Pages

Wednesday, May 25, 2016

MAJALIWA AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO ZAMBIA

WAT01 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watanzania waishio Zambia kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Lusaka Mei 24, 2016. Majaliwa alikwenda Zambia kumwakilisha  Rais John Magufuli kwenye Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- ADB uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAT1 
Baadhi ya Watanzania  waishio Zambia wakimsikiliza Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa wakatia lipozungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Lusaka.  Majaliwa  alikwenda Zambia kumwakilisha Rais John Magufuli kwenye  mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB, Mei 24, 2016. (Picha na  Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAT3 
Baadhi ya Watanzania  waishio Zambia wakimsikiliza Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa wakatia lipozungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Lusaka.  Majaliwa  alikwenda Zambia kumwakilisha Rais John Magufuli kwenye  mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB, Mei 24, 2016. (Picha na  Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAT4 
Baadhi ya Watanzania  waishio Zambia wakimsikiliza Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa wakatia lipozungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Lusaka.  Majaliwa  alikwenda Zambia kumwakilisha Rais John Magufuli kwenye  mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB, Mei 24, 2016. (Picha na  Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAJALIWA AKUTANA NA KAGAME LUSAKA

index 
Waziri Mkuu, Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame  kwenye  Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia ambako walihudhuria mkutano wa Benki ya  Maendeleo ya Afrika – ADB, Mei 24, 2016, Majaliwa alimwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WASIFU WA TIMU ZA MEXCO, ARGENTINA NA CHILE KABLA YA KOMBE LA COPA AMERICA

CHI1 
Timu ya taifa ya Chile ni maarufu kama “La Roja”. Timu hii ilitengeneza historia kwa mara ya kwanza mwaka jana ilipoifunga Argentina magoli 4-1 katika fainali ya Copa America na kuchukua ubingwa wa ligi hiyo tangu kuanziashwa kwa Ligi hii.
Timu ya taifa ya Chile “La Roja” yenyewe iko kwenye kundi D ikijumuishwa na timu za taifa za Panama, Bolivia na Argentina, bado hili ni moja kati ya kundi gumu kwenye michuano ya mwaka huu. Je itafanikiwa kuingia fainali mwaka huu na hata kuchukua ubwingwa tena katika kombe hili? Majibu yote tutayapata katika Copa America 2016 StarTimes pekee


CHI2
Timu ya taifa ya Mexico ni maarufu kama “El Tri”, ni timu yenye historia ya kipekee kwenye fainali za kombe la dunia. Imeshiriki mara 14, haijawahi kushinda taji hili, iko katika nafasi ya 19 kwenye viwango vya FIFA
Katika copa America iko kundi C ambalo ni kundi gumu haswa! Ikiwemo Uruguay, Jamaica na Venezuela. Mwaka 1991 ilifanikiwa kuingia fainali na kucheza na Argentina lakini wakagonga mwamba na kupigwa bao 2-1. Hivyo hivyo kwa mwaka 1999 ilipocheza na Colombia katika fainali na kupigwa 1-0.
Je mwaka huu watajitahidi kuchukua ubingwa? Yote utayapata StarTimes


CHI3 
Argentina ni nchi inayopatikana barani America ya kusini. Mwaka jana timu hii ilifanikiwa kuingia katika fainali na kutolewa na mabingwa Chile waliochukua ushindi wa bao 4-1 katika kombe la COPA America na kuifanya chile iibuke kidedea katika fainali hiyo. Mwaka huu Argentina itashiriki katika mashindano ya Copa America, bila kumsahau kiungo mchezaji Messi ndani, je watafanikiwa kuingia katika fainali au hata kuchukua Ubingwa? StarTimes tutarusha mechi zote LIVE ndani ya channel za michezo

Serikali yaboresha Sekta ya hali ya hewa na kufikia ya kiwango cha kimataifa.

HALI 
Na Anitha Jonas – MAELEZO.
“Wahenga wanasema penye nia pana njia na haja ya mja hunena, muungwana ni vitendo.” Hatimae Serikali imetimiza ndoto zake za kuwa na kituo bora chenye kutoa  taarifa za uhakika zinazohusu masuala ya hali ya hewa katika kiwango cha Kimataifa.
Serikali imeweza kufanikisha hili kwa kupitia taasisi yake ya Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ambapo mpaka sasa imefanikiwa kuboresha huduma hizo kwa asilimia 80. Haya ni mafanikio makubwa kutokana na ukweli kwamba kufahamu habari za hali ya hewa kunasaidia sana kupanga shughuli za kiuchumi na maendeleo.
Hilo limejidhihirisha hivi karibuni katika taarifa ya tahadhari kuwepo kwa mvua zitakazo ambatana na upepo kutokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua sambamba na uwepo wa kimbunga Fantala katika Bahari ya Hindi.
Taarifa hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Hali ya Hewa, Dkt. Agness Kijazi na kusema mvua hizo zinatarajiwa kunyesha kuanzia Aprili 13-16,2016 ambapo kutakuwa na mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24. na hili limetokea kama lilivyotabiriwa. Wenye kuchukua tahadhari wamesha hivyo na kuepuka madhara yatokanayo na mafuriko. Waliohama baadhi ya sehemu za mabondeni, walishukuru baada ya kuona makazi yao ya awali yakifunikwa kabisa na maji.
Mvua hizo zilikuwa zikiathiri mkoa wa Tanga, Dar es Salaam, Pwani,Morogoro pamoja na visiwa vya unguja na Pemba.
Kuthibitisha kuwa kituo hicho kinatoa taarifa za uhakika ni pale ambapo mwaka jana Dkt. Agness Kijazi alitangaza kuwepo na mvua za EL-NINO kuanzia mwanzoni mwa mwezi Septemba–Desemba 2015. Hii ilithibitika baada kushuhudia kuwepo kwa mvua hizo katika maeneo mbali mbali ya nchi ambapo        mvua hizo zilisababisha mafuriko na uharibifu wa miundombinu,makazi na mazao ya wakulima.
Utabiri huo wa kuaminika unatokana na TMA kuboresha mtandao wa vituo na usimikaji wa mitambo ya hali ya hewa pamoja na kuongeza idadi ya vituo vya hali ya hewa ambapo vituo vitatu vyenye mitambo ya kisasa vimejengwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kilwa Masoko- Lindi, Mpanda-Katavi na Songwe.Vituo hivi vimechangia kuongeza upatikanaji wa takwimu na taarifa za hali ya hewa kwa shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi nchini.
Kwa sasaSerikali kupitia TMA imeanzisha kituo cha kupimia hali ya hewa na Kilimo kiitwacho Agromet Station hukoMatangutuani Pemba na hivyo kuongeza idadi ya vituo vya kutoa huduma za hali ya hewa katika sekta ya Kilimo na kufikia vituo 15 nchini,hivyo kuongeza ubora wa taarifa zinazotolewa.
Kwa upande wa taarifa za anga ya juu Mamlaka imeimarisha huduma za Usafiri wa Anga kwa kuboresha mtambo wa kupima hali ya hewa katika anga za juu (Modernization of Upper Air System) katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere Dar es Salaam (JNIA) pamoja na kufufua kituo cha kupima taarifa za anga ya juu kilichopoTabora.

MBUNGE WA MAFINGA MJINI ATOA MSAADA WA AMBULANCE JIMBONI KWAKE

MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi akizindua
gari la kubeba wagonjwa (ambulance) 
 
 Na fredy mgunda,iringa
MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi kwa kushirikiana na asasi ya kimataifa ya Rafiki Surgical Mission ya Australia ametoa msaada wa gari la kubeba wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa iliyopo katika jimbo lake hilo.
Gari hilo aina ya Toyota Hiace lenye thamani ya Sh Milioni 40 lilikabidhiwa jana kwa uongozi wa halmashauri ya mji wa Mafinga inayosimamia uendeshaji wa hospitali hiyo katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mashujaa, mjini Mafinga.
Akikabidhi msaada huo Chumi alisema; “napenda ifahamike kwamba gari hilo limenunuliwa na asasi hiyo ambayo mimi ni rafiki yao mkubwa. Uadilifu na uaminifu kwa taasisi hiyo umetufanya tushirikiane vyema katika mambo mengi kwa faida ya wananchi wa jimbo langu la Mafinga.”
Alisema  gari hilo la wagonjwa ni rafiki kwa wagonjwa na wajawazito kwa kuwa lina vifaa tiba vinavyoweza kutumika kutolea huduma wakati wakipelekwa hospitalini.
Baada ya kukabidhi gari hilo, Chumi ambaye ni mbunge wa kwanza wa jimbo hilo jipya, mkoani Iringa alikumbusha vipaumbele vyake kwa wapiga kura wake kuwa ni kuhakikisha linapata huduma bora ya maji, elimu, afya na miundombinu ya barabara.
Akishukuru kwa msaada huo, Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Dk Innocent Mhagama alisema kabla ya msaada huo, hospitali hiyo ya wilaya ilikuwa na gari moja tu la kubeba wagonjwa.
“Pamoja na kuhudumia hospitali hiyo ya wilaya, gari hilo moja lilikuwa likihudumia vituo vingine 18 vya kutolea huduma katika wilaya hiyo hivyo,” alisema.
Alisema kupatikana kwa gari hilo jipya kutasaidia kuboresha huduma hiyo  kwa kuokoa maisha ya wagonjwa na maisha ya mama na mtoto ambayo ni kipaumbele katika utoaji wa huduma za afya.
Akizungumzia huduma ya mama na mtoto katika hospitali hiyo ya wilaya, Dk Mhagama alisema kwa wastani wajawazito 500 wanajifunga kila mwezi hospitalini hapo.
“Kati yao wajawazito zaidi ya 100 huwa wanapata huduma za dharula huku wastani wa wajawazito 10 wakipatiwa huduma za rufaa,” alisema.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Charles Makoga alisema halmashauri yake kwa kushirikiana na mbunge huyo itahakikisha inatekeleza ahadi mbalimbali zilizotolewa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk John Magufuli, mbunge na madiwani ili kuboresha huduma kwa watu wake.

Mfumo wa usimamizi wa nyaraka kidijiti kuongeza kasi ya utendaji Serikalini.

mo1 
Katibu mkuu wizara ya habari,utamduni,sanaa na michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza jambo wakati  menejimenti ya wizara hiyo ilipofanya ziara ili kujifunza mfumo wa usimamizi wa nyaraka kidijitali unavyofanya kazi katika  ofisi za wizara ya ujenzi,uchukuzi na mawasiliano leo jijini Dar es Salaam.Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Faustin Kamuzora na Naibu katibu mkuu wizara ya habari,utamaduni,sanaa na michezo Bi.Nuru Khalfan Mrisho.
mo2 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Faustin Kamuzora akieleza jambo kwa menejiment kutoka  Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo walipofika ofisini hapo ili kujifunza mfumo wa usimamizi wa nyaraka kidijitali.
Watumishi pamoja na Menejimenti  kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Kaimu mkuu wa masijala ya wazi Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Bi.Bupe Munisi(wa kwanza mwenye nguo ya njano) jinsi mfumo wa  usimamizi wa nyaraka kidijiti(DMIS) unavyofanya kazi .
mo4Menejimenti ya Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakiwa katika ziara mafunzo ya mfumo wa usimamizi wa nyaraka kidijitali unavyofanya kazi katika  ofisi za wizara ya ujenzi,uchukuzi na mawasiliano.
……………………………………………………………………………………………………………………….
Na Daudi Manongi.
Mfumo wa usimamizi wa nyaraka kidijiti utaongeza kasi serikalini na hivyo kuchochea maendeleo chanya katika kila nyanja.
Hayo yamesemwa leo na Katibu mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel wakati wa mafunzo yanayotolewa na Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano kwa Menejimenti ya wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakati walipotembelea mfumo wa usimamizi wa nyaraka wa kidijiti.
Alisema pia kuwa mfumo huu una faida nyingi na ndio ambazo zimeifanya wizara hii kutaka kujifunza ni pamoja na suala la gharama na kwa kuwa serikali ya awamu ya tano iko katika jitihada kubwa za kupunguza matumizi na kwa kuwa bajeti ya shajala ni kubwa katika taasisi nyingi za serikali hivyo mfumo huu wa kidijiti utasaidia kupunguza garama kwani hapatakuwa na haja ya kutumia karatasi na hivyo kupunguza gharama kubwa.
Prof Elisante pia aliongeza kuwa mfumo huu utaongeza usiri wa nyaraka hizi na kwa sasa zitakuwa zinasomwa na yule tu aliyekusudiwa na kutoa pongezi kwa ofisi ya rais manejimenti ya umma kwa kuhamasisha matumizi ya mfumo huu kwani ukitumiwa vyema utakuwa na manufaa sana.
Kwa upande wake Katibu mkuu wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Faustin Kamuzora alisema kuwa mfumo huo ulijengwa miaka mitatu iliyopita na unaweza kutumika katika wizara yeyote kwani una ufanisi mkubwa sana kwani kwa sasa utaweza kuangalia mafaili gani yameingia  kwa mfumo wa kidijitali na  kwa namna hii itapunguza garama na muda kwani hatutakuwa tunatumia karatasi tena.
Prof.Kamuzora alizitaka Taasisi na Wizara mbalimbali kuwapa elimu ya kutosha watunza kumbukumbu kwani wao ndio wahusika wakuu wa kwanza wa mfumo huu na hivyo kuwataka wahusika kuwapa mafunzo ya kompyuta na kuboresha vifaa kama scanner maofisini mwao.
Nae mmoja wa watunza kumbukumbu kutoka wizara Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Felomena Swai alisema amenufaika na mafunzo hayo na yatawasaidia katika utunzaji wa kumbukumbu kwani sasa watapeleka barua kwa wakati  na kurahisisha utunzaji wa mafaili.

TUGHE TAA HQ YAPATA VIONGOZI WAPYA

index 
Viongozi wapya wa TUGHE tawi la TAA Makao Makuu, wakiwa katika picha ya pamoja.
……………………………………………………………………………………………………………
TAWI la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) la Makao Makuu ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA-HQ), limepata viongozi wake wapya katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa Transit uliopo katika jengo la Kiwanja cha Ndege cha Zamani (TBI).
TAA ni wakala wa Serikali iliyoanzishwa tarehe 29 Novemba 1999 kwa Tangazo la Serikali Na.404 la mwaka 1999 chini ya kifungu cha 3 cha Sheria Na. 30 ya mwaka 1997 ya Wakala wa Serikali. Wakala hii ilirithi majukumu ya iliyokuwa Idara ya Viwanja vya Ndege (Directorate of Aerodromes) chini ya Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, ulizinduliwa rasmi mnamo tarehe 3 Desemba 1999.
Viongozi hao wamepatikana baada ya uliokuwepo kumaliza muda wao, na  waliochaguliwa katika uchaguzi huo uliosimamiwa na Katibu Mkuu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Gaudence Kadyango,  ni pamoja na Mwenyekiti Bw. Nasib Elias aliyezoa kura zote 28, baada ya kutokuwa na mpinzani, huku katibu mkuu akichaguliwa Bi. Aziza Kipande aliyepata kura 15 akimshinda Bi. Caroline Mntambo aliyepata kura 13.
Wajumbe watatu ambao ni Bi. Mwanaisha Omari, Bw. Joel Mwakamele na Bi. Frida Omari walipitishwa bila kupingwa na wajumbe waliotoka idara mbalimbali za TAA HQ.
Naye Bi. Irene Sikumbili alipata kura zote 14 za wanawake na kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake na Katibu Mkuu wake ni Bi. Mwanahawa Mdee aliyepata kura 11 akimshinda Bi. Kipande aliyepata kura tatu.
Walioshinda katika nafasi  ya ujumbe katika kamati hiyo ni Bi. Glory Mollel na Bi. Pendo Pascal; wakati Bi. Mntambo ameukwaa uweka hazina na Bi. Magreth Mushi ni mwakilishi wa vijana, huku hakukuwa na mwakilishi wa walemavu kutokana na kutokuwa na mlemavu.
Naye mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Bw. Abdi Mkwizu alipata nafasi ya kuwapongeza viongozi wateule wa TUGHE na kuwaahidi ushirikiano mzuri kutoka upande wa mwajiri.
Katika kutoa neno la shukrani kwa wajumbe, Mwenyekiti Bw. Elias aliwashukuru wajumbe wote kwa kuonesha imani yao ya dhati kwake na kuwaahidi kuendeleza mshikamano na mahusiano mema yaliyojengwa na uongozi uliomaliza muda wake baina ya wafanyakazi na mwajiri, lakini pia baina ya wafanyakazi wenyewe.
Bw. Elias pia ameahidi kuhakikisha wafanyakazi ambao si wanachama wa TUGHE wanajiunga na chama hiki  kwani kina manufaa makubwa kwao yakiwemo ya kutetewa pindi mfanyakazi anapokuwa kwenye matatizo na mwajiri wake .
Naye msimamizi, Bw. Kadyango ambaye aliukabidhi uongozi mpya katiba, aliwashukuru wajumbe wote kwa kumaliza zoezi la uchaguzi kwa amani na kusisitiza kuwa na ushirikiano mzuri na mwajiri, kudumisha uhusiano mwema kazini kati ya waajiri na waajiriwa, kudumisha uhusiano mwema baina ya wafanyakazi wao kwa wao, kusimamia uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi na hali bora za kazi, ili kufikia malengo.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA SHERIA NA MAHUSIANO TAA

No comments:

Post a Comment