPITIA WATOTO XPRIZE WAZINDULIWA DODOMA

Profesa-MsanjilaNaibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa
Simon Msanjila (kulia) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mradi wa kukuza
teknolojia kupitia watoto XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa
wiki. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka
Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim
Kaoneka na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira
Rodrigues.
(Picha na Modewjiblog)
Kwa kutambua uwezo walionao watoto katika kubuni vitu mbalimbali, Taasisi
ya XPRIZE iliyo na makazi yake nchini Marekani, imezindua mradi wa
XPRIZE nchini ambao utahusisha watoto ambao hawapo shuleni ukiwa na
malengo ya kukuza teknolojia ya dunia kwa kutumia uwezo walionao watoto
wa miaka 5-12.
Akielezea mradi huo, Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, alisema
kuwa wameanzisha mradi huo kwa kutambua uwezo ambao wanao watoto na

kama wakiwezeshwa wanauwezo wa kufanya mambo makubwa.Alisema
dunia ina watoto wengi ambao hawapo shuleni kwa sababu mbalimbali na
hivyo mradi huo utakwenda kufanyika kupitia watoto ambao hawapo
mashuleni na watawapatia vifaa mbalimbali ili waweze kupimwa uwezo wao
katika kazi zinazohusiana na teknolojia.“Dunia
ina watoto Milioni 57 ambao hawapo shuleni tutawatumia kama hao kwa
sababu tunaamini watoto wanaweza kufanya mambo mengi lakini
wanachohitaji ni kuwezeshwa ili waweze kukamilisha mambo wanayofanya,”

Wambura-Sitakubali Rasilimali za Taifa hili zichezewe.

a1 
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura(wa pili kushoto) akipata msaada wakati akiteremka toka katika kiwanja cha shirika la utangazaji Tanzania(TBC) kulipojengwa nyumba za watumishi wa shirika hilo ambazo hazijaisha kwa zaidi ya miaka 20 sasa na kutoa maagizo ya kumalizia nyumba hizo au kuwapa Halmashauri ya Kisarawe ili wajenge Hostel za wanafunzi.(Picha na Daudi Manongi-WHUSM)
a2Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa shirika la utangazaji Tanzania(TBC) Bi.Joselin Lugola akitoa mrejesho kuhusu nyumba za shirika hilo zilizo kisarawe mkoani Pwani ikiwemo kukamilisha upatikanaji wa hati  wa eneo hilo na kuliendeleza ili watumishi wa TBC wa kisarawe walitumie kwa makazi.
a3 
Kaimu mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Bi.Nahya Mansour(wa kwanza kushoto) akimskiliza Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura(hayupo pichani) wakati akitoa maagizo juu ya nyumba za Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) zilizopo eneo la kimani Kisarawe mkoa wa  Pwani.wengine pichani ni Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Kisarawe Bi.Mwanamvua Mrindoko(wa pili kushoto).
a4 
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa shirika la utangazaji Tanzania(TBC) Bi.Joselin Lugola wakati alipofanya ziara katika nyumba za shirika hilo zilizopo kisarawe mkoani Pwani.
……………………………………………………………………………………….
Na.Daudi Manongi-WHUSM
Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura ametoa wito kwa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) kutunza Rasilimali za Taifa kwa kuwa ni pesa inayotoka na jasho la mlipa Kodi na ingeweza kutumika kwa kazi nyingine kuliko uharibifu unaofanyika katika kiwanja cha Shirika hilo kilicho eneo la kimani ambako zimejengwa nyumba za wafanyakazi wa shirika hilo waliopo kisarawe mkoa wa Pwani.
Mhe.Wambura alisema hayo wakati alipotembelea eneo la shirika hilo ili kupata mrejesho wa maagizo aliyotoa wakati alipofanya ziara ya kwanza katika eneo hilo Aprili 2011 mwaka huu na kuipatia siku saba Idara ya Miradi ya shirika hilo ikishirikiana na Halmashauri ya kisarawe kufanikisha upatikanaji wa hati miliki ya eneo hilo la makazi ya wafanyakazi wa shirika hilo.
“Taratibu za Kisarawe za upatikanaji wa hati zimekamilika na sasa wamepeleka ile Rasimu kwa kamishna wa hati kanda ya mashariki ,na maelezo tumeyaskia kwamba kulikuwa na kupishana katika uaandaaji wa hati ndo maana ikachelewa lakini kwa sasa hivi bado tunaitaji kulinda rasilimali za Taifa.Tunaitaji kuzuia uhalibifu”,Alisema Mhe Wambura.
Aidha Mhe Wambura ametoa maagizo kwa shirika hilo kuangalia uwezekano wa kuendeleza makazi hayo kwa kuwa mpaka sasa imepita miaka 20 eneo hilo halijaendelezwa na shirika hilo au kufanyiwa uwekezaji wowote au wakabidhi eneo hilo kwa halmashauri ya kisarawe ili wajenge hostel za wanafunzi na kuongeza kwamba yeye hatakubali eneo hilo lipotee kwa uharibifu kwa wananchi  kubomoa nondo na kuuza kama vyuma chakavu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) Bi.Joselin Lugola alimwahidi waziri huyo kuwa watahakikisha kwenye bajeti ya mwaka 2017/18 suala hilo linashughulikiwa  na kudai kwamba mara nyingi wanaweka pesa ya ukarabati lakini inakatwa lakini wataanza ukarabati kwa awamu kwa mikoa ya Arusha na Mwanza na makao makuu kwa hiyo hata izi za kisarawe zitakarabatiwa mara moja.

TAARIFA KWA WATANZANIA WOTE WAISHIO NCHINI UINGEREZA [TUJUMUIKE UK].

 Kikosi kazi cha watanzania wanaoishi Falme za UINGEREZA na EIRE YA KASKAZINI (TZUK Diaspora Taskforce, kwa kifupi, TZUK-DTF) kiliasisiwa na Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe mwaka 2014, kutokana na kutokuwepo na chombo/Jumuiya madhubuti ya kuwaunganisha Watanzania waishio hapa Uingereza
TZUK-DTF ilianza na wajumbe 11 wakiwemo maofisa wa ubalozi 2 kikiwa na majukumu makubwa ya kuwa kiunganishi kati ya watanzania na ubalozi wao hapa Uingereza pamoja na kupanga na kuratibu ufufuaji wa Jumuiya ya watanzania ambayo itakuwa shirikishi zaidi na endelevu. Mnamo mwishoni mwa mwaka 2015, chini ya Naibu Balozi, Mheshimiwa Msafiri Marwa, ilikubaliwa kwamba ili kutimiza malengo yake kwa ufanisi zaidi yaliyohusisha kuratibu ufufuaji wa Jumuiya ya watanzania Uingereza na kuhakikisha kwamba Jumuiya hiyo inakuwa na Katiba iliyo bora zaidi, ilionekana ni vyema TZUK-DTF ikawa na wajumbe zaidi watakaojumuisha watanzania wa kada mbalimbali walioko Uingereza wakiwemo waliokuwa viongozi wa mikoa wa Jumuiya na baadhi ya wale walioshiriki katika michakato ya uasisi wa katiba na uundwaji wa Jumuiya ya watanzania Uingereza. 
Kikosi Kazi hiki kipya kilikutana rasmi tarehe 05 Mwezi wa Kumi na Mbili, 2015, chini ya uongozi na ulezi wa Mheshimiwa Naibu Balozi, Msafiri Marwa, ambapo kiliainishiwa majukumu yake kama ifuatavyo:
1. Kujadili na kuziwekea mikakati ya ufumbuzi changamoto mbalimbali zilizokabiliwa na TZUK-DTF katika kutimiza majukumu yake ikiwemo na zile ambazo ziliikabili Jumuiya ya watanzania iliyokuwepo.
2. Kupitia maoni ya watanzania yaliyokuwa yamekusanywa tayari, ikiwemo na katiba za Jumuiya ili Jumuiya iwe na katiba bora zaidi itakayoongeza ufanisi katika shughuli zaJumuiya.
3. Kuhakiki na kuboresha muundo wa Jumuiya utakaokidhi mahitaji ya sasa ya watanzania waishio Uingereza.
4. Kuzikusanya na kuzipitia taarifa zote zitakazopatikana za fedha za Jumuiya enzi za uhai wake na kuzijumuisha kwenye Jumuiya mpya itakayoundwa
5. Kutengeneza na kuratibu njia bora zamawasiliano miongoni mwa wanajumuiya.
6. Kusimamia kipindi cha mpito kitakachopelekea kuundwa kwa Jumuiya ya watanzania Uingereza ikiwemo kuratibu uanzishaji/uimarishaji wa Jumuiya za watanzania za mikoani kwa mujibu wa katiba mpya, na 
7. Kuandaa na kusimamia mkutano mkuu wa watanzania wote wa Uingereza wenye madhumuni ya kutoa ripoti nzima ya TZUK-DTF, kupitisha katiba mpya, kutambulisha Kamati Kuu na uongozi mpya wa Jumuiya, kujadili na kuhakiki mipango na mikakati ya shughuli mbalimbali za Jumuiya kwa mwaka ujao, na Kikosi Kazi kuvunjwa rasmi na kukabidhi madaraka ya  usimamiaji na uendeshaji wa Jumuiya ya watanzania kwa uongozi mpya wa Jumuiya.
Kama watanzania wa  Uingereza mlivyoshiriki  katika upendekezaji wa katiba mpya na kutoa maoni juu ya Jumuiya yenu, tunaendelea kuwatia moyo kushiriki kwa moyo mmoja na wa kizalendo pindi tutakapoitisha mikutano ya watanzania kwenye mikoa mliyoko mwezekuhakikisha safari hii ya kuwa na Jumuiya iliyo/zilizo imara inafikia mwisho ulio mwema
 Ahsanteni

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT. ALI MOHAMED SHEIN AAPISHWA KUWA MJUMBE WA BARAZA LA MAWAZIRI

sg1 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman akimuapisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri ili aweze kushiriki na kutekeleza majukumu yake kwenye Baraza hilo huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia tukio hilo katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
sg2 sg3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
sg4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman mara baada ya tukio la uapisho.  PICHA NA IKULU
………………………………………………………………………………………………………………
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein leo asubuhi tarehe 02 Mei, 2016 ameapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri ili aweze kushiriki na kutekeleza majukumu yake ndani ya Baraza hilo.
Rais Shein ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, tukio ambalo limeshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Viongozi wengine walioshuhudia tukio hilo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo mchana ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Mawaziri, uliopo Ofisi ya Rais TAMISEMI Mjini Dodoma.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
02 Mei, 2016

KIKAO CHA KAMATI YA NIDHAMU MEI 3, 2016

wambura 
Kikao cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kinafanyika kesho Jumanne Mei 3, 2016 kwenye ukumbi wa ofisi za shirikisho zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Kikao hicho cha kupitia mashauri mbalimbali yaliyowasilishwa TFF, ilikuwa kifanyike Jumapili Mei Mosi, lakini kiliahirishwa kwa sababu ya wajumbe wengi walikuwa na udhuru.
Wadau watakaojadiliwa kesho ni pamoja na Kocha Mkuu wa Azam FC ya Dar es Salaam, Stewart Hall na wachezaji wake wakiwamo John Bocco, Shomari Kapombe, Aishi Manula na Kipre Tchetche.
Wengine ni nyota wa Young Africans SC ya Dar es Salaam ambao ni Amissi Tambwe na Donald Ngoma wakati kutoka timu ya JKT Rwakoma ya Mara wamo Paulo Jinga, Zephlyn Laurian na Idrisa Mohamed.
Wengine ni Ismail Nkulo, Said Juma, Idd Selaman na Edward Amos wa Polisi Dodoma, kadhalika Abel Katunda wa Transit Camp ya Dar es Salaam na daktari wa Coastal Union ya Tanga, Dk. Mganaga Kitambi.
Pia Herry ‘Mzozo’ Chibakasa wa Friends Rangers ya Dar es Salaam naye atajadiliwa na Bunu Abdallah ambaye ni Kocha Msaidizi wa JKT Oljoro ya Arusha.

MECHI YA NDANDA VS YANGA

 Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Ndanda FC ya Mtwara na Young Africans umerudishwa nyuma kwa siku moja na sasa itachezwa Mei 14, 2016 badala ya Mei 15, 2016 kama ratiba ya awali inavyosomeka.
Taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema sababu za kurudisha nyuma mchezo huo Na. 218 utakaofanyika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara ni kuipa timu ya Young Africans nafasi ya kujiandaa na kusafiri kwenda nchini Angola kwenye mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Mbali ya mechi hiyo, kuna michezo miwili ambayo imesogezwa mbele kwa siku moja. Mechi hizo ni kati ya Simba na Mwadui ambayo sasa itachezwa Mei 8, 2016 badala ya Mei 7, 2016.
Sababu za mchezo huo kusogezwa mbele ni kwamba Mei 7, 2016 kutakuwa na mchezo wa kimataifa utakaozikutanisha Young Africans dhidi ya Esperanca ya Angola kuwania Kombe la Shirikisho.
Mchezo mwingine uliosogezwa mbele ni kati ya Kagera Sugar dhidi ya Azam FC ambao sasa utafanyika Mei 8, 2016 badala ya Mei 7, 2016.
Sababu za mchezo huo kusogezwa mbele ni Uwanja wa Kambarage Shinyanga. Mei 7, 2016 uwanja huo utakuwa na mchezo kati ya Stand United ya Shinyanga dhidi ya Coastal Union ya Tanga.
Kadhalika Ligi Kuu Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea  kesho Mei 3, 2016 kwa mchezo mmoja ambao Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Jumatano Mei 4, 2016 Azam FC ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu ya Pwani kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Michezo hiyo itaanza saa 10.000 jioni na kurushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni ya Azam. 

KAMATI YA RUFAA YA NIDHAMU

wambura

Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kesho Jumanne Mei 3, 2016 saa 5:00 asubuhi itatangaza uamuzi wa rufaa nane zilizowasilishwa na kujadiliwa za viongozi, mchezaji na timu tatu zilizoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara 2015/2016.
 Kamati hiyo itatangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Mikutano wa ofisi za TFF, zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Jumla ya rufaa nane zinazohusu timu, kocha, viongozi na mchezaji mmoja zilijadilikuwa na kamati hiyo kwa Jumapili Mei mosi, 2016 kwenye ofisi za TFF jijini.
Rufaa zilizojadiliwa kwenye kikao hicho ni za:
  1. Timu ya Geita Gold
  2. Choki Abeid ambaye ni Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Geita Gold FC
  3. Denis Richard Dioniz – Kipa wa Geita Gold
  4. Fatel Rhemtullah – Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora
  5. Saleh Mang’ola – Mwamuzi wa Soka wa Mkoa wa Dodoma
  6. Timu ya Soka ya Polisi Tabora
  7. JKT Oljoro Fc ya Arusha
  8. Yusufu Kitumbo – Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora
Wadau hao wa soka walikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Nidhamu baada ya kamati hiyo kuwatia hatiani na kuwaadhibu kwa makosa ya kupanga matokeo ya michuano ya Ligi Daraja la Kwanza. Wakata rufaa wote walihudhuria kikao cha rufaa zao.   

Waziri Makamba awasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha

jan1 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
jan2 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
jan3 
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akitoa ufafanuzi kuhusu wizara hiyo leo Bungeni mjini Dodoma.
jan4Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Andrea Kigwangalla (kushoto) akiwa Bungeni leo mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Dkt. Ashatu Kijaji.
jan5 
Baadhi ya Wabunge wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
jan6Mwanafunzi wa kidato cha tatu kutoka shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza Getrude Clement akiwa Bungeni leo mjini Dodoma kwa  mwaliko wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba ambapo Serikali imetambua na kuthamini mchango wake kwenye  utunzaji wa mazingira. Mwanafunzi huyo alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi, uliofanyika New York Marekani.
jan7Mashududa walihusika katika zoezi la kuchanganya udongo wakati wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964, wakiwa Bungeni leo mjini Dodoma kwa  mwaliko wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba ambapo Serikali imetambua na kuthamini mchango wao katika kuuenzi na kuulinda Muungano wa Tanzania.
jan8Mwanafunzi wa kidato cha tatu kutoka shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza Getrude Clement (wa pili kushoto) ambaye alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi, uliofanyika New York Marekani akiwa na wanafunzi wenzake Bungeni leo mjini Dodoma.
jan10 
Naibu Spika Dkt Tulia Ackson na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe January Makamba wakiwa katika picha ya pamoja na mashuhuda waliohusika katika zoezi la kuchanganya udogo wakati wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964. Mashuhuda hao walikuja kutembelea Bunge leo Mei 2, 2016.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma)
………………………………………………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma.
Serikali inaendelea kusimamia mazingira na kuhakikisha mifuko ya plastiki inayotumika nchini iwe ni ile inayokidhi viwango vianvyokubalika ili kuondokana na changamoto ya kuzagaa kwa mifuko hiyo katika maeneo mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba alipokuwa akitoa hoja ya wizara yake kuidhinishiwa maombi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Makamba amesema kuwa sababu kubwa ya kusambaa kwa mifuko plastiki inatokana na mifuko hiyo kutolewa bure na hivyo kuchafua mandhari na kuziba mifereji sehemu mbalimbali hali inayosababisha athari kubwa katika mazingira.
“Asilimia kubwa kwenye mito, maziwa na fukwe za bahari imejaa mifuko ya plastiki, hali hii ni hari kwa usalama wa mazingira yetu” alisema Makamba.
Akiwasilisha hotuba yake, Waziri Makamba amesisitiza kuwa mifuko ya plastiki isiyotakiwa kutumika nchini ni ile yenye unene chini ya maikroni 50 ambayo hairuhusiwi kuzalishwa wala kuingizwa.
Kwa mujibu wa maelekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016, Waziri huyo amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imekamilisha kanuni mpya ya mifuko ya plastiki zinazorekebisha viwango vya unene unaoruhusiwa kutoka Maikroni 30 kwenda Maikroni 50.
Waziri Makamba amesema kuwa kanuni hizo tayari zimesainiwa kupitia tangazo la Serikali Na.271 la mwaka 2015 na kutolewa katika Gazeti la Serikali Julai 17, 2015 na kupewa Na. 29.
Kwa upande wake mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16 wa kidato cha tatu anayesoma shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza Getrude Clement ambaye alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi, uliofanyika New York Marekani amewahimiza Watanzania kutunza mazingira na kufauata maelekezo yanayotolewa na Serikali na wataalamu wa mazingira ili kuyatunza mazingira wanamoishi.
Getrude amesema kuwa amefarikjika kwa kuwawakilisha vijana wa Tanzania na dunia kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi ambapo mataifa 175 yalikutana kusaini makubaliano ya Paris.
Katika kuwahimiza vijana kujenga tabia ya kutunza mazingira, Getrde amewaasa vijana hasa wanafunzi kusimamia sauala la utunzaji wa mazingira wakiwa shuleni kwa kwa kujiunga na klabu mbalimbali ambapo yeye amejiunga na klabu ya “Mali Hai” iliyopo shuleni anaposoma.
Kwa upande wa Watanzania kwa ujumla kwenye utunzaji wa mazingira, Getrude amesema kuwa ni vema wajifunze kutoka mataifa mengine yanavyosimamia utunzaji wa mazingira hasa matumizi ya mifuko ya plastiki.  
Mwanafunzi huyo amekaribishwa na kutambulishwa kwa wabunge leo mjini Dodoma kwa heshima ya kuliwakilisha vema taifa wakati wa utiaji saini makubaliano ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki moon alimkaribisha Getrude kwa viongozi hao na kusema “Ni furaha yangu kumualika Getrude Clement ambaye pia ni mwakilishi wa vijana anayeishi Tanzania na anaziwakilisha sauti za vijana”.

Wafanyakazi TBL Group Dar,Mwanza , Mbeya,Arusha walivyosherehekea Mei Mosi

tb1Wafanyakazi wa TBL Dar es salaam  katika maandamano wakiandamana wakati wa maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi Duniani Mei Mosi zilizofanyika jana Duniani kote Kitaifa sherehe hizo zimefanyika mkoani Dodoma huku Rais Dk. John Pombe Magufuli akiongoza sherehe hizo.
t1Wafanyakazi wa TBL mkoani Arusha   katika maandamano wakiandamana wakati wa maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi Duniani Mei Mosi zilizofanyika jana
t2Wafanyakazi wa TBL mkoani Mbeya  katika maandamano wakiandamana wakati wa maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi Duniani Mei Mosi zilizofanyika jana
t3
Wafanyakazi wa TBL mkoani Mbeya  katika maandamano wakiandamana wakati wa maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi Duniani Mei Mosi zilizofanyika jana
t4
Wafanyakazi wa TBL wakiwa katika sherehe hizo mkoani Mwanza

Vyeti vya kuzaliwa wilayani Micheweni Pemba havitolewi kwa misingi ya kisiasa

???????????????????????????????????? 
Na Masanja Mabula –Pemba
SERIKALI ya Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba imekanusha  taarifa zilizotolewa na wananchi ya kwamba vyeti vya kuzaliwa katika Wilaya hiyo hutolewa kwa misingi ya kisiasa .
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Abeid Juma Ali aliyaeleza hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara  ambao baadhi yao waliodai kwamba kuna ubaguzi juu ya utoaji wa vyeti vya kuzaliwa
Alisema kuwa  kwa kipindi cha miezi mitano tangu ashike wadhifa huo  tatizo la upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa  kwa watoto  katika wilaya hiyo limeanza kupatiwa ufumbuzi .
Alifahamisha kuwa kwa kushirikiana na watendaji wa Ofisi ya Vizazi na Vifo   , ameanza kulipunguza tatizo hilo , ambapo watoto wengi wameweza kupatiwa vyeti kwa wakati na bila usumbufu .
“Mtoto hana chama iweje basi  nimbague kwa misingi ya siasa , natambua wajibu na majukumu yangu kwani mimi ni mtumishi wa umma na ninawatumikia wananchi wote pasi na ubaguzi ”alifahamisha .
Awali mfanyabiashara Ali Salimu Ali (Baraka) wa Wingwi alisema kwamba kunahitaji kuangaliwa upya Ofisi inayohusika na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwani imekuwa ikichelewesha kupatikana kwa vyeti kwa baadhi ya watoto .
Alieleza kwamba wapo watoto wamefikia umri wa kwenda skuli lakini hawana vyeti  vya kuzaliwa , licha ya kwamba kumbukumbu zao zipo katika Ofisi ya vizazi na vifo lakini zimeshindwa kufanyiwa kazi .
“Vyeti vya kuzaliwa bado ni tatizo , kwani kuna baadhi ya watoto wamefikia umri wa kuanza skuli , lakini hawana vyeti , tunaomba hii Ofisi  inayohusika na utoaji wa vyeti uiangalie upya  nahisi kama kuna  ubaguzi fulani hivi  ”alisema  .
Kikao hicho  pia kilihudhuriwa na Madiwani wa Wilaya hiyo ambapo Mkuu wa Wilaya alitumia fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara kuwapa ushirikiano wakati wanapokusanya mapato  yatokanayo na biashara zao.

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA

kib1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016
kib2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016
kib3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016
PICHA NA IKULU

Serikali kutumia dola milioni 690 kuimarisha miundombinu ya Bandari ya Dar es Salaam

TPA1 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Injinia Alois Matei akiwaeleza  waandishi habari kuhusu mradi wa maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam utakaogharimu kiasi cha Dola za Marekani milioni 690 ambapo mradi huo unafadhiliwa na Serikali, Benki ya Dunia,Trade Mark East Afrika na DFID, kulia ni Afisa Mawasiliano Mwandamizi  wa Mamlaka hiyo Bw. Focus Mauki na mwisho Kapteni Abdullah Mwingamno wa TPA Bandari ya Dar es Salaam.
TPA2 
Mhandisi Mkuu  wa TPA Bi Mary Mhayaya akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa Flow meter mpya ya Kigamboni ambao umeshakamilika na hivyo kuwezesha mafuta yote yanayoingia  nchini kupitia Bandari ya Dar es Salaam kupimwa na kujulikana kiasi halisi kilichoingizwa hapa nchini ili kuiwezesha Serikali kupata mapato stahiki ikiwemo kodi .
TPA3
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa ya Mamlaka ya Bandari TPA iliyokuwa ikitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Injinia Alois Matei kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezi leo

No comments:

Post a Comment